Pages

Pages

Sunday, August 25, 2013

WALAU WAZIRI WA UCHUKUZI DK HARRISON MWAKYEMBE AMETHUBUTU KWA KUUFURAHISHA UMMA WA WATANZANIA KWA KUPIGA TANZANIA KUWA UCHOCHORO WA MADAWA YA KULEVYA NCHINI.


NIMEWAHI kuandika hivi karibuni kuhusu uzembe uliopo serikalini katika udhibiti dawa za kulevya. Nilieleza kwa kina jinsi nchi yetu ilivyotumbukia kwenye lindi la uchafu wa dawa hizo.
Leo nchi yetu imekuwa uchochoro wa wauzaunga, vijana wamejiajiri kwenye biashara haramu ya kusafir
isha dawa hizo! Imefika mahali sasa Mtanzania akisafiri nje ya nchi anakaguliwa mara mbili tatu, yaani hatuaminiki tena. Aibu gani hii ?.
Vyombo vya dola vimebaki na visingizio vilevile kila siku, eti hii ni biashara ya kimataifa. Wenye biashara ni vigogo, mara wana fedha nyingi na visingizio kibao.
Visingizio hivyo hivyo utavisikia kwenye ujangili wa meno ya tembo, eti ni vigogo wenye fedha nyingi. Utamsikia waziri mzima anajipiga kifua bila hata aibu, eti ninayo majina yao, lakini hata siku moja hayataji.
Lakini wiki iliyopita, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe aliufurahisha umma wa Watanzania kwa ujasiri wake wa kutaja majina ya wafanyakazi saba wa serikali aliodai kuwa walihusika katika kupitisha mabegi tisa ya dawa za kulevya yenye uzito wa kilo 180 katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, kwa kuwa siku hiyo walikuwa zamu, na hivyo walitakiwa kubaini mzigo huo.
Huu ndiyo ujasiri unaotakiwa. 

Kama kweli tumeamua kupambana na dawa hizo, basi kila kiongozi aige mfano wa Dk Mwakyembe.
Hata hivyo, kilichofanywa na Dk Mwakyembe ni kama tone tu ndani ya maji ya bahari. Ilitakiwa Serikali nzima ionyeshe msimamo kama huo.
Mwakyembe yeye amegusia upitishaji wa dawa kwenye viwanja vya ndege, lakini dawa hizo pia hupitia baharini na nchi kavu. Bado hatujawa na nia ya dhati ya kupambana nazo.
Ni kweli kwamba biashara hii ni ya mitandao ya kimataifa, lakini walau tunaweza kupambana ili kuiepusha nchi yetu na balaa au aibu hii.
Mfano aliouonyesha Dk Mwakyembe siyo kwenye dawa tu za kulevya tu, bali hata katika utendaji wake. Tumeshuhudia mambo kadhaa ya mafanikio katika wizara yake, kwa mfano kuongezeka kwa mapato bandarini, unazishwaji wa treni ya abiria na mengineyo mengi.
Uthubutu huu ndiyo unatakiwa kwa mawaziri wote katika Serikali hii. Maendeleo yanataka uthubutu wa hali ya juu. Tatizo mawaziri wengi hawana uthubutu huo, wengine wanatafuta masilahi yao, wengine ni uzembe tu umetawala.
Hata hivyo, inatia moyo kuona mawaziri wanaothubutu kama Dk Mwakyembe. Tunahitaji mawaziri na watendaji wote wa serikali wenye ujasiri kama huo.
chanzo, jumamtanda

YANGA SPORT CLUB YAANZA LIGI KUU YA VODACOM KWA VITISHO, YAITANDIKA ASHANTI UNITED KWA BAO 5-1 UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM


MABINGWA Yanga, jana walianza safari ya kutetea taji lao kwa kishindo baada ya kuionea Ashanti United kwa ‘kuisigina’ na kipigo cha mabao 5-1, huku mahasimu wao, Simba wakipelekwa puta na vijana wapya Ligi Kuu, Rhino Rangers na kuponea chupuchupu kwa kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 mjini Tabora. 


