Pages

Pages

Wednesday, July 24, 2013

SUGU, LEMA WAMWAGA SERA ZA CHADEMA JIJINI MBEYA


 Mbunge wa Mbeya Mjini -Chadema Joseph Mbilinyi aka Sugu akihutubia Mamia ya wananchama wa Chadema kwenye mkutano wa hadhara mbeya
 Picha juu ni Sehemu ya mamia ya wafuasi wa chadema wakimsikiliza Mbunge wa Mbeya Mjini-Chadema Joseph Mbilinyi na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Walipokua wakihutubia mkutano wa hadhara.
Mbunge wa Mbeya Mjini-Chadema Joseph Mbilinyi aka Sugu(wa nne kushoto)na mbunge wa arusha mjini-chadema godbless lema(wa tatu kulia)wakiwa kwenye mkutano wa hadhara mjini mbeya

WALIOFARIKI DUNIA KATIKA VITA YA KAGERA YA MWAKA 1978/1979 KUKUMBUKWA JULAI 25/ 2013 MOROGORO.

 
 Askari wa jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) kikosi cha maombolezi kikiwa katika mazoezi ya kutoa heshima za mwisho kwa  mashujaa waliofariki dunia katika vita ya Kagera mwaka 1978 na 1979 wakati wa gwalide la pamoja la jeshi la magereza, Polisi na JWTZ katika maandalizi ya mwisho ya kilele cha maadhimisho ya siku kuwakubuka mashujaa hao ambayo yataadhim
ishwa kimkoa kwenye mnara wa kumbukumbu wa Posta julai 25 mkoani Morogoro. PICHA JUMAMTANDA.BLOG
 Askari wa jeshi la polisi wakiwa katika gwalide
 Askari wa jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) nao wakiwa katika gwalide la pamoja.
 Hapa ni askari wa jeshi la magereza wakiwajibika kwa ajili ya maandalizi hayo.
Askari wa jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) Mteule daraja la kwanza, Jonas Philipo kulia akitoa maelekezo eneo la barabara ya Stesheni.
Hapa Aande Philipo kulia akifafanua jambo kwa viongozi wakuu wa mkoa ndani ya jeshi na serikali.
 Moshi ukiwa umezagaa baada ya kulipuliwa kwa mizinga mitatu katika maandalizi hayo.
Hapa vikosi vyote vya JWTZ, Polisi na Magereza vikiingia katika eneo la mzunguko wa posta ambapo ndiko kutaadhimishwa sherehe hizo kimkoa julai 25/ 2013.

