Ndikumana |
Na Mahmoud Zubeiry,
Kampala
MSHAMBULIAJI
wa zamani wa Simba SC, Suleiman Yamin Ndikumana kwa sasa ndiye anaongoza kwa
kufunga mabao katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati,
CECAFA Tusker Challenge inayoendelea mjini hapa.
Ndikumana
aliyewahi pia kucheza Norway na Uturuki, jana alifunga bao la tatu katika
mashindano haya, akiichezea Burundi dhidi ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars.
Sasa
anamzidi kwa bao moja, John Bocco ‘Adebayor’ wa Kilimanjafo Stars.
Jumla ya
mabao 17 hadi sasa yamefungwa katika mechi 16 za makundi yote matatu,
zilizopigwa kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala.
Bocco anafungana
na mshambuliaji mwingine wa Burundi, Christopher Nduwarugira, wakati wachezaji
wengine ambao hadi sasa kila mmoja amefunga bao moja ni Farid Mohamed, Yussuf
Ndikumana wa Burundi, Mohamed Jabril wa Somalia kwa penalti, Geoffrey Kizito wa Uganda, Yonatal Kebede Teklemariam, Haruna
NiyonzimUganda, David Ochieng, Clifton Miheso na Jean Mugiraneza.
Kwa sasa
Bocco anayechezea Azam FC ya Dar es Salaam, ndiye mshambuliaji pekee kwenye
kikosi cha Bara, baada ya washambuliaji wengine, Mbwana Samatta na Thomas
Ulimwengu wanaochezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemomkrasia ya Kongo (DRC)
kuzuiliwa na klabu yao.
WAFUNGAJI CECAFA TUSKER CHALLENGE
2012
Suleiman
Ndikumana Burundi 3 (1 penalti)
John Bocco Tanzania 2
Chris
Nduwarugira Burundi 2
Yussuf
Ndikumana Burundi 1
Mohamed
Jabril Somalia 1(penalti).
Geoffrey
Kizito Uganda 1
Brian Umony Uganda 1
Yonatal
Teklemariam Ethiopia 1
Haruna
Niyonzima Rwanda 1
Jean
Mugiraneza Rwanda 1
David
Ochieng Kenya 1
Clifton
Miheso Kenya 1
Farid
Mohamed Sudan 1
.................xxx.............xxx.............xxx.................
KAZIMOTO, KAPOMBE HATARINI KUWAKOSA WASOMALI JUMAMOSI
Kazimoto |
WACHEZAJI wawili
wa Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, beki Shomary Kapombe na kiungo Mwinyi
Kazimoto, walishindwa kumaliza mechi za jana, baada ya kuumia na sasa wako
hatarini kuikosa mechi ya mwisho ya Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika
Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge dhidi ya Somalia, Desemba 1.
Wachezaji
hao wa klabu ya Simba, wote waliumia kipindi cha pili na kutolewa, nafasi ya
Kapombe ikichukuliwa na Issa Rashid wa Mtibwa Sugar nay a Mwinyi ikichukuliwa
na Shaaban Nditi wa Mtibwa pia.
Wote
walitoka wakichechemea, kuashiria wamepata maumivu makali kidogo na Kocha Mkuu
wa Stars, Mdenmark, Kim Poulsen alisema ataangalia hali zao leo na kesho.
Kim pia
alisema kwamba sasa imetosha kuzungumzia suala la washambuliaji Mbwana Samatta
na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)
kama watajiunga na timu hiyo au la.
“Kwangu sasa
lazima ifikie wakati iwe inatosha, sitaki kuwazungumzia tena wachezaji hao,
waulizeni TFF,”alisema Poulsen baada ya kuulizwa kama mawasiliano na klabu yao
kama yanaendelea juu ya kuombea ruhusa.
Mazembe
imekataa kuwaruhusu wachezaji hao kwa sababu michuano ya Challenge haimo kwenye
kalenda ya FIFA.
