Dar es Salaam.
Suala la kukwama kufungwa kwa ndoa ya Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Vicky Kamata limechukua sura mpya baada ya mzazi mwenza wa mchumba wa mbunge huyo, kukanusha taarifa kwamba alikwenda Dodoma kwa lengo la kuomba msaada kwa viongozi wa Bunge.
Suala la kukwama kufungwa kwa ndoa ya Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Vicky Kamata limechukua sura mpya baada ya mzazi mwenza wa mchumba wa mbunge huyo, kukanusha taarifa kwamba alikwenda Dodoma kwa lengo la kuomba msaada kwa viongozi wa Bunge.
Kauli ya mama huyo imezidisha utata katika sakata
la kukwama kufungwa kwa ndoa hiyo iliyokuwa ifanyike Jumamosi baada ya
kutokea habari kuwa mwanamke mmoja alikwenda bungeni mjini Dodoma kutaka
kuonana na Spika kwa lengo la kuomba Bunge limsaidie kupata haki yake
kabla ya harusi hiyo kufungwa na hivyo kusababisha harusi kutofanyika.
Kamata, ambaye alijizolea umaarufu kutokana na
wimbo wake wa “Wanawake na Maendeleo” na baadaye kuingia bungeni katika
uchaguzi wa mwaka 2010, alikuwa afunge ndoa na mtu aitwaye Charles
Gardiner Jumamosi iliyopita jijini Dar es Salaam, lakini haikufanyika
kutokana na mbunge huyo kuwa mgonjwa kiasi cha kulazwa hospitali maeneo
ya Tabata.
Jana, Kinavi Dadi, ambaye ni mzazi mwenza wa Gardiner, alikanusha kufunga safari hadi Dodoma kwa lengo hilo.
“Ni kweli kwamba Charles ni baba watoto wangu,
lakini sijawahi kwenda Dodoma na wala sifahamu chochote kuhusu safari
hiyo. Nadhani inatosha,” alisema mama huyo na hakutaka mazungumzo zaidi.
Baadaye kidogo mmoja wa ndugu wa Kinavi, ambaye
aliomba asitajwe jina lake gazetini, alikiri ndugu yao kufunga ndoa na
Gardiner Juni 2004 na kujaliwa kupata watoto wawili, lakini
walitofautiana na baadaye ndoa yao kuvunjwa mwaka 2012.
“Ni kweli kwamba dada yetu alifunga ndoa na
Charles, lakini pia ni kweli kwamba walipeana takala halali two years
ago (miaka miwili iliyopita), kwa hiyo taarifa kwamba eti amezuia ndoa
isifungwe, siyo za kweli na wala huko Dodoma hajawahi kwenda,” alisema.
Alisema taarifa kwamba aliyepata kuwa mke wa
Gardiner alikwenda Dodoma kuomba msaada wa Bunge zimewaumiza sana kama
familia kutokana ukweli kwamba Kinavi ndiye anayefahamika kuwa mke wa
kwanza.
“Ndugu yetu analia sana kutokana na kuumizwa na
wale wanaomchafua. Sisi katika familia tumelelewa kwa maadili hivyo
Kinavi siyo mtu wa kuzuia ndoa ya Gardiner maana walishatengana,
mawasiliano yaliyopo ni yale yanayohusu watoto ambao wana haki ya wazazi
wote wawili. Hatujui waliozitangaza hizo habari walikuwa na malengo
gani,” alisisitiza.
Bungeni Dodoma
Wakati hayo yakiendelea, habari kutoka bungeni
Dodoma zinasema mwanamke aliyedaiwa kuwa mke wa Gardiner ni ‘feki’ na
alikuwa wa kutengenezwa na baadhi ya wabunge kwa lengo la kumtibulia
Kamata.
Mpango huo unadaiwa kuwahusisha wabunge wanawake
wanne; watatu kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) na mmoja kutoka Chadema
ambao awali waliapa kwamba ndoa ya mbunge mwenzao isingefungwa.
No comments:
Post a Comment