Pages

Pages

Thursday, October 31, 2013

MWILI WA MWANAMKE ALIYEUAWA NA ASKARI WA TARANGIRE BADO UNAENDELEA KUSOTA MOCHWAR




NA mwandishi wetu,
Maiti ya mwanamke Emeliana Kibuga(42) mkazi wa kijiji cha Kash Babati vijijini anaedaiwa kuuawa na askari wa hifadhi ya Tarangire octoba 16 inaendelea kusota katika chumba cha maiti katika hospitali ya wilaya ya Babati.
Hali hii imaetokana na ndugu kususia mwili huo kwa madai kuwa polisi wanawakinga wauaji wa ndugu yao huku wakishindwa kutoa taarifa sahihi juu ya mauaji hayo ambapo wamedai kuwa hawatauzika mwili huo ambapo kama hawatapokea taarifa hiyo basi wataupeleka mwili huo kwa mkuu wa mkoa ukakae hapo hadi kupata taarifa za mauaji ya ndugu yao.
Kwa mujibu wa ndugu wa marehem ambae ni mwenyekiti wa mtaa wa Unjej bwana Rashid Kijogoo alisema kuwa mume wa marehem alitekwa na askari wa hifadhi hiyo ya Tarangire octaba 14 saa nane za usiku nyumbani kwake kijijini hapo Kash na kumwacha mkewe lakini pia octaba 16  mkewe ambae kwa sasa ni marehem nae alitekwa na askari hao hao na kupelekwa kusikojulikana.
Alisema kuwa askari hao 6 wakiwemo wanawake wawili walifika katika kitongoji hicho na kumchukua marehem nyumbani kwake majira ya saa nne asubuhi kwa madai ya kwenda kufanya mahojiano nae na kumrudisha majira ya jioni huku akiwa chini ya ulinzi mkali wa askari hao wakiwa na  silaha za moto ambapo pia mwanamke huyo alionekana akivuja dam sehemu mbalimba;li za mwili wake.
Alisema kuwa baaada ya kufika nyumbani hapo askari hao walionekana kumhoji jambo marehem na kuondoka nae kwa mara nyingine ambapo kwa mara hii marehem hakuonekana tena hadi octoba 17 mwili wake ulipookotwa katika pori la hifadhi ya Tarangire huku akiwa amengolewa meno, na kutobolewa macho pamoja na kuvunjwa shingo.
Kijogoo alisema kuwa mwili huo unaodaiwa kuokotwa na askari wa hifadhi ya Tarangire ulipelekwa katika hospitali ya Wilaya, Mrara.
Kwa upande wake mtoto wa marehem aliyejulikana kama Christina Elias Kibuga alisema kuwa octoba 16 majira ya saa kumi jioni walikuja Watu sita wakiwemo wanawawe wawili waliovalia kiraia na wanaume wane, mmoja akiwa amevalia sare za jeshi la wananchi Tanzania (JWZT) ambapo walikuja na mama yao huku wakimhoji kwa ukali,
“Ilikuwa ni saa kumi jioni ikiwa ni siku mbili tangu baba atekwe usiku na siku hiyo nae mama alitekwa asubuhi na kurudishwa jioni na askari hao sita, mmoja akivalia nguo za jeshi walimleta mama yetu huku akiwa anavuja dam sehem nyingi na kumgombeza kuwa wawaonyeshe kitu alichosema kiko nyumbani, mama yetu alinyamaza tu ndipo walipomwambia tena kuwa kumbe hutaki bali umetusumbua bure kuja hadi huku, sasa leo utatutambua, wakaondoka nae tena hadi leo hatujamuona tena bali tunasikia kuwa ameuawa” alisema mtoto huyo huku akibubujikwa na machozi mfululizo.
Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Akili mpwapwa alipohojiwa juu ya tukio hilo la mauaji, alikiri kuuawa kwa mwanamke huyo na kukanushwa kuuawa na askari hao kwa madai kuwa mwanamke huyo alikufa kwa mshutuko wa kuhojiwa.
Hata hivyo jambo hili limepingwa vikali na ndugu pamoja na majirani wa marehem huyo kwa madai kuwa mwili huo ulikutwa ukiwa na majereha mwili mzima iikiwemo kutobolewa macho, kuvunjwa shingo na meno kuonyesha kipigo kikali juu ya ndugu yao pia sehem za siri kuchubuka ambayo ni dhahiri ndugu yao alibakwa.
Nae Daktari wa hospitali ya wilaya ya Babati, Dr. Palagyo alithibitisha marehemu huyo kutobolewa macho, kuvunjwa shingo pamoja na meno sambamba na kuvuja dam sehem za siri hali iliyopelekea kifo chake.
Utekaji huo uliosababisha mauaji ya mwanamke huyo unafuatiwa na operesheni maalum ya kusaka majangili wanaojihusisha na uwindaji haramu wa meno ya tembo katika hifadhi mbalimbali za Taifa unaoendelea hapa nchini.