Katika mechi ya Yanga iliyopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Vijana wa Jangwani walitawala mchezo tangu mwanzo mpaka mwisho, huku Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora Rangers wakilazimika kukomboa mabao baada ya kutangulia kufungwa mara mbili.
 
Iliwachukua Yanga dakika 10 tu tangu kuanza mchezo kufunga bao la kwanza lililowekwa kimiani na Jerryson Tegete aliyemalizia kwenye kamba pasi nzuri ya Simon Msuva na kumtungua kipa wa Ashanti, Ibrahim Abdallah.
 
Hussen Sued kuzuiwa na Tegete kabla ya kuvuka mstari huku tayari Kipa Ally Mustapha akiwa ameshapitwa na mpira.
 
Ashanti walikuwa na nafasi nyingine ya kusawazisha dakika ya 24 kufuatia shuti kali la Sued kumlazimisha Mustapha kufanya kazi ya ziada kulipangua na kuwa kona.
 
Dakika tatu baada ya kuanza kipindi cha pili, Msuva aliipeleka Yanga mbele na kufanya matokeo kuwa 2-0, kabla ya Tegete kufunga bao la tatu dakika ya 57, na kisha Haruna Niyonzima kufanya matokeo kuwa 4-0 dakika ya 73.
 
Ashanti walifunga bao la kufutia machozi dakika ya 90 kupitia kwa Shaaban Juma, kabla ya Nizar Khalfan kufunga nao la tano.
Akijitetea na kipigo hicho, Kocha wa Ashanti Hassan Banyai alisema kikosi chake kinahitaji muda zaidi.
 
Tabora:
Mjini Tabora, Simba wakishangiliwa na umati mkubwa, walibanwa vilivyo na wageni wa Ligi Kuu, Rhino Rangers na kulazimisha sare ya mabao 2-2 kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
 
Katika mechi hiyo iliyochelewa kuanza kufuatia utata wa vibali vya wachezaji, Joseph Owino, Abel Dhaira na kukosekana kwa leseni ya Betram Mwombeki, timu zote zilishambuliana kwa zamu.
 
Iliwachukua Msimbazi dakika 8 tangu kupulizwa filimbi ya kuanza mchezo kufunga la kwanza kupitia Jonas Mkude aliyeunganisha kwenye kamba kwa kichwa kona maridadi ya Issa ‘Baba Ubaya’ Rashid.
 
Wenyeji Rangers walisawazisha bao hilo dakika ya 35 kupitia Iman Noel.
 
aliyepiga mpira wa adhabu ndogo na kwenda moja kwa moja wavuni, kabla ya dakika moja baadaye Simba kuongeza bao la pili likifungwa na Mkude kwa kiki ya penalti.
 
Penalti hiyo ilitokana na kiungo Amri Kiemba kuchezewa faulo ndani ya eneo la hatari na beki wa Rangers, Daniel Manyenya, aliyeishia pia kuonyesha kadi ya njano kwa kosa hilo.
 
Sekunde chache kabla ya mapumziko, Rangers walifunga bao la kusawazisha, ambalo lilikataliwa na Mwamuzi Amos Paul kutoka Mara kwa madai kuwa kabla ya bao hilo, kipa wa Simba alifanyiwa madhambi.
 
Kipa wa Rangers, Abdul Mtumwa alifanya kazi kubwa kuokoa mpira wa kichwa kutoka kwa Joseph Owino kufuatia kona iliyochongwa na Baba Ubaya dakika ya 20.
 
