Pages

Pages

Monday, February 17, 2014

LULU AKIRI MAPENZI NA KANUMBA

Dar es Salaam.
 Mwigizaji maarufu wa filamu nchini, Elizabeth Michael Kimemeta, amekiri mahakamani kuwa na uhusiano wa kimapenzi na aliyekuwa mwigizaji mwenzake, Steven Kanumba na pia kuwa ugomvi na Kanumba siku ya tukio la kifo cha mwigizaji huyo, lakini akakana mashtaka ya kumuua bila kukusudia.
Lulu ambaye yuko nje kwa dhamana anakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, akidaiwa kumuua Kanumba bila kukusudia, kinyume cha Kifungu cha 195 cha Kanuni za Adhabu (PC), April 7, 2012, nyumbani kwa marehemu Kanumba, Sinza Vatican.
Jana Lulu alipandishwa kizimbani mahakamani hapo na kujibu mashtaka hayo kwa mara ya kwanza tangu alipofunguliwa kesi hiyo, ambapo alikana kumuua Kanumba bila kukusudia.Kesi hiyo namba 125 ya mwaka 2012 inasikilizwa na Jaji Rose Teemba.
Kukubali kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Kanumba, ni miongoni mwa mambo manane ambayo mshtakiwa huyo aliyakiri mahakamani hapo jana, kama mambo yasiyobishaniwa katika kesi hiyo.
Mambo mengine ambayo Lulu aliyakiri mahakamani hapo yaliyoko katika maelezo ya kesi hiyo ni pamoja na jina na anuani yake, kwenda nyumbani kwa Kanumba usiku wa tukio hilo, kuwa na ugomvi na Kanumba pia Kanumba kumzuia kutoka nje ya chumba alipojaribu kutoka ili akimbie.
Mengine ni kufanikiwa kutoka nje ya chumba cha Marehemu Kanumba, kumweleza mdogo wa Kanumba (Seth Bosco) kuwa Kanumba ameanguka, kukamatwa kwake na polisi eneo la Bamaga, saa 11 Alfajiri ya usiku wa tukio hilo na kwamba kweli anashtakiwa kwa kosa la kumuua Kanumba bila kukusudia.
Kama jana Lulu angekiri mashtaka hayo baada ya kusomewa, basi mahakama ingemtia hatiani na kumhukumu adhabu ambayo ingeona inafaa kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo, baada ya kukana mashtaka hayo, sasa kesi hiyo itaingia katika hatua nyingine ya usikilizwaji kamili (trial), ambapo upande wa mashtaka utalazmika kuwaita mashahidi wake mahakamani ili kuthibitisha kuwa Lulu alimuua Kanumba bila kukusudia.
Pia Lulu atalazimika kujitetea yeye binafsi na pia kuwaita mahakamani mashahidi wa kumtetea na kisha mahakama itaandaa na kutoa hukumu yake.
Wakili wa Serikali, Mbogo aliiarifu mahakama kuwa wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo, upande wa mashtaka utakuwa na mashahidi wanne ambao ni pamoja na Seth Bosco, Daktari binafsi aliyekuwa akimhudumia Kanumba, Dk Paplas Kageiya, Ester Zephania na Askari D/Sgt Ernatus wa Kituo cha Polisi Oysterbay.
Pia Wakili Mbogo aliwasilisha mahakamani vielelezo viwili vitakayotumika kama sehemu ya ushahidi katika kesi hiyo ambayo ni taarifa ya kitabibu ya uchunguzi wa chanzo cha kifo cha Kanumba na ramani ya eneo la tukio.
Lulu kwa upande wake, mawakili wake Peter Kibatala na Fulgence Massawe waliiarifu Mahakama kuwa wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo kwenye utetezi watakuwa na mashahidi watano na vielelezo viwili. Hata hivyo hawakutaja majina ya mashahidi hao.

Sunday, February 16, 2014

TEMBO WAENDELEA KUTEKETEA TANZANIA, JESHI LA POLISI SINGIDA, MTWARA YAWASHIKILIA WATU WANNE BAADA YA KUWAKAMATA NA KILO 130 ZA MENO YA TEMBO.



Photo: African elephant TEMBO AKIONYESHA ISHARA YA HATARI KWAKE.

Meno ya Tembo yanayosakwa na wafanyabiashara wakubwa huku soko lake likitajwa kuwa nchini China.

SINGIDA/MTWARA.

