Bw Joseph J. Mungai akifafanua jambo wakati
alipowasilisha barua yake ya wazi kwa tume ya elimu ya kufeli kwa
asilimia 60 kwa wanafunzi wa kidato cha nne mwaka jana
...............................................................................................
ALIYEKUWA
waziri wa elimu na mbunge mstaafu wa
jimbo la Mufindi Kaskazin Joseph Mungai
awaonya wanasiasa kuacha
kuamua bila kuzingatia ipasavyo
utafiti na ushauri wa kitaaluma kuhusu Elimu ya Taifa letu.
Mungai aliyasema hayo leo wakati akiwasilisha barua yake ya wazi
kwa tume ya elimu ya kufeli kwa
asilimia 60 mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012 iliyoundwa na waziri mkuu Mizengo Pinda .
Alisema
kuwa ili kukuza kiwango cha elimu nchini ni vema
wanasiasa wakaachana kabisa na
utaratibu wa kuingilia na kutoa ushauri wao katika elimu
bila kuwasikiliza wataalam kwani kwa
kufanya hivyo kunachangia elimu
kuyumba .
“Ninawapongeza
kwa kuteuliwa na ahsante kutupa fursa wadau wa elimu kuwaletea maoni na au/ushauri”
“Mimi
ni mdau wa elimu, niliyewahi kuwa Mwenyekiti mwanzilishi wa Mufindi Education
Trust (MET) iliyoanzisha katika wilaya ya Mufindi na kuziendesha kwa mika
zaidi ya 10 Sekondari 9 za: (1) JJ Mungai (2) Sadani ( 3)
Itengule ( 4) Igowole ( 5) Itandula ( 6)
Mgololo ( 7 ) Kibengu ( 8) Mdabulo na ( 9) Nyololo; ambazo sasa ni za serikali.
Aidha nimewahi kuwa waziri wa Elimu na Utamaduni mwaka 2000 hadi 2005”
Alisema kuwa Kufeli mwaka 2012 kidato cha Nne (KIV) kwa
asilimia 60 halikuwa tukio lililoibuka ghafla bali waliofeli ( Division 0)
mtihani huo waliongezeka kutoka mwaka 2007:9.7% ; 2008:16.3%; 2009:27.5%;
2010:49.6%; 2011:46.4% na sasa 2012:60%
Mungai alisema
kuwa Kabla ya hapo waliofeli kidato cha Nne (KIV) WALIPUNGUA kutoak
mawka 1998:24:3%:; 1999:20.0% 2000:21.6% 2001:22.6%, 2002:12.7%; 2003:12.2%,
2004:8.7%, 2005:10.7%, 2006:10.9%, na 2007:9.7% wastani wa kufeli 2004 hadi
2007 ni 10%.
Tazama hotuba ya bajeti ya Waziri wa Elimu na Utamaduni ya mwaka
2005/2006 kielelezo Na. 75.4 ukurasa wa 100; na BEST ( Basic Statics in
Education, National Data) ya miaka
husika.
Wakati
Kati ya 2004 na 2007 waliofeli kidato cha Nne
walikuwa wastani wa 10% ambayo inavumilika. Kwa nini kati ya 2007 na 2008
kulikuwa na mruko kutoka 9.7% hadi 16.3%? Huo ukawa ndio mwanzo wa kuonge
zeka kila mwaka
hadi kufikia 60% ya mwaka
huu!!!!! Wizara ya Elimu na OWM-TAMISEMI baada
ya matokeo mabaya ya mwaka 2010 walifanya “utafiti kudadisi sababu za ufaulu huo mbaya” na taarifa yake ipo
kwenye maktaba a Wizara” na iliandaliwa kauli ya waziri isomwe Bungeni”, lakini hadi leo haikusomwa. Ukweli ulifichwa; na mficha ugonjwa kifo
kitamuumbua. Nukuu zangu kutoka Taarifa moja
isiyo ya siri ya ndani ya wizara ya Elimu.
“Kwa
maoni yangu maboresho ya Elimu ya Serikali ya Awamu ya Tatu ambayo yanaweza kusomwa katika maandiko mawili
ya Wizara ya Elimu yaitwayo: (a) Nyaraka za Elimu 1999 hadi
2005, na ( b) Sheria ndogo za Elimu au kanuni za Elimu zilizotungwa kuyapa
maboresho hayo uzito w akisheria
yamepelekwa NYARAKA ZA KALE (ACHIVES) kabla
ya wakati wake….Maboresho yamewekwa kando moja baada ya jingine au
hayakusimamiwa ipasavyo na Elimu yetu imerudi ilivyokuwa kabla ya mwaka 2000”
Kuhusu ushauri
wake kwa elimu ya Tanzania
alisema kuwa Elimu ni nyenzo muhimu sana kuliko zote katika kuboresha nguvu kazi
ya Taifa na kuchochea maendeleo ya nchi ameamua kutonyamaza na kuwa muwazi
kabisa, ingawaje mimi ni mwanasiasa niliyestaafu.
Kwa hiyo NASHAURI mambo yafuatayo:
Kwanza kuwe na utaratibu sahihi wa kupanda madarasa kwa ufaulu (
achievement based progression) uliowekwa
na waraka wa Elimu Na. 1& 2 wa 2002 urejeshwe na uimarishwe bila
kuchelewa kuasnzia Darasa la kwanza,
la pili na la Tatu ambayo
Mwalimu Mkuu siku zote anayo madaraka
ya kukalilisha, kama mwanafunzi
hajazijua “K” 3: kusoma, kuandika na kuhesabu.
Alisema
Mungia kuwa jambo la pili
ni tume ya Mhe. Waziri Mkuu ifanye kwanza REJEA ya maandiko ya Wizara ya
Elimu niliyoyataja akatika 4(a) na (b)
hapo juu yaliyomo maboresho ya elimu ya 2002-2005 yaliyofanikisha
kufaulu vizuri katika Elimu ya Msingi na Sekondari miaka ya 2004-2007; badala ya kutumia muda
mwingi na fedha nyingi kugundua upya gurudumu.
Wakati
jambo la tatu alisema ni Taasisi ya
Elimu Tanzania ( Tanzania Institute of
Education –TIE) iagizwe na iachiwe
kutekeleza wajibu wake wa
kisheria chini ya Sheria ya Elimu ya 1995 wa kuandaa na kuboresha mitala.
Pia
wanasiasa tuache kuamua bila kuzingatia
ipasavyo utafiti na ushauri wa kitaaluma kuhusu Elimu ya Taifa letu.
“Kutokana na uamuzi mbaya na kuchelewa kuchukua hatua ya marekebisho kila inapobidi; Elimu yetu
imerudi ilikokuwa kabla ya mwaka 2000.
Rika zima la kielimu limepotea!!!sasa tunavuna kilichopandwa vibaya. Kwa hiyo TUJISAHIHISHE kwa kuacha
kuingilia na kuamua bila kuzingatia
utafiti na ushauri fwa kitaaluma ili tusije kuumbuliwa tena na matokeo
mabaya kama hayo ya kidato cha Nne ya mwaka 2012. Aidha inafaa matokeo ya
mitihani yawe yanatangazwa kwa uwazi
hata kama ni mabaya kwa sababu, narudia “ anayeficha maradhi kifo kitamuumbua”
No comments:
Post a Comment