VINARA wa Ligi Kuu ya Vodacom,
Yanga wameamua kwenda kambini mjini Bagamoyo kujiandaa na mechi
yao dhidi ya Azam itakayochezwa Jumamosi ya wiki
hii kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar
es Salaam .
Kwa mujibu wa habari
zilizopatikana jana kutoka ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake makutano ya
motaa ya Twiga na Jangwani, wamekwenda huko kutokana na wachezaji kuhitaji
mazingira bora na yenye utulivu.
Chanzo hicho kimedokeza
kwamba, kutokana na ugumu wa mechi hiyo itakayozikutanisha timu zinazoshika
nafasi mbili za kwanza katika logi hiyo, inatarajiwa kuwa yenye ushindani
mkubwa.
“Unajua Azam ipo vizuri sana , imekuwa ikitoa
upinzani mkubwa hasa inapokutana nasi. Tumeona ni bora wachezaji wakienda
kufanya maanmdalizi tukiwa nje ya Dar es Salaa, tukiamini wachezaji watapata
nafasi ya utulivu,” kilisema chanzo hicho.
Mechi hiyo inatarajiwa kuwa
na upinzani mkubwa kwani kila timu itahitaji kushinda ili kujiweka katika
mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo iliyoanza Septemba 15.
Wakati Yanga ikitaka kutwaa
taji la 23 tangu kuanza kwa ligi ya taifa mwaka 1965, Azam inasaka ubingwa wa
kwanza tangu kuanzishwa kwake Juni 24, mwaka 2007.
Yanga inayoongoza ligi hiyo
kwa pointi 36, itakuwa ikisaka ushindi ili kuendeleza ubabe wao kwa timu hiyo
No comments:
Post a Comment