Makazi
ya muda ya waathirika wa mafuriko kijiji cha Mateteni baada ya nyumba
zao kumoka kutokana na maji ya mafuriko hayo. PHOTO/MTANDA BLOG
MOROGORO.
KAMATI ya Maafa Mkoa wa Morogoro
inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya Kilosa, Elias Tarimo imeshindwa kutoa
takwimu za waathirika wa mafuriko ndani ya siku moja kama ilivyoagizwa
na Rais Jakaya Kikwete mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mafuriko
hayo yalitokea katikati ya wiki iliyopita Kijiji cha Magole na
kusababisha uharibifu mkubwa wa mali na miundombinu. Pia, yalisomba
nyumba, vyakula na vifaa mbalimbali vya nyumbani, mahakama na shule.
Akizungumza
na Redio One jana, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera alisema kazi
inaendelea kwa sababu wanataka kuhakiki watu halisi waliopatwa na maafa
hayo.
“Tunataka kutumia fursa hii kumwambia Rais kuwa
tulighafilika hata kutoa takwimu zile za watu 12,000, ambazo (Rais)
alisema hazina uhalisia... kwa sasa tunataka kufanya uhakiki wa kina
tujue thamani ya hasara,” alisema Bendera na kuongeza:
“Tunataka
kujua hasa mali zilizoharibiwa, kuna nyumba zilizobomoka kabisa, kuna
zilizoingiliwa na maji lakini hazikubomoka, kuna zilizoharibiwa nusu,
kuna watu wangapi wanahitaji misaada ya haraka na huduma nyingine.”
Mwandishi
wa habari hizi aliyefika eneo la tukio, alishuhudia kazi ya uhakiki
ikiendelea maeneo yaliyoathirika huku Tarimo akishiriki kufanya kazi
hiyo.
“Kazi ipo hatua za mwisho hadi leo (jana) jioni
tunatarajia kukamilisha uhakiki na kumkabidhi mkuu wa mkoa...kwa sasa
tupo hatua za mwisho mwisho na itakapokuwa tayari nitawapatia bila
kuficha,’’ alisema Tarimo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mvomero,
Anthony Mtaka alisema wilaya inaendelea na uhakiki na kwamba, watatoa
taarifa baada ya kukamilika ambayo itakuwa
No comments:
Post a Comment