TANZANIA KUTOA TARAKA KWA NCHI ZA RWANDA, KENYA NA UGANDA.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjJ26H5Kj6oZ0nPm_s5cQBGSv2AwS9ZVW__gTfeQoBMIf496Apw4TwrFtPD83H9k75wAF4WKXYCcaWlzy6Nxj2D0OMQp49Ujx87X2f9fUK9duUuY9hXKKmzqW0C6ZIiwWtGOl8INzcoHkTw/s400/Samwel_Sitta.jpgWAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema Tanzania itatoa talaka kwa nchi za Rwanda, Kenya na Uganda ambazo zimeamua kuanzisha Jumuiya ya hiari nje ya Jumuiya ya Afrik
a Mashariki.


Sitta alisema kutokana na nchi hizo kuonekana kuitenga Tanzania na Burundi ambazo ni wanachama wa jumuiya hiyo, wameshaanza mazungumzo ya kushirikiana kiuchumi, kisiasa na nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo (DRC).


Kauli hiyo ya Sitta inatokana na mikutano ya mara kwa mara inayofanywa na marais Uhuru Kenyata wa Kenya, Paul Kagame (Rwanda) na Yoweri Museveni (Uganda) kuzungumzia masuala mbalimbali ya kushirikiana nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.


Waziri Sitta alibainisha msimamo wa Tanzania kutengwa na nchi hizo tatu jana bungeni, alipokuwa akijibu maswali ya wabunge mbalimbali waliokuwa wakitaka kujua kauli ya serikali juu ya vikao vinavyofanywa na marais hao watatu.


Mbunge wa Viti Maalumu Rukia Ahmed (CCM), aliitaka serikali ipeleke pendekezo bungeni la kujitoa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kabla haijapewa talaka kutoka kwa Rwanda, Uganda na Kenya ambazo zimekuwa zikifanya mikutano inayojadili masuala ya jumuiya bila kuihusisha serikali ya Tanzania.


Akijibu hoja hiyo Sitta, alisema ni mapema kwa Tanzania kupeleka bungeni hoja ya kujitoa katika jumuiya hiyo kwa kuwa kinachofanywa na nchi hizo kimeshafikishwa kwa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa nchi wanachama ambaye atakitolea ufafanuzi katika kikao kitakachofanyika wiki mbili zijazo.


Sitta alifafanua kauli ya Waziri mwenzake wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, hivi karibuni ya kwamba Tanzania inasubiri talaka akisema yenyewe ndiyo yenye uwezo wa kutoa talaka kwa jumuiya hiyo kwa kuwa inamiliki asilimia 52 ya eneo lote huku nchi zilizobakia zikigawana asilimia 48 iliyobakia.


“Hawa wenzetu wanafanya utoto wa kutuzunguka, sisi tunatumia hekima za mzee Mwinyi aliyesema ‘mwongo, mwongoze’. Kama wao wana hila zozote juu yetu, siku si nyingi tutazibaini, kama ni ndoa kwenye jumuiya basi sisi ndio tutakuwa tumeoa…hivyo tutatoa talaka wakati wowote,” alisema.


Naye Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela (CCM), aliitaka serikali isiendelee na hatua zozote kwenye jumuiya hiyo ambayo inaonekana kuelekea kuvunjika.


