Pages

Pages

Friday, April 24, 2015

wadau wasusa uongozi ADFA

Bertha Ismail – Arusha

Kamati huru ya uchaguzi wa uongozi mpya wa chama cha soka wilaya ya Arusha,  imefunga Rasmi pazia la uchukuaji fom wa kugombea nafasi mbali mbali katika chama hicho.



Zoezi la uchukuaji fom wa kugombea uongozi wa ADFA, ulianza rasmi April 15 na kufungwa mapema jana april 20 ambapo wadau wengi wa soka wameonekana kuogopa nafasi hizo zilizoachwa wazi na kupelekea idadi ndogo ya wagombea huku nafasi zingine zikikosa wagombea.



Awali wadau wengi jijini Arusha walionekana kutolea macho viti hivyo kabla tarehe ya uchaguzi kuanza lakini baada ya tarehe ya uchaguzi kutangazwa wengi wameonekana kukaa nyuma kutazama wachuaji fom bila kujishughulisha.



Akizungumza na gazeti hili, katibu wa kamati huru ya uchaguzi, Hussein Lembarity alisema kuwa nafasi zilizo wazi ni nafasi 10 ambazo kila mmoja ingefaa kuwa na wagombea watatu hadi watano lakini ambao ni zaidi ya watu 30 lakini anashangazwa na watu waliojitokeza ni watu 10 tu huku baadhi ya nafasi zikigombewa na mtu mmoja au wawili na zingine zikikosa kabisa wagombea.



“Mwanzo tulipochgauliwa tu watu wengi sana walijitokeza kuponda uongozi uliopo na kuahidi kuchukua fom za kupindua uongozi huu lakini baada ya kuanza kutoa fom watu wanachenga hali iliyopelekea nafasi zingine kukosa wagombea huku zingine zikiwa na mashaka ya kupita ila kwa sababu tumefunga pazia hilo hatuna budi kukubali matokeo na sasa ni nafasi ya kuweka pingamizi hadi april 24 kwa gharama ya 50,000”



Akitaja majina ya wagombea hao alisema kuwa nafasi ya mwenyekiti imegombewa na mtu mmoja ambae ni Omary Walii, makamu mwenyekiti mgombea mmoja Elisha Sironga huku nafasi ya katibu mkuu Zakayo Mjema akitetea nafasi yake na mpinzani ni Abdul Kondo na katibu msaidizi mgombea ni Athumani Juma na mweka hazina mmoja, Omary Kondo.



Kwa upande wa wajumbe wa mkutano mkuu wagombea ni Mwalizo Nassoro na Ayub Juma Kilabula huku nafasi ya uwakilishi wa vilabu akigombea mtu mmoja, Robert Munisi.





“Hao ndio wagombea na tumebandika majina hayo ukutani mwa uwanjan wa Sheik Amri Abeid kwa ajili ya watu kuleta pingamizi za wagombea hawa kama hawajatimiza sifa ya kugombea uongozi wa soka wilaya ikiwemo kuwa mkazi wa hapa jijini, elimu ya kidato cha nne, au kama hana uzoefu wa mpira wala taaluma ama aliwahi kuhukumiwa kwa kosa lolote”.



Uchaguzi huo wa ADFA unatarajiwa kufanyika mapema may 2 mwaka huu katika ukumbi wa viwanja vya Sheik Amri Abeid huku wajumbe na vilanu vyote vikitakiwa kulipa ada au kusajiliwa ili kuwa wajumbe halali wa mkutano huo na kupata kiongozi watakaempenda na kumwamini.





Mwishoo………………………

Taekwondo kufuana jumamosi

Bertha Ismail - Arusha

Vilabu  nane kutoka jijini Arusha zinatarajia kupimana uwezo katika mchezo wa Taekwondo katika ligi maalum  inayotarajiwa kutimua vumbi appril 25 mwaka huu katika viwanja vya Complex vilivyoko njiro jijini hapa kwa ajili ya kuchagua wachezaji watakaowakilisha mkoa katika mashindano ya kitaifa ya Mei mosi.



Vilabu vya Taekwondo vinavyojifua katika viwanja mbali mbali kwa ajili ya mashindano hayo ni pamoja na Tripple ‘A’, Naura, kili, Kijenge pamoja na Meru, Chishwea, M.S na AICC ambapo kila mchezaji anasaka nafasi ya kuchaguliwa kuunda timu ya mkoa itakayo wakilisha katika mashindano hayo ya mei mosi yatakayofanyika jijini hapa may 1 mwaka huu.



Akizungumza na gazeti hili, katibu mkuu wa shirikisho la mchezo wa Taekwondo Tanzania, Shija Shija alisema kuwa wametoa nafasi kwa vilabu mbali mbali kujiandaa na mashindano ya mei mosi itakayosaidia kuendelea kuwanoa wachezaji katika mashindano ya kitaifa baadae watakapokua wanachagua timu itakayowakilisha nchi kwenye mashindano ya Afrika hapo septemba kule Brazavile, Congo.



“Mashindano haya ni ya wazi kwa vilabu vyote Tanzania kushiriki ili kuwanoa zaidi wachezaji wao na tutaandaa mashindano mbali mbali kwa wachezaji kutoka ndani na nje ya nchi lengo ni kuwajenga wachezaji wetu kimashindano zaidi wazidi kuleta medali mbali mbali za kimataifa kama mashindano yaliyopita”



Mkurugenzi wa ufundi wa mchezo wa Taekwondo mkoa wa Arusha Richard Kitolo aliliambia gazeti hili kuwa wameandaa mashindano yao maalum ya ndani ili kuchagua wachezaji wazuri watakaoshiriki michuano ya mei mosi ambayo wao watatayatumia mashindano hayo  kuchagua timu ya mkoa itakayowakilisha katika mashindano ya kitaifa baadae.



