Pages

Pages

Monday, November 25, 2013

NYUMBA ZA ASKARI ZIMA MOTO ARUSHA NI KAMA MAGOFU YALIYODUMU KWA ZAIDI YA MIAKA 50



Jeshi la zima moto na ukoaji Maafa mkoa wa Arusha linakabiliwa na changamoto
ya uchakavu wa nyumba uliodumu kwa miaka zaidi ya 50 ambapo pia
uchakavu huo wa nyumba unaenda sanjari na uhaba wa Vyoo hali ambayo
inasababisha ongezeko la magonjwa kutokana na nyumba hizo
kugeuka kuwa makazi ya Mbu.


Aidha nyumba hizo zilizojengwa mwaka 1954 ambapo mpaka sasa hazijaweza
kufanyiwa marekebisho ya aina yoyote ile imesababisha nyumba hizo kugeuka kama magofu.


Hayo yamelezwa na Andrew James Mbate ambaye ni kamanda Zima moto na
uokoaji mkoa wa Arusha wakati akiongea na wafanyakazi wa jeshi hilo
mara baada ya kumuaga aliyekuwa kamanda wa jeshi hilo Bw Jesward
Ikonko hivi karibuni jijini Arusha.


Kamanda Andrew alisema kuwa nyumba hizo za jeshi zilijengwa miaka
mingi iliyopita lakini toka kujengwa kwake mwaka 1954 mpaka sasa
hazijaweza kufanyiwa marekebisho ya aina yoyote ile jambo ambalo
linasababisha wafanyakazi pamoja na familia zao ziweze kuishi maisha
ya taabu na kuugua kila mara.


“tunaweza kusema kuwa nyumba hizi zimegeuka nyumba za mbu kwani kwa
juu hazijaweza kuzibwa na baridi yote inapita lakini pia hata kwa juu
kwa kuwa kuna uwazi mkubwa sana unasababisha mbu kukaa kama nyumbani
kwani sasa hali hiii kwa kweli inasababisha wafanyakazi wetu washindwe
kufanya kazi zao kwa ufanisi na kufuraia makazi’aliongeza hivyo.


Pia alisema kuwa mbali na nyumba hizo kugeuka chakavu sana lakini pia
hata suala la vyoo navyo ni chakavu kwa kiwango cha hali ya juu jambo
ambalo ni hatari kwa afya za watumiaji


“tunaweza kujiuliza kuwa choo kilichojengwa mwaka 1954 mpaka sasa
kitakuwaje na kinatumiwa na familia nyingi je kwa hali hii wafanyakazi
wataweza kufuraia maisha au ndo wataboreka “alihoji Kamanda huyo.


Kutokana na hali hiyo alisema kuwa ni vema kama mchakato  wa nyumba
hizo za watumishi sasa zikageukia upande wa Wizara kutoka katika
mikono ya Jiji la Arusha kwani kama zitakuwa chini ya wizara zitaweza
kupata marekebisho makubwa ambayo yataongeza utendaji kazi mzuri wa
wafanyakazi.



Akiongelea suala zima la utendaji kazi wa kikosi hicho cha zima moto
mkoa wa Arusha alisema kuwa mkoa wa Arusha unakabiliwa na tatizo la
ujenzi holela hali ambayo inasababisha wakati mwingine washindwe
kuokoa baadhi ya nyumba ambazo zinateketea kwa Moto hivyo basi ni vema
kama kamati ya mipango miji wakati mwingine ikawa inatoa elimu kwa
wananchi wanaotaka kujenga nyumba zao.



MWANAMKE AUAWA KWA KUCHOMWA NA KISU NA MUMEWE AKIWA KATIKA WODI YA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA

Gervas Kadaga(25) anaetuhumiwa kumuua mkewe akiwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.

MAMA mkubwa wa Gervas aliyejitambulisha kwa jina la Martha Lugenge alisema kuwa vijana hawa walikutana Madibila kila mmoja akiwa katika shughuli zake ndipo walipoamua kuishi pamoja.




Mwanamke mkazi wa kijiji cha Mahango kata ya Madibila wilayani Mbarali mkoani Mbeya aliyefahamika kwa jina la Jitihada Mamga(20) ameuawa kwa kuchomwa kisu na mumewe aliyefahamika kwa jina Gervas Kadaga(25) ambaye pia ni mkazi wa kijijini hapo.



Tukio hilo limetokea Novemba 21 majira ya saa 1:00 jioni baada ya kutokea ugomvi baina ya wapenzi hao ambapo marehemu alikutwa na majeraha tisa ya kisu katika sehemu mbalimbali za mwili wake.



Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Bw. Diwani Athumani alisema kuwa marehemu alifia nyumbani kwake ambapo mtuhumiwa ambaye amelazwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya naye amejeruhiwa kwa kuchomwa na kisu tumboni.



Hata hivyo Kamanda Athumani alisema kuwa hadi sasa hakijafahamika chanzo halisi cha ugomvi huo ambapo Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi wa tukio hilo huku mtuhumiwa akiwa amewekwa chini ya ulinzi wa polisi katika hospitali ya rufaa ya Mbeya alikolazwa.



Akizungumza katika hospitali ya rufaa alikolazwa mama mkubwa wa Gervas aliyejitambulisha kwa jina la Martha Lugenge alisema kuwa vijana hawa walikutana Madibila kila mmoja akiwa katika shughuli zake ndipo walipoamua kuishi pamoja.



