Pages

Pages

Friday, April 26, 2013

Breking neeeeeeeeews:Hatimaye Lema apigwa pingu,atupwa rumande

Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema akizungumza na wanahabari             Arusha, Tanzania
TAARIFA  zilizotufikia hivi punde zinadai kwamba Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema amekamatwa na Askari wa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha, imedaiwa kwamba Lema alikamatwa usiku baada ya Polisi kuamua kuvunja mlango wa nyumba yake.
Majira ya saa tisa usiku Habar mpya ilizungumza na Mbunge huyo na kudhibitisha kuwa Askari hao waliizingira nyumba yake kwa lengo la kumtoa, hata hivyo Mbunge huyo akuweza kumalizia sentesi yake na simu ikakatika na alipotafutwa tena siku yake iliita bila kupokelewa na badala yake ilizimwa.
Taarifa hizo zimeeleza kwamba baada ya mabishano ya muda mrefu nyumbani kwa kada huyu hatimaye alikubali kukamatwa na kuchukuliwa na gari la Polisi usiku na kupelekwa kituo kikuu cha polisi Arusha (Central Polisi).
Kukamatwa kwake kulikuja baada ya polisi kuvunja mlango na kuingia ndani na kuendesha msako wa nguvu humo ndani vifaa vyake mawasiliano kama  laptop, ipad na simu vipo mikononi mwa Polisi.

Taarifa za nyumba ya Mbunge huyo kuzingirwa na Askari hao zilisambaa haraka mjini Arusha na wananchi wengi wakajitokeza kushuhudia tukio hilo,b
aada ya kumfikisha Lema Central police Arusha alisachiwa na kuingizwa lumande.
Lema alikuwa ameambatana na magari ya wafuasi wa Chadema waliomsindikiza ili kushuhudia kinachojili hapo kituoni, baada ya kumtupa ndani,polisi  waliwafukuza wafuasi hao wa Chadema hapo kituoni na kuwaambia hawatakiwi kuonekana hapo...
Chanzo: habari mpya

LEMA: RC AMENITUMIA UJUMBE WA VITISHO.

Kwa ufupi
“Kwanza nani kamwambia anataka kukamatwa? Yeye anatakiwa kusaidia polisi, kwani wale vijana 13 waliokamatwa kwa ajili yake wapo mahabusu anasubiriwa atoe maelezo.”http://www.mwananchi.co.tz

ARUSHA. 
MBUNGE wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amedai kupokea ujumbe wa vitisho kwa simu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Lema alidai kuwa ujumbe huo umeandikwa kupitia simu ambayo namba 0752960276 na unaosomeka: “Umeruka kihunzi cha kwanza, nitakuonesha kuwa mimi ni serikali, ulikojificha nitakupata na nitakupa kesi ninayotaka mimi.”
Alisema baada ya kupata ujumbe huo, alimjibu kuwa “nimekupata nimekuelewa nipo tayari kwa lolote.”
Hata hivyo, Mulongo amekana kumtumia Lema ujumbe huo... “Nimepata hizi taarifa wewe ni kama mtu wa nane kuniuliza. Sijatuma huo ujumbe na siwezi kuwa na mawazo ya kumtumia ujumbe huo kwani kama ningetaka kumkamata tangu jana pale Chuo cha Uhasibu ningemkamata.”

Hata hivyo, alihoji sababu za mbunge huyo kujificha kama anajijua kwamba hana kosa. “Kwanza nani kamwambia anataka kukamatwa? Yeye anatakiwa kusaidia polisi, kwani wale vijana 13 waliokamatwa kwa ajili yake wapo mahabusu anasubiriwa atoe maelezo.”

kuwa na mawazo ya kumtumia ujumbe huo kwani kama ningetaka kumkamata tangu jana pale Chuo cha Uhasibu ningemkamata.”