Akijibu swali hilo, Sitta alisema serikali haijakaa kimya bali imeamua kutoshiriki vikao vyote ambavyo nchi za Kenya, Rwanda na Uganda zitakuwa zimeshayazungumzia masuala husika na kuamua kuwa na msimamo wa pamoja nje ya jumuiya.


Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF), alihoji serikali inangoja utafiti gani juu ya kutengwa kwao kiuchumi na nchi hizo tatu wakati Kenya wameshaingia makubaliano ya kibiashara na Ethiopia na Sudan.


Katika jibu lake, Sitta alisema Tanzania imeshafanya mazungumzo na nchi za DRC na Burundi kushirikiana katika nyanja mbalimbali.
Alisema kuwa DRC ndiyo yenye manufaa makubwa kiuchumi kwa Tanzania kuliko Rwanda, Uganda, Kenya na Burundi kwa sababu mizigo mingi hutegemea bandari ya Dar es Salaam.


“Burundi nao wanatengwa kama tunavyofanyiwa sisi, lakini tumeamua kushirikiana kikamilifu na DRC pamoja na Burundi ambao tuna imani wana manufaa makubwa kwetu,” alisema.


Hivi karibuni Tanzania iliingia kwenye mgogoro na Rwanda baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa ushauri kwa Rais wa Rwanda, Kagame kuketi chini na waasi wa nchi hiyo ili kuzungumzia masuala ya amani kwa nchi yao. TANZANIA DAIMA

Tuesday, October 29, 2013

UNYAMA HUU.......ADHABU YA RUNGU NA PANGA YATUMIKA KUMPELEKA MTOTO SHULE

Victoria Mukama (10) baada ya matibabu
Sehemu za mwili alizojeruhiwa na baba yake.

Mwalimu wa zamu wa Shule ya Msingi Airport, Damali Obadia alisema tukio hilo la ajabu lilitokea majira ya saa mbili na nusu asubuhi ambapo akiwa ofisini alimuona mzazi huyo akiwa na mtoto huku akiendelea kumpiga wakielekea ofisini.


KATIKA hali isiyokuwa ya Kawaida, Baba mmoja aliyejulikana kwa jina la Oscar Mukama mkazi wa Isengo Airport Jijini Mbeya amemjeruhi vibaya binti yake Victoria Mukama (10) kwa kumpiga sehemu mbali mbali za mwili wake akitumia vifaa vyake vya ulinzi likiwemo Lungu.

Kwa mujibu wa Mwalimu wa zamu wa Shule ya Msingi Airport, Damali Obadia alisema tukio hilo la ajabu lilitokea majira ya saa mbili na nusu asubuhi ambapo akiwa ofisini alimuona mzazi huyo akiwa na mtoto huku akiendelea kumpiga wakielekea ofisini.

Alisema mzazi huyo baada ya kufika walimu walimpokea na kumuuliza kwa nini anampiga kiasi hicho mtoto wake alijibu mtoto ni wa kwake mwenyewe na alizaa kwa manufaa yake hivyo haoni sababu ya kuulizwa kuhusu kipigo kwa mwanaye.

Aliongeza kuwa baada ya walimu kumweleza kuwa kitendo alichokifanya ni cha kinyama na hakipaswi kutendeka Mzazi huyo alitoa kisu na kuwatishia walimu ikiwa ni pamoja na kutoa matusi makali dhidi yao ambapo walimu walifanikiwa kumtuliza na kumuomba amwache mtoto ili walimu wamwadhibu.

Alisema baada ya mzee huyo kuondoka na kumwacha mtoto walimpigia simu mama wa mtoto ambaye baada ya kufika shule alizimia kutokana na hali aliyomkuta nayo mtoto wake ambapo Walimu walitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Mtaa kisha kwenda Polisi kuchukua Fomu namba tatu (PF3) kwa ajili ya matibabu.

Mama mzazi wa binti huyo Teodora Paulo alisema yeye na mume wake hawakuwepo nyumbani ambapo baada ya kurejea kutoka Msibani majira ya asubuhi walimkuta binti yao hajaenda shule na walivyomuuliza sababu ya kutoenda shule alijibu alikuwa havioni viatu vyake.

