Pages

Pages

Wednesday, June 19, 2013

LEMA NA MBOWE WATAKIWA KUJISALIMISHA POLISI, WALIOKAMATWA JANA 67WAPEWA DHAMANA


Mbunge wa jimbo la Arusha mjini godbless Lema pamoja na Mwnykiti wa kambi ya upinzani Bungeni Freman Mbowe wakielekea polisi.

Na Bertha Ismail, Arusha
Jeshi la polisi limewataka Mwenyekiti wa kambi ya upinzani bungeni Freeman Mbowe pamoja na Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kujisalimisha polisi kwa hiari yao wenyewe kama shmu ya kutii shria bila shuruti.

Aidha pia jeshi hilo linawashikilia watu  67 wakiwemo wabunge wanne wa kambi ya upinzani  kwa kosa la kufanya mkusanyiko usikuwa na kibali katika kiwanja cha Soweto jijini hapa.
Akiongea na waandishi wa habari kamishina wa polisi Paul Chagonja Alisema kuwa wanawasaka wabunge hao baada ya kukimbia kusiko julikana mapema jana mara baada ya kufanya mkutano pasipo kuwa na kibali cha mmiliki wa kiwanja(AICC) pamoja na jeshi la polisi .
Aliwataja  wabunge ambao wamekamatwa na jeshi hilo  kuwa ni pamoja na mbunge wa singida Tundu Lissu ,Mbunge viti maalumu Joyce Nkya,mbunge wa Mbulu Mustafa Akunay pamoja na Saidi Arifu ambapo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mapema kesho mara baada ya kupata mthamana wakiwa katika kituo kikuu cha polisi mkoa
Sanjari na hilo pia kamishina huyo alisema kuwa  jeshi hilo linawataka viongozi hao wawili wa kambi ya upinzani kuja kutoa ushaaidi wa mlipuko wa bomu  uliotokea Jun 15 katika kiwanja cha Soweto wakati mkutano wa chadema wa kufunga kampeni ulipokuwa unafanyika kwani viongozi hao walidai kuwa wanao ushaidi wa kutosha wa picha na video zinazoonyesha muhusika wa kitendo hicho cha ulipuaji wa bom uliosababisha watu 3 kufariki dunia na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa.
“kama kweli mbowe na lema wanamapenzi mema na wakazi wa Arusha na uchungu wa damu ya wananchi iliyomwagika wajitokeze kulisaidia jeshi la polisi kutoa ushaidi huo ,ili muhusika aweze kufikishwa kwenye vyombo vya dola kwani polisi sio wauaji bali wasimamia ulinzi na haki ya wananchi wake na kama basi wataona hawataki kutoa ushaidi kwetu na wanatuisi vibaya kama wanavyo sema basi wapeleke ushaidi huo kwa Rais wa nchi maana yeye ndie Amiri  jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama hapa nchi”alisema Chagonja

Aliongeza kuwa kama wataona pia huko apafai kupeleka  basi watafute shehe au padre wapeleke ushaidi huo na hatu kali za kisheria zitachukuliwa kwa mtu huyo ambaye ameusika ,aidha alibainisha kuwa endepo hawata fanya hivyo sheria itafata mkondo wake kama inavyosema kuwa iwapo mtu anaushaidi wa kosa la jinai na anakaa nao pasipo kuutoa   kwa vyombo vya dola basi mtu Yule nae atachukuliwa sheria ya yeye pia kufunguliwa kosa la jinai.

Pia aliwataka wakazi wa mkoa wa Arusha kuendela na shughuli zao huku wakijipusha na makundi ya kisiasa pamoja na mikusanyiko isiyokuwa na kibali  kwani kufanya ivyo ni kuendeleza machafuko huku wahusika wakiwa wanatafuta mkono wao kwenda kinywani .
Aidha aliwataka waandishi wa habari kuwa wazalendo kwa nchi yao na kutumia kalamu  pamoja na kamera zao kulinda na kutunza amani ya nchi ikiwemo  kuheshimimu sheria kwa kuandika habari za kweli zenye kulinda amani kuliko kuleta machafuko.

