Katika hali ya kuhakikisha ulinzi na usalama wa wananchi na mali
zao unaimarika mkoani Arusha, jeshi la polisi mkoani hapa limegawa pikipiki 12
kwa wakuu wa vituo vya polisi katika kila wilaya.
Katika ugawaji huo akimkaribisha mkuu wa ulinzi na usalama
wa mkoa, kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas alisema kuwa wameamua
kugawa pikipiki hizo kwa kila wilaya ili kurahisisha ufikaji mapema wa eneo la
tukio linalohisiwa kuwa na uhalifu kabla haujatokea au kuleta madhara.
kamanda Sabas akifungua mktano |
Sabas alisema kuwa kazi ya ulinzi na usalama wa wananchi na
mali zao na nchi kwa ujumla ni ngumu sana bila vifaa ikiwemo usafiri hivyo
jeshi la polisi kwa kulitambua hilo wameamua kununua pikipiki hizo 12 na kugawa
katika kila wilaya ambapo amewataka askari hao kutumia pikipiki hizo kwa
ustaarabu ili kuweza kutimiza malengo yaliyokusudiwa ikiwa ni kuwahi eneo la
tukio haraka mara tu wahisipo uhalifu au kupata taarifa ya uhalifu.
Akigawa pikipiki hizo mkuu wa usalama wa mkoa ambaye pia ni
mkuu wa mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo aliwataka askari hao kutumia usafiri
huo katika shughuli mbali mbali za kiusalama ambapo amewaahidi atakayefanya
vizuri kazi yake kwa umakini, usahihi na uadilifu atampa zawadi ya shilingi
milioni 1.
Pia amewataka watendaji wa kila wilaya kuhakikisha wanawapa askari
wa jeshi la polisi ushirikiano wa kutokomeza uhalifu kwani serikali haifurahii
mrundikano wa mahabusu katika magereza hivyo wawafichue waadhibiwe utokomee
ambapo amewataka watendaji hao kuepuka kuwa sehemu ya wahalifu au kuwaficha au
hata kuendekeza uhalifu bali wautokomeze.
Pia amewataka askari hao kutambua kuwa pindi wawapo kazini
katika kutokomeza uhalifu wasiangalie cheo cha mtu kwani sheria haina cheo,
umri wala jinsia kwani kwenye sheria kila mtu ni sawa hivyo kuwataka sheria
hiyo isiwaonee wananchi wa hali ya chini tu bali hata viongozi wanaoshiriki
uhalifu nao waadhbiwe kulingana na sheria za jamhuri ya muungano wa Tanzania .
baadhi ya askri walioshuhudia ugawaji pikipiki |
Aidha pikipiki hizo 12 zilizotolewa na jeshi la polisi
ziligawiwa kwa kila wilaya huku zikiwakilishwa na wakuu wa vituo wa wilaya husika(ma O.C.D) ambapo wilaya
zilizopokea pikipiki hizo ni pamoja na wilaya ya Ngorongoro, Karatu, Monduli,
Arusha mjini, Longido Arumeru.
Sanjari na hilo zoezi la ugawaji pikipiki hizo zinaenda
sambamba na utambulisho wa siku ya uzinduzi wa usafi wa jiji la Arusha, ambapo
mkuu huyo alisema kuwa siku ya usafi jijini utakuwa unafanyika kila ijumaa
jioni ambapo amewataka wafanyabiashara wenye maduka mijini au masokoni na
wanajamii kwa ujumla kujitokeza kufanya usafi katika maeneo yao kuanzia saa 12
jioni.
No comments:
Post a Comment