Arusha, Tanzania
TAARIFA zilizotufikia hivi punde
zinadai kwamba Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema amekamatwa
na Askari wa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha, imedaiwa kwamba Lema
alikamatwa usiku baada ya Polisi kuamua kuvunja mlango wa nyumba yake.
Majira ya saa tisa usiku Habar mpya
ilizungumza na Mbunge huyo na kudhibitisha kuwa Askari hao waliizingira
nyumba yake kwa lengo la kumtoa, hata hivyo Mbunge huyo akuweza
kumalizia sentesi yake na simu ikakatika na alipotafutwa tena siku yake
iliita bila kupokelewa na badala yake ilizimwa.
Taarifa hizo zimeeleza kwamba baada ya mabishano ya muda mrefu nyumbani kwa kada huyu hatimaye alikubali kukamatwa na kuchukuliwa na gari la Polisi usiku na kupelekwa kituo kikuu cha polisi Arusha (Central Polisi).
Kukamatwa kwake kulikuja baada ya polisi kuvunja mlango na kuingia
ndani na kuendesha msako wa nguvu humo ndani vifaa vyake mawasiliano
kama laptop, ipad na simu vipo mikononi mwa Polisi.
Taarifa za nyumba ya Mbunge huyo kuzingirwa na Askari hao zilisambaa haraka mjini Arusha na wananchi wengi wakajitokeza kushuhudia tukio hilo,b aada ya kumfikisha Lema Central police Arusha alisachiwa na kuingizwa lumande.
Taarifa za nyumba ya Mbunge huyo kuzingirwa na Askari hao zilisambaa haraka mjini Arusha na wananchi wengi wakajitokeza kushuhudia tukio hilo,b aada ya kumfikisha Lema Central police Arusha alisachiwa na kuingizwa lumande.
Lema alikuwa ameambatana na magari ya wafuasi wa Chadema waliomsindikiza ili kushuhudia kinachojili hapo kituoni, baada ya kumtupa ndani,polisi waliwafukuza wafuasi hao wa Chadema hapo kituoni na kuwaambia hawatakiwi kuonekana hapo...
Chanzo: habari mpya
No comments:
Post a Comment