Alisema baada ya kumsaidia kutafuta na kutofanikiwa kuviona baba yake ambaye nayeb alikuwa amejiandaa kwa ajili ya kwenda kazini kwake anakofanya kazi ya Ulinzi alimwamuru mwanaye kuvaa sare za shule na kwenda naye hivyo hivyo kwa kile alichodai anampeleka shule.

Alisema alishikwa na butwaa hadi kupoteza fahamu baada ya kumkuta mtoto amejeruhiwa huku akiwa amepigiwa simu na mumewe kwamba aende shule kumchukua mtoto wake lakini hakujua kama amepigwa kiasi cha kumjeruhi mtoto sehemu mbali mbali za mwili wake.

Akizungumzia kisa cha kupigwa kwake baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya katika Chumba cha dharula, Victoria Mukama (10) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Airport alisema wakiwa njiani kuelekea shuleni alishangaa akianza kupigwa bila kuelezwa sababu ni nini.

Alisema alianza kupigwa tangu wanatoka nyumbani hadi wanafika shule iliyoumbali wa Mita 250 kutoka Nyumbani hadi Shuleni akitumia Virungu na fimbo huku akiwa ameshika kisu mkononi kwa ajili ya kuwatishia wanataka kumuokoa.

Kutokana na tukio hilo Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta Mtuhumiwa huyo wa unyanyasaji wa watoto baada ya kufunguliwa kwa jarada lenye namba MB/IR/9563/2013 katika kituo cha kati cha Polisi Mbeya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Pambogo Esia Edward ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Shule hiyo alisema kitendo kilichofanywa na mtuhumiwa huyo hitendo hakipaswi kufumbiwa macho hivyo ni lazima sheria ichukue mkondo wake kwa kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa ndani ya jamii.

Aliongeza kuwa hajawahi kusikia mtuhumiwa huyo kama amewahi kujihusisha na ukatili wa namna hiyo na kuongeza kuwa huwa anatoa ushirikiano vizuri katika ngazi ya mtaa na kuhudhuria vikao mbali mbali vinavyoitishwa pamoja na kuchangia mada.

Nao majirani wa mtuhumiwa huyo walidai kuwa tabia ya Mwanaume huyo kufanya unyanyasaji inafichwa na mkewe ambaye anaonekana kuwa muoga wa kupigwa na mumewe na kuongeza kuwa anatabia ya kuandika makosa anayotendewa na mkewe.

Walisema awali amewahi kuoa mke na kuzaa nae watoto watatu lakini mkewe huyo alikimbia baada ya kuona tabia ya unyanyasaji imezidi kutoka kwa Mwanaume huyo aliyetajwa kuwa ni jamii ya watu wa Mosoma Mkoani Mara ambako tabia kandamizi dhidi ya wanawake na watoto bado zinafanyika.
CREDIT: MBEYA YETU

Wednesday, October 23, 2013

ZIWA MANYARA HATARINI KUPOTEA KWA UKAME

 
Mkutano wa siku mbili wa kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Arusha (RCC) Umeelezwa kwamba  Ziwa Manyara lipo hatari ya kutoweka kabisa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo uharibifu wa mazingira kunakotokana na kilimo pembezoni mwa mito kama juhudi za maksudi hazikuchulia kutunza mazingira yanayozunguka maeneo ya mito mbalimbali inayoingia ziwani humo.


Hali jii imetokana na kuongezeka   kwa shughuliza kibianadamu   hussani za kiuchumi na kusababisha pia ziwa manyara kujaa udongo na matope pamoja  uharibifu mkubwa  wa mazingira.


Akiwasilisha mada kuhusu  changamoto za uhifadhi katika hifadhi ya ziwa Manyara,Muikolojia katika hifadhi hiyo Bibi  Christina  Kiwanga amesema kukosana kwa utashi wa kisiasa ni changamoto kubwa katika kuliokoa ziwa hilo.


