Mkutano unafanyika leo mjini London kujadili mkakati mpya wa utakaotumika baada ya ule wa malengo ya milenia.
Malengo
hayo yaliwekwa mwaka elfu mbili kuimarisha maisha ya watu katika nchi
maskini na walitumai kuwa yangefikiwa mwishoni mwa mwaka 2015.
Aidha
malengo hayo yananuia kukabiliana na maswala kama viwango vya umaskini,
magonjwa , njaa na ukosefu wa elimu lakini mafanikio yamekuwa kidogo
sana ikilinganishwa na matumaini ambayo watu walikuwa nayo.
Waziri
mkuu wa Uingereza, David Cameron, anafanya mazungumzo na Rais Ellen
Johnson Sirleaf wa Liberia na Rais Susilo Bambang Yudhoyono wa
Indonesia, wenyekiti watatu wa jopo la umoja wa mataifa litakalopewa
jukumu la kuweka mkakati mwingine mwaka 2015 kwa sababu ya malengo ya
milenia.
No comments:
Post a Comment