Kutokana na
kukosekana kwa washambuliaji hao, Stars sasa inabaki na mshambuliaji mmoja tu
kikosini, John Bocco ‘Adebayor’ wa Azam FC, ambaye Watanzania wanatakiwa
kumuombea dua asiumie ili aendelee kuibeba timu yao ya taifa..............xxx.................xxx................xxx................
JOHN BOCCO AGEUKA LULU KUJMPALA, WATU WAANZA KUFIKA BEI
John Bocco |
Na Mahmoud Zubeiry,
Kampala
SOKA ya
nguvu aliyoonyesha mshambuliaji wa Tanzania Bara, John Bocco ‘Adebayor’ katika
mechi mbili za Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA
Tusker Challenge zimemfanya awe lulu katika mashindano haya yanayoendelea mjini
hapa.
Mawakala
mbalimbali waliopo mjini Kampala wameanza kuulizia uwezekano wa kumtafutia timu
Ulaya mchezaji huyo wa Azam, lakini uongozi wa timu ya Bara, Kilimanjaro Stars
mjini hapa umewataka wawasiliane na klabu yake, Azam FC ya Dar es Salaam moja
kwa moja.
Lakini pia
kuna uwezekano klabu ya SuperSport United ya Afrika Kusini, iliyomfanyia
majaribio Agosti mwaka huu ikamfikiria tena mchezaji huyo kutokana na kiwango
kikubwa alichoonyesha hadi sasa kwenye mashindano haya.
Japokuwa hakufunga
bao juzi kwenye mechi na Burundi, lakini kazi aliyoifanya wengi walikubali yeye
ni mshambuliaji mzuri haswa kutokana na mfumo wa sasa wa kocha wa Stars,
Mdenmark Kim Poulsen kumtumia peke yake mbele.
Bocco ana
mabao mawili kwa sasa, wakati mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Suleiman
Yamin Ndikumana ndiye anayeongoza kwa mabao katika michuano hii.
Ndikumana
aliyewahi pia kucheza Norway na Uturuki, juzi alifunga bao la tatu katika
mashindano haya, akiichezea Burundi dhidi ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars.
Jumla ya
mabao 25 hadi sasa yamefungwa katika mechi 18 za makundi yote matatu,
zilizopigwa kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala.
Bocco
anafungana na mshambuliaji mwingine wa Burundi, Christopher Nduwarugira na
mchezaji mwenzake wa Azam, Khamis Mcha ‘Vialli’ wakati wachezaji wengine ambao
hadi sasa kila mmoja amefunga bao moja ni Farid Mohamed, Yussuf Ndikumana wa
Burundi, Mohamed Jabril wa Somalia kwa penalti, Geoffrey Kizito wa Uganda, Yonatal Kebede Teklemariam, Haruna
NiyonzimUganda, David Ochieng, Clifton Miheso na Jean Mugiraneza, Dadi Birori,
Chiukepo Msowoya, Miciam Mhone, Patrick Masanjala, Amir Hamad Omary na Yosief
Ghide.
WAFUNGAJI CECAFA TUSKER CHALLENGE
2012
Suleiman
Ndikumana Burundi 3 (1 penalti)
John Bocco Tanzania 2
Khamis Mcha Zanzibar 2
Chris
Nduwarugira Burundi 2
Yussuf
Ndikumana Burundi 1
Mohamed
Jabril Somalia 1(penalti).
Geoffrey
Kizito Uganda 1
Brian Umony Uganda 1
Yonatal
Teklemariam Ethiopia 1
Haruna
Niyonzima Rwanda 1
Jean
Mugiraneza Rwanda 1
Dadi Birori Rwanda 1
David
Ochieng Kenya 1
Clifton
Miheso Kenya 1
Farid
Mohamed Sudan 1
Chiukepo
Msowoya Malawi 1
Miciam Mhone
Malawi 1
Patrick
Masanjala Malawi 1
Amir Hamad
Omary Eritrea 1
Yosief Ghide
Eritrea 1(penalti).
No comments:
Post a Comment