Mrembo Eveline katika picha ya pamoja na wenzake waliotwaa tatu bora, ambapo kwa upande wa kushoto ni Happy Tarmo na kulia ni Merry Joel |
Mrembo Evaline
Baasa (19) amefanikiwa kutwaa taji ya Ulimbwende wa wilaya ya Kataru kwa mwaka
2014 na kuwabwaga wenzake wanane katika kinyanganyiro kilichofanyika katika
ukumbi wa Ngorongoro Camp uliopo mjini hapa.
Evaline amekua
mrembo wa kwanza kwa wilaya hiyo tangu kuanzishwa kwa wilaya ya karatu ambapo
alibahatika kujinyakulia kitita cha shilingi laki tano na pia kuingia katika
shindano la miss Arusha linalotarajiwa kufanyika mwezi june sambamba na hilo
amepata udhamini wa maandalizi yote kwa ajili ya kushiriki shindano lililoko
mbele yake.
Mshindi wa
pili alikuwa Happy Tarmo (19) ambaye alijinyakulia fedha taslim shilingi laki
tatu na kufuatiwa na Merry Joel (21) aliyezawadiwa shilingi laki mbili na
mshindi wa nne ikienda kwa Veronica John
(21) na washiriki wenzake watano ambapo alipata kifuta jasho cha shilingi elfu
themanini kila mmoja.
Hili
lilikuwa shindano la kwanza kwa wilaya ya Karatu ambalo lilikuwa kivutio kikubwa
kwa wakazi wa wilaya hiyo kufuatia ushindani mkubwa uliojitokeza kwa washiriki
wote kuwa na sifa zote hali iliyowapa kazi ya ziada majaji waliokuwa
wakiongozwa na mratibu wa miss kanda ya kaskazini Faustine Mwandago.
Mashabiki wa
tasnia ya urembo mjini Karatu waliokuwa wakiongozwa na diwani wa Karatu mjini Jubilate
Mnyenye walilipuka kwa shangwe baada ya jaji mkuu Mwandago kumtangaza
mlimbwende Evaline kuwa ndiye mshindi wa
miss Karatu 2014 matokeo yaliyoungwa mkono na wadau wote wa tasnia ya urembo
waliohudhuria onyesho hilo.
, Mlimbwende Eveline Baasa akiwa katika picha ya pamoja na majaji wa shindano hilo wakiongozwa na jaji mkuu Faustine Mwandago ( watatu kutoka kulia aliyvalia shati la mistari) |
Hili
linakuwa shindano la kwanza kwa ngazi ya kitongoji cha wilaya ya Karatu kwa mkoa
wa Arusha wenye vitongoji vitatu ambavyo ni Karatu, Monduli na kituo cha Arusha
mjini ( Arusha city center).
Aidha baada
ya kitongoji cha Karatu kumpata mrembo wake, wiki ijayo kinyang’anyiro cha pili
kitafanyika kitongoji cha monduli na
kitongoji cha mwisho kitakua cha arusha city
kitakachofanya baadae mwaka huu ikiwa ni mchakato wa kumpata miss Arusha.
Aidha kila
kitongoji kitatoa warembo wane kila kitongoji ambapo kutakuwa na jumla ya warembo
12 ambapo watashiriki katika kinyanganyiro cha kumsaka mrembo wa mkoa wa Arusha
Mgeni rasmi
katika shindano hilo la miss Karatu alikua ni mhifadhi mkuu wa mamlaka ya Ngorongoro
Fredy Manongi ambaye aliwakilishwa na afisa uhusiano wa mamlaka ya hifadhi ya
ngorongo Adam Akyoo ambaye aliwataka warembo kutumia fursa walionayo kupambana
na ujangili kwa kutoa taarifa za watu wanajishughulisha na ujangili.
Akyoo
alisema kuwa kupambana na ujangili siyo lazima kushika mitutu ya bunduki
kumzuia mwindaji bali utoaji wa elimu pia unaweza kusaidia kupunguza kama si
kumaliza kabisa tatizo la ujangili nchini.
Kwa upande
wake diwani wa karatu mjini, Jublet Mnyenye alisema kuwa amefurahishwa na
waandaji wa kinyang’anyiro hicho cha kumsaka mlimbwende wa Karatu pia karatu
mjini kuwa wenyeji wa mashindano hayo kwa mara ya kwanza wilayani humo ambapo
ameahidi kusapoti mashindano hayo mara nyingine yatakapofanyika kwa kujitolea
ukumbi, zawadi za washindi pamoja na maandalizi yote kwa ujumla.
Kinyanganyiro
hicho cha aina yake kilichoburudishwa na msanii Snura “mama wa majanga” kilidhaminiwa
na Makampuni mbalimbali na wadau wa urembo wilayani humo wakiwemo kinywaji cha Redd’s, ZARA tour, hifadhi ya
mamlaka ya Ngorongoro, Beauty point Cosmetics pamoja na mdau wa ulimbwende Mh,
Steven Siay.
Snura "mama wa majanga" alitoa burudani ya aina yake katia shindano hilo |
No comments:
Post a Comment