Alisema yeye alipewa taarifa za tukio hilo siku inayofuata na kwamba alipofika alikuta ndugu wa marehemu wameuchukua mwili wa mtoto wao kwa ajili ya taratibu za mazishi na kwamba hajui chanzo cha ugomvi uliosababisha wapigane visu.



Mama huyo alisema kuwa vijana hao hawajawahi kupata mtoto na kwamba hawajaanza kuishi pamoja muda mrefu; ''Wote ni watoto, kwani wameanza kuishi muda mrefu? wamekutana kila mmoja akiwa katika kazi zake, ndipo walipoanza kuishi kama mke na mume,''alisema  Na Mbeya yetu

MHE PROF JUMA ATHMAN KAPUYA ADAIWA KUTOLEKEA NJE YA NCHI AKIDAIWA KUPUNGUZA MAKALI TUHUMA ZA KUMPACHIKA UJAUZITO MWANAFUNZI WA SEKONDARI JIJINI DAR ES SALAAM.

SAKATA LA KAPUYA KUBAKA NA KUTISHIA KUUA LACHUKUA SURA MPYA,KAPUYA ATOROKA NCHINI,VIGOGO WA POLISI WATUHUMIWA KUMTOROSHA, SOMA HABARI YOTE HAPA. 
 

MHE PROF JUMA KAPUYA.
 
Na Karoli Vinsent 
SIKU chache baada ya Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), kudaiwa kutoweka nchini kukwepa mkono wa sheria dhidi ya tuhuma za kutishia kumuua binti anayedaiwa kumbaka, vigogo wa polisi wanadaiwa kuhusika kumsaidia kutimkia nje, Habari24 limedokezwa.




Habari24 limezipata, zinaeleza kuwa siku mbunge huyo akikamilisha taratibu za kusafiri, ndiyo siku ambayo Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni lilikuwa limekamilisha kufungua jalada la tuhuma zake na liliweka mtego wa kumnasa.


“Wakati Polisi Kinondoni wakiweka mtego wa kumnasa, baadhi ya polisi walimjulisha na hata kumsaidia kuhakikisha anasafiri nje ya nchi,” alisema mmoja wa maofisa wa juu wa polisi nchini. 



Hata hivyo, kuna utata na kauli zinazopingana kuhusu mbunge huyo. Taarifa nyingine zinasema kuwa mbunge huyo ambaye amepata kuwa waziri, anadaiwa kusafiri kwenda nchini Sweden kwa masuala ya kikazi, na kwamba atakuwepo huko kwa muda usiopungua mwezi mmoja. 



Chanzo kingine kimedokeza kuwa mbunge huyo alidai ametumwa kazi na kigogo mmoja serikalini na atakuwepo nchini humo miezi miwili hadi mitatu. 



Hata hivyo, haijajulikana kazi anayokwenda kuifanya Kapuya ingawa kuna taarifa safari hiyo imelenga kutuliza upepo mbaya wa kuandamwa na tuhuma za ubakaji ambazo zipo polisi hivi sasa. 



Tayari Profesa Kapuya alishafunguliwa jalada namba OB/RB/21124/13 katika Kituo cha Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam juzi.




Hata hivyo Jeshi la Polisi limesisitiza kuwa linamsaka mbunge huyo ndani na nje ya nchi. 


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alikaririwa juzi kuwa watamtafuta Kapuya nchi yoyote atakayokwenda iwapo tuhuma dhidi yake zitathibitika. 



Alisema mtandao wa polisi ni mkubwa, hivyo si rahisi kwa mtuhumiwa yeyote kuukwepa mkono wa sheria endapo itahitajika kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. 



“Sisi tunashirikiana na polisi wa nchi mbalimbali duniani, ndiyo maana inakuwa rahisi kwa mtuhumiwa aliyetoroka nchi fulani kukamatwa nyingine na kurejeshwa kwao. 




“Nataka niwaondoe hofu wale wote wanaodhani polisi haiwezi kumkamata mtu akikimbia nchini, tuna mkono mrefu sana, na hatufanyi kazi kinyume na taratibu zetu,” alisema.



Kamanda Wambura pia alikiri polisi kufungua jalada la Kapuya, huku akiweka wazi kuwa kinachofanyika hivi sasa ni uchunguzi wa tuhuma zake. 



Alisema miongoni mwa maeneo wanayoyafanyia uchunguzi ni kubaini kama ujumbe ulio katika simu ya binti anayedai kubakwa na kutishiwa maisha unatoka katika simu ya mbunge huyo.



“Tumefungua jalada, lipo kwa ajili ya uchunguzi na tukibaini kuwa ni nani anahusika na tuhuma hizo tutamsaka na kumkamata popote alipo,” alisema Wambura. 



Gazeti la Tanzania Daima limekuwa likiandika namba ya simu ya Prof. Kapuya ambayo huwa anaitumia kutuma ujumbe wa vitisho kwa binti huyo, ingawa kuna vyombo vingine vya habari viliamua kuandika kwa mtazamo tofauti na kumtuhumu dada wa binti aliyebakwa kuwa ni mtu mzima na kuwa ana uhusiano na Kapuya, na wana watoto. 



Simu hiyo namba 0784993930 inayodaiwa kumilikiwa na Profesa Kapuya, mbali ya kutuma ujumbe mfupi wa maneno ya kutishia kuua, pia ndiyo inayodaiwa kutumika kutuma pesa kwa njia ya mtandao kwenda kwa binti huyo. 