Aidha watu hao wakiwmo na wabunge wao wameachiwa mapema leo kwa mdhamana hadi hapo juni 21 watakaporudi tena.

MAHAKAMANI YA HAKIMU MKAZI KISUTU YAMWACHIA HURU, IDDY SIMBA JIJINI DAR ES SAALAAM.


Idd Simba

Na Happiness Katabazi
HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, hivi punde imemwachiria huru Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Idd Simba, Mkurugenzi wa Bodi hiyo ambaye alikuwa Diwani wa Kata Sinza (CCM), Salum Mwaking’inda, Meneja Mkuu wa shirika hilo Victor Milanzi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Simon Group , Simon Kisena waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wa shirika hilo kwa sababu Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk.Eliezer Feleshi kuwasilisha hati ya kutokuwa na haja ya kuendelea kuwashitaki washitakiwa hao chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002. 

Simba anayetetewa na wakili maarufu nchini Alex Mgongolwa walifikishwa na mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Mei 27 mwaka jana wakikabiliwa na makosa ya kula njama,matumizi mabaya ya madaraka na kughushi na hujumu uchumi. 

Hivyo kuanzia sasa washitakiwa hao wapo huru.

MWALIMU WA MASOMO YA ZIADA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUBAKA KATOTO KA MIAKA 10.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athmani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba lilitokea juzi hivi karibuni katika kijiji cha Itunge wilaya ya Kyela mkoa wa Mbeya.
JESHI la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Mwalimu wa Masomo ya Ziada akituhumiwa kumbaka Mwanafunzi wa darasa la nne mwenye umri wa miaka 10.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athmani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba lilitokea Hivi karibuni katika kijiji cha Itunge wilaya ya Kyela mkoa wa Mbeya.
 
Alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Ipyana Gidion(30),kyusa,mkulima mwalimu wa masomo ya ziada (tuition) katika kituo cha Itunge Moravian   mtaa wa Mbugani Wilayani Kyela Mkoani hapa.
 
Alisema Mtuhumiwa huyo alimbaka mtoto mwenye umri wa  miaka 10, kyusa,mwanafunzi  darasa  la  nne  katika Shule ya msingi Mbugani mkazi wa Itunge “a” na kumsababishia maumivu makali mwilini.
 
Kamanda Diwani alisema  mbinu iliyotumika ni kuwaruhusu wanafunzi aliokuwa akiwafundisha  kuondoka na kubaki na mhanga kisha kumbaka katika chumba anachotumia kufundishia (darasani).
 
Aliongeza kuwa  mtuhumiwa  aliwahi kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani kwa kosa la kubaka na kutoka kwa rufaa na kwamba mhanga amepatiwa matibabu na kuruhusiwa ambapo taratibu zinafanywa ili mtuhumiwa afikishwe mahakamani.(Joseph 

MWANAMKE AVAMIWA NA CHATU NA KISHA KUMEZWA


Linda Laina Nyatoro,mwanam
ke kutoka nchini south africa alifikwa na mauti baada ya chatu kuingia ndani ya nyumba anayoishi na kumshambulia kisa kummeza kabisa.

 Na hizo ndizo picha za chatu alivyokutwa tayari kesha mmeza
chanzo. jumamtanda

HII NI TASWIRA YA VURUGU ZA ARUSHA KABLA NA BAADA YA POLISI KUWATAWANYA WANANCHI ENEOHILO.

ASKARI WAKIWA WAMEIMARISHA ULINZI.VIZUIZI MBALIMBALI VIKIWA VIMEWEKWA BARABARANI WAKATI WA VUR
UGU ZA WANANCHI NA POLISI JIJINI ARUSHA LEO.
 VIZIWIZI MBALIMBALI VIKIWA VIMEWEKWA BARABARANI WAKATI WA VURUGU ZA WANANCHI NA POLISI JIJINI ARUSHA LEO.MOTO UKIWA UNAWAKA KATIKATI YA BARABARA WAKATI WA VURUGU HIZOWASAMALIA WEMA WAKIMSAIDIA MTOTO BAADA YA KUTOKA VURUGU HUKU NYUMA YAO KUKIWA NA KUNDI KUBWA LA ASKARI.Sehemu ya umati wa waombolezaji wa wahanga wa mlipuko wa bomu wakiwa katika viwanja vya Soweto mjini Arusha wakiwa kwenye maombolezo muda mfupi kabla ya polisi kuwatawanya na kuwapiga mabomu