Chadema: Hakuna kusubiri mjadala wa Serikali tatu

 
Chadema kimepinga kauli ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kuhusu hatima ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 kikisema mchakato wa sasa wa Mabaraza ya Katiba, usiwe kikwazo cha mjadala wa muundo wa Serikali Tatu.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chadema, John Mnyika alisema Dar es Salaam jana kuwa hatima ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 utakaotokana na mchakato wa mabadiliko ya Katiba unaoendelea, siyo suala la kusubiri.
Akizungumza na mwandishi wetu juzi kuhusu kauli ya Waziri wa Katiba na Sheria Mathias Chikawe kwamba endapo mapendekezo ya Serikali Tatu yatapitishwa, kuna hatihati ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 kufanyika, Jaji Warioba alisema: “Tuachieni muda… hayo mengine ni hisia tu. Ni kweli tunayajua lakini acheni tumalize hili kwanza ( la Mabaraza ya Katiba). Hii ndiyo hatua tuliyopo sasa.”
Lakini jana Mnyika alisema: “Hatuwezi kusubiri hadi Mabaraza ya Katiba yakamilishe mchakato kama alivyoeleza Jaji Warioba katika gazeti lenu la Mwananchi toleo la leo, (jana),” alisema Mnyika kwa simu.
Jaji Warioba alitaka suala la muundo wa Serikali Tatu utakavyokuwa lisiwe hoja kwa sasa kwa kuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba inachokifanya ni kukusanya maoni kupitia Mabaraza ya Katiba na kisha kuandaa rasimu itakayopelekwa bungeni kwa ajili ya majadiliano na kwamba mjadala huo utawachanganya wananchi endapo utaingizwa katika hatua hii ya ukusanyaji maoni.
Lakini Mnyika alisema: “Mijadala hii haiwezi kusubiri mpaka hatua ya Mabaraza ya Katiba, inapaswa kuanza wakati huu kupitia mabaraza yanayosimamiwa na Tume na Mabaraza yanayoendeshwa na makundi ya kijamii. “Pia, masuala hayo ya mpito pamoja na marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, ni mambo ambayo yanapaswa  kutolewa ufafanuzi wa ziada na Serikali zaidi ya kauli ambayo Waziri wa Sheria na Katiba Mathias Chikawe ameitoa kupitia gazeti la lenu la leo (jana).”
Alisema kimsingi bado kunahitajika mjadala wa masuala ya mpito kwa sababu kuna uwezekano kwamba Katiba Mpya, ya Muungano au ya Zanzibar na ya Tanganyika, isiwe tayari kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2015, endapo suala la Serikali tatu litapita.
Alisema kwa upande mwingine, rasimu ya Katiba iliyotolewa imeibua mjadala juu ya mkwamo wa kikatiba (constitutional stalemate), ambao ni muhimu upatiwe suluhisho akisema chama chake kinapendekeza mchakato wa Katiba Mpya ya Tanganyika uanze mara moja ili uende sambamba na huu wa Katiba Mpya ya Muungano. Alisema ilikuwa vyema yote yakajadiliwa katika Bunge la Agosti 27, mwaka huu.
Waziri Chikawe alikaririwa na gazeti hili juzi akisema: “Uwepo wa Serikali tatu utafumua mfumo mzima wa utendaji ndani ya Serikali. Hatuwezi tena kufanya uchaguzi wa Rais na wabunge 2015, hatuwezi kufanya chochote nje ya Katiba ya Serikali Tatu kwa kuwa kinachofuata ni kuunda Katiba nyingine inayohusiana na Serikali tatu.
Waziri Chikawe afafanua
Juzi, Waziri Chikawe alitoa ufafanuzi juu ya utata wa hoja zake kwa kuipongeza Tume ya Jaji Warioba kwa kazi inayofanya huku akisema anaunga mkono msimamo wa CCM wa kutaka kuendelea na muundo wa Muungano wa Serikali mbili.


Alisema mchakato wa kuandika Katiba Mpya unapaswa kuangaliwa kwa jicho pana zaidi ya lile la Uchaguzi Mkuu wa 2015.

SUMAYE AONYA 'WAUZA UNGA' WASIJE WAKAONGOZA TANZANIA.


Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye amewatahadharisha Watanzania kuwa makini na watu wanaotaka madaraka kwa kugawa fedha katika sehemu mbalimbali za nchi au majimbo akionya wanaweza kujikuta wakimweka madarakani kiongozi anayejihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
“Hivi kama mtu anaweza kuhonga sehemu kubwa ya wapigakura katika jimbo la uchaguzi au hata katika nchi kama nafasi anayosaka ni urais; tumeshajiuliza hizo fedha nyingi hivyo anapata wapi? Kama anajihusisha na biashara hizo chafu akipata nafasi hiyo watoto wetu watapona?” alisema Sumaye jana na kuongeza:
“Haya ni maswali muhimu ya kujiuliza tunapoelekea mwaka kesho kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na mwaka 2015 wakati wa Uchaguzi Mkuu.”
Alisema hayo mjini Morogoro kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (Mviwata).
Akizungumza kwa tahadhari alisema haizungumzii Serikali yake iliyoko madarakani wala mtu yeyote, bali tabia mbaya, Sumaye alisema biashara ya dawa za kulevya inahusisha fedha nyingi na mitandao mipana ambayo isipodhibitiwa inaweza kulitumbukiza taifa katika janga.
Alisema Katiba Mpya siyo mwarobaini wa matatizo yanayolikabili taifa bali, utekelezaji na usimamizi wa sheria na kwamba jambo muhimu ni kuwa na Serikali itakayosimamia na kutekeleza sheria ili kulinda yale yaliyoelekezwa katika Katiba.
“Katiba haiwezi kumzuia mwizi kwenda kuiba na sheria haitamzuia mwizi kwenda kuiba ila itatamka adhabu ya kupewa huyo mwizi. Kwa hiyo ili vyote hivi viwe na maana ni lazima awepo mtu au chombo cha kumkamata huyo mwizi na kumfikisha katika mikono ya sheria na chombo hicho ni Serikali. Kama haiwezi kufanya hiyo kazi kwa ukamilifu tutaishia kulalamika tu na maonevu na maumivu yataendelea kuumiza jamii.”
“Kwa hiyo hata Katiba iwe nzuri namna gani na ikatamka kuwa rushwa ni adui wa haki na hata ikatoa adhabu kali sana kwa kosa hilo; kama tutaweka viongozi madarakani kwa rushwa, hiyo Katiba wala haitatusaidia. Hivyo Katiba nzuri mpya lazima iambatane na Serikali safi yenye kusimamia masilahi ya umma. Huwezi kumweka madarakani mwenyekiti wa kijiji au diwani au mbunge au hata Rais kwa rushwa ya kuwanunua wapigakura halafu utegemee Katiba Mpya itajibu matatizo ya jamii.”
Azungumzia Mviwata
Sumaye alisema Mtandao huo wa Wakulima Wadogo Tanzania ndiyo unaojua tatizo la kilimo na shida zao na ndiyo unaotakiwa kuulizwa cha kufanya ili kilimo chetu kibadilike na mkulima afaidike...
“Kama hatuwahusishi na kuwashirikisha katika sera, mipango na programu za kilimo, basi tujue kuwa sera, mipango na programu hizo zitashindwa.”
Alisema Tanzania ni nchi ambayo wananchi wake wengi wanategemea kilimo kwa maisha yao na uchumi wa taifa pia kwa kiasi kikubwa hutegemea sekta hiyo, lakini bado ni duni na hakijamkomboa mkulima mwenyewe wala uchumi wa taifa... “Nchi na watu wake bado ni maskini pamoja na kuwa watu wachapakazi wapo na ardhi kubwa na nzuri yenye rutuba ipo

CHADEMA YAWANG'ANG'ANIA MADIWANI WALIOTIMULIWA

http://www.bongocelebrity.com/wp-content/uploads/2012/12/Godbless-Lema-Arusha.jpgCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimefungua kesi ya madai, yenye gharama zaidi ya Sh. milioni 35.1 dhidi ya waliokuwa madiwani wake watano, waliofukuzwa jimbo la Arusha Mjini.
Madiwani hao ni Charles Mpanda (Kaloleni), John Bayo (Elerai), Estomih Mallah, (Kimandolu), Rehema Mohamedi (Viti Maalumu) na Reuben Ngowi (Themi).

Chadema wamefungua madai yao kupitia wakili wao, Method Kimomogolo na yanatarajiwa kutaj

wa kesho mbele ya msajili wa wilaya, Mahakama Kuu kanda ya Arusha, Wilbad Mashauri.
Kesi hiyo inatokana na hatua ya madiwani hao, kushindwa kuhudhuria kwenye kesi yao, walilofungua mahakama kuu kanda ya Arusha, mbele ya Jaji Kakusolo Sambo, wakiiomba ifanyie mapitio  uamuzi wa kulipa gharama za kesi, uliotolewa na aliyekuwa  hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya Arusha, Charles Magesa.

Hata hivyo, Jaji Sambo aliamua kesi hiyo kwa kufuta shauri hilo Aprili 02, mwaka huu, baada ya madiwani hao kutoonekana mahakamani hapo, bila taarifa mara mbili mfululizo na aliwataka kulipa gharama za usumbufu.

Novemba 22, 2012 Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha iliwaamuru madiwani hao waliotimuliwa Chadema kulipa zaidi ya Sh. milioni 15 na kila mmoja alitakiwa kulipa Sh. milioni 3.1 ndani ya miezi miwili, kama gharama za kesi waliyokuwa wamefungua, kupinga kufukuzwa uanachama, vinginevyo watapelekwa magereza.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Charles Magesa alitoa hukumu hiyo baada ya Chadema kushinda kesi hiyo na kuwaamuru kulipa Sh. milioni 15 ndani ya miezi miwili, wakishindwa watapelekwa gerezani.