Kipindi cha pili, Rangers walibadilika na kufanya mashambulizi makali na kufunga bao la kusawazisha dakika ya 70 kupitia Stanslaus Mwaktos aliyefunga kwa kiki ya adhabu ndogo iliyomponyoka kipa wa Simba.
MWANANCHI

ZUIO LA KUTAKA ISIUZWE NYUMBA YA ALIYEKUWA MKURUGRNZI WA UTUMISHI WA BENKI KUU (BoT) AMATUS LIYUMBA LAKWAMA.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEimck5I-_vQ4Lwe-pCXpvt3KHwU-ccLuOgWZGn4bD_8sJRH3NF-J49iKOIa0Dufe2lWPu62SxJlgxtMgbZHgYQCF74pTVBuTxZhz-FlplzhXPfYL0nMKUS7q4ca70H8zEumnsMbAFl7MLK1/s1600/Lyumba.jpg 
MAHAKAMA ya Wilaya ya Kinondoni imetupilia mbali pingamizi la mke wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi wa Benki Kuu (BoT), Amatus Liyumba, Aurelia Ngowi la kupinga mumewe kuuza mali za familia na kumfukuza kwenye nyumba wanayoishi.

Kesi hiyo imefunguliwa mbele ya Hakimu Jackline Rugemalila katika mahakama hiyo, Dar es Salaam. Mahakama hiyo ilihamia Mbezi Africana iliko nyumba hiyo kufan

ya ukaguzi ili kujiridhisha juu ya pingamizi zilizotolewa na pande zote mbili.
 
Ngowi alipinga mumewe kuuza mali za familia na kumfukuza, wakati kesi ya msingi ya madai ya talaka ikiendelea, jambo ambalo Liyumba akiongozwa na Wakili wake, Sweetbert Nkuba alikuwa akilipinga, kwa kudai nyumba hiyo ni ya biashara na si ya kuishi familia, kama inavyodaiwa.

 
“Baada ya kusikiliza pande zote mbili, mahakama hii imeona kuwa nyumba hiyo ni ya biashara na si ya kuishi familia, kama ilivyoelezwa katika zuio la mshitaki,” alisema Hakimu Rugemalila.

 
Katika hati ya madai, Aurelia anaiomba mahakama iweke zuio la muda ili Liyumba asiuze mali za familia, pia asiuze nyumba iliyopo Africana Mbezi Beach katika kiwanja namba 2232/2233, ambayo walikuwa wanaitumia kama makazi ya familia.

 
Anaiomba mahakama iamuru waendelee kuishi katika nyumba hiyo, wakati shauri hilo la likiendelea, pia alipe gharama za uendeshaji wa kesi.


Katika hati ya kiapo, inayounga mkono madai yake, Aurelia anadai alifunga ndoa na Liyumba mwaka 1978 mkoani Kilimanjaro na kupata watoto wanne.

 
Anadai mwaka 1980 walianza kuishi kwenye nyumba iliyopo Africana. Anadai waliendelea kuishi katika nyumba hiyo na baadaye waliamua upande wa nyumba, waweke hoteli inayoitwa Amjen Executive pamoja na biashara nyingine, zilizokuwa zinawaingizia kipato kwa ajili ya kutimiza mahitaji ya familia.

 
Kwa mujibu wa hati ya kiapo, baada ya Liyumba kutoka gerezani ambako alikuwa anatumikia kifungo, alihama nyumbani na kuanza kuuza mali mbalimbali yakiwemo magari, kiwanja cha ekari 50 kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani na kiwanja cha Tabata.

 
Alidai kuwa Julai 18 mwaka huu, Liyumba aliwafukuza yeye na watoto wake na kufunga nyumba hiyo pamoja na eneo la biashara, waliyokuwa wakiitegemea kwa ajili ya kupata fedha za matumizi ya kila siku, kisha akaweka walinzi ambao wanawazuia kuingia.

 
Aurelia alidai baada ya kufanya uchunguzi, aligundua kuwa mume wake anauza mali walizochuma pamoja. Alidai endapo mahakama haitaweka zuio, atapata hasara kubwa. Liyumba alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela, baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma.

 
Alimaliza kutumikia kifungo hicho Septemba 23 mwaka juzi. Kesi ya msingi ya madai ya talaka, itatajwa tena Septemba 16, mwaka huu.
chanzo jumamtanda blog.
 

madhabahu ya kanisa la KKKT usharika wa Segerea lachomwa moto jijini Dar

kanisa_3b018.jpg
Mchungaji Usharika wa Segerea wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Noah Kipingu akionyesha sehemu ya madhabahu ya kanisa hilo, iliyoungua moto baada ya kurushiwa vitu vinayosadikiwa kuwa ni mabomu ya petroli na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana.Picha na Salim Shao.


Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Jimbo la Kati, Usharika wa Segerea Wilaya ya Ilala, limechomwa moto na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana.

Tukio hilo lilitokea saa saba usiku, wakati waumini wa kanisa hilo wakiwa katika mkes
ha wa maombi ya maandalizi ya mkutano wa injili unaoanza leo.

Mchungaji wa kanisa hilo, Noah Kipingu alisema wakati wakiwa katika maombi ghafla walisikia sauti ya kitu kilichorushwa kutoka nje ya kanisa kikiambatana na moto, ambapo kilianguka madhabahuni na kuanza kuunguza baadhi ya vifaa vya kanisa.

"Tukiwa tumesimama mbele ya madhabahu kwa njia ya mduara ndipo nyuma ya madhabahu ukatokea mlipuko mkubwa kwa sauti ya kishindo, na moto ukatanda madhabahu," alisema Kipingu na kuongeza kuwa.

"Katika namna ya kibinadamu hakuna aliyeweza kuvumilia, kila mtu alikimbia akitafuta namna ya kujiokoa."



Kipingu alisema kuwa alipobaini kuwa ulikuwa ni moto wa mafuta aliwaambia waumini wake waingie ndani kwa ajili ya kuuzima, wakati wakiuzima moto huo walipata taarifa kuwa gari la Mchungaji, Toyota Cresta lenye namba za usajili T 482BAF lililokuwa nje ya kanisa lilikuwa likiwaka moto. 

"Baadhi ya waumini waliokuwa ndani walikwenda nje kushirikiana na mlinzi kuuzima moto huo, tunamshukuru Mungu kwamba matukio yote mawili tumeyashinda kwa uwezo wake," alisema.

Kipingu alisema kuwa shambulizi hilo lilizua taharuki kubwa kwa waumini wake, na kwamba baadhi ya watu waliwaona watu wanne wakikimbia kutoka eneo la kanisa baada ya kutukio hilo.

Shukuru Thobias mmoja wa waumini waliokuwepo kanisani wakati tukio hilo likitokea, anasema aliona vitu kama mshale vikianguka madhabahuni na vilipodondoka vililipuka kama moto.

"Moto ulianza kuunguza Biblia na makapeti, ndipo tukaanza kukimbia kwenda nje kuchukua mchanga na kuanza kuuzima. 

Baada ya hapo tulianza kukimbia huku wengine wakidondoka na kujeruhiwa kidogo miguuni. Niliporudi baadaye niligundua zilikuwa ni chupa tatu za bia zilizokuwa zimetengenezwa bomu la petroli," alisema Thobias.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo hakuna mtu aliyepoteza maisha na kulitaja kuwa ni jaribio la kiharifu lililoshindwa.

"Hakuna mtu aliyepoteza maisha, lilikuwa jaribio ambalo halikufanikiwa. Wakati tukio linatokea waumini walikuwa kanisani kwa hiyo waliwahi kuuzima moto kabla haujaleta madhara," alisema Kova.

Matukio ya makanisa kuchomwa moto

Mei 26, 2012, Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) lililopo Mtaa wa Kariakoo mjini Unguja, lilichomwa moto usiku na watu wasiofahamika.

Monday, August 19, 2013

HIVI NDIVYO MAJAMBAZI WATATU WALIVYONASWA WAKIKIMBIA BAADA YA KUIBA FEDHA JIJINI DAR ES SALAAM.

MAJAMBAZI HAO WAKIWA NDANI YA GARI LA POLISI BAADA YA KUIBA KIASI CHA FEDHA KATIKA KITUO CHA MAFUTA ENEO LA MALAPA HATIMAYE KUNASHWA KWENYE MAKUTANO YA BARABARA ZA MANDELA NA NYERERE DAR.