Tuesday, June 18, 2013

HIVI NDIVYO ANAVYOELEZA MBUNGE JOSHUA NASSARI BAADA YA KUPATA KIPIGO, PIA ASHANGAZWA NA WABUNGE WENZAKE WA MONDULI KUFURAHIA KUPIGWA KWAKE.


Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akiwa kitandani hospitalini
Akielezea kupigwa kwake, Mbunge Joshua Nassari akizungumza na Mbowe  na Nyalandu hospitalini hapo,  alisema alikuwa kwenye kata yake ya uchaguzi lakini ghafla alizingirwa na watu zaidi ya 30.
 
Alisema katika kundi pia walikuwamo watu watatu wenye asili ya Kisomali  ambao wawili kati yao ni wakazi wa jimbo lake la Arumeru.
 
“Walinishambulia na kunipiga  hali iliyonilazimu kukimbilia kwenye gari langu na kutoa bastola ili kujihami, lakini wakati nakimbia  nilizidiwa nguvu na watu hao na kuamua kukimbia sehemu asiyoijua ili kuokoa uhai wangu,” aliongeza Mbunge huyo.
 
“Hivi siasa kwa kweli tunakwenda pabaya maana mtu anashambuliwa bila sababu, nimeumizwa mimi pamoja na mawakala na viongozi wa Chadema waliokuwa Makuyuni,” alisema.

BREAKIN NEWZZZZ:- MBUNGE WA CCM NKASSI MWENYE TABIA YA KUSEMA OVYO ATOA MPYA TENA BUNGENI LIVE SASA HIVI!!

1741 
Mbunge wa Nkassi Kaskazini Ali Mohamed Keissy.
pohon ganja di rumah osama biin laden (1)
Mbunge wa Nkassi Ali Mohamed Keissy nchini Tanzania hivi karibuni alipendekeza nchi hiyo kuruhusu ulimaji wa bangi kama zao la biashara nchini humo, akieleza kwamba zao hilo linaweza kuleta faida kubwa nchini humo kuliko Tumbaku. Nilipata nafasi ya kuzungumza nae kwenye kipindi chetu cha Jamii na Maendeleo (Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya America-VOA)


BUNGENI MUDA HUU............ Mbunge wa Nkassi Kaskazini Ali Mohamed Keissy ANAKINUKISHA BUNGENI MUDA HUU......... ANATAKA WALE WOTE WALIODHULUMU SHIRIKA LA NDEGE WAFUFULIWE HATA KAMA WAMEKUFA ILI MIFUPA YAO ISAGWE SAGWE IWE HUKUMU YAKO;;; (rekodi aliyonayo mbunge huyu aliwahi kusema kuwa endapo serikali haitapeleka maji jimboni kwake atawabeba kwenye gari wanawake ambao hawajaoga kwa muda wa siku tatu na kuwapeleka bungeni ili wakakinukishe kikwapa mjengoni)PIA NI WIKI ILIYOPITA TU ALIULIZA KAMA ILE GESI YA MTWARA NI YA KUJAMBA AMA LAA...........

MTOTO: NILIPIGWA RISASI NA POLISI.

Abubakar Adam (11) akiwa Hospitali ya Mount Meru mjini Arusha jana baada ya kujeruhiwa wakati wa tukio la kushambuliwa kwa bomu kwenye mkutano wa Chadema.