“Sisi wenyewe tumeamua kuandaa mashindano yetu ya ndani kabla hayo ya mei mosi hayajafika ili kuanza mchujo wa wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kupambana na mchujo wa pili tutaufanya kwenye mashindano hayo ya mei mosi kupata timu ya mkoa”



“Sisi mashindano haya kwetu ni mazuri na tutatumia kuchagua timu ya Mkoa,  lakini changamoto kubwa inayotukabili kwa sasa ni wachezaji wachache kutokana na wazazi kutoruhusu watoto wao kushiriki katika mchezo hasa wasichana hivyo tuwaombe wazazi wawaruhusu watoto kushiriki katika michezo kama hiyo kuwajenga kiakili na afya pia”

Mbulu wafurahia RCL



Chama cha soka wilaya ya Mbulu, Kimeipongeza shirikisho la Soka nchini kwa kutambua umuhimu wa wilaya hiyo kimichezo na kuwapa nafasi ya kuwa moja ya vituo vitatu vya michuano ya ligi ya mabingwa wa mikoa Tanzania inayotarajia kutimua vumbi may 2 mwaka huu.

Michuano hiyo ya RLC itashirikisha jumla ya timu 27 nchini katika vituo vitatu vya Mbulu (Manyara) , lindi na Sumbawanga ambapo kila kituo inatarajiwa kuwa na timu tisa ambapo kwa Mbulu kutakuwa na timu ya Madini (Arusha), alliance school (Mwanza), Bariadi united (Simiyu) zingine ni  Baruti (Mara), Lukirini fc (Geita), Mtwivila City (Iribga), RAS Kagera fc (Kagera) pamoja na Small Prison (Tanga) na Watumishi fc (Shinyanga).

Ugeni huo mkubwa umewapa motisha kubwa wakazi na viongozi wa soka wilaya ya Mbulu na kufurahia nafasi hiyo adimu huku wakitoa shukrani zao za dhati kwa shirikisho la soka Tanzania kwa kutambua mchango wao huku wakisema kutumia michuano hiyo kama mafunzo kwao.

“Kiukweli tumefurahi sana TFF kutuletea michuano hii kwani itakuwa kama fursa kwetu ya kujifunza nini wenzetu wanafanyaga na tujifunze kwa kuiga ili na sisi tusonge mbele kisoka kwani imekuwa ikituuma sana zaidi ya miaka 10 hatujaonja ligi kuu na miaka mitano hatujui ligi daraja la kwanza likoje” alisema katibu wa soka wilaya ya Mbulu Fortunatus Kalewa.

“Tunashukuru timu nyingi zimeshaweka oda ya sehemu za malazi na viwanja vya mazoezi ikiwemo timu ya madini fc ya Arusha hivyo naamini itakuwa fursa kwetu kuwaleta wachezaji wa timu mbali mbali za mkoani hapa kuja kuiba mbinu wanazotumia wenzetu katika mashindano hadi wanasonga mbele na kuwakilisha mikoa yao katika ligi za ngazi za juu”

Kituo hicho cha Mbulu mashindano ya ligi ya mabingwa wa mikoa inatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Nyerere wilayani mbulu mkoani Manyara ambao uko katika hali nzuri kimandhari na uzio ingawa majukwaa bado ni changamoto.

Mwisho………………….



ndondo cup kutikisa Arusha Leo

Mkoani Arusha leo kunataraji kufanyika michuano ya NDONDO CUP itakayoshirikisha jumla ya timu nane kutoka mkoani hapa.


Lengo la michuano hiyo ni kuwakutanisha wapenda soka mkoa wa Arusha pamoja na kuwapa nafasi wa mashabiki wa mchezo huo Mkoani hapa kukutana sehemu moja.

Michuano hii itaanza kutimua vumbi siku ya Ijumaa ya tarehe 24/04/2015 na kufika tamati siku ya jumapili.
Mshindi wa kwanza katika michuano hii atapata zawadi ya fedha taslimu shilingi laki tano (500,000) pamoja na kikombe, mshindi wa pili atajipatia fedha taslimu shilingi laki tatu (300,000).

Timu zitakazoshiriki katika michuano ya NDONDO CUP 2015 ni FFU OLJORO, TANZANITE SPORTS FOUNDATION, RED STAR, TANZANITE VETERAN, LEMARA BOYS, NJIRO SPORTS, SMALL NYOTA na UMBRELA GARDEN.

Ratiba katikIMA MICHUANO HIYO NI KAMA IFUATAVYO


FFU OLJORO VS TANZANITE SPORTS CLUB, TANZANITE VETERAN VS RED STAR, LEMARA BOYS VS UMBRELA GARDEN, NJIRO SPORTS VS SMALL NYOTA
Michezo yote itapigwa siku ya ijumaa kwa mfumo wa bonanza na nusu fainali itakuwa siku ya jumamosi wakati mchezo ya fainali utapigwa siku ya jumapili.

Michuano hii itafanyika katika uwanja wa AICC uliopo karibu na round about ya KIJENGE. muda ni kuanzia saa 4 asubuhi mpaka 12 jioni.

Katika michuano hii kutakuwa pia na burudani toka kwa bingwa wa kucheza na baiskeli dunia (BMX CHAMPION) VICK GOMEZ, pamoja na wasanii wa Bongo flava akiwemo G NAKO, CHABA, KINGS, na mchekeshaji KATARINA.