Tangu gazeti hilo na Blogs hii vianze kuandika tuhuma hizi nzito, kumekuwapo na kusuasua kwa mtuhumiwa huyo kutiwa hatiani na Jeshi la Polisi. 



Harakati za kufungua jalada dhidi ya Kapuya zilizoanza wiki iliyopita ziliendelea hadi juzi ambapo polisi walitumia zaidi ya saa 12 kumhoji binti huyo anayedaiwa kubakwa ili kupata ukweli wa sakata hilo. 




Akiwa polisi, binti huyo alikutana na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi ya Oysterbay (OCD) na OC-CID wake na kutoa maelezo ya awali kabla ya viongozi hao kumruhusu ayaweke malalamiko yake katika maandishi kwa ajili ya kufunguliwa mashitaka. 



Wachambuzi wa masuala ya kijamii waliotoa maoni yao kuhusu sakata hili na mwandishi wa blogs hii wote kwa pamoja wameonyesha hali ya kushangaza kwa Jeshi la polisi nchini limeshindwa kumchukulia hatua Profesa huyu kwa vitendo vya kinyama alivyofanya huku wengine wakiinyoshea kidore Wizara ya Jinsia na Watoto kwa kushindwa kumchulia hatua profesa huyo. 



Katika hali ya kushangaza waziri wa Jinsia na Watoto Sophia Simba mala kwa mala amekuwa akikinyoshea kidole chama cha Demokrasia Chadema kuwa kinavuruga amani ya nchi. 



huku akishindwa hatu kumsaidia mototo huyo aliyebakwa na Kuongozi huyo wa Ccm akati ndio jukumu lake kwenye wizara kuliko mambo haya ya vyama vya siasa ambavyo haviko kwenye wizara yake, 
chanzo jumamtanda blog

MAMA YAKE ZITO KABWE, SHIDA SALUM: NI BORA MHE ZITTO ZUBERI KABWE ANGETIMULIWA KABISA CHADEMA

DAR ES SALAAM. 
SIKU moja baada ya Kamati Kuu ya Chadema kumvua uongozi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Taifa wa chama hicho, Zitto Kabwe, mama yake mzazi, Shida Salum ametoa ya moyoni akieleza kuwa kilichomkuta mwanaye kimefunika mabaya mengi yaliyopangwa afanyiwe.

“Kwa upande wangu naona kama ni ushindi kwa Zitto kutokana na jinsi ninavyojua hali ilivyo, mambo yalikuwa ni mengi mno na nikwambie tu, Zitto kuvuliwa uongozi kumefunika hayo yaliyokuwa yamekusudiwa kufanywa dhidi yake. Nilikuwa naomba Mungu  kila siku ili afukuzwe Chadema,” alisema mama huyo wakati akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Tabata, Dar es Salaam.
Shida Salum alisema kuwa Mungu amemnusuru mwanaye na kusisitiza, “Watu walikaa na kutengeneza ripoti ya siri kuhusu Zitto na kuiweka kwenye mtandao kisha kuituma kwa wanachama wa Chadema wanaowafahamu. Mpaka wanafikia hatua hiyo maana yake ni kwamba wamejaribu njia zote za kummaliza, lakini wameshindwa.”
Alisema kutokana na hali ilivyo hivi sasa amemnyang’anya mwanaye kwa muda simu zake zote za mkononi, kompyuta mpakato (Laptop) pamoja na iPad ili asiwasiliane na watu, kwa maelezo kuwa wapo wenye nia mbaya wanaomsaka kumpa pole za kinafiki. “Kwa sasa nataka mwanangu atulize akili.”
Shida Salum, mbali na kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, pia ni  mwasisi wa  Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (Shivyawata) na Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Viungo (Chawata).
Zitto pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Dk Kitila Mkumbo juzi walivuliwa uongozi kutokana na uamuzi wa kikao cha Kamati Kuu kilichokutana kwa siku mbili, kuanzia Novemba 20 mwaka huu katika Ukumbi wa Blue Pearl jijini Dar es Salaam, wakituhumiwa  kukisaliti chama.
Mbali ya kuwavua uongozi Zitto, Dk Mkumbo pamoja na  aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho mkoani Arusha, Samson Mwigamba, pia Kamati Kuu imewapa siku 14 wajieleze kwa nini wasifukuzwe uanachama.
Kwa uamuzi huo Zitto amebaki na wadhifa wa ubunge wake wa Jimbo la Kigoma Kaskazini na Uenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).
Katika ufafanuzi wake wa jana, Shida aliwataka wanachama wa Chadema kuwa watulivu kwa maelezo kuwa Zitto hajafukuzwa uanachama, “Siku nyingi walikuwa wanamwinda na hata hilo jambo ambalo Chadema wanasema amefanya, hawana uhakika nalo.”
Juzi wakati akisoma uamuzi wa Kamati Kuu,  mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu alisema wamebaini kuwapo kwa mkakati mkubwa wa watu hao kutimiza malengo hayo ambao umeandikwa katika waraka unaoitwa ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013’, ambao umeandaliwa na kikundi kinachojiita ‘Mtandao wa Ushindi’.
Alisema kikundi hicho vinara wake wapo wanne,  Zitto anajulikana kama Mhusika Mkuu (MM), Mkumbo (M1), Mwigamba (M3) na mtu mwingine wa nne ambaye alieleza kuwa hajatambulika na anatumia jina la M2.
 MWANANCHI

MHE ZITTO ZUBERI KABWE: SITATOKA CHADEMA NG'O, NITAKUWA MTU WA MWISHO KUJITOA KATIKA CHAMA HICHO KWA HIARI.