IKIWA ni muda mfupi baada ya Rais Jakaya Kikwete kukiri kuwa vita dhidi ya ujangili ni tatizo sugu linaloielemea Tanzania, Jeshi la Polisi mkoani Mtwara na Singida linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kukutwa wakisafirisha nyara za Serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Maisha Maganga alisema kuwa jeshi hilo limewakamata watu watatu wakiwa na meno ya tembo 58 yenye uzito wa kilogramu 130.6 yenye thamani ya Sh700.3 milioni.


Kamanda alieleza kuwa watuhumiwa hao walikamatwa saa 11:00 alfajiri katika Kijiji cha Chungu Kata ya Nanyumbu, Wilaya ya Nanyumbu Mkoa wa Mtwara wakiwa katika kizuizi cha barabara ya Mtambaswala – Mangaka wakielekea jijini Dar es Salaama.


“Tunawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kupatikana na nyara za Serikali ambazo ni meno ya tembo 58 yenye uzito wa kilogramu 130.6 na thamani ya 700.3 milioni, ambapo ni sawa na tembo 29 waliouawa yakiwa ndani ya gari aina ya Toyota Land Cruiser,” alisema Kamanda Manganga.


Alisema mbinu waliyotumia watuhumiwa hao ni kukata sakafu ya gari ya chini ya kiti cha nyuma ya dereva na kutengeneza tanki la bandia na kuweka meno hayo kisha kuweka kapeti juu yake.


Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Hamidu Ngunde (40) dereva, Geraldat Lukas (36) dereva na Boniphace Kosan (29) wote wakazi wa jijini Dar es Salaam na kusema kuwa gari iliyotumika kusafirisha meno hayo ni mali ya Hilali Rashid.


Wakati huo huo, Kamanda wa polisi Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela, alisema wamefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja, Februari 13 mwaka huu saa 2.30 asubuhi katika kizuizi cha Mazaoa ya Misitu na Chakula kilichopo katika Kijiji cha Ukimbu Kata ya Mgandu, tarafa ya Itigi, Wilaya ya Manyoni.


Alisema mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia gari aina ya Toyota lenye namba T.797 CQL kusafirisha nyara za Serikali kutoka Kijiji cha Mwamangembe kwenda Itigi Mjini.


“Nyara alizokamatwa nazo mtuhumiwa zilikuwa zimewekwa kwenye mabegi mbalimbali ya nguo,” alifafanua. Kamwela alisema uchunguzi wa awali, umeonyesha kuwa vipande hivyo 21 vinakadiriwa kuwa vya tembo wanne, vina uzito wa kilogramu 49 na thamani ya Sh43.1 milioni. MWANANCHI.

WAFANYABIASHARA WAMJIA JUU RAIS JAKAYA KIKWETE, WAMTAKA KUTAJA MAJINA YA VINARA WA UJANGILI NCHINI.


Rais Jakaya Kikwete.
 
BAADHI ya wafanyabiashara wa mikoa ya Kaskazini pamoja na kumpongeza  Rais Jakaya  Kikwete, lakini wamemtaka awataje mapapa 40 wa ujangili aliobainisha Jijini London, kwani ndiye Amiri Jeshi Mkuu na hakuna kitu kilicho na mamlaka juu yake.

Walisema alipokabidhiwa uongozi aliapa kuilinda na kuitetea katiba ya Tanzania pamoja na kuhakikisha ustawi wa raia  na rasilimali za taifa.https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjUM_ENVa3lBHi8jAzFmYex8G9fPkUfQH-afws67IJILgyTA_M90844xEmR7OMnAOqoz15HfPB2t_X-2i955nkcQ_JG5Bjh2AkZiDWVgGb1HkI6LPApAAvqd99xv4AOc_j8AGvBpy7SxX32/s1600/1_kenya_elephant_mountain_bull_FB_620x465.jpg
Walitoa maoni hayo walipozungumza na NIPASHE kuhusu  kauli yake Jijini London wakati wa  mkutano ya wanyamapori na kwenye mahojiano maalumu na televisheni ya CNN ya  Marekani  na Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC.
 
Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Wakulima (TTCCIA) mkoa wa Kilimanjaro, Patrice Boysafi, akizungumzia maelezo ya Rais alisema :
 
“Yeye ni mlinzi mkuu wa katiba, watu na rasilimali za nchi hii yakiwamo meno ya tembo, alitakiwa aamuru  mapapa wa ujangili wakamatwe na kufikishwa mahakamani”.
 