Bibi Kiwanga ametaja changamoto nyingine ni pamoja na kukosekana kwa mipango endelevu katika baadhi ya vijiji kuhusu umuhimu wa uhifadhi sanjari na elimu.


Muikolojia  huyo amewambia wajumbe wa kamati ya Ushauri ya Mkoa   wa Arusha kwamba  shughuli za Biandamu hususani za kilimo na za kiuchumi zimechangia kwa kiwango kikubwa  hifadhi hiyo kuwa katika hatari ya kutoweka.


Naye Meneja Ujirani Mwema makao makuu ya Tanapa BWANA Ahmed Mbugi amesema  umuhimu wa maeneo ya Mapito ya (SHOROBA) na mitawanyiko ya wanyama katika hifadhi amesema asilimia 80 ya Shooba  zilizokuwepo miaka ya nyuma zimetoweka kabisa.


Amesisitiza kwamba ni lazima  wananchi  walinde  uasilia  wa mapito ya  wanyama pori kutokana na umuhimu wa maeneo hayo

Mbungi amefafanua kwamba awali kulikuwa na  Maeneo ya SHOROBA yenye ukubwa  wa ekari 40,000 katika hifadhi za Arusha Kilimanjaro,manyara lakii maeeo haya yamepungua.


Aidha   amesisitiza kwamba wanasiasa wanachangia kuhujumu   maeneo haya ya uhifadhi kutokana na kukosekana  kwa kuchukuwa maamuzi mazito ya kuyalinda maeneo hayo kwa kuogopa wapiga kura hali inayoleta changamoto mbalimbali pindi wanapotoa taarifa za kulinda maeneo hayo.


Pia ameeleza kwamba asilimia 70 ya mapato yanayotokna na uhifadhi  yanatumika  katika usajidia  utekelezaji w amiradi ya kijamii ikiwemo ya afya,elimu, maji, na miradi ya barabara.


Amesema migongano baina ya wanyamapori na  binadamu inachangiwa na binadamu kuingilia maeneo ya mapito ya wanyamapori hivyo kuwakosesha njia za kupita hali inayoharibu mazingira.


Amesisitiza kwamba  hatua hii inasababisha kuathiri shughuli za utalii ambapo idadi ya watalii hupungua sanjari na shughuli za   uchumi kuathirika Mbali na  hali hii katika kipindi cha mwaka  1957/63 na 1987/`988 uoto wa asilimia   hususani misitu ulipungua kwa asilimia 13.5 wakati  maeneo ya kilimo yaliongezeka  kwa asilimia 10.9.


Aidha  maeneo ya ushorobo yaliyotumika kwa  shughuli za kilimo kati ya mwaka 1997/98 yaliongezeka  kati ya asilimia  8.35 hadi 11.41

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Lazaro Maasae yeye amesema kasi  ya ziwa manyara kuendeleoa kujaa ugondo na matope ni ya kasi zaidi

Tuesday, October 22, 2013

KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI (SACP) MSTAAFU JAMES KOMBE AFARIKI DUNIA KATIKA HOSPITALI YA OCEAN ROAD JIJINI DAR ES SALAAM.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiqwdOY6OdlsY4TeClN4MUVnbzYC2Pc-O0KNXndCiYVrIICH1ANJIUpoelwSDzfT0bM9kfytvZxVRBY-Z6eYP6zfZH-TwB2I3BruZPfMBTFzRAVweFrqcb_LbFjXAqMjqWH3FS39bQokV3L/s400/POLISI-762018.jpg 
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.
ALIYEKUWA kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha usalama barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) mstaafu James Kombe amef
ariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia kifo hicho Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Advera Senso alisema, Kombe alifariki Oktoba 22 mwaka huu na taratibu za mazishi zinaendelea.

Aidha Senso alisema Marehemu Kombe alizaliwa mwaka 1950 huko Mwika mkoani Kilimanjaro na alijiunga na Jeshi la Polisi tarehe 15 mwezi machi mwaka 1970 baada ya kuhitimu elimu ya sekondari mwaka 1969 nchini Uganda ambapo alipandishwa vyeo na kupewa madaraka mbalimbali.