Hata hivyo, alihoji sababu za mbunge huyo kujificha kama anajijua kwamba hana kosa. “Kwanza nani kamwambia anataka kukamatwa? Yeye anatakiwa kusaidia polisi, kwani wale vijana 13 waliokamatwa kwa ajili yake wapo mahabusu anasubiriwa atoe maelezo.”
Alisema Mbunge huyo, anajua kazi ambayo, ilifanya chuo cha uhasibu na ndiyo sababu anajificha... “Alifanya kazi yake nikazomewa, kama ningetaka kutumia madaraka yangu asingekuwa salama … nadhani Lema anahitaji kusaidiwa ili abadilike.”
Kuhusu madai ya kujificha, Lema alisema haitajisalimisha polisi licha ya Mulongo kuagiza akamatwe kwa kuwa kuna taratibu za kufuatwa polisi inapomhitaji mbunge ambaye amechaguliwa na watu.

Alisema kama polisi wanamuhitaji, wanapaswa kumuita na pia kuwasiliana na Ofisi ya Spika wa Bunge.

“Naomba ieleweke kuwa mimi sijawakimbia polisi, siogopi kesi na wala siogopi jela nitaendelea na shughuli zangu waje kunikamata barabarani,” alisema Lema.

Akizungumzia tukio la juzi, Lema alidai kuwa mkuu huyo wa mkoa ndiye aliyekuwa chanzo cha vurugu kwa kukosa weledi wa kuzungumza na wanafunzi wenye majonzi.

Alisema alikwenda chuoni hapo baada ya kuitwa na wanafunzi na kabla ya kuzungumza, alikutana na uongozi wa chuo, akiwamo Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Arusha.
“OCD Arusha aulizwe kazi ambayo nilifanya kutuliza hasira za wanafunzi na tutasambaza DVD zaidi ya 3,000 kwa wakazi wa Arusha kujionea tukio hili ambalo sasa limebadilishwa na kuwa la kisiasa,” alisema Lema.
Mwanafunzi, Henry Kago(22) aliyeuawa kwa kuchomwa kisu na watu wasiojulikana na kusababisha wanafunzi kucharuka chuoni hapo anatarajiwa kusafirishwa leo kwenda Iringa kwa mazishi.

SOMA MAGAZETI YA LEO IJUMAA ARIL 26/ 2013.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

UDHALILISHAJI KWA WANAMKE KATIKA KUMBI ZA STAREHE.

HUU NI UZALILISHAJI KWA MWANAMKE WA KITANZANIA LKN WAKO WAPI WALE WATETEZI WA KUTETEA HAKI ZA WANAWAKE ?.
UDHALILISHA HUU UNAFANYWA KATIKA KUMBI ZA BAR ZA STAREHE ILI KUVUTIA WATEJA, SERIKALI IANZE KAZI YA KUDHIBITI WAMILIKI WA KUMBI WANAORUHUSIWA VITENDO HIVI NA WANAWAKE WENYE NAO WACHUKULIWE HATUA KALI ZA KISHERIA KWANI TUNA AMINI KUWA TABIA HIZI ZINAWEZA KUKOMESHWA NA MAMLAKA HUSIKA.

 JE HAKUNA KAZI NYINGINE ZAIDI YA KUJIDHALILISHA KATIKA KUMBI ZA STAREHE ?.

Monday, April 22, 2013

CHADEMA,,CCM NI MAKOMBORA

Wabunge waliosimamishwa ni Tundu Lissu (Singida Mashariki), Godbless Lema (Arusha Mjini), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Mbeya Mjini), Highness Kiwia (Ilemela), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini) na Ezekiah Wenje (Nyamagana).http://www.mwananchi.co.tzKatibu mkuu wa CCM taifa Abdulahaman Kinana akiwahutubia wanachama hicho na wananchi katika mkutano wa hadhala wa kuimarisha uhai wa chama hicho katika ziara ya siku tisa ambapo ilihitimishwa katika uwanja wa shule ya Kiwanja cha Ndege mkoani Morogoro. Picha Juma Mtanda.
MWANZA. 
WABUNGE sita wa Chadema waliosimamishwa bungeni wameamua kwenda kuwashtaki Spika Anne Makinda na Naibu wake Job Ndugai kwenye majimbo yao.