ARUSHA/DODOMA. 
WAKATI watu waliofariki kwenye tukio la kurushwa bomu katika mkutano wa Chadema ikifikia watatu baada ya jana kufariki kwa mtoto Amir Ally (7), mtoto mwingine wa miaka kumi na moja aliyejeruhiwa, amedai kwamba alipigwa risasi na polisi kwenye tukio hilo.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe naye ametoa tamko kuwa chama chake kina ushahidi wa kutosha wa watu waliohusika na tukio la kurushwa bomu katika mkutano wa kamp
eni wa chama hicho.
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Arusha Medical Lutheran Center (ALMC), Dk Paul Kisanga alisema jana kuwa, Amir alifariki jana asubuhi baada ya kupata majeraha makubwa kichwani yaliyodhuru ubongo wake.
Dk Kisanga alisema huyo ni mmoja wa watoto watano, waliojeruhiwa wakati wakitoka madrasa huko Kaloleni, jirani na Uwanja wa Soweto kulipokuwa na mkutano na alifariki jana asubuhi hospitalini hapo.
Alisema watoto wengine wawili ambao ni ndugu; Fatuma na Sharifa Jumanne wamepelekwa Nairobi kwa matibabu zaidi baada ya miili yao kukutwa na vyuma. 

Dk Kisanga aliwataja watoto wengine waliojeruhiwa kuwa ni Fahad Jamal (7) ambaye yupo ICU akisubiri timu ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na hali yake kutoruhusu kusafirishwa. 

Pia yupo Abubakar Adam (11) ambaye amejeruhiwa mguuni na amelazwa katika Hospitali ya Mkoa, Mount Meru.
Mtoto aeleza kupigwa risasi
Adam alisema jana kuwa alipigwa risasi na mtu aliyekuwa amevalia sare za polisi, wakati akitoka madrasa akiwa na ndugu yake, Fahdi katika eneo la Soweto.
Alisema akiwa njiani, aliona watu wakimkimbiza mtu na ghafla alishangaa kupigwa risasi na kuanguka chini.
“Namkumbuka aliyenipiga risasi alikuwa amevaa sare za polisi,” alisema Adam mwanafunzi katika Shule ya Msingi Levolosi huku akitokwa machozi.
Muuguzi wa zamu, katika katika wodi ya watoto katika Hospitali ya Mount Meru, Asha Semdeli alisema jana kuwa mtoto huyo ana vyuma viwili katika mguu wake.
“Tunasubiri afanyiwe upasuaji kwani tayari mashine ya X-ray inaonyesha vyuma kuwepo katika mguu wa Adam siwezi kusema ni risasi au la,” alisema Semdeli.  
CHANZO MWANANCHI

HUYU NDIYE BIBI ALIYETISHIA KUGEUZA GESI KUWA MAJI ENDAPO SERIKALI ITANG'ANG'ANIA NA MPANGO WA KUSAFIRISHA GESI HIYO KUTOKA MTWARA KWENDA DAR ES SALAAM KWA NJIA YA BOMBA.


