Kijana akiwa amembeba nyoka baada ya kucharangwa kwa mapanga akitoka naye nje ya uzio wa kanisa hilo
Nyoka
aina ya chatu aliyetolewa nyumbani kwa mfanyabiashara maarufu jijini
Arusha Joseph Magesse akivutwa na wananchi kuelekea kwenye kanisa
katoliki la karsamatiki eneo la Sakina jijini Arusha ambapo aliuawa kwa
kucharangwa na shoka na wananchi wenye hasina na imani hizo za
kishirikina
MMOJA wawananchi akiwa ameshika shoka akiendelea kumchoronga chatu huyo
Mabaki ya mwili wa chatu huyo baada ya kucharanwa
Nyumba yamfanyabishara ambapo alikutwa nyoka huyo na chini ni sehemu ya magari ya mfanyabiashra huyo
Katika hali
isiyokuwa ya kawaida tukio la kuonekana kwa chatu mkubwa eneo la
sakina. kata ya kiranyi lilivuta hisia ya wakazi wa jiji la Arusha na
viunga vyake.
Tukio hilo
la aina yake kutokea katika jiji hili lilitokea majira ya saa moja na
nusu asubuhi wakati wenyeji wakiwa katika pilikapilika za kujiandaa
kwenda kwenye shuguli za ujenzi wa taifa.
Chanzo cha
habari hizi zinasema kuwa mmiliki wa chatu huyo ni Tajiri maarufu ambaye
pia ni mfanyabiashara wa madini aitwae Joseph Magessa mwenyeji wa
Musoma
Taarifa
zinadai kuwa mmiliki wa chatu huyo leo alikuwa na safari ya kwenda Dar
na familia yake ambapo huku nyuma alimuacha kijana ambaye anasadikiwa
kuwa mtoto wa ndugu yake ambaye aliwafungulia geti na kutoka na gari
Chanzo
hichi ambacho jina lake limehifadhiwa zinadai kuwa baada tu ya kijana
huyo kurudi ndani alikutana na chatu huyo kitendo kilichomfanya atoke
ndani kwa kasi huku akipiga kelele za kuomba msaada kwa majirani.
Baada ya
kelele hizo majirani walitoka kusaidia ambapo kwa wakati huyo taarifa
zilisha sambaa hali iliyofanya idadi ya watu kuwa wengi katika eneo
hilo.
Mashuhuda
wanadai kuwa chatu huyo alikuwa amefunikwa kichwani na kitambaa cha
baibui huku kiwiliwili chake kikiwa kimefunikwa na kitambaa cheupe
kilichokuwa kimeandikwa maandishi yanayo fanana ya kiharabu.
Wanachi kwa
kuona hali hiyo waliamua kumburuza chatu huyo kuelekea katika Kanisa la
KKKT Lutheran ambalo alipo mbali na eneo hilo.
Hata hivyo
baada ya kufika hapo chanzo kilidai kuwa mmiliki wa chatu huyo hakuwa wa
kanisa hilo hali iliyopelekea wananchi kumburuta tena kanisa la ST.
Monica ambapo mmiliki alikuwa muumini wa kanisa hilo
Chatu huyo mwenye ukubwa wa futi 12 alipigwa na wananchi ambao walikuwa na hasira kali
Katika
harakati za kumuua chatu huyo ambaye anakisiwa kufikia ulefu