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe (kushoto)akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Picha na Edwin Mjwahuzi.  

DAR ES SALAAM. 
ALIYEKUWA Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe amesema kuwa hana mpango wa kujiondoa Chadema na kusisitiza kwamba atakuwa mtu wa mwisho kujitoa ndani ya chama hicho kwa hiari yake.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana katika mkutano aliouandaa kwa pamoja na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo, Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini alisema kwamba amekuwa mwanachama wa Chadema tangu akiwa na umri wa miaka 16 hivyo haiyumkiniki akikimbia chama hicho.
Zitto na Dk Kitila walivuliwa nyadhifa zao wiki iliyopita wakihutumiwa kukihujumu chama hicho.
“Kuna watu ambao walitegemea kuwa leo hii ningejibu mapigo, ‘ningezodoa,’ watu wengine kwa majina kama ilivyo kawaida kwa siasa za Tanzania. Natambua pia kama ilivyo kawaida wakati wa migogoro kwa vyama hapa Tanzania, kuna watu walitegemea leo ningetangaza kinachoitwa ‘maamuzi magumu’,” alisema na kuongeza:
“Natambua kuwa wapo ambao wangependa kutumia nafasi zao kudhoofisha mapambano ya siasa za demokrasia nchini mwetu, napenda wanachama wa Chadema na wapenda demokrasia wote nchini watambue kuwa, mimi bado ni mwanachama mwaminifu wa chama hiki na nitakuwa wa mwisho kutoka kwa hiari yangu.”
“Kinachoendelea ndani ya chama chetu ni mapambano ya kukuza demokrasia. Ni mapambano baina ya wapenda demokrasia dhidi ya wahafidhina, waumini wa uwajibikaji dhidi ya wabadhirifu na wapenda siasa safi dhidi ya watukuzao siasa majitaka.”
Alisema kuwa atafuata taratibu zote za ndani ya chama katika kuhitimisha jambo hilo.
“Mimi sitoki, wanaotaka nitoke, wanitoe wao,” alisema Zitto.
Zitto alisema Chadema ndicho chama kilichomlea na kumfikisha hapo alipo sasa, hivyo hata siku moja hatokuwa chanzo cha kuvunjika kwa chama hicho.
“Ningependa hata mtoto wangu akikua, awe pia mwanachama wa chama hiki, nimejiunga na chama hiki nikiwa na umri wa miaka 16 mpaka sasa nina miaka 37, nimetumia muda mrefu zaidi Chadema kuliko kipindi chote cha maisha yangu, Chadema ni kama maisha yangu, kukivunja chama hiki ni sawa na kujivunja mimi mwenyewe, kitu ambacho siwezi,” alisema Zitto.
 MWANANCHI.

Thursday, November 21, 2013

TANZANIA WASHIRIKI KWENYE KUNGAMANO LA TEHAMA LA DUNIANI LA SHIRIKA LA USIMAMIZI WA MAWASILIANO DUNIANI I.T.U

Katibu Mkuu wa ITU ambalo ni Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia Mawasiliano Duniani Dr. Hamadoun Toure akisikiliza Maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Prof. John Nkoma. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Makame Mbarawa. Katikati ni Waziri wa ICT wa Thailand.

Na Innocent Mungy - Bangkok Thailand

Tanzania inashiriki katika Kongano la TEHAMA la Dunia linaloandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia Mawasiliano Duniani (ITU-International Telecommunications Union) linalofanyika katika jiji la Bangkok nchini Thailand.

Kongano hilo lenye Kauli Mbiu ya Kuchochea Mabadiliko Katika Ulimwengu wa TEHAMA, unashirikisha nchi wananchama wa ITU na wasio wanachama, Makampuni ya Mawasiliano Duniani, Taasisi na wasimamizi wa sekta ya Mawasiliano Pamoja na Serekali, wanashiriki Kongano hili katika kipindi ambacho mabadiliko makubwa katika Sekta ya Mawasiliano.

Mabadiliko haya yanapelekea dunia kuwa na Changamoto ya Kuyakubali Mabadiliko hayo na kukabiliana na Changamoto zake kwani faida za mabadiliko ni kubwa kwa Jamii Habari duniani. Akizungumza jijini Bangkok, Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa amesema Tanzania iko tayari kwa na imeshapokea mabadiliko na imetekeleza mikakati ya kuhakikisha Tanzania inapokuwa mabadiliko bila tatizo.

Aidha Mheshimiwa Mbarawa amesema Tanzania inatambua umuhimu wa mabadiliko katika TEHAMA hususan kipindi hiki cha dijitali kwani ndio njia pekee ya kuharakisha maendeleo ya watanzania kwa ufanisi.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Prof. John Nkoma amesema Tanzania tayari  mstari wa mbele kuhakikisha inachochea mabadiliko ya teknolojia ya habari na mawasiliano ili wananchi wafaidike na huduma za Mawasiliano. "Tuna mfumo mzuri wa usimamizi wa leseni za muingiliano wa teknolojia, sheria na kanuni nzuri ambazo zinawezesha mabadiliko katika TEHAMA kunufaisha watanzania. Tayari Tanzania imeingia katika mfumo wa Utangazaji wa digitali na tunaendelea kuweka mazingira mazuri ya kuwepo kwa huduma nyingi zaidi kurahisisha maisha ya watanzania". Amesema Profesa Nkoma.