KIKONGWE Somoe Issa, anayekadiriwa kuwa na umri zaidi ya miaka 90, ambaye aliwahi kutishia kuigeuza gesi kuwa maji iwapo serikali itaendelea kulazimisha kusafirisha kwenda Dar es Salaam, sasa hajulikani alipo. 
Taarifa zilizoifikia MTANZANIA Jumapili ambayo ipo mkoani Mtwara, zilidai kuwa bibi huyo baada ya kutoa tishio hilo sasa amefichwa, ili asiweze kutekeleza lengo lake hilo. 
Bibi Somoe, anayeaminika kama Mkuu wa Kaya ya Msimbati, kijiji ambacho gesi asilia iligundulika, sasa hajulik
ani alipo, huku ndani ya kijiji hicho ulinzi mkali ukiwa umeendelea kutawala.
Ulinzi umeimarishwa katika kijiji hicho, lengo likiwa ni kuhakikisha hakuna mtu anayefika karibu na nyumba aliyokuwa akiishi bibi huyo.
MTANZANIA Jumapili, lilifika katika kijiji hicho juzi, ambako liliweza kuzungumza na Mwenyekiti wa Kijiji cha Msimbati, Salum Athuman Tostao, ambaye alikiri kuwa bibi huyo hayupo na wala haifahamiki alikopelekwa.
“Ni kweli bibi huyu hajaonekana tangu palipotokea vurugu na watu wa usalama waliokuwa wakitaka kumuiba, kama unavyofahamu kulikuwa na mtu aliyejifanya mwandishi wa habari alitaka kumuiba bibi huyu, lakini wanakijiji wakamshtukia na kuchoma gari lake moto.
“Kutokana na hali hiyo, mpaka sasa hatufahamu alipo na hatujui kama ni serikali au wanafamilia wamemficha, kwa sababu kwanza hawaturuhusu hata sisi ambao ni viongozi kufika maeneo ya nyumba aliyokuwa akiishi kwa sababu wanadhani tutaleta watu wengine wasiokuwa waaminifu kwa familia hiyo,” alisema Tostao.
Gazeti hili lilipomtafuta mtoto wa bibi huyo, Manzi Faki, alikataa kuzungumza chochote kuhusu mama yake, lakini aliitaka serikali kutekeleza ahadi zake kwa Wanamtwara.
“Hilo suala la mama sitaki kulizungumzia kabisa… jambo la muhimu serikali inapaswa kufahamu kuwa sisi wana Mtwara tunataka itekeleze ahadi ilizotuahidi ndipo waje kuchukua hicho kidogo wanachokitaka, zaidi ya hapo kijumla gesi haitoki,” alisema Faki.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mtandi, Salum Waziri, alieleza kuwa bibi huyo anaaminiwa na wanakijiji wenzake kutokana na uwezo wake wa kuzuia mambo yasiyotakiwa ndani ya jamii, sambamba na kuleta riziki pale wanapokwenda kumuomba.
“Kwa kweli sasa ulinzi mkali umeimarishwa na wanakijiji, hakuna mtu anayefika nyumbani kwake, hata sisi wenyewe hatuthubutu, ndiyo maana hatufahamu alikopelekwa.
“Nakumbuka bibi aliwahi kutumiwa na kampuni ya Artumas kukwamua mashine iliyokuwa imenasa katika mchakato wa uchimbaji wa gesi hiyo baharini, ambapo wazungu hao walihangaika kuita wahandishi nje ya nchi, lakini wote wakashindwa, ndipo waliponong’onezwa kuhusu bibi huyo wakamwendea na akaja kunasua.
“Wakampa zawadi ya kumjengea nyumba, haya ni mambo ambayo yalitokea mwaka 1994, kiujumla yapo mengi ambayo yametufanya tumwamini sana,” alisema Waziri.
Januari mwaka huu, Afisa usalama mmoja anayedaiwa kufahamika kwa jina la babu alijikuta katika wakati mgumu kiasi cha gari lake kuchomwa moto huku yeye mwenyewe akikimbilia kusikojulikana baada ya kuzuka vurugu kubwa wakati akimshawishi bibi huyo asizuie gesi kwenda Dar es salaam. 
Inadaiwa kuwa mwanausalama huyo alitumwa na viongozi wa juu wa serikali baada ya bibi huyo kutamka wazi kuwa gesi haitoki Mtwara kauli ambayo iliwafanya viongozi kupata wasiwasi na hivyo kumtuma mtu huyo ili amshawishi bibi huyo.
Wakati bibi huyo akizungumza na mwanausalama huyo inadaiwa kuwa aliwaita wajukuu zake wamsikilize ndipo vurugu kubwa zilipoibuka na kusababisha mwanausalama huyo atimue mbio huku akilitelekeza gari lake.
Juzi na jana baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wakizungumza na gazeti hili walisema wao hawazuii gesi kutumiwa na Watanzania, ila wanataka gesi hiyo ichakatwe hapohapo mkoani Mtwara na ndipo isafirishwe kuelekea sehemu nyingine.
Vurugu kuhusu gesi hii ya Mtwara zilianza kuibuka Novemba mwaka jana, wananchi wa mkoa huo walikuwa wakipinga ujenzi wa bomba la gesi kwenda Dar es Salaam. 
Pamoja na vurugu hizo kuzimwa mara kadhaa na Jeshi la Polisi, ambao sasa wanashirikiana na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), lakini bado MTANZANIA Jumapili imeshuhudia hali ya amani haijaweza kurejea mkoani humo.
Baadhi ya watu mkoani hapa, bado wanaendeleza visasi kwa kuchoma nyumba za wenzao, huku JWTZ wakidaiwa kuwapiga raia kila mara hata inapotokea kuwa wamezomewa.

