Chemba iliyobomoka ikiwa wazi maeneo ya Mwenge
Hapa ni chemba Hiyo ambayo ipo wazi na pembeni ya barabara ya mwenge kukunja kuelekea mama ngoma
Mawe yakiwa yamewekwa kuzuia magari yasipite hapo baada ya chemba hiyo kubomoka
Hapa ni njia ya kukunja ya magari yanayotoka Njia ya mama ngoma eneo la mwenge
Chemba iliyobomoka maeneo ya mwenge jiji dar imekuwa kero
kwa watumiaji wa barabara ya kutoka mwenge kuelekea afrika sana.Chemba
hiyo ambayo ilibomoka baada ya gari la mizigo kutumbukia hapo na
kusababisha kuharibika kwake.Mtandao wetu wa Dj sek blog ulifanya
mahojiano na waendesha bajaj na wafanyabiashara wa eneo hilo ambao
walisema shimo hiilo limekuwa ni hatari kwa watumiaji wa barabara hiyo
kwani kuna magari mengi yametumbukia hapo baada ya kupasuka kwa shimo
hilo.
Waliongeza kuwa baada
ya chemba hiyo kupasuka Dawasco walikuja wasafisha tu uchafu uliokuwemo
humo na kuweka alama za tahadhari kisha wakaondoka.Sasa imepita
takribani wiki moja sasa toka dawasco wameliona tatizo hilo lakini
hakuna matengenezo yoyote ya chemba hiyo,pia wameongeza kwa kusema
ifikapo jioni huwa shida sana kwa magari kupishana eneo hilo kwani
magari yanayotoka afrika sana inabidi kukunja kwa kutumia upande wa
magari yanayotoka barabara inayotoka kwa mama ngoma,hivyo kusababisha
foleni kubwa na usumbufu.Watumiaji wa eneo hilo wameiomba manispaa ya
Kinondoni kutatua tatizo hilo kwani mvua zinazoendelea kunyesha zitaleta
madhara kwa kuwa chemba hiyo itakuwa inamwaga maji machafu nje ambayo
itapelekea magonjwa.
No comments:
Post a Comment