Taasisi kadhaa toka Tanzania zinashiriki Kongano hili kutoka Tanzania ikiwa ni pamoja na W ziara ya Afya, Kamisheni ya Sayansi na  Teknolojia,  DTBi ya wavumbuzi na wagunduzi, NICTBB inayosimamia mkongo wa Taifa, MaxCom.

Timu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania katika Maonesho ya ITU Telecom World

Kongano hili linafanyika kwa siku nne kuanzia tarehe 19 - 22 Novemba 2013. Tanzania inashiriki na kauli Mbiu ya nchi "Tanzania: Africa Strategic ICT Hub". Pamoja an Kongano pia yako Maonesho ya ICT yenye nia ya kuonesha jinsi nchi zinavyochochea maendeleo kwa raia wake kupitia TEHAMA. Banda la Maonesho la Tanzania limevutia watu wengi wanafikia kujifunza jinsi Tanzania imeweza kuchochea mabadiliko katika TEHAMA na jinsi wananchi wanafaidika na huduma mbalimbali zinazotolewa nchini.

Aidha Baadhi ya Taasisi zinazoshiriki zinaangalia uwezekano wa kuchochea zaidi upatikanaji wa huduma zao kwa kuwa na washirika katika shughuli zao. Leo asubuhi Ujumbe wa Tanzania ulishiriki katika Mkutano Maalum wa Wawekezaji Katika Sekta ya Mawasiliano ulioendeshwa na Naibu Katibu Mkuu wa ITU Bwana Houlin Zhao. 

Timu Tanzania I kuifanya mikakati ya kushiriki kikamilifu katika siku mbili zilizobaki. Hapa wakipeana taarifa ya Matukio ya siku ya pili.

Tuesday, November 19, 2013

HII NDIYO HABARI KAMILI YA YULE MFANYABIASHARA ALIYEUA MTU MMOJA KISHA NAYE KUJIUA NA KUJERUHI WENGINE WATATU KATIKA KISA CHA WIVU WA MAPENZI ILALA JIJINI DAR ES SALAAM

Polisi wakikagua gari walilokuwa wakisafiria watu wanne kabla ya kushambuliwa kwa risasi na mtu alitajwa kuwa jina la Gabriel Munisi aliyedaiwa kuua watu wawili na yeye kujiua baada ya kujeruhi wengine jana asubuhi jirani na Club ya Wazee, Ilala, jijini Dar es Salaam. Picha ndogo polisi wakikagua silaha iliyotumika.Picha na Silvan Kiwale  
DAR ES SALAAM. 
MFANYABIASHARA wa magari, Gabriel Munisi (35), jana alijiua baada ya kumuua mtu mmoja na kujeruhi wengine watatu jijini Dar es Salaam katika tukio linalohusishwa na wivu wa mapenzi.
Munisi, ambaye alikuwa mkazi wa Mwanza, aliwapiga risasi watu watatu akiwamo mchumba wake, Christina Alfred katika Mtaa wa Bungoni Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.
Baada ya kumpiga risasi mchumba wake huyo na kudhania kwamba amemuua, inadaiwa kwamba Munisi aliendelea kuwamiminia risasi watu wengine na kumuua mdogo wake Christina, Alpha (22).
Katika tukio hilo, Christina na mtu anayedaiwa kuwa mchumba wake mpya, Francis Shumila wamelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kujeruhiwa. Mama yake Christina, Helen Alfred amelazwa katika Hospitali ya Amana baada ya kujeruhiwa pia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marieta Minangi alisema Munisi alikutwa na bastola moja, magazini mbili na yalikutwa maganda 14 ya risasi zilizotumika na risasi mbili ambazo zilikuwa hazijatumika.
Tukio hili limetokea mwezi mmoja baada ya mwandishi wa habari wa ITV, Ufoo Saro kujeruhiwa kwa risasi na mzazi mwenzake, Anthery Mushi.
Katika tukio hilo, Mushi alijiua baada ya kumuua mama mzazi wa Ufoo na inaaminika pia tukio hilo lilisababishwa na masuala ya mapenzi.
Lilivyotokea
Mashuhuda waliokuwapo katika tukio hilo walisema mauaji hayo yalitokea saa 1.15 asubuhi baada ya Munisi kufika Ilala Bungoni na kwenda katika Klabu ya Wazee iliyo jirani na eneo yalipotokea mauaji na kunywa supu kabla ya kusogea karibu na lango la nyumba anakoishi mchumba wake.
Mmoja wa majirani, Noel Gerald alisema alimuona Munisi akiwa amesimama karibu na lango la nyumbani kwa kina Christina.
Alisema baadaye waliona gari aina ya Toyota Hilux, Surf, likitoka katika lango la nyumba hiyo na mara walimuona Munisi akimwamuru dereva ashushe kioo lakini alikataa na kudai kwamba ndipo alipoamua kuwapiga risasi waliokuwamo kwenye gari hilo.
 MWANANCHI

MFANYA BIASHARA AUA WATU 2 KISHA NAE KUJIUA

Mapema leo asubuhi milio ya risasi zaidi ya kumi ilisikika eneo la Ilala

Bungoni karibu na baa maarufu ya Wazee (Club ya Wazee), watu watatuwakiripotiwa kufariki kutokana na tukio hilo linaloelezwa kuwa limetokana na wivu wa kimapenzi.