MMOJA WA WATU WANAOSADIKIWA KUWA NI JAMBAZI AKIWA CHINI YA ULINZI KANDO YA BARABARA YA MANDELA AKIPILEKWA KUUNGANISHWA WENZAKE KWENYE GARI KUPELEKWA KITUO CHA POLISI BUGURUNI DAR ES SALAAM LEO.

MAJAMBAZI WAWILI WAKIWA NYANGANYANGA BAADA YA KUPATA KICHAPO CHA MBWA MWIZI KUTOKA KWA POLISI.

ASKARI WENYE PIKIPIKI WAKIONDOKA ENEO LA TUKIO BAADA YA KUFANIKIWA KUWANASWA MAJAMBAZI HAO.
MOJA YA PIKIPIKI AINA YA BAJAJ INAYOSADIKIWA PIA KUIBWA NA MAJAMBAZI HAO IKIWA IMEPAKIWA KWENYE GARI LA POLISI, PIA MSAFARA UKISINDIKIZWA NA TRAFIKI MWENYE PIKIPIKI KUELEKEA KITUO CHA POLISI CHA BUGURUNI. chanzo, jummtanda blog  



WAZIRI WA UCHUKUZI ASHINDWA KUWATAJA VIGOGO WANAOHUSIKA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA NCHINI.

Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe.
 
WAZIRI wa Uchukuzi Dk. Harisson Mwakyembe jana alishindwa kuwataja vigogo wanaohusika na biashara ya dawa za kulevya nchini na badala yake akawataja watu waliofanikisha kupita kwa bidhaa hiyo haramu iliyokamatwa hivi karibuni nchini Afrika Kusini.
 
Waziri huyo pia alisimulia bidhaa hiyo ilivyopitishwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa waJulius Nyerere (JNIA), uliopo jijini Dar es Salaam na kukamatwa Afrika Kusini ikidaiwa kusafirishwa na wasanii wa hapa nchini.
 
Wengi wa watu waliotajwa kuwasaidia wauza ‘unga’ na wasafirishaji ambao hadi sasa hawajulikani, ni wafanyakazi wa uwanja huo katika idara mbalimbali.
 
Wafanyakazi wa uwanja huo waliotajwa kusaidia usafirishaji wa dawa walizokamatwa nazo Watanzania wawili Agnes Gerald “Masogange” na Melisa Edward nchini Afrika Kusini ni Koplo Ernest wa Jeshi la Polisi Tanzania, Zahoro Mohamed Seleman ambaye ni mbeba mizigo uwanjani hapo, Yusuph Daniel Issa, Jackson Manyonyi, Juliana Thadei na Mohamed Kalungwa ambao ni maofisa wa usalama wa uwanja huo.
 
Hatua ya Dk. Mwakyembe kutangaza kuwataja hadharani vigogo wa dawa za kulevya ilisubiriwa kwa kiasi kikubwa na wananchi ambapo jana waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliingia katika Wizara ya Uchukuzi kuanzia saa 7:30 mchana hadi saa 8:40 wakati waziri huyo alipoingia na kutoa taarifa yake kwa umma.

Dk. Mwakyembe alisema baada ya serikali kupata taarifa ya kukamatwa kwa Watanzania Julai 5 mwaka huu katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo nchini Afrika Kusini na kubaini wahusika walianzia safari jijini Dar es Salaam, waliamua kupitia mfumo mzima wa kamera za uwanja wa ndege wa JNIA (CCTV) na kubaini matukio yaliyohusika moja kwa moja na usafirishaji wa dawa hizo.
 
Alisema waliangalia mfumo wa kamera kuanzia saa 9:25 hadi 10:30 alfajiri ya Julai 5 na kubaini namna mkakati huo ulivyofanikishwa.
 
“Saa 9:28 alfajiri kamera zinamuonyesha kijana mbeba mizigo kwa jina la Zahoro akiwa anazunguka zunguka eneo la kuingia abiria mithili ya mtu mwenye miadi fulani, na kisha eneo jingine alionekana Issa akitoka nje ya jengo na kuingia tena huku akiongea na simu na hili haliruhusiwi,” alisema Mwakyembe.
 
