.

.
Saturday, April 20, 2013

1:18 AM
  


Naibu katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Dr Patrick Makungu, akisoma hutuba ya kufunga  Kongamano la 27 la Sayansi la Taasisi ya taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binanamu Tanzania (NIMR)na kongamano la pili la afya moja afrika  lililoandaliwa na  Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kwa kushirikiana na Kituo cha Utafiti na Udhibiti wa Magonjwa Ambukizi cha Nchi za Kusini mwa Afrika (SACIDS) na Mtandao wa “Afya Moja” Afrika ya Kati na Mashariki (OHCEA) na kufanyika kwa siku nne kuanzia tarehe 16-19 April 2013 katika Hoteli ya Snow Crest, Arusha. Dk. Makungu alifunga kongamano hilo kwaniaba ya Katibu Mkuu wake, Dk Florens Turuka. 

Katika Mkutano huo pia wanasayansi chipukizi kadhaa walitunukiwa tuzo mbalimbali zikiwapo tuzo ya Mwanasayansi bora anaechipukia iliyotoka kwa Prof. Wencelaus Kilama na kuchukuliwa na Emmanuel Kifaro pamoja na Grades Stanley, Tuzo ya ya Kisayansi ya Mlima Kilimanjaro ilikwenda kwa Erick Lymo na Alfred Geofrey, Tuzo ya Mwanasayansi bora Mwanamke Kijana iliyotoka kwa Dr. Maria Kamm na ilichukuliwa na Zainab Mchome.

Naibu katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Dr Patrick Makungu, akimkabidhi Tuzo Erick Lymo aliyetwaa Tuzo ya Kisayansi ya Mlima Kilimanjaro





Naibu katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Dr Patrick Makungu, akimkabidhi Tuzo Grades Stanley aliyetwaa Tuzo ya Mwanasayansi Anayechipukia.




Naibu katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Dr Patrick Makungu, akimkabidhi Tuzo Zainab Mchome aliyetwaa Tuzo ya Mwanasayansi Bora Mwanamke Kijana.





Naibu katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Dr Patrick Makungu, akimkabidhi Tuzo Alfred Geofrey aliyetwaa Tuzo ya Kisayansi ya Mlima Kilimanjaro.


 Mgeni Rasmi na viongozi wa meza kuu wakipiga pichya pamoja na  Washindi wa Tuzo hizo za Kisayansi kwa Wanasayansi Chipukizi ambapo lengo ni kuhamasisha zaidi Vijana hao katika kujiendeleza na kufanya tafiti za kina.
*******  ********

0 comments:

Post a Comment