 
Dereva mmoja wa tax kituo cha Bungoni ambaye alikuwa shuhuda wa kwanza, alisema mapema leo asubuhi alipata mteja aliyehitaji kupelekwa sehemu, ila kabla hawajafika huko walipokuwa wanataka kwenda jamaa ambaye ndiye alikuwa ni muuwaji alimuomba akatishe safari na kumtaka ampeleke sehemu
nyingine.(P.T).         
                                                                               Dereva huyo aliendelea kusimulia kuwa alimpeleka jamaa mpaka eneo la tukio hilo kwenye nyumba iliyopo pembeni mwa Hotel mpya iitwayo MM.


Mara baada ya kufika hapo, jamaa alitoa sh. 5,000 na kumkabidhi dereva ila cha kushangaza ni kitendo cha jamaa huyo kutoa bastola wakati akiwa anaelekea kwenye geti la nyumba. 


Wakati jamaa anaelekea getini mlango ulifunguliwa na gari aina ya Toyota Surf ilitoka ikiwa na watu wanne ndani, mwanaume mmoja ambaye alikuwa akiendesha gari , mama mmoja na wadada wawili. 


Jamaa akiwa na bastola alianza kuwashambulia watu waliokuwa ndani ya gari hilo na kumpiga risasi dereva na mdada mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Carol.Baada ya dreva tax kuona hali imechafuka ilimbidi akimbie. 


Vyanzo vingine vinaeleza kuwa katika tukio hilo jamaa pia alimpiga risasi ya mgongoni mama wa mwanamke aliyemuua na pia alimpiga msichana mwingine risasi ya mguu. 


Mtuhumiwa na dereva aliyekuwa akiendesha gari walifariki palepale huku msichana mmoja akielezwa kufariki akiwa njiani kuelekea hospitali.


Bado haijafahamika moja kwa moja chanzo cha mauaji hayo licha ya watu wengi kudai kuwa ni wivu mapenzi

MADIWANI WALIOFUKUZWA CHADEMA ARUSHA BADO WAANDAMWA.


picha ni kutoka maktaba ya BERTHA BLOG
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Arusha, kimewafungulia mashtaka mengine ya madai madiwani wake watano waliofukuzwa uanachama mwaka juzi na kuwataka walipe Sh35 milioni ikiwa ni gharama za usumbufu.
Kesi hiyo ilifunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kwa Msajili wa Mahakama hiyo. Kwa mara ya kwanza kesi hiyo ilitajwa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Hii ni kesi ya pili kufunguliwa na Chadema dhidi ya madiwani hao.
Novemba mwaka jana, Mahakama Kuu Kanda ya Arusha mbele ya Hakimu Charles Magesa ilitoa hukumu ya kuwataka walipe Sh15 milioni ikiwa ni gharama za usumbufu wa kuondoa shauri lao mahakamani kupinga kufukuzwa katika chama hicho.
Katika kesi iliyofunguliwa hivi karibuni kwenye mahakama hiyo, iligawanywa mara mbili; Dai la kwanza ni Sh20 milioni na dai la pili ni Sh15 milioni.
Chama hicho katika kesi hiyo nambari 34 na 35 ya mwaka 2013, pia imefungua madai dhidi ya madiwani hao na kuwataka wakilipe kwa madai kuondoa shauri walilofungua dhidi ya chama hicho mahakamani hapo kwa kupinga kufukuzwa sanjari na kuomba kupunguziwa kiwango cha fedha walichopaswa kulipa mahakamani hapo.
Madiwani waliofukuzwa ni Estomih Mallah, Rehema Mohammed, John Bayo na Ruben Ngowi wanaowakilishwa na Wakili Gwakisa Sambo.
Wadaiwa hao walihudhuria kusikilizwa shauri hilo, lakini Charles Mpanda hakuonekana mahakamani hapo na kesi hiyo itatajwa tena Desemba 4 mwaka huu.
Chadema kiliwafukuza madiwani hao kikiwatuhumu kukisaliti baada ya kuingia makubaliano ya kugawana madaraka na CCM, kuongoza Manispaa ya Arusha.
Uongozi wa chama hicho ulipinga mchakato wa kumpata Meya wa Jiji la Arusha, Gaudence Lyimo kikidai haukuwa halali na haki. Madiwani hao bila ridhaa ya chama chao walikubaliana na CCM kugawana madaraka, lengo likiwa ni kuondoa mgogoro uliosababisha na matokeo hayo.

Hata hivyo, walikwenda mahakamani kupinga kufukuzwa uanachama, lakini walishindwa na uchaguzi uliporudiwa Chadema ilishinda.

Monday, November 18, 2013

CHAWAKI WAIBUA SHUTUMA NZITO KWA VIONGOZI WA CCM NA HALMASHAURI

Na, Bertha Ismail-Kiteto

CHAMA cha Wakulima na Wafugaji wilayani Kiteto mkoani Manyara(CHAWAKI) kimeibua shutuma dhidi ya viongozi wa CCM wilaya na mkoa wa Kiteto Mkoani Manyara.

Aidha pia Baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya hiyo inayoongozwa na mwenyekiti wa chama hicho tawala limelezwa kuwa chanzo cha mgogoro katika eneo linalodaiwa kuwa la hifadhi ya Jamii ya Emborley Murtangos kwa kujenga mfumo wa matabaka yanayosababisha kuwepo kwa mapigano kati ya jamii ya wakulima dhidi ya wafugaji.