TUHUMA NZITO KWA FFU DHIDI YA BOMU ARUSHA


MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amefichua siri kuhusu tukio la mlipuko wa bomu lililotokea jusi katika viwanja vya Soweto, jijini Arusha.

Katika kauli yake jana, Mbowe ameibua tuhuma nzito dhidi ya Jeshi la Polisi, ambapo alidai kuwa askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) ndiye aliyerusha bomu hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa,baada ya kutembelea majeruhi katika Hosp

itali ya Selian, Mbowe alisema chama chake kina ushahidi wa kutosha juu ya askari huyo kurusha bomu.

Mbowe ambaye pia ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni,alisema wamefanikiwa kupata ushahidi wa kutosha juu ya tukio hilo baya linalochafua taswira ya nchi.

Alisema chama chake kipo tayari kuweka ushahidi huo hadharani, iwapo Serikali itaendelea kufanya siasa na kuficha ukweli.

“Tunao ushahidi wa kutosha, ikiwamo wa picha za video unaoonyesha shambulio la bomu na risasi lilivyofanyika katika mkutano wangu jusi eneo la Soweto.

“Picha zinaonesha wazi aina ya silaha zilizotumika kwenye shambulio lile ni tatu, bomu la gurumeti ambalo lilitupwa na askari wa FFU aliyekuwa kwenye uniform.

“Kutokana na ushahidi huu tulikuwa tumewaeleza Polisi kama wataendelea kuficha tutaueleza umma na tutaiambia dunia, kwani aina ya silaha zilizotumika ni SMG na bastola.

“Makasha ya risasi kama ushahidi wa jambo hili zilizotumika tuliyaokota eneo la tukio na tayari tumeyarekodi na kuyakabidhi kwa askari waliokuwa wakichunguza tukio lile,” alisema Mbowe.

Hata hivyo Mbowe alipinga tamko la Serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uratibu na Bunge), William Lukuvi na kusema kauli yake ni ya kitoto mbele ya jamii.

“Kauli ya Serikali kupitia kwa Lukuvi kwamba vurugu zilisababishwa na vikundi, wanasiasa na mashirika yasiyo ya kiserikali ambavyo havijulikani ni sawa na kuwadhihaki Watanzania,” alisema.

Kutokana na hali hiyo Mbowe alisema tayari wanasheria wa chama hicho akiwemo Mabere Marando, Tundu Lissu na Profesa Abdallah Safari wanashughulikia suala hilo.

Alisema baada ya polisi huyo kurusha bomu, alikimbilia katika gari ya Toyota Land Cruizer yenye rangi ya bluu akiongozana na askari mwenzake ambapo gari hilo liliondoka kwa kasi, huku likisindikizwa kwa kukingwa na gari ya TDI hadi kituo cha polisi.

SPIKA

Alisema anashangazwa na hatua ya Spika wa Bunge Anne Makinda, kushindwa kuguswa na jambo hilo ambalo limelitikisa taifa na kuruhusu Bunge liendelee.

Alisema Spika Makinda, ameendelea kuongoza Bunge licha ya Hotuba ya Waziri Kivuli wa Fedha kuwekwa kando kutokana na tukio hilo lililovuta hisisa za watu wengi.

“Kila linapotokea tukio kubwa la mauaji kama haya shughuli za Bunge husimama ili kulishughulikia, lakini Spika hakushtuka hata pale alipoona wabunge wote wa Chadema hawapo bungeni.

“Spika Makinda ameshindwa hata kunipigia simu hata ya kunipa pole kama mbunge niliyenusurika kuuawa …. Yaani hawajaona sababu sababu ya kufanya hivyo na huenda watu waliokufa hawana thamani kwao, wameona ni sawa na kuku.

