JUMLA ya wanafunzi 6,838 waliofaulu mtihani wa darasa la saba
mwaka huu, mkoani Arusha, wamekosa nafasi ya kujiunga na masomo ya
Sekondari kutokana na uhaba wa nyumba vya madarasa 172 .
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Arusha, Evelyine Itanisa alitoa taarifa hiyo, juzi
katika kikao cha kamati ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato
cha kwanza mwaka 2013 mkoani Arusha.
Itanisa
alisema wanafunzi hao, wanatoka katika halmashauri sita za mkoa Arusha
na ni halmashauri moja tu ya Karatu ambayo imeweza kuwachukua wanafunzi
wote waliofaulu mwaka huu.
Alisema
katika jiji la Arusha wanafunzi 2420 wamekosa nafasi kutokana na uhaba
wa vyumba vya madarasa 61, Ngorongoro wanafunzi 441 wamekosa nafasi
kutokana na uhaba wa vyumba 11.
Alisema Halmashauri ya Arusha vijijini wanafunzi 1880 wameshindwa kujiunga na sekondari kutokana na uhaba wa vyumba 47.
“Pia
Halmashauri ya Longido kuna wanafunzi 140 ambao wanahitaji madarasa
manne, Meru wanafunzi 1,159 wakiwa na mahitaji ya vyumba 29, wilaya ya
Monduli wanafunzi 807 wamekosa nafasi kutokana na kukosekana madarasa
20”alisema Itanisa.
Alisema
kutokana na hali hiyo, ameziagiza halmashauri hizo sita za mkoa wa
Arusha kuiga mfano wa halmashauri ya Karatu, kwa kuhakikisha zinajenga
vyumba vya madarasa vya kutosha ili kuhakikisha wanafuzi wote
waliofaulu wanapata nafasi.
“Ili
kuhakikisha watoto waliofaulu wote wanaendelea na sekondari, kila
halmashauri inapaswa ihakikishe inakamilisha ujenzi wa madarasa kabla
ya februari mwakani “alisema Itanisa.
Hata
hivyo, Katibu Tawala huyo alisema kiwango cha ufaulu kwa Mkoa wa
Arusha, kimekuwa kikipanda kwa miaka mitatu sasa mfululizo ambapo mwaka
huu jumla ya wanafunzi 26,464 wamefaulu mitihani kati ya wanafunzi
37,493 waliofanya mitihani.
“Matokeo
haya yanafanya Mkoa wa Arusha uwe umefaulisha kwa asilimia 70.6 na
waliofaulu ni wavulana 12,608 na wasichana 13,856”alisema Itanisa.
No comments:
Post a Comment