Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magessa S. Mulongo alipokuwa akielezea juu ya ziara ya Rais kwa waandishi wa habari |
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho
Kikwete anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku tatu katika jiji
la Arusha kuanzia November 1 mwaka huu.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa
Stanslaus MuIongo Wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini mapema jana
kwake.
Mulongo alisema kuwa ziara hiyo inaanza rasmi november moja ambapo ataanza kuzindua hospitali ya Oluturmet iliyopo katika halmashauri ya arusha vijijini ambayo hapo awali ilikuwa ni kituo cha afya na sasa imepandishwa hadhi na kuwa hospitali.
Aidha amefafanua kuwa siku hiyo ya kwanza pia ataweka jiwe la msingi katika barabara zinazojengwa jijini hapa ambazo mradi huo ni kwa hisani ya benki ya dunia pamoja na serikali yaTanzania.
Mulongo aliongeza kuwa baada ya hapo mheshimiwa
rais atamalizia na uzinduzi wa nembo ya jiji la Arusha ambayo itazinduliwa
rasmi katika makumbusho ya jiji ambapo uzinduzi huo itaambatana na sherehe za
kusherehekea uzinduzi huo.
mnara wa mwenge ni Moja ya alama iliyoko kwenye nembo mpya ya jiji likiwa katika ukarabati na kupakwa
rangi kwa ajili ya sherehe za uzinduzi wa nembo ya jiji la Arusha
Pia aliongeza
kuwa siku hiyo hiyo rais atatumia fursa hiyo kuongea na wananchi wa jiji la
Arusha katika uwanja wa kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid.
Mulongo pia alitoa wito kwa wananchi wa jiji la Arusha kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo wa jiji la arusha hususan pale ambapo Rais atakapo hutubia wananchi wa jiji la Arusha katika uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid .
Alisema novemba mbili Rais ataendelea na ziara yake
katika taasisi ya Nalson Mandela ambapo atazindua rasmi taasisi hiyo na
baada ya hapo atatembelea kiwanda cha kutengenezea vyandarua cha A to Z
kuona shughuli zinazofanywa na kiwanda hicho pamoja na kusikiliza changamoto wanazokabiliana
nazo pamoja na kuona namna ambavyo serikali itaweza kuwasaidia kuzitatua
Mulongo alisema kuwa siku ya tatu Rais anatarajia kwenda kufungua shule ya
msingi ya Sokoine iliyopo ndani ya eneo la jeshi la kulinda
taifa(JWTZ) iliyopo wilayani Monduli na baada ya hapo ataenda
kuweka jiwe la msingi la upanuzi wa barabara kutoka Arusha hadi minjingu.
Awali Meya wa Jiji la Arusha Gaudence Lyimo alisema
kuwa kupatikana kwa cheti hicho kunaipa mamlaka iliyokuwa Halmashauri ya
Manispaa ya Arusha nafasi ya kutumia rasmi hadhi ya Jiji.
Mea wa jiji la Arusha Mheshimiwa Gaudence Lyimo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo ofisini kwake juu ya uzinduzi wa nembo ya jiji. |
Alisema Hii inawafanya kubadilisha kuanzia nyaraka
zote za vitendea kazi pamoja na Nembo ya Manispaa ambapo sasa watatumia Nembo
mpya.
Lyimo aliongeza kuwa Halmashauri hiyo ilianza tangu
mwaka 1948 ikiwa ni Halmashauri ya Mji baada ya kukua kwa mji ambapo
ilibandishwa hadi na kuwa Manispaa mwaka 1980.
Kutokana na kupanuka kwa shughuli katika eneo la
kilomita za mraba 93, Serikali iliamua kupandisha hadhi ya eneo hilo hadi kufikia
kilomita za mraba 2,008.
Sanjari na hilo
alisema kuwa hadhi hiyo ni kwa mujibu wa tangazo la Serikali namba 341 la
Oktoba 14, mwaka 2011,”
No comments:
Post a Comment