Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika akizungumza na
waandishi wa habari kwenye makao makuu ya chama hicho Dar es Salaam
jana. Kulia ni Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene. Picha na Joseph
Zablon.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), kimetangaza ratiba ya uchaguzi wake wa ndani, inayoonyesha
kuwa kitapata mwenyekiti mpya ifikapo Desemba 13, mwaka huu.
Ratiba
iliyotolewa na chama hicho Dar es Salaam jana imeeleza kuwa uchaguzi
huo wa mwenyekiti, utatanguliwa na chaguzi nyingine za ngazi za
majimbo, mkoa, wilaya, kata na tawi.
“Uchaguzi
utaanza Aprili, mwaka huu na tunatarajia umalizike Desemba mwaka huu
kwa kumchagua mwenyekiti taifa,” alisema Mkurugenzi wa Habari na
Uenezi, John Mnyika.
Alisema
kuanzia Aprili hadi Septemba kutafanyika chaguzi katika ngazi za msingi
ambazo zinajumuisha matawi, majimbo na wilaya kabla uchaguzi huo
haujafanyika katika ngazi ya mkoa kuanzia Novemba.
“Uchaguzi
ngazi ya taifa utahusisha pia jumuiya za chama ambazo ni Baraza la
Wanawake Chadema (Bawacha), Baraza la Vijana (Bavicha), Wazee, Kamati
Kuu na Baraza Kuu Taifa,” alisema.
Nafasi nyingine zitakazoshindaniwa ni za wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa.
chanzo:mwananchi
No comments:
Post a Comment