Hata hivyo tayari wadaiwa hao walishalipa deni hilo, isipokuwa John Bayo, ambaye anadaiwa Sh. 507,000 na Mpanda anayedaiwa Sh. milioni 1.5 na tayari mahakama hiyo, ilishatoa hati ya kukamatwa kwao toka Februari 19, 2013.

Katika shauri hilo, Wakili Kimomogolo alisema kuwa, wateja wake (Chadema) walishawasilisha mahakamani hapo fedha kwa ajili ya kuwahudumia waliokuwa madiwani wakiwa gerezani.

Madiwani hao walitimuliwa Chadema baada ya kuingia muafaka wa kiti cha umeya wa Jiji la Arusha, bila kupata baraka za chama.  

CHANZO: NIPASHE

Wednesday, July 17, 2013

SIRI YAFICHUKA, SPIKA ANNE MAKINDA ATUHUMIWA KUONGOZA KUDHALILISHA WAANDISHI WA VYOMBO VYA HABARI.



Na Bryceson Mathias, Morogoro.
WANDISHI waandamizi wa Vyombo vya Habari nchini,Wamemshutumu moja kwa moja Spika wa Bunge, Anne Makinda, wakimtuhumu kuwa kuwa anaongoza kudhalilisha Utu wa Wandishi na Vyombo wa Habari.
Wakizungumza katika mahojiano ya Jicho letu ndani ya habari Julai 13, 2013 kujadili Rasimu ya Katiba, Mhariri wa Gazeti la Jamhuri Deodatus Balile alisema,
“Mimi Simung'unyi Maneno, Spika Makinda anaong
oza kwa kuvidhalilisha Vyombo vya habari na Utu wa Wandishi”.alisema Balile.
Upande wake, Allan Lawa, wa Baraza Habari Tanzania (MCT) alisema, Spika anafanya hivyo akijua fika kuwa aliwahi kuwa Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu akishugulikia Habari’
Walidai, wanamshangaa Makinda kudhalilisha Wandishi na Vyombo vya habari na kuwaita Wanahongwa na Wabunge ili wawaandike vizuri, lakini amesahau kuwa wakati wa Mchakato wa Ubunge wake na kinyang’anyiro cha U-Spika, vilimsaidia na hakusema vinahongwa!.
Mtangazaji Dotto Bulendu aliongoza majadiliano Startv-Mwanza na wageni Balile na Lawa, na Stumai Gerge alikuwa na Mhadhiri wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Dk. Ayub Rioba na Pili Mtambalike wa MCT,  
Rioba alisema, ziko Demokrasia za aina Mbili ya kuletwa ambayo katika utekelezaji wake huwa na maslahi kwa walioileta, na ile iliyoibuliwa na wananchi (created) utekelezaji wake una faida kwa wahusika, na kusema Rasimu haikuandika na Jaji Joseph Warioba pekee, ila wajumbe wote 30, akihofu vitu vilipitishwa Warioba akiwa hayupo .
Aidha, Pili Mtambalike (MCT), akihojiwa na Stumai alisema, kuna maeneo ya Rasimu katika Uhuru wa Habari lazima yapitiwa upya; ili tusirudi tena nyuma kwenye Sheria gandamizi kwa wandishi na ugumu wa kupata habari, “tunakwenda mbele haturudi nyuma”.alisema Mtambalike!
Mbali ya waandishi kusema ukikiandika Chama tawala mwandishi unaonekana Mchochezi na kupendelea Upinzani, na ukikiandika Chama pinzani unaonekana Mzalendo, Wachangiaji nchini pia walipigilia Msumari wakiwaunga Mkono wandishi wakidai, habari zao kamaa Waajiri zinapuuzwa, wanasia ambao ni waajiriwa ni kipaumbele kwa watawala.

CHADEMA YADAI KUNASA SIRI ZA CHAMA TAWALA.


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefanikiwa kunasa siri za mipango ya hujuma zilizokuwa zimeandaliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata nne za Jiji la Arusha, Tanzania Daima Jumatano limebaini.

