Mwili wa kiongozi wa zamani wa Palestina, Yasser Arafat, umefukuliwa
kutoka kaburi lake liloko ukingo wa Magharibi mjini Rammala ili
kuwawezesha kuufanyia uchunguzi kubaini iwapo aliuwawa kwa sumu.
Bwana Arafat alifariki dunia mwaka 2004 nchini Ufaransa baada ya kuugua kwa kipindi kifupi.
Maradhi
yaliyopelekea kifo chake hayakubainika. Uamuzi wa kuufukua mwili wa
Yasser Arafat katika kaburi lake lililoko ukingo wa Magharibi unafuatia
makala ya televisheni iliyodai kupata mabaki ya madini ya kitonoradi
aina ya Polonium kwenye nguo zake.
Wapalestina
wengi wanashuku kwamba huenda Israel ilihusika katika kifo cha kiongozi
huyo. Israel imekuwa ikikanusha shutuma hizo.
Uchunguzi wa mauaji dhidi ya Bwana Arafat umeanzishwa nchini ufaransa kufuatia ombi lililowasilishwa na mjane wake.
...............xxx........xxx.......xxx.....
Katu hatuondoki Goma'' wasema M23
Kiongozi wa waasi wa M23 ambao wiki jana waliuteka mji wa Goma
Mashariki mwa DRC, wanasema katu hawataondoka Goma hadi serikali
itakapotimiza matakwa yao.
Kiongozi wa
kundi hilo, Jean-Marie Runiga alisema kuwa wapiganaji wake wataondoka
mara moja ikiwa Rais Joseph Kabila, ataitikia matakwa yao ambayo ni
pamoja na kuivunja tume ya uchaguzi.
Serikali ya Congo hata hivyo imepuuza matakwa hayo kama ya kipuuzi.
Uganda
ambayo imekuwa ikipatanisha pande hizo mbili kwenye mkutano mjini
Kampala, awali ilisema walikubali kuondoka Goma bila vikwazo.
Mnamo Jumamosi, serikali za nchi za Maziwa makuu ziliwapatia waasi hao makataa ya siku mbili kuondoka Goma.
No comments:
Post a Comment