Baadhi ya vyeo alivyopitia na miaka ya kupata vyeo hivyo katika mabano ni pamoja na Sagenti wa Polisi (1973) Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1977), Mkaguzi wa Polisi (1984), Mrakibu Msaidizi (1986), Mrakibu wa Polisi(1991), Mrakibu Mwandamizi (1995), Kamishna Msaidizi wa Polisi (1998) na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (2002) hadi alipostaafu mwaka 2010.

Baadhi ya nafasi alizowahi kuzitumikia katika Jeshi la Polisi ni pamoja na kuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) katika wilaya za Dodoma, Tarime, Serengeti na Arusha pamoja na Kuwa Mkuu wa Polisi wa Mkoa (RPC) katika mikoa ya Lindi, Arusha, Kigoma pamoja na Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza ghasia Tanzania na hadi anastaafu alikuwa mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Tanzania.

Monday, October 21, 2013

Saturday, October 19, 2013

UNYAMA WA HALI YA JUU: WATU WASIOFAHAMIKA WAMUUA KWA KUMKATAKATA KICHWANI NA TUMBONI ERNEST (45) mkazi wa mbeya

Baadhi ya majirani wakiwa jirani na mwili wa marehemu Seba wakisubiri polisi kuja kuuchukua mwili huo

Mwili wa Marehemu Seba ukiwa umefunikwa na branketi


Add caption


SEBA ERNEST MWAKASULA[45] ameuawa  kwa kukatwa kichwani na  tumboni na vitu vyenye ncha kali  na mtu au watu wasiofahamika kisha mwili wake kutupwa mita chache kutoka nyumbani kwake.

Mke wa marehemu JOYCE DANIEL[39]amesema waliagana na marehemu majira saa mbili usiku akimtaarifu kuwa asubuhi ya octoba 19 mwaka huu atasafiri kuelekea Wilaya ya CHUNYA kwa ajili ya kujenga makaburi.

Aidha imedaiwa baada ya kutoka nyumbani kwa mke mdogo marehemu alipita kilabuni ambapo watu kadhaa walimwona marehemu akipata viburudisho.

Baadhi ya majirani wamesema kuwa hawakusikia sauti yoyote ya mtu kuomba msaada ingawa ni karibu na makazi ya watu hali inayosadikika mauaji kufanywa eneo jingine na mwili kutupwa karibu na nyumbani kwake

Mwenyekiti wa kijiji cha NSONYANGA ASUMILE MTAWA amesema alipata taarifa kutoka kwa mtendaji wa kijiji ambapo walifika eneo la tukio na kukuta marehemu amekatwa kichwani na utumbo ukiwa nje.

Diwani wa kata ya Mahongole BROWN MWAKIBETE amesema kuwa kitendo kilichofanywa na wauaji hao ni cha kinyama ambapo amewataka wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi li watuhumiwa wakamatwe ili kujibu tuhuma za mauaji.

Mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi na Daktari kisha kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa mazishi.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya DIWANI ATHUMANI amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kutoa wito kwa mtu au watu wanaowafahamu wliohusika na tukio hilo watoe taarifa polisi il wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Picha na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu

MTOTO WA KIKE WA MIAKA MIWILI AJIFUNGUA WATOTO MAPACHA.

UKISTAAJABU ya musa utayaona ya firauni ndivyo ilivyotokea kwa mtoto wa miaka miwili ambaye amejifungua mtoto.

Mtoto huyo aliyefahamika kama Xiao Feng alijifungua kwa njia ya upasuaji katika hospit
ali moja mjini Xuaxi nchini China.

Kwa mujibu wa taarifa, madaktari waligundua kuwa mtoto Xiao alikuwa na mimba baada ya kupelekwa na mama yake.Binti wa miaka 14 akiwa na mtoto wake katika Manispaa ya Moshi.Picha ya Maktba.


Awali mzazi wake huyo aligundua kuwa tumbo la binti yake lilikuwa kubwa isivyo kawaida hivyo alimpekeka hospitali kujua kulikoni.