Wakitangaza uamuzi huo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi ya Mbugani, Mwanza jana, walisema pia watakwenda kwenye majimbo ya wabunge wawili wa CCM, Mwigulu Nchemba (Iramba Magharibi) na Livingstone Lusinde (Mtera) ili kueleza jinsi wabunge wa upinzani wanavyokandamizwa bungeni.

Ndugai, ambaye ni Mbunge wa Kongwa (CCM), aliwasimamisha wabunge sita wa Chadema kuhudhuria vikao vitano vya Bunge kutokana na kile alichokiita kufanya vurugu bungeni. 

Hatua hiyo ya Ndugai aliyoichukua Aprili 17, mwaka huu ilipata baraka za Spika Makinda Ijumaa iliyopita.

Wabunge waliosimamishwa ni Tundu Lissu (Singida Mashariki), Godbless Lema (Arusha Mjini), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Mbeya Mjini), Highness Kiwia (Ilemela), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini) na Ezekiah Wenje (Nyamagana). Katika mkutano huo ulioanza saa 9.30 alasiri na kumalizika saa 12.00 jioni, ulihudhuriwa na wabunge wanne kati ya hao. 

Mbilinyi ndiye aliyekuwa wa kwanza kuhutubia akifuatiwa Mchungaji Msigwa, Kiwia na Wenje. Lissu na Lema hawakuhudhuria.

Akizungumzia ziara yao katika majimbo ya viongozi hao wa Bunge, Mchungaji Msigwa alisema itakuwa ya kuwashtaki kwa kuendesha Bunge kuwapendelea wabunge wa CCM hata wanapofanya makosa ya wazi.

Alidai kuwa wabunge wa CCM ndiyo vinara wa lugha chafu bungeni na kuwatolea mfano Mwigulu na Lusinde. 

Pia alizungumzia tusi zito lililotolewa na Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba, Aprili 17, mwaka huu.

“Kila mtu alimshuhudia Serukamba alipoporomosha tusi zito, lakini Spika na Naibu wake hawakuchukua hatua zozote.

“Lissu na sisi wengine tumeadhibiwa kwa kosa la kuomba mwongozo wa Spika. Hapa wananchi mnaona kuna haki kweli, ?” alihoji Mchungaji Msigwa huku akishangiliwa na wafuasi wa chama hicho.

Alisema watapita kwenye majimbo ya wabunge wa chama hicho waliosimamishwa ili kuwaelimisha wapigakura wao.

Alisema wataanza ziara majimboni kesho wakianzia Iramba Magharibi kumshtaki Nchemba. Baada ya hapo watakwenda Singida Mashariki kwa Lissu ili kuwapa ukweli wapigakura wake.

Mchungaji Msigwa alisema baada ya hapo watakwenda Kongwa kwa Ndugai na kisha Mtera kwa Lusinde kabla ya kuelekea Njombe Kusini kwa Makinda. Pia watakwenda Iringa, Mbeya, Kilimanjaro na Arusha.

Hata hivyo, ziara ya wabunge hao kwenda mkoani Mbeya imekwaa kisiki baada ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Athumani Diwani kukataa kutoa kibali.

Kumlipua kigogo CCM
Mchungaji Msigwa ameahidi pia kulipua bomu la kigogo wa ngazi ya juu wa CCM, ambaye alidai kuwa anajihusisha na ujangili wa meno ya tembo atakaporejea bungeni baada ya kumaliza adhabu yake wiki hii.

Wenje ataja safu ya 2015
Wenje aliwaambia wafuasi wa chama chake kuwa kimejipanga kushinda Uchaguzi Mkuu wa 2015 na CCM wanapaswa kujipanga kuondoka madarakani.