Mfumo huo wa matabaka umedaiwa kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoani hapa Lucas Kasmir Ole Mukus kwa kudaiwa kuchangisha  fedha kwa wafugaji  kwa ajili ya kukusanya kiasi cha shilingi 150,000,000/= ili kuwezesha kuendesha operesheni ya kuwaondoa wakulima na kuwaacha wafugaji katika eneo hilo hali iliyoleta mtafaruku baina ya viongozi hao, wafugaji na wakulima.

Hata hivyo ili kuthibitisha hivyo, CHAWAKI  kinaeleza kuwa katika operesheni iliyobarikiwa na viongozi hao kupitia vikao vya kimila vinavyopigiwa chapuo na mwenyekiti wa CCM mkoa kwa  kuhamasisha  wafugaji ambao wengi wao ni wamasai kuchanga ngombe kwa madai ya kuwatoa wakulima kwa kuwaita wavamizi  ili kuwabakiza wafugaji pekee katika hifadhi hiyo.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara  wa kufunga ziara yake, mjumbe wa halmashauri kuu-Taifa(M-NEC) Emmanuel John Papian uliofanyika kwenye kijiji cha Engusero mbele ya ,mwenyekiti wa CHAWAKI Hassani Loosiok anaeleza kuwa mfumo huo wa matabaka ya ukabila unaojengwa na viongozi hao endapo hautadhibitiwa eneo hilo halitakuwa na amani kamwe.

“Hii ishu ya hifadhi imeshakuwa hot cake...Tatizo linaloonekana hapa kwanza kuna tatizo la tafsiri ya hukumu ya hifadhi ya emborley murtangos,hukumu ilielekeza haimhitaji mkulima ama mfugaji kufanya shughuli zake katika eneo hilo la hifadhi,lakini  nimebaini kuwa hakuna mkutano mikuu ya vijiji saba vilivyofanya uamuzi wa kupatikana kwa hifadhi ya emborley murtangs kama inavyotajwa hali inayoonyesha kuwa viongozi wanaochochea mgogoro huo wana maslahi na hifadhi hiyo bubu” alisema Losiok.

Aliwataka viongozi kuchukua jukumu la kuhakikisha kuwa wanadumisha uhusiano mzuri kati ya pande zote mbili kutokana na ukweli kuwa hali hiyo ya jamii ya wafugaji imekuwa ikitumika kupitia mikutano ya kimila inayohudhuriwa na viongozi hao kuchangisha fedha za kuondolewa kwa wakulima  kitendo ambacho kitaendelea kusababisha machafuko makubwa kwa kuwa tabaka la wafugaji limekuwa likibebwa na viongozi hao na hii inatokana na kuwa wengi wa viongozi hao ni wamasai ambao nao ni wafugaji na wana ngombe wanaolishwa  katika hifadhi hiyo.

“Hali hii inajenga taswira ya chuki baina ya wakulima na wafugaji…,nimesoma barua ya mkurugenzi kwa niaba ya RC inayowataka wenyeviti, watendaji vijiji,kata na tarafa ya kuwaondoa wafugaji na wakulima lakini hawa jamaa wanawatoa wakulima pekee hali itakayo sababisha vita baina ya wakuma na wafugaji ambapo mbeleni wafugaji wataleta fujo isiyoisha baina yao na serikali kwa kuchukua fedha zao kwa kuwalaghai.

Alisema kulingana na taswira ya eneo hilo kwa kipindi chote hicho cha mgogoro huo halmashauri licha ya kuwaondoa wakulima kwa kuvunja makazi yao, tangu mwaka 2002, eneo hilo halikuwa  limesajiliwa kama hifadhi bali ndio limesajiliwa  Oktoba 25 mwaka huu chini ya wizara ya Mambo ya ndani kitengo cha usajili wa vyama vya siasa badala ya wizara ya maliasili na utalii, huku CHAWAKI wakisajili Oktoba 7 kupitia wizara ya Mali Asili na Utalii.

Msemaji wa CHAWAKI Hassan Loosiok alisema mbele ya M-NEC huyo kuwa baraza la Madiwani la halmashauri hiyo limekuwa likishiriki kupotosha pamoja na kupuuza maamuzi ya wananchi wa vijiji kwani eneo hilo lilitengwa na wananchi wa vijiji saba kama eneo la hifadhi ya jamii na sio hifadhi ya Emborley  Murtangos huku vijiji vitano  vikiendesha mikutano mikuu na kuamua kujitoa kwenye mpango wa hifadhi wa Emborley murtangos.

“Sasa sisi tunasema sehemu ya kushtakia ni hapa CCM ambacho ndicho chama wanachokitumikia kuwa ifikie mahali muwaambie waheshimiwa madiwani waheshimu maamuzi ya wananchi wasifanye mambo kwa matakwa binafsi..,M-nec tunao ushahidi wa vijiji vitano kujitoa kwenye mpango wa  hifadhi hiyo na hili litakuthibitishia kuwa CCM haina madiwani watetezi wa wananchi bali ni madiwani wanaotetea maslahi yao binafsi.

Alivitaja vijiji vilivyojitoa kwenye mpango huu kuwa ni Nati,Emarit,Engusero-Sidani,Kimana na Lotepes,huku vijiji vya Namelok na Ndiligishi vikiwa bado havijafanya mikutano mikuu ya vijiji.