Aliongeza kuwa wakati kamera zikimuonyesha Issa, pia alionekana Koplo Ernest akiranda randa eneo la uhakiki wa hati za kusafiria akiwa na dalili za kusubiri kitu na ilipofika saa 10:15 alfajiri waliingia watu watatu.
 
Aliwataja watu hao ni Agnes Masogange, Melisa Edward na Nasoro Mangunga wakiwa na mabegi tisa ambapo katika eneo hilo anaonekana tena Koplo Ernest akiwasaidia abiria kupanga mizigo na wakati huo huo mbeba mizigo Zahoro akisaidia kuweka vizuri mizigo ya kina Masogange na wenzake kabla ya kuizungushia karatasi za nailoni.
 
“Huu mtandao ni mkubwa na unahitaji uadilifu kwani baada ya shughuli hiyo tulimuona Yusuph akimuondoa mfanyakazi mwenzake yule Manyonyi na kukalia kiti cha mkaguzi wa mizigo na hili lilifanyika kwa dakika sita. Baada ya kufanikisha kazi hiyo akamwachia mwenzake jukumu alilokuwa nalo,” aliongeza Dk. Mwakyembe.
 
Alisema jambo jingine walilobaini ni kucheleweshwa kwa mbwa wa ukaguzi wakati mizigo hiyo ikipitishwa na kwamba ukaguzi wa kutumia mbwa ulifanyika wakati mabegi yenye dawa hizo yalipoingizwa katika sanduku la chuma na mbwa kunusa sanduku badala ya mabegi.
 
Aliongeza kuwa mkakati mwingine uliofanikisha hatua hiyo ni kwa Mangunga kuruhusiwa kusafiri siku hiyo hiyo licha ya kutokuwa na tiketi, na kwamba alilipa dola 60 kufanikisha safari yake ya dharura.
 
Uamuzi wa wizara
Kutokana na hali hiyo Dk. Mwakyembe alisema serikali imeiagiza Mamlaka ya Uwanja wa Ndege (TAA) kuwapiga picha watu wote watakaokamatwa na dawa za kulevya na kusambazwa katika vyombo vya habari, kampuni iliyomuajiri Nasoro imfukuze kazi mtumishi wake huyo na asikanyage uwanja wa ndege wa JNIA.
 
Waziri huyo pia alilitaka Jeshi la Polisi limkamate Zahoro na kumuunganisha na wenzake kujibu mashitaka ya jinai chini ya sheria ya kuzuia dawa za kulevya sura ya 95 ya mwaka 1996.
 
Dk. Mwakyembe aliitaka TAA kuwafukuza kazi wafanyakazi wake wanne ambao ni maofisa wa ulinzi uwanjani hapo na kisha wakamatwe na kufunguliwa mashitaka, huku Jeshi la Polisi likitakiwa kumchukulia hatua za kinidhamu Koplo Ernest.
 
Mbali na hatua hizo, pia Dk. Mwakyembe alisema serikali inaiagiza Idara ya Usalama wa Taifa kuendesha uchunguzi wa kina kwa maofisa wake waliokuwa zamu Julai 5 mwaka huu, kwa kuchelewa kuwafikisha mbwa wa kubaini dawa hizo katika muda muafaka wa kukagua mizigo.
 
Wakati Dk. Mwakyembe akielezea hali hiyo kwa Tanzania, taarifa zilizopatikana na gazeti hili zinabainisha kuwa nchini Afrika Kusini mtandao huo ulijipanga kufanikisha upitishaji wa dawa hizo aina ya Cyrsatl Methamphetamine au “TIK” pasipo kubughudhiwa.
 
Taarifa zinaeleza baada ya Masogange na wenzake kufanikiwa kupita katika maeneo ya ukaguzi ya uwanja wa Oliver Tambo, Mangunga alifanikiwa kuondoka uwanjani hapo na mabegi matatu yenye jumla ya kilo 60 bila kujulikana.
 