Alitoa kali alimpotaja Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa kuwa Rais na Freeman Mbowe, Waziri Mkuu. 

Wengine aliowataja na kuwapa vyeo ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Waziri wa Fedha), Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Kilimo), Lema (Mambo ya Ndani), John Mnyika (Nishati) na Wenje (Mambo ya Nje).

PROF. LIPUMBA: WAKAZI WENGI WA DAR ES SALAAM WANAKABILIWA NA UMASKINI WA KUPINDUKIA

1
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba, amesema theruthi tatu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wanakabiliwa na umasikini wa kutisha kutokana wakazi wake kuishi kwa sh 640 kwa siku.
Akizungumza na wandishi wa habarijijini jana, Lipumba alisema  Kongamano la kujadili maendeleo ya mkoa huo,limeandaliwa na chama chake,Taasisi ya Demokrasia ya nchini Denmark huku washiriki 130 kutoka taasisi za serikali, viongozi wa dini na mashirika.
Lipumba alisema chimbuko la umasikini huo ulichangiwa na ongezeko la watu huku wengi wao wakikabiliwa na ukosefu wa ajira za kuelewka.
Alisema jiji hilo lenye idadi ya wakazi wapatao milioni 4.5, kati ya hao ni milioni 1.3 wenye ajira, wengine ajira zao ni zile za kubahatisha.
 “Haingii akilini kwa maisha ya jiji la Dar es Salaam mtu aweze kuishi kwa sh 640 hii si kweli, wote tunajua maisha ya jiji hili yalivyo”alisema.
 Katika kupunguza tatizo la ajira, Lipumba alisema mikakati ya makusudi ya kuanzisha viwanda ambavyo vitachechemua uchumi.
Alivitaja baadhi ya viwanda hivyo ni vya ngozi, mavazi, umeme, viatu na vingine ambapo alitahadharisha kuwa kusiwe na urasimu kwa watu watakaojitokeza kwa ajili ya kutaka kuanzisha viwanda hivyo.  
 Aidha, sekta ya elimu bado inakabiliwa na changamoto lukuki ambazo zinahitaji mjadala mpana katika ambao utasaidia kuupatia ufumbuzi wa kudumu.
 Alisema bila ya kuwa na elimu bora ambayo itazalisha wataalamu mbambali wakiwemo wale wa sayansi, nchi hii haiwezi kusonga mbele  kimaendeleo, ambayo ni kiu ya muda mrefu kwa wananchi.
 “Na hii elimu yetu bado inakabiliwa na matatizo kutokana watoto wetu kufundishwa lugha ya Kiswahili na wanapofika sekondari lugha inayotumika ni kingereza hali inayowafanya wafeli mitihani yao”alisema.
 Ukiachilia mbali wanafunzi hao kushindwa matumizi ya kingereza bado wapo ambao wanamaliza elimu ya msingi hawajui kusoma vitabu vya Kiswahili.
Baadhi ya washiriki kwa nyakati tofauti walisema ukusanyaji wa makato bado katika Halmashauri hauridhishi, wakati mwingine yanayokusanywa ni asilimia 40 lakini mipango yake yanazidi ya kawaida kwa asilimia 70.
 Mratibu wa Kongamano na Taasisi ya vyama na Demokrasia (DIPD), Anemon Birkebaek, alisema atatumia uzoefu wake kwa kuwaunganisha vijana wa Denmark na wapa ili waweze kubadilishana uzoefu katika kujiletea maendeleo.

Saturday, April 20, 2013

WATU MILIONI 14 WANUFAIKA NA HUDUMA YA MATIBABU YA MABUSHA NA MATENDE TANZANA: DK. MWELE.