Nao matabibu hao wakafanya kazi yao ya kumpiga picha za mionzi ya jua ‘x-rays’ na kubaini mtoto huyo alikuwa amebeba mwenzake tumboni.

Walimfanyia upasuaji ambao ulimalizika kwa mtoto huyo kuzaa watoto pacha.
chnazo: mtanda blog 

MAWAZIRI, WAZIRI KOMBANI: KUTAJA MSHAHARA WA MTUMISHI WA UMMA NI KINYUME CHA SHERIA.ZI

File:Jakaya Kikwete - Partnerships for Development - World Economic Forum on Africa 2011 - 2.jpgRAIS JAKAYA KIKWETE ANAYELIPWA MSHAHARA ZAIDI YA SH36 MIL KWA MWEZI KUTOKANA NA KAZI YAKE YA URAIS.
IMG_9964

WAZIRI MKUU MIZENGO KAYANDA PINDA ANALIPWA MSHAHARA WA SH26 KWA MWEZI.

DAR ES SALAAM.
SIKU chache baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe kutaja hadharani mishahara ya Rais Kikwete na Waziri Mkuu, Mize
ngo Pinda, serikali imekataa kuizungumzia mishahara hiyo.

Msimamo wa Serikali kutotaja mishahara ya viongozi wakuu unatofautiana na utamaduni wa nchi nyingine kama Marekani, Afrika Kusini, Ufaransa na Kenya ambazo mishahara ya wakuu wake huwekwa wazi kwa umma.

Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema akiwa wilayani Igunga Mkoani Tabora, alisema Rais Kikwete anapokea zaidi ya Sh30 milioni kwa mwezi (sawa na Sh360 milioni kwa mwaka) ikiwa ni marupuru na mshahara kwa mwezi bila kodi, huku Pinda akipokea Sh 26 milioni kwa mwezi.

Akizungumza na Mwananchi kwa simu jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani alisema kiongozi yeyote haruhusiwi kutaja mshahara wa mtu mwingine kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria ya utumishi wa umma.

“Kuutaja mshahara wa mtu mwingine ni kinyume cha sheria na kosa, siyo utaratibu. Kwani wewe upo tayari watu waujue mshahara wako?” alihoji.

Aliongeza kuwa ingawa mishahara ya viongozi hao inatokana na kodi za wananchi, sheria ndiyo inayozuia watu kuyataja malipo hayo hadharani na kwamba hayupo tayari kuutaja mshahara wa rais au kiongozi mwingine labda mtu huyo autaje yeye mwenyewe.

“Siwezi kutaja mshahara wa bosi wangu wala wa kwangu mwenyewe. Wewe unaujua mshahara wa Obama (Rais wa Marekani)?” alihoji tena.

Akizungumzia mishahara ya marais wa nchi nyingine duniani kuwekwa wazi, Kombani alisema kila nchi ina utaratibu wake na kwamba Tanzania haijafikia hatua hiyo.

Alipotafutwa kulizungumzia suala hilo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue simu yake ya mkononi iliita bila kupokewa. 

Gazeti hili pia liliwasiliana na Naibu Mtendaji Mkuu mwenye jukumu la kuanzisha na kuongoza Idara ya Mageuzi ya Kilimo Ofisi ya Rais Ikulu, Peniel Lyimo ambaye alisema yeye si mhusika. “Masuala yote yanayohusu utumishi yapo Wizara ya Utumishi,” alisema Lyimo.

Akianika mshahara wa Waziri Mkuu, Zitto alisema kwamba kiongozi huyo analipwa Sh11.2 milioni kama mbunge, Sh8 milioni kama waziri na Sh7 milioni kwa nafasi yake ya Waziri Mkuu, hivyo, kumfanya kupokea zaidi ya Sh300 milioni kwa mwaka.

Hata hivyo, Kombani alilionya gazeti hili kuandika taarifa za mishahara ya watu kwa kuwa kufanya hivyo ni kosa.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Bashiru Ally alisema Mwalimu Nyerere aliwahi kutaja mshahara wake hadharani na kuhoji viongozi wanaotaka mishahara yao isitajwe wanaficha nini. 
chanzo":MWANANCHI