Alisema Rais yuko juu ya mamlaka yote ndiye  Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, hivyo hana na sababu ya kumuogopa mtu anatakiwa ataje watuhumiwa hao wanaofahamika kuwa ni waharibifu wa mali za umma.
 
“Ni kiongozi mkuu ana mamlaka nikisikia  amesema anawajua mapapa wa ujangili tulitegemea  atoe amri  ya kuwakamata na kuwashitaki maana ndiye Amiri Jeshi Mkuu, hana cha kuficha wala kuhofia,” alisema Boysafi.
Alihoji  kama wanafahamika kwa nini hadi sasa mtandao haujavunjwa? Ni nini kinakwamisha kama wanafahamika?
 
 Boysafi alisisitiza kuwa  kuwa wanajulikana, idadi yao pamoja na viongozi wao, hivyo Rais alitakiwa kutoa maagizo kwenye vyombo vya dola ili washughulikiwe  siyo katika televisheni wala redio za kigeni au kwenye majukwaa ya jumuiya ya kimataifa. 
 
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TTCIA Arusha Adolf Ulomi, alisema  wanatarajia  kuona hatua zikichukuliwa baada ya Rais kueleza kuwa wafanyabiashara hiyo wanafahamika.
 
Alisema kwa kuwa watuhumiwa wanajulikana na kiongozi wao yuko Arusha, wanategemea kuona polisi na vyombo vya dola vikichukua hatua ya kuwakamata , kushtakiwa, kuvunja mtandao na kukomesha ujangili.
 
Kwa mujibu wa Ulomi, kama jambo linafahamika ni wazi wana usalama wako porini wanawatafuta majangili hao na wanachotaka ni  wakamatwe na washtakiwe.
 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCIA Mkoa wa Kilimanjaro, Boniface Maliki, akizungumzia kadhia hiyo ya ujangili alisema,  Rais alitoa taarifa hizo baada ya gazeti la Daily Mail la London kuripoti ujangili, lakini hakuwahi kuzizungumza humu nchini.
 
Alisema inaelezwa kuwa vigogo wa biashara hiyo wako Arusha lakini habari zinafahamika baada Daily Mail kuishambulia Tanzania…  kwanini taarifa  hazikuwahi  kutolewa kabla? Na kuuliza mbona  maelezo hayakupatikana akiwa nchini?
 
Alisema wafanyabiashara wanataka kuona ushahidi wa mambo yaliyozungumzwa London ukibainisha watuhumiwa na hatua zikichukuliwa dhidi ya majangili waliochafua sifa ya taifa.
 
Kuhusu kuomba msaada jumuiya ya kimataifa, walisema si jambo baya lakini kwa vile walilenga kupata  vifaa vya kisasa na vyenye  teknolojia  ni jambo jema.
 
Kwa upande wa utendaji, alisema hakuna haja ya kuomba msaada nje kwa kuwa wapo watendaji wanaoweza kukamilisha operesheni za ulinzi wa wanyamapori kinachotakiwa ni utashi wa kisiasa.
 
Wafanyabiashara  wengine  walimpongeza Rais Jakaya Kikwete,  kwa kugundua mtandao wa  majangili 40, wakiongozwa na kinara aliyeko mkoani Arusha na kushauri akamatwe bila kujali.
 
Diwani wa Kata ya Mererani, Justiny Nyari , ambaye pia ni mfanyabiashara wa madini, alimpongeza Rais kwa jitihada za kufuatilia na kugundua mtandao  huo.
 
Alisema  Rais anastahili pongezi kwa sababu bila kufuatilia huwezi kugundua mtandao huo na kueleza kuwa maelezo hayo ni kweli kwa vile ni Rais Kikwete ana mamlaka makubwa ya  nchi.
 
Mfanyabiashara  mwingine Aisha Juma, anayemiliki  duka la nguo na viatu jijini Arusha, alisema kauli ya Rais  ni nzito hivyo kinachotakiwa ni mtuhumiwa awe amejulikana , kukamatwa na kuchukuliwa hatua.
 
Alimpongeza Rais kwa kugundua mtandao huo na kutaka mtuhumiwa namba moja akamatwe na ajulikane  ili umma umtambue na sio kuzungumza  na kuacha suala hilo kuishia hewani. CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Friday, February 14, 2014

baadhi ya majengo ya chuo cha polisi (CCP) yaungua kwa moto



Hakuna mtu aliyeripotiwa kudhurika na Mkuu wa Chuo hicho Kamishana Msaidizi wa Polisi Matanga Mbushi ameahidi kutoa taarifa kamili baadaye.
 



