Ngassa baada ya kufunga la kwanza |
Salum Abubakar akimiliki mpira mbele ya kiungo wa Somalia |
Bocco akipiga kichwa mpira kwenye lango la Somalia |
Kapombe akifanya kazi yake |
Ngassa akimiliki mpira mbele ya beki wa Somalia |
Kipa wa Somalia akiokoa moja ya hatari langoni mwake |
Kocha Poulsen |
Wachezaji wa aStars Mwinyi Kazimoto kulia na Amir Maftah wakiwa na rafiki yao jukwaani |
Amri Kiemba akimpongeza Ngassa kufunga |
John Bocco akimburuza Msomali |
Bocco akifanya vitu, angalia miguu |
Bocco anapongezwa na wenzake baada ya kufunga |
Bocco anamuacha mtu |
Amri Kiemba kulia |
Bocco mawindoni |
Yondan anaokoa |
Mrisho na mpira wake baada ya kufunga mabao matano |
Na Mahmoud Zubeiry,
Kampala
TANZANIA
Bara, Kilimanjaro Stars imefuzu kuingia Robo Fainali ya michuano ya CECAFA
Challenge, baada ya kuilaza Burundi mabao 7-0 katika mchezo uliofanyikakwenye
Uwanja wa Lugogo mjini hapa.
Matokeo hayo
yanaifanya Bara itimize pointi sita baada ya kucheza mechi tatu na sasa,
wakishinda mbili na kufungwa moja.
Stars,
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager leo ilionyesha kandanda safi na
kusisimua mashabiki wa Tanzania waliokuja kuoiunga mkono hapa, akiwemo Mbunge
wa Kondoa Kaskazini, Alhaj Juma Nkamia.
Iliwachukua
sekunde 48 tu Stars kupata bao la kwanza, kupitia kwa mshambuliaji wa Simba SC,
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premum Lager pia, Mrisho Khlfan Ngassa
aliyewazidi ujanja mabeki wa Somalia.
Kabla
hawajakaa vizuri, Somalia walipachikwa bao la pili, dakika ya 23 lililofungwa
na Ngassa tena, aliyeunganisha kona nzuri ya Issa na Rashid.
John Bocco
‘Adebayor’ alifunga bao la tatu katika mchezo wa leo na la tatu kwake katika
mashindano haya dakika ya 26 akiunganisha kwa kichwa krosi ya Issa Rashid
kutoka wingi ya kushoto.
Bocco tena
aliwainua vitini mashabiki wa Tanzania kwa kufunga bao la nne kwa kichwa,
akiunganisha krosi ya Ngassa dakika ya 41.
Ngassa
alifunga bao la tatu katika mchezo wa leo dakika ya 44 na la tano kwa Stars
baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa Hussein Abdallah kufuatia shuti kali
la Salum Abubakar ‘Sure Boy Jr.’
Somalia
ilipata pigo dakika ya 30, baada ya kipa wake namba moja, Mohamed Abdullah
kuumia baada ya kugongana na Bocco na kutoka, nafasi yake ikichukuliwa na
Hussein Abdallah.
Kipindi cha
pili Stars walirejea na moto wao na tena na kufanikiwa kupata mabao mawili
zaidi yaliyotiwa kimiani na Ngassa yote dakika za 73 pasi ya Erasto Nyoni na 74
pasi ya Ramadhani Sinago ‘Messi’.
Kwa kufunga
mabao matano, Ngassa sasa ameingia kwenye mbio za kaiti cha dhahabu akikwa anaongoza,
akifuatiwa na Bocco ambaye ana manne hivi sasa.
Kocha wa
Stars, Mdenmark Kim Pouslen baada ya mchezo huo, alisema aliwapongeza vijana
wake kwamba wamejitahidi kucheza vizuri na akasifu pia hali nzuri ya Uwanja wa
Lugogo kuwa ilichangia ushindi huo.
Mbunge
Nkamia alisema kwamba amevutiwa na soka ya vijana leo na anaamini wana uwezo wa
kurejea na Kombe nyumbani. Nkamia aliwapongeza wadhamini wa Stars kwa kuchangia
mafanikio ya timu hiyo tangu waanze kuidhamini na akaomba Watanzania zaidi
wajitokeze mjini hapa kuisapiti timu hiyo.
Waandishi wa
Habari waliopo mjini hapa pia wamevutiwa mno na kiwango cha timu hiyo na kusema
wana wana imani itafika mbali.
Wallace
Karia, Mjume wa Kamati ya Utendaji ya TFF aliye hapa Uganda amesema
amefurahishwa na kiwango cha timu na anaamini itafika mbali.
Meneja wa
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, wadhamini wa Kilimanjaro Stars, George
Kavishe ametuma salamu za pongezi kwa ushindi wa leo na mafanikio ya kutinga
Robo Fainali na kusema anatakia mafanikio zaidi timu hiyo.
Katika
mchezo wa leo, kikosi cha Stars kilikuwa; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Issa
Rashid, Shomari Kapombe, Kevin Yondan/Ramadhani Singano, Shaaban Nditi, Mrisho
Ngassa, Salum Abubakar, John Bocco/Christopher Edrwad, Frank Domayo/Athumani
Iddi na Amri Kiemba.
Somalia;
Mohalim Abdullahi/Hussein Abdallah dk30, Ali Mohamed, Said Mahamud, Ali Dadir,
Sadaq Abdikadir, Mohamed Salah, Abdikarim Abubakar, Abdallah Mohamed/Hamza Mukhtar,
Ahmed Abdikadir Dahir/Muhad Hajji na Ali Ahmed Ali.
Katika
mchezo mwingine uliopigwa kwenye Uwanja wa Nankurunkuru, Burundi ilishinda 1-0
bao hivyo kuongoza Kundi B baada ya kufikisha pointi tisa.
No comments:
Post a Comment