Hiki ndicho kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15.
Winchi likiokoa mabaki ya moja ya gari lililoangukiwa na kifusi.
VIDEO IKIONYESHA JINSI JENGO LILIVYOANGUKA JIJINI DAR LEO.
Rais Jakaya Kikwete (katikati) akiangalia hali ya uokoaji inavyoendelea.
Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, akitoa maelekezo ya jinsi ya kuondoa kifusi eneo la tukio.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki (katikati) akifuatilia shughuli ya uokoaji.
Watu mbalimbali wakiondoa kifusi.
Askari aliyejuu ya farasi akihakikisha usalama eneo hilo.
Baadhi ya watu wakilisukuma gari ambalo pia lilikuwa kwenye ajali hiyo.
Mama Salma Kikwete (kulia) na Rais Kikwete wakiangalia kifusi.
Kijana aliyenusurika katika ajali hiyo akinywa kahawa.
LEO majira ya saa mbili na nusu asubuhi Watanzania wameingia kwenye
vilio baada ya jengo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa
ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri mtaa wa Indira Ghandi jijini
Dar es Salaam, kuanguka na kuwafunika watu waliokuwa eneo hilo na
kusababisha wengine kupoteza maisha. Mpaka sasa haijajulikana idadi
kamili ya watu waliokuwemo ndani yake,.
Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea, huku nondo nyembamba zikionekana na kuacha maswali miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo.
Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea.
Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea.
Taarifa zilizotufikia mchana huu
zinadai kuwa idadi ya majeruhi wa ghorofa lililoporomoka jijini
Dar es Salaam imefikia 18 wakati watu wanne wanadaiwa kupoteza
maisha na jitihada za uokoaji bado zinaendelea .
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.