“Masogange kilichomponza ni pale alivyokuwa anajiremba baada ya kuruhusiwa kupita katika vizuizi vyote. Kiuhakika hakukamatwa katika mashine bali ilikuwa ni ukaguzi usio rasmi uliofanywa na polisi. 
 
Nadhani huyu askari aliyewashika hakujua mpango huo,” kilisema chanzo chetu ndani ya Jeshi la Polisi. http://j2wisdom.blogspot.com

DPP AMTETEA WAZIRI MKUU



MKURUGENZI wa Mashitaka (DPP), Eliezer Feleshi, amesema haoni mantiki yoyote au uhalali wa Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), kumshitaki Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Alisema hayo janai wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari, baada ya kufungwa kwa mkutano wa siku tatu wa mawakili wa Serikali wafawidhi, wakuu wa upelelezi wa mikoa na vikosi vingine vya Polisi Alisema kauli aliyotoa Pinda bungeni, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu kuhusu Polisi kutumia nguvu kwa wananchi, ililenga wanaokaidi kukamatwa na kufikishwa mbele ya sheria na si kupiga na kuua kama ilivyotafsiriwa na wengi.
 
“Sijapata taarifa kwa maandishi juu ya azma ya kumshitaki Waziri Mkuu, lakini Pinda hajavunja sheria kwa kauli yake aliyotoa,” alisema.

Alisema kwa jinsi alivyosikia maelezo ya Waziri Mkuu bungeni, kama LHRC wanamshitaki kwa jinai Waziri Mkuu, haoni uhalali wa mashitaka hayo. 

Usahihi wa Pinda Alisema Waziri Mkuu alieleza hatua zinazochukuliwa dhidi ya mvunja sheria, na kufafanua kuwa Mtanzania yeyote ana haki kwa mujibu wa sheria, lakini pia ana wajibu, ndiyo maana vipo vyombo na kila chombo kimepewa mamlaka na wajibu wa kutekeleza.

Alifafanua, kwamba kilichoongelewa ni dhana ya mkusanyiko ambayo ni haki kwa mujibu wa Katiba, ikiwemo uhuru wa kukutana, kutoa mawazo na kufanya mawasiliano.

Hata hivyo, alikumbusha kuwa Sheria ya Jeshi la Polisi, inasema ili mkusanyiko ufanyike, lazima taarifa itolewe kwa kiongozi wa Polisi wa eneo husika.

 
Sheria hiyo inasema, kama mkusanyiko una nia ya kutenda kosa na ikafanyika hivyo, kuna chombo kilichopewa dhamana ya kuhakikisha mkusanyiko haramu unatawanyika na sheria hiyo inaruhusu Polisi kutawanya mkusanyiko haramu.

“Unatarajia nini kama kuna watu wanafanya fujo na polisi wana mamlaka ya kuwakamata waliofanya fujo?” Alihoji Feleshi na kuongeza kuwa dhana ya matumizi ya nguvu ni ya kisheria pia.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, akizungumza kwa simu na gazeti hili, alisema utaratibu wa Polisi kulazimika kutumia nguvu upo. Aliutaja utaratibu huo kwamba unatumika hasa katika mikusanyiko isiyotakiwa, ambapo Polisi hulazimika kutoa tangazo la angalizo mara kadhaa kutaka watu watawanyike.


“Tangazo linapotolewa, Polisi kwa kutumia kipaza sauti husema, tawanyikeni, tawanyikeni na kusisitiza hivyo mara kadhaa, hapo wanaopaswa kutawanyika wakikaidi, nguvu hutumika ingawa inaweza isiwe ya kupiga risasi, pengine virungu, yote hiyo si kupiga?


“Risasi ni kitu cha mwisho, labda uwe unashambuliwa wewe (polisi), hata ikiwa hivyo, ukipiga risasi kuna maeneo ya kupiga, si kichwani, polisi wana mafunzo ya kupiga maeneo ya miguuni, hivyo kutumia nguvu kwa polisi kupo,” alisema Jaji Werema.