Wachezaji wa Azam wakimbeba juu kocha wao Stewart Hall baada ya
kuwaongoza kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi kwa kuifunga Jamhuri ya
Pemba katika fainali iliyofanyika Januari 12 Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Picha na Jackson Odoyo.
KOCHA Stewart Hall anatarajiwa kusaini
mkataba mpya na timu ya Azam FC wakati wowote kuanzia sasa, hatua itakayomfanya
kuingia kwenye orodha ya makocha wa klabu wanaolipwa vizuri barani Afrika.
Hall, raia wa Uingereza anatarajiwa kuwasili leo tayari kusaini mkataba mpya,
akichukua nafasi ya Boris Bunjak aliyejiunga na Azam kuchukua nafasi ya
Mwingereza huyo kabla naye kutimuliwa Jumatatu wiki hii.
Kutimuliwa Bunjak, raia wa Serbia
kulikuja siku mbili tangu Azam kunyukwa 3-1 na Simba na kuporomoka kutoka
nafasi ya pili ya msimamo Ligi Kuu mpaka ya nne.
Rais wa Sofapaka, Elly Kalekwa aliimbia Capital Sport kuwa, Azam wamemwomba
radhi Hall na kumwahidi mkataba mnono ambao wameshindwa kumzuia.
"Sikupenda kuondoka kwake, lakini siwezi kumzuia. Azam wamempa mkataba
unaofanya kuwa miongoni mwa makocha wanaolipwa zaidi Afrika."
"Kwanza walimwambia [Hall] wangependa
kuendelea kuwa naye na kumwomba radhi kwa kufukuzwa kulikotokana na mapendekezo
ya wachache," alisema rais huyo wa Sofapaka.
"Hall ni mweledi, tangu alipoingia mkataba na sisi. Azam walipomfuata
alinipa taarifa na baada ya majadiliano tumekubali aende," Kalekwa alisema
kwa huzuni.
Naye Bunjak alisema amepokea uamuzi huo kwa shingo upande na mshangao mkubwa
hasa ukizingatia kuwa sababu ni matokeo ya kufungwa na Simba.
Bunjak alisema ameiongoza Azam kwa mafanikio kabla ya kucheza na Simba,
akishinda mechi tano, sare tatu na kubaki nafasi ya pili kipindi kirefu.
Hata hivyo, Bunjak amesema anakubali hatua iliyochukuliwa dhidi yake, lakini
akihoji vigezo vilivyotumika mpaka akafukuzwa.
ìHakuna timu isiyofungwa, kufungwa ni sehemu ya mchezo na ndiyo mpira
wenyewe," alisema Bunjak.
"Haiingii akilini kama kigezo ni kufungwa
na Simba. Inawezekana ni uamuzi tu uliokuwapo hasa kwa vile wanasema,
"kocha anaajiriwa ili afukuzweî,î alisema Bunjak.
Alisema ni vigumu kumfukuza kocha kwa kufungwa mechi moja. "Ina maana timu
hii (Azam FC) haitakiwa kufungwa hata mchezo?"
Bunjak alisema inashangaza kocha anatimuliwa kutoka timu iliyo nafasi ya pili
kwenye msimamo, tena ikiwa na mechi moja pungufu ya nyingine.
ìNimekubali, wamenilipa fedha zangu, sina jinsi kwa sasa nasubiri kurejea
nyumbani Serbia
siku mbili zijazo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Bodi ya Azam, Hall atawasilileo kutoka Kenya na
anatarajia kuanza kazi kesho katika mechi dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Chamazi.
No comments:
Post a Comment