Mwenyekiti wa TACINE Atanasi Kapunga akiongea katika mkutano huo |
Mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela Akiwa anafungua rasmi mkutano wa umoja wa majiji TACINE uliofanyika jiji Arusdha hivi leo |
washiriki wa mkutano mkuu wa TACINE wakiwa wanamsikiliza mgeni rasmi akiwa anafungua mkutano
Wito umetolewa kwa Halimashauri zote nchini kutafuta njia
mbadala za kuongezea Mapato yake ya ndani
tofauti na ilivyizoeleka kutegemea mapato yatokanayo na ushuru
mbalimbali wanaokusanya katika halimashauri zao.
Wito huo umetolewa jana
na mkuu wa ya wilaya ya Arusha John Mongela wakati akifungua mkutano mkuu wa asasi
ya umoja wa majiji Tanzania TACINE inaowakutanisha wakurugenzi pamoja na mameya wa majiji
tanzania uliofanyika mkoani hapa.
Alibainisha kuwa watendaji wa halimashauri zote hapa nchini wanatakiwa kuangalia namna
ya kuleta maendeleo katika halimshauri zao kwa kuunda miradi mikubwa yenye tija
ambayo inaweza kukuza mapato ya halmashauri zao.