Watu
wanane wamekufa baada ya nyumba kadha kufukiwa na maporomoko ya ardhi
katika eneo la bonde la Kerio, magharibi mwa Kenya, jana usiku.
Maporomoko
ya ardhi yamesababishwa na mvua kubwa zilizonyesha katika bonde hilo.
Eneo la Kerio pia limekumbwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa
inayonyesha.
Chama cha Msalaba Mwekundu
cha Kenya kinasaidia jitihada za uokoaji na kutoa taarifa kwamba miili
miili ya watu wanane imeonekana na watu wengine watano waliokolewa
mapema leo.
Watu wengi hawana makaazi kutokana na nyumba zao kusombwa na maji au kufukiwa na maporomoko ya ardhi.
............xxx.............xxx.............xxx............
Wahamiaja haramu 18 wafariki Misri
Balozi
wa Somalia nchini Libya Bwana Abdikani Mohamed Waeys amesema ana
taarifa ya vifo vya raia 18 vilivyotokea kutokana na ajali ya lori
nchini Libya.
Wasomali hao wanaotajwa kuwa wahamiaji haramu, 23 wameripotiwa kujeruhiwa huku wengine wakiwa katika hali mbaya.
Balozi
Abdikani amesema lori hilo lililokuwa limebeba mifuko ya saruji
walimokuwa wamejificha Wasomali hao, lilipinduka na kusababisha vifo,
na kusema idadi yao walikuwa 120 wakiwemo wanaume na wanawake wote
wakiwa ni Wasomali.
Katika miaka ya hivi karibuni idadi ya wahamiaji haramu ambao wamefariki wakijaribu kuvuka baharini imeongezeka.
chanzo ;BBC
No comments:
Post a Comment