Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Mwigulu Nchemba
---
Hodihodi KIBAHA! WANACCM NA WANANCHI
WOTE WA MIKOA YA DSM, PWANI NA MORO, NAWAKARIBISHA KTK MKUTANO WA
HADHARA NITAKAOHUTUBIA KIBAHA. NJOO UPATE UKWELI, UPATE MATUMAINI UANZE
MWAKA VIZURI. NITAWAPOKEA MADIWANI WAWILI WANAOHAMIA CCM TOKEA CHADEMA.
TAYARI DIWANI WA IHANJA AMEJIUZURU JANA UDIWANI KWA KUKATAZWA KUSHIRIKI
SHUGHULI ZA MAENDELEO NA VIONGOZI WA CHADEMA TAIFA. NITAHIMIZA SHUGHULI
ZA MAENDELEO, KUKAGUA MIRADI NA PIA NITAONGELEA WABUNGE SABA 7 WA
CHADEMA WALIOOMBA KUHAMIA CCM TOKEA CHADEMA NA MAMBO YALIOWASIBU.
TAMKO RASMI LA BAVICHA MKOA WA TANGA KUHUSU KATIBU WA BAVICHA MKOANI WA TANGA BW DEOGRATIAS KISANDU.
NAPENDA kutoa taarifa kwa umma kutokana na habari zinazoandikwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari, huku chanzo cha habari hizo kikiwa ni Katibu wa BAVICHA Mkoa wa Tanga, Bwana Deogratias Kisandu, ambazo zimekuwa zikionesha kuwa vijana wa Mkoa wa Tanga tuna walakini katika chama chetu cha CHADEMA.
Leo katika baadhi ya vyombo vya habari, Bwana Kisandu amenukuliwa akitoa taarifa kuwa yeye pamoja na makatibu wenzake nchi nzima, wamepanga kufanya maandamano ya kuupinga uongozi wa juu wa kitaifa wa BAVICHA.
Kwa kutambua na kuheshimu kuwa moja ya misingi muhimu ya uendeshaji wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na mabaraza yake ni vikao, ambavyo vipo kwa mujibu wa Katiba, miongozo, taratibu, kanuni na itifaki za chama, vijana wa CHADEMA Mkoa wa Tanga, ambao mimi ndiye msemaji wao kikatiba, tunaamini Bwana Kisandu anazidi kupotoka.
Kwa hiyo basi, kama ambavyo nimeshapokea malalamiko kutoka kwa vijana wa Tanga baada ya hatua yake ya awali ya Bwana Kisandu kutoa taarifa kwa vyombo vya habari, bila kuzingatia katiba, maadili na itifaki ya chama, akibeba propaganda nyepesi za Sekretarieti ya CCM, juu ya suala la kadi mbili kwa Katibu Mkuu wetu Dkt. Willibrod Slaa, kuna haja ya kufanya vikao kuangalia na kujadili mwenendo wa kiongozi mwenzetu huyo.
Kwa sababu kama vijana makini wa CHADEMA, chama ambacho kinaamini katika kutoa utumishi bora, mikakati madhubuti, sera imara kwa ajili ya maendeleo endelevu ya Watanzania wote, ambao wamekosa uongozi bora na siasa safi kutokana na ufisadi na ubadhirifu wa CCM, lazima tuwe makini na kila mwenzetu yeyote yule ambaye anaonekana kufanya kazi ya CCM kwa kutumia jina la CHADEMA.
Tunapenda kumkumbusha Bwana Kisandu kuwa atumie muda wake pia kuisoma vyema
katiba ya CHADEMA hasa katika Sura ya 10 inayozungumzia Maadili ya Viongozi, Sifa mahususi za viongozi na maadili ya wanachama, kifungu
10.1(1-13), toleo la mwaka 2006.
katiba ya CHADEMA hasa katika Sura ya 10 inayozungumzia Maadili ya Viongozi, Sifa mahususi za viongozi na maadili ya wanachama, kifungu
10.1(1-13), toleo la mwaka 2006.
Kuhusu masuala ya ushiriki wa vijana kwenye shughuli mbalimbali za chama ikiwemo mikutano ya M4C, Bwana Kisandu anapaswa kuelewa kuwa vijana kutokana maeneo mbalimbali ya nchi, ukiwemo Mkoa wa Tanga tumekuwa tukishirikishwa, kupitia utaratibu maalum unaopangwa na Ofisi ya Katibu Mkuu, ambao tunaamini mpaka sasa umetoa fursa kwa wanachama wote, wakiwemo wazee, wanawake na vijana kukieneza na kukiimarisha chama maeneo mbalimbali ya nchi.
Na maamuzi yote ya msingi kwa uendeshaji wa Baraza hasa kwa Mkoa wa Tanga yatafanyika kupitia vikao na hatua zitachukuliwa kwa kufuata katiba, kanuni, maadili, itifaki na miongozo ya chama.
*Aron J Mashuve*
*Mwenyekiti wa BAVICHA*
*Mkoa Wa Tanga*
chanzo:hakingowi blog
No comments:
Post a Comment