Mkutano
wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
na wenyeviti wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kupata maoni yao juu
ya changamoto zilizojitokeza katika ligi hiyo umefanyika juzi (Mei 11
mwaka huu).
Klabu
za VPL zilizohudhuria mkutano huo ni Azam, Coastal Union, JKT Ruvu,
Mbeya City, Mgambo Shooting, Mtibwa Sugar, Polisi Morogoro, Ndanda FC,
Ruvu Shooting, Stand United na Tanzania Prisons.
Simba na Yanga hazikuhudhuria mkutano huo, na wala klabu hizo hazikutoa udhuru wowote wa kutokuwepo.
Maazimio
ya mkutano huo ni kuwa kwa misimu mitatu ijayo kuanzia msimu wa
2014/2015 klabu zimekubaliana ziruhusiwe kusajili wachezaji watano wa
kigeni. Kamati ya Utendaji ya TFF itatoa uamuzi wa mwisho juu ya suala
hilo katika kikao chake kijacho.
Pia
klabu hizo zimekubali timu zao za U20 kuanzia msimu ujao zicheze ligi
ya mkondo mmoja. Hata hivyo, utekelezaji wa hilo utategemea na
upatikanaji wa mdhamini wa ligi hiyo ambapo TFF inafanya jitihada za
kumpata mdhamini huyo.
Vilevile
Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake, Lina Kessy
amezishauri klabu za VPL kuanzisha timu za wanawake, ambapo klabu hizo
zimesema zitaufanyia kazi ushauri huo
No comments:
Post a Comment