Na Bertha Ismail-Arusha
Makocha na wataalam wa soka toka TFF wameonyesha kuridhishwa
na viwango vya wachezaji wa timu za mikoa ya Arusha na Manyara kwenye michezo ya
mashindano ya kuwasaka nyota wa soka watakaoiongezea nguvu timu ya Taifa stas.
Hali hiyo imeonekana baada ya mechi kabambe ya awali
iliyochezwa na timu za mikoa hiyo miwili iliyofanyika kwenye uwanja wa sheikh
Amri Abeid ulioko jijini Arusha.
Mashindano hayo ya TFF yanayoshirikisha mikoa yote ya hapa
nchini kwa kuwashindanisha mikoa miwili miwili na timu zao za mikoa kwa vijana
wenye umri chini ya miaka 25 lengo ni kupata wachezaji bora watakaounda timu
mpya ya Taifa star ili kuiboresha timu iliyopo hapa nchini na nje ya nchi.
Kocha Keneth Mwaisabula akizungumza baada ya mchezo huo
uliomalizika kwa timu ya mkoa wa Arusha kuibuka ushindi wa magoli 2-1 alisema
kuwa ameridhishwa na viwango vya wachezaji hao ambapo wamepata matumaini ya
kupata timu mpya nzuri itakayomudu ushindani.
“Kwa mchezo huu tu pekee kabla ya kwenda kwenye mechi nyingine
Manyara tumeshapata matumaini ya kupata
wachezaji wenye uwezo wa kuichezea timu ya Taifa star ukizingatia hata maumbo
yao pia yanaongeza kiwango cha matumaini”
Akizungumzia mashindano hayo Mwaisabula alisema kuwa mpango
huo wa TFF wa kusaka wachezaji wenye uwezo wa kuichezea timu ya Taifa utakuwa
na mafanikio makubwa kutokana na uwezo unaoonyeshwa na timu hizo za mikoa hasa
katika ushambuliaji.
“Nahisi mpango huu wa kusaka nyota wa soka utakuwa na mafaniko
makubwa kwani katika michezo iliyochezwa mkoa wa Kilimanjaro kati ya timu ya
mkoa huo naTanga pamoja na huu wa Arusha na Manyara tumeshuhudia wachezaji
wengi wenye uwezo wa hali ya juu ila wameshindwa kuonekana kwa kuwa tu hawachezi
katika timu za madaraja ya juu” alisema Mwaisabula.
Aidha mashindano hayo yaliyofanyika katika uwanja wa Sheik
Amri Abeid jijini Arusha uliibua furaha za wakazi wa mji huo kwa kelele na
shangwe baada ya kushuhudia mchuano mkali baina ya timu hizo mbili hasa baada
ya kujipatia bao la kwanza la kichwa lililofungwa dakika ya 18 kutoka kwa kapteni
wake Salum Wally baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Ramadhani Yego.
wachezaji wa ziada ya timu ya Arusha |
Goli hilo lililobaki hadi mda wa mapumziko ililipa changamoto
timu ya Manyara na faraja kwa timu ya Arusha ambapo baada ya kurudi uwanjani
iliongeza goli la pili dakika ya 52 kutoka kwa Joseph msafiri goli ambalo
liliinua hasira za wachezaji wa Mkoa wa Manyara ambapo Chunga Said Zito
aliipatia timu yake ya mkoa wa Manyara goli moja la kifuta machozi dakika ya
65.
Timu hizo mbili zinatarajia kucheza mechi nyingine ya
marudiano jumatano ya wiki hii marchi 5 katika mkoa wa Manyara ili
kujihakikishia upatikanaji wa nyota hao kwa usahihi zaidi.
No comments:
Post a Comment