“Jeshi la Polisi, wamekuwa na kazi ya kuchunguza mambo yasiyoisha, inakuwaje waue wenyewe halafu wajichunguze? msione misafara ya magari ya viongozi yanakuja hapa hospitali ni unafiki mtupu.

“Wanawajua wauaji, tutayaweka haya yote hadharani sura za wauaji zitaonekana na suala hili tutalipigania mpaka haki itendeke ikibidi hata mpaka umoja wa mataifa,” alisema Mbowe.

Hata hivyo, aliishauri serikali kwa kuiambia kuwa kama haitaki ushindani wa vyama vya upinzani ni vema ikavifuta vyama vya siasa vilivyopo kulikoni kuendelea kuwaua wananchi wasio na hatia wakiwemo watoto wadogo wanaposhiriki shughuli za siasa.

SHILINGI MILIONI 100

Katika hatua nyingine, Serikali imeamua kutenga Sh milioni 100 kama zawadi kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazofanikisha kunaswa kwa mhalifu au watu wenye mtandao wa ulipuaji mabomu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, alisema bungeni mjini hapa jana, kuwa kila mtu mmoja atakayetoa taarifa za siri na za uhakika kufanikisha kukamatwa kwa mhalifu huyo, atapatiwa Sh milioni 10 “hadi fedha hizo ziishe na serikali ina uwezo wa kuongeza fedha zaidi hadi mtu huyo apatikane.”

Lukuvi,alikuwa akitoa kauli ya Serikali kuhusu mlipuko uliotokea katika mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi katika Kata ya Sowote, Arusha, Jumamosi iliyopita. Mkutano huo, ulikuwa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Alisema mtu yeyote atakayetoa taarifa hizo atahakikishiwa usalama wake na polisi.

Alisema watu wawili walikufa katika tukio hilo, ambao ni Judith William (48) na Ramadhani Juma (15), huku watu 70 wakijeruhiwa, watatu vibaya na kati yao wawili hali zao ni mbaya.

Alisema uchunguzi wa awali, umeonyesha mlipuko huo ulikuwa wa bomu la kurushwa kwa mkono, lililorushwa kutoka upande wa mashariki kuelekea magharibi, kulikokuwa na gari aina Fuso lililokuwa likitumika kuhutubia.

“Jaribio la polisi kutaka kumfuata aliyerusha bomu hilo lilizuiliwa na makundi ya wananchi, ambao walianza kuwashambulia polisi kwa mawe na kuwazomea na hivyo polisi kulazimika kuanza kujiokoa badala ya kumsaka mhalifu huo.

“Aina ya urushaji wa bomu hilo, hautofautiani na mbinu iliyotumika kwenye shambulio jingine la bomu lililotokea Mei 5, mwaka huu, katika Kanisa Katoliki la Olasiti katika jiji hilo hilo la Arusha,” alisema.

“Nataka niwaambie wahalifu hao kuwa njama zao za kutugawa kwa misingi ya dini, makabila, rangi, rasilimali na itikadi za vyama zitashindwa.

“Tutapambana nao usiku na mchana kwa silaha zote tulizonazo mpaka tutakapowashinda na kuwafikisha mbele ya mikono ya sheria,” alisema.

MBATIA

Naye Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), James Mbatia, ameitaka Serikali kuchukua hatua za haraka kukabiliana na hali ya uvunjifu wa amani iliyopo nchini.

Mbatia alitoa taarifa hiyo mjini Dodoma jana, wakati akizungumzia tukio la bomu lililotokea mkoani Arusha.

Alisema imekuwa kawaida ya Serikali yanapotokea matukio ya mauaji kama ya Arusha, kutoa majibu mepesi.

"Zamani ilikuwa nadra kutokea kwa matukio ya kuuana wenyewe kwa wenyewe, sasa imekuwa kama utamaduni.

“Hii inatokana na wenye mamlaka kutoa majibu mepesi ambayo hayana utekelezaji, tunapaswa kusema na kutenda, vinginevyo nchi inaelekea kubaya," alisema Mbatia.

“Kuanzia matukio ya Mtwara na matukio ya mabomu Arusha, kauli zinazotolewa na Serikali ni za kubabaisha.

CHANZO MTANZANIA