Kiongozi wa kanisa katoliki Tanzania, Muadhama Kadinali Polycarp Pengo
KIONGOZI wa kanisa katoliki Tanzania, Muadhama Kadinali Polycarp Pengo amewataka wakristo kutolipa kisasi kufuatia kuuawa kwa Padri Evarist Mushi huko Zanzibar.
Amesema wakristo kulipa kisasi
hakutawasaidia kwani ni kinyume cha mafundisho ya dini ya kikristo na
sheria za nchi. Kadinali Pengo ameitaka Serikali kuwa makini na watu
ambao wanataka kuivuruga amani ya nchi kwa kisingizio chochote kile.
Kiongozi huyo amevitupia lawama vyombo
vya usalama wa nchi kwa kutochukua hatua za tahadhari kwani kulikuwa na
ishara ya uhalifu kupitia vipeperushi vilivyosambazwa huko Zanzibar.
No comments:
Post a Comment