KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA, LIBERATUS SABAS ALIPOKUWA AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI (HAWAPO PICHANI) MAPEMA LEO OFISINI KWAKE JUU YA MSAKO WA LEMA
Jeshi la polisi mkoani Arusha
linamsaka aliyekuwa mmbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kwa tuhuma
za kushambulia mwili pamoja na upotevu wa simu pamoja na fedha.
Akiongea na waandishi wa habari jijini hapa kamanda polisi Lebaratus Sabas
alisema kuwa jeshi la polisi linamsaka lema na wenzake ambao idadi yake
hawajatajwa kwa tuhuma za kushambulia mwili wa watu wawili tukio lililofanyika
october 28 mwaka huu katika kata ya daraja mbili.
Alisema kuwa jeshi la polisi lilipokea taarifa za malalamiko kutoka kwa
watu wawili waliojulikana kwa jina la Ibrahimu Juma pamoja na Maritin Daniel
wote wakazi wa daraja mbili kuwa aliyekuwa mbunge wa jimbo la arusha mjini
Godbless Lema akiwa na wanzake walimvamia na kuwashambulia kwa ngumi pamoja na
kuwanyanganya simu aina ya samsang yenye samani ya shilingi laki tatu pamoja na
fedha taslim kiasi cha shilingi laki mbili kisha kuondoka na kuwaacha.
Alisema kuwa watu hao waliamua kutoa taarifa polisi na jeshi la polisi
linamsaka lema kwa ajili ya kujibu tuhuma hizi .
Gazeti hili lilimtafuta lema kujibu tuhuma hizi akupatikana kwani simu yake ya
kiganjani ilikuwa imezimwa.
wakati huo huo jeshi la polisi linaashikilia watu wawili kwa tuhuma za kukutwa
na vitambulisho feki wakati wa uchaguzi wa udiwani wa kata ya daraja mbili
uliofanyika jana jijini hapa.
Akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha aliwataja watu hao
kuwa ni pamoja na Amosi Rajabu ambaye alikutwa akiwa na kitambulisho bandia
chenye namba 45036846 huku mungine akijulikana kwa jina la Lukas Thomas manya
ambaye naye alikamatwa na kitambulisho bandia ambapo alisema namba yake ilikuwa
imefutika .
Alisema kuwa watuhumiwa wote hawa wapo chini ya ulinzi wanashikiliwa na jeshi
la polisi kwa ajili ya upelelezi na pindi utakapo kamilika watafikishwa
mahakamani .
No comments:
Post a Comment