KOCHA
maarufu wa riadha, Samwel Tupa, ameulalamikia uongozi wa Riadha
Tanzania (RT), kwa kutumia jina lake kama kocha aliyeondoka na
wanariadha waliokwenda nchini New Zealand kwa maandalizi ya mashindano
ya Jumuiya ya Madola yanayotarajia kufanyika Glasgow, Scotland, Julai
mwaka huu.
Akizungumza kwa njia ya simu akiwa jijini
Arusha, Tupa alisema hajui sababu iliyofanya uongozi huo kufanya hivyo,
na kwamba mara ya mwisho aliwasiliana na Katibu Mkuu wa RT, Suleiman
Nyambui, ambaye alimtaka wabaki ili waandae mashindano ya taifa
yanayotarajiwa kufanyika Juni.
“Nyambui aliponiambia hivyo, nilimwambia mimi kama kocha siwezi
nikabaki wakati wanariadha wangu wanakwenda, huko watafundishwa na nani,
akadai watakuwa na kocha wa China, lakini mimi sikuafiki hilo na
nikajua watakuwa wamebadilisha jina la kocha anayeenda, ila cha
kushangaza naona kwenye vyombo vya habari kwamba nimeenda huko,”
alisema.
Alisema mbali na yeye kuachwa, pia wamemuacha mwanariadha mwingine,
Michael Damson, ambaye naye alikuwepo katika orodha ya kwenda na
aliambiwa apeleke pasipoti, ila kaachwa bila taarifa yoyote.
“Baniani mbaya kiatu chake dawa na kidole kidogo kinashika mpini wa
jembe, lakini hakiingii kwenye bakuli ya mboga, mimi siwezi kulalamika
sana, lakini ninachohoji kwanini watangaze jina langu kwamba nimekwenda
wakati nimeachwa bila kupewa taarifa yoyote?” alihoji kocha huyo wa
kimataifa ambaye ni mkufunzi pekee Tanzania wa mchezo huo
aliyethibitishwa na Shirikisho la Riadha la Kimataifa (IAAF).
Alisema kwa kuonyesha kwamba uongozi huo unakubali kazi zake,
waliamua kuondoka na mwanariadha wake, Michael Gwandu bila kumpa taarifa
na kuamua kuwasiliana na kocha msaidizi.
Alipotafutwa Rais wa RT, Anthony Mtaka, alitaka atafutwe makamu
wake, William Kallaghe, ambaye alidai ahusiki na benchi la ufundi,
hivyo atafutwe Kaimu Katibu Mkuu wa RT, Ombeni Zavalla, ambaye pia
alisema anayejua utaratibu wa safari hiyo ni Nyambui, yeye hajui lolote
No comments:
Post a Comment