Wilaya 94 zimefikiwa katika zoezi la unyweshaji dawa za Matende na Mabusha  na utoaji elimu linaloendeshwa chini ya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti magonjwa yasiyopea kipaumbele (NTD) unaoratibiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Mkurugenzi Mkuu wa NIMR Dakta Mwelecele Malecela ameyasema hayo mjini Arusha wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika Kongamano la 27 la taasisi hiyo la  Sayansi la Kongamano la Pili la Afya Moja Afrika  linaloendelea mjini humo.
Dk. Malecela amesema watu milioni 14 wamenufaika na huduma ya matibabu ya mabusha na matende  katika wilaya hizo 94 ambazo zimefikiwa katika zoezi la ugawaji dawa na tiba.
Aidha alieleza kuwa katika wilaya ya pangani jumla ya watu mia mbili waliokuwa wanasumbuliwa na mabusha wamepatiwa tiba kwa njia ya upasuaji na tayari wamerejea katika hali ya kawaida na kuweza kuendelea na shughuli za maendeleo ya jamii yao.

Dk. Malecela amesema Programu ya kudhibiti Metende na Mabusha imeandaa mkakati maalum wa elimu kwa umma utakaowawezesha watanzania kupata elimu na mbinu za kuwawezesha kushiriki harakati za kitaifa za kutokomeza magonjwa hayo nchini ambayo yameleta hofu na mashaka katika jamii kufuatia imani potofu.
Mkurugenzi Mkuu huyo wa NIMR ameitaka jamii kushiriki katika zoezi la unyweshaji dawa kwa miaka mitano mfululizo bila kuchoka ili kuweza kumaliza dozi na hiyvo kuweza kujikinga na maambukizi na hatimaye kutokomeza magonjwa hayo.
Dk. Malecela amesema Wilaya ya Tandahimba, mkoani Lindi imefanikiwa  kupunguza wagonjwa wa matende na mabusha na kufikia kiwango cha chini ya asilimia moja kutokana na  jitihada za pamoja zinazoendelea za kutokomeza magonjwa hayo chini ya Mpango wa Taifa wa Kutokomeza magonjwa yasiyopewa Kipaumbele.
Pamoja mbu wa malaria aina ya Anopheles, ugonjwa wa Matende na mabusha pia huambukizwa kwa na mbu aina ya  Culex. 
Magonjwa haya  pia husababishwa na minyoo inayoishi kwenye damu na maji damu ambayo husababisha madhara makubwa kwenye miguu ,matiti, mikono na makende.
Mbu aina ya Anopholes huweka mazalia yake katika maji yaliyotuama ambapo Culex huweka mazalia yake katika maji machafu yakiwwemo yale katika mashimo ya choo na madimbwi.
Aidha Dk.Mwele amesema kuwa serikali imefanya jitihada kubwa sana kwani mfuko wa rais wa kupambana na matende na mabusha umeonyesha mafanikio makubwa na kuwezesha watu kupata matibabu kwa njia ya upasuaji.
Wagonjwa 480 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa mabusha katika mkoa wa Lindi katika mwa huu, ambapo wagonjwa 54 kati yao wamekwishafanyiwa upasuaji huo Mwezi April mwaka huu.

Dk. Mwele Malekela ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa NIMR akifungua Mjadala juu ya Utafiti wa udhibiti wa ugonjwa wa mabusha na matende kwa nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Baadhi ya washiriki ambao ni watafiti wakifuatilia mada za mjadala huo.
Dk. Upendo Mwingira akitoa mada yake juu ya matumaini ya kutokomeza Ugonjwa wa Matende na Mabusha hasa kufuatia utafiti wake Wilayani Tandahimba.
Mmoja wa watafiti
Sehemu ya washiriki wakifuatilia majidiliano hayo juu ya ugonjwa wa matende na Mabusha.
Watoa mada mbali mbali kutoka nchi za Afrika wakitoa mada zao juu ya Tathmini ya ugonjwa wa Mabusha na Matende katika nchi zao.