Hata hivyo  kulingana na halmashauri kusajili eneo hilo kupitia kitengo cha vyama ya siasa Loosiok alisisitiza kuwa ,madiwani hao hawana mamlaka ya kumiliki ardhi ama mamlaka ya kutumia dola  kuwaondoa wakulima na wafugaji kwa mujibu wa sheria Na 5/1999 kwa kuwa ardhi hiyo ni mali ya kijiji na sio mali ya halmashauri ya wilaya hiyo.

Mbali na hali hiyo  alikwenda mbali kwa kumtupia lawama mwenyekiti wa CCM mkoani hapa Lucas Ole Mukus kwa kumtuhumu  kuendesha vikao vya mila vyenye lengo la kukusanya fedha hizo ,huku na baadhi vikimshirikisha mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo bi Jane Mutagurwa aliyeandika barua  Kumb:Na,HMW/KT/E/09/VOL II/13 ya Novembe 5,2012 kwa wenyekiti wa Mila wa vijiji 31 kuchangisha fedha za kuwaondoa wavamizi.

Akipokea malalamiko hayo mjumbe wa halmashauri kuu Emmanuel John Papian alisema kulingana na mwenendo mzima wa mgogoro huo amebaini baada ya kutembelea kata zote za halmashauri ya wilaya hiyo kuwa mgogoro huo umengiliwa na ukabila,siasa za viongozi ambao hawaweze kutoa Haki na Usawa kwa kuwa baadhi yao ni wadau.

Kulingana na ugumu wa kufikia muafaka wa mgogoro huo,Papian alisisitiza kuwa CCM itakachofanya ni kuhakikisha wanataraji kupeleka ombi hilo kwa waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda kutatua mgogoro huo kwa kuwa hakuna njia nyingine ya kufikia muafaka ispokuwa yeye tu.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mainge Lemalali alikiri kuendeshwa kwa zoezi hilo la ukusanyaji wa fedha ambap alisema lililenga kujenga shule na pia fedha nyingine zikielekezwa kulipia deni la kesi walizonazo juu ya hifadhi hiyo juu ya kuwatoa wakulima ,huku mwenyekiti wa CCM mkoani hapa Lucas Ole Mukus akieleza vikao vya kimila vililenga kuhimiza kuchangia mfuko wa elimu na kutaka kuwapuuza wanaomshtumu.
MWISHO


MASHINE ZA KIETRONIKI (EFD) ZINA HARUFU ZA KIUFISADI, ZASABABISHA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUFUNGA MADUKA JIJINI DAR ES SALAAM.

Makaduka yakiwa yamefungwa katika Mtaa wa Kongo jijini Dar es Salaama jana kutokana na wafanyabiasha kugoma ili kushinikiza  Mamlaka ya Mapato  kusitisha matumizi ya mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFD). PICHA|SALIM SHAO.
DAR ES SALAAM. 
WAFANYAKAZI wa Kariakoo jijini Dar es Salaam jana walifunga maduka yao kupinga utaratibu mpya wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wa kutoza kodi kwa kutumia mashine za elektroniki (EFD).

Wafanyabiashara walifanya mgomo huo ili kushinikiza kuonana na ama Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa au Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda.
Wanadai kuwa mashine hizo za EFD zinauzwa bei ghali ya kati ya Sh800,000 hadi Sh1.2 milioni, gharama ya kuzifanyia matengenezo zinapopata hitilafu ni kubwa na pia wanadai kuwa kuna harufu wa ufisadi kwenye suala hizo kwa kuwa ni kampuni chache zilizochaguliwa kuuza mashine hizo.
Maduka karibu yote hayakufunguliwa tangu alfajiri tofauti na ilivyozoeleka na hata wafanyabiashara wachache waliojaribu kufanya hivyo walilazimika kuyafunga kwa hofu ya kufanyiwa vurugu na wenzao.
Baadhi ya maduka ya vifaa vya umeme, magodoro na friji yaliyopo Mtaa wa Uhuru yalikuwa wazi lakini baada ya muda mfupi yalifungwa.
Hata hivyo, maduka yaliyoko kwenye Soko Kuu la Kariakoo yalikuwa wazi muda wote.
Mgomo huo ulianza baada ya wafanyabiashara hao kupeana taarifa wakihamasishana kutokufungua maduka yao kushinikiza kusikitishwa kwa matumizi ya mashine hizo za kukokotoa kodi.
Msimamo wa Serikali.
Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya alisema mgomo wa wafanyabiashara wa Kariakoo hauwezi kubadili msimamo wa Serikali wa kukusanya kodi kwa kutumia mashine za EFD. Alisema suala la bei haliwezi kuwa kigezo cha kugoma kwa kuwa baada ya kununua fedha zao zitarejeshwa kidogokidogo kwenye marejesho ya kodi.
“Changamoto iliyopo ni kwamba wafanyabiashara wengi hawajui kama fedha hizo wanazonunulia mashine watarejeshewa kwenye makato ya kodi. Hatuwezi kuzibadilisha mashine hizo kwa kuwa siyo kama simu za mkononi, zimetengenezwa kwa mfumo maalumu wa TRA,” alisema.
Aliitaka TRA kuwaelimisha wafanyabiashara kuhusu manufaa ya kutumia mashine hizo.
TRA yakaza uzi. 
MWANANCHI