Habari kutoka vyanzo mbalimbali vya kuaminika, zimebainisha kuwa CHADEMA katika uchaguzi huo kilifanikiwa kushinda kata hizo baada ya kuvunja ngome ya CCM iliyok
uwa ikiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba.

Kwa mujibu wa habari hizo, mipango karibu yote iliyokuwa ikifanywa na CCM, ikiwemo halali na haramu, ilivuja na kufika mikononi mwa wapinzani wao ndani ya muda mfupi hata kabla ya utekelezaji.

Imedaiwa kwamba baadhi ya watu waliokuwa katika kambi ya CCM, waliamua kwa siri kufichua mipango hiyo na kuifikisha kwa mahasimu wao kutokana na kile kilichodaiwa kuchoshwa kushiriki katika mambo ya kidhalimu.

Habari zinasema maofisa kadhaa wa CCM ambao wamekuwa wakiratibu na kusimamia mipango karibu yote miovu dhidi ya wapinzani, waliamua kwenda kinyume na makubaliano hayo, na kwa njia ya siri wakafanikiwa kutoa mpango mzima hadharani.

Mmoja wa maofisa wa CHADEMA ambaye awali alikana taarifa hizo, kabla ya kukiri baada ya kubanwa, amedai zilifikishwa kwao na watu wenye mapenzi mema na nchi.

“Hata nasi awali tulishangaa, lakini tulilazimika kuziamini baada ya kuzifanyia kazi na kubaini kwamba zilikuwa za kweli.

“Kwa mfano taarifa za kuwepo kwa mipango ya kutumbukiza kura bandia, kununua shahada za kupigia kura ilivuja mapema nasi tukaamua kuweka mitego kila mahali tulipoambiwa, kiasi cha kuwafanya washindwe kutimiza lengo lao,” alisema ofisa huyo.

Habari zimezidi kufichua kuwa, kambi hiyo ya CCM ilianza kuyeyuka mapema mchana wa Jumapili, siku ambayo ilikuwa ya uchaguzi, baada ya kuhisi kuwa mambo yao yamekwama kutokana na viongozi na vijana wao kuonekana katika maeneo yote muhimu yaliyokuwa yamepangwa na chama hicho tawala kuendesha hujuma zake.

Chanzo kimoja cha habari cha kuaminika kimeliambia Tanzania Daima kuwa ‘usaliti’ huo wa baadhi ya watendaji wa chama hicho tawala umetokana na kutopendezwa na mtindo wa utendaji kazi za kisiasa unavyoendeshwa na Mwigulu na baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho tawala.

“Wameanza kuchoshwa na siasa za majitaka ambazo zimezidi kulichafua taifa na kuangamiza maisha ya watu.

“Ni kweli tunataka ushindi, lakini wengi hawataki utokane na kuumiza watu ambao wana haki ya kuunga mkono na kufuata chama wanachotaka,” kimesema chanzo hicho, ambacho kimeomba jina lake lisitajwe kutokana na sababu za kiusalama.

Mbali na sababu hizo, taarifa zimebainisha kuwa sababu nyingine zilizowafikisha baadhi ya watendaji wa CCM kusaliti, ni kasi ya CHADEMA kuungwa mkono na wananchi, pamoja na vitisho, na vitendo vingi vya ukatili ambavyo viongozi na wanachama wa chama hicho pinzani wamekumbana navyo.

Hadi sasa, viongozi wakuu wote wa CHADEMA wameonja adha ya polisi kwa kukamatwa, wengine kupigwa na hata kufikishwa mahakamani kwa tuhuma mbalimbali.

“Tunao wanachama waaminifu ambao wamo ndani ya CCM na wamekuwa sehemu muhimu ya intelijensia ya chama chetu,” alitoboa mmoja wa maofisa wa CHADEMA.

Katika uchaguzi huo mdogo wa udiwani katika kata nne za Jimbo la Arusha ambao ulifanyika Jumapili CHADEMA iliweza kushinda kata zote.

Awali uchaguzi huo uliahirishwa mwezi uliopita kutokana na mlipuko wa bomu katika mkutano wa kampeni za CHADEMA uliosababisha vifo vya watu wanne na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa. 
CHANZO TANZANIA DAIMA.