Askari wanafunzi wakipambana na moto kwa kila jinsi.

Mapambano na moto yanaendelea

Baadhi ya vitu vikiokolewa kutoka katika jengo lililowaka moto.

Juhudi za kuondoa vifaa vilivyookolewa kabla ya kuteketea kwa moto

Wanafunzi wakipambana na moto






Sare za askari zikiwa zimeokolewa toka katika jengo hilo.

Moja ya kifaa kilichopo chuoni hapo ambacho pia kilikuwa kikitumika kwa shughuli za kuzima moto katika jengo hilo .Mkuu wa chuo hicho Matanga Mbushi amesema taarifa kamili ya moto huo itatolewa baadae.


Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz akiwa na mkuu wa Chuo cha taaluma ya Polisi kamishana msaidizi wa polisi Matanga Mbushi wakishuhudia zoezi la uzimaji moto katika jengo hilo.




CHANZO MATUKIO ISSA MICHUZI

Wednesday, February 12, 2014

HILI NI TAMKO LA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (TRA) JUU YA MGOMO WA WAFANYABIASHARA NCHINI

 
ISO 9001: 2008 CERTIFIED
 
TAARIFA KWA UMMA
Mamalaka ya Mapato Tanzania inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania na wafanyabiashara kwa ujumla Kuwa inasikitishwa  na mgomo wa wafanyabishara kwa kufunga maduka maeneo mbali mbali nchini.
 
Ifahamike kuwa Matumizi ya mashine ya EFD ni jambo la kisheria  na lilipitishwa na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2011.
 
Pamoja na sheria kupitishwa, viongozi wakuu wa nchi walikwisha litolea tamko kwa nyakati tofauti kwa kuanzia na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete katika hotuba yake ya kufunga mwezi wa Machi 2011.
 
Pia Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohammed Gharib Billal alikazia jambo hili tarehe 8 Mwezi November mwaka 2013.
 
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mhe. Mizengo Peter Pinda alilitolea tamko pia Mwezi Desemba 2013  wakati akiahirisha Bunge kwa kusisitiza msimamo wa serikali kwa utekelezaji wa kisheria wa matumizi wa mashine za EFD.
 
Tarehe 29 Janauri 2014, Waziri wa Fedha Mhe Saada Mkuya Salum aliweka bayana msimamo wa Serikali kwa kusisitiza kuwa Matumizi ya mashine za EFD ni swala la kisheria na litaendelea kutekelezwa kwa mujibu wa sheria akisisitiza kuwa muda wa mwisho wa nyongeza kwa wafanyabishara kununua mashine ilikuwa ni Tarehe 31 Januari 2014 baada ya kuongeza muda mara tatu kwa nyakati tofuati.
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pia kwa nyakati tofauti na maeneo  tofuati imelitolea tamko jambo hili na itaendelea kufanya hivyo.
 
Kwa masuala ya kiutendaji yaliyolalamikiwa yamefanyiwa kazi na yanaendelea   kufanyiwa kazi ikiwemo utoaji wa Elimu kwa umma.
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania  inapenda kuwafahamisha wafanyabiashara na umma kwa ujumla kuwa watu wanaolazimisha wafanyabishara wenzao kufunga maduka kwa kuwatishia na  kuwashurutisha wanavunja sheria kwa kusababisha uvunjifu wa amani nchini na hivyo mkono wa sheria utawafikia. Pia imefahamika kuwa baadhi ya watu wanaoshurutishwa kufunga biashara sio walengwa bali hutumika kuhalalisha azma ya wale wenye nia mbaya.
 
TRA imekuwa ikipokea taarifa na maombi kutoka kwa baadhi ya wafanyabishara na wananchi wema wakiomba ulinzi ili wafungue maduka yao na kufanya biashara maana ndio ajira yao na mahali pakujipatia riziki ya kila siku.
 
Ifahamike kwamba wale wote wanaoshinikiza na kulazimisha wenzao kugoma wanavunja sheria kwa kuwalazimishwa wafanyabiashara kugomea agizo halali la kisheria hivyo kwa wale wote wanaotishiwa au kushurutiswa watoe taarifa kwa  kupiga simu namba zifuatazo 0786 800 000, 0713 800333, 0800 110016 au barua pepe info@tra.go.tz
 
“PAMOJA TUNAJENGA TAIFA LETU”
IMETOLEWA NA KAIMU KAMISHNA MKUU
MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA
                                                                                     chanzo: jumamtanda blog

Monday, February 3, 2014

NCHIMBI: TUMEKUBALI KUWAJIBIKA KWA MAKOSA YALIYOFANYWA NA POLISI

“Baada ya kuonekana raia wamefariki kukatokea ushawishi wa kutaka baadhi ya watu wabebe dhamana ya askari ambao walionekana hawajatekeleza majukumu yao inavyotakiwa.” Nchimbi.


ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi amesema yeye pamoja na mawaziri wenzake watatu walikubali kuwajibika kutokana na makosa yaliyofanywa na askari waliokuwa wakitekeleza Operesheni Tokomeza Ujangili.


Dk Nchimbi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini (CCM), alisema kuna uhalifu wa hali ya juu katika mbuga za wanyama, ambao baada ya miaka 10 unaweza kumaliza wanyama kwenye mbuga hizo.


Akizungumza na wakazi wa Manispaa ya Songea kwenye Viwanja vya Kiblang’oma, Kata ya Lizaboni Songea katika kilele cha maadhimisho ya miaka 37 ya CCM, alisema Serikali ilifanya uamuzi wa kuwasaka majangili na kuwatokomeza.


Alisema katika operesheni hiyo, wananchi wapatao 11 na askari sita waliuawa jambo lililosababisha matatizo makubwa...


“Baada ya kuonekana raia wamefariki kukatokea ushawishi wa kutaka baadhi ya watu wabebe dhamana ya askari ambao walionekana hawajatekeleza majukumu yao inavyotakiwa.”


Alisema yeye na wenzake waliwajibika baada ya kutafakari kazi inayofanywa na askari katika nchi hii kwani wanalala usiku na kung’atwa na mbu kwa ajili ya wananchi, pia wanapambana na majambazi na hata kupoteza maisha wakati mwingine wakati wakilinda raia.


Hata hivyo, alimshukuru Rais Kikwete kwa kumpa heshima kubwa ya kumsaidia katika kipindi cha miaka minane na kuwatoa hofu watu wa Songea kwa kuwahakikishia kuwa kasi ya maendeleo katika jimbo lake haitapungua.


Uteuzi wa Dk Nchimbi na mawaziri wengine Khamisi Kagasheki (Maliasili na Utalii), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) na Dk David Mathayo (Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi) ulitenguliwa mwishoni mwa mwaka jana baada ya malalamiko ya wabunge kutokana na matatizo yaliyojitokeza kwenye Operesheni Tokomeza.

Ally Bananga Ang’ara Mkutano wa Kamepeni Chadema Kata ya Sombetini hii leo huku Lema akizidi Kukemea chuki za Udini na Ukabila

Lema na Bananga
Mbunge wa Arusha Mjini ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu Chadema, Mh Godbless Lema akimpa wosia mgombea wa chama hicho katika kinyang’anyiro cha kuwania udiwani Kata ya Sombetini katika mkutano mkubwa uliofanyika hii leo katika viwanja vya Mbauda Sokoni.
umatiSehemu ya umati wa wananchi waliohudhuria mkutano huo
Sombetini
Lema jukwwaniLema akiwa jukwaani
BanangaMh Godbless lema akimnadi mgombea wa Chadema kata ya Sombetini, Kamanda Ally Bananga
KishoaKamanda wa Chadema kutoka Iramba, mwanadada Jesca Kishoa akitambulishwa jukwaani na Mh Lema katika mkutano huo
Kishoa
Alipopata fursa ya kuzungumza, Bi Jesca Kishoa aliielezea na kuisifu Arusha na watu wake ni chachu ya mabadiliko nchini na kwamba hata historia ya nchi inaeleza hivyo. Akasisitiza zaidi na kusema kwamba kama kuna mtu anapingana na upepo huu wa mabadiliko atakuwa ni sawa na abiria wa ndege kaachwa na ndege sasa anakodisha baiskeli ili akimbize ndege, jambo ambalo halitamuwezesha kuiwahi ndege, sawasawa  na ambavyo alidai mabadiliko hayazuiliki.
DSC_0063“Amsha amsha” ya nyumba kwa nyumba, gari kwa gari, mtaa kwa mtaa ikiongozwa na Mh Lema sambamba na mgombea Bananga wakikatiza mitaa ya Mbauda
DSC_0067Maandamano kuelekea ilipo ngome ya Chadema eneo la Ngusero, Sombetini
DSC_0077Mbunge wa Arusha Mjini na viongozi wengine wakiserebuka nyimbo za hamasa zilizokuwa zinapigwa katika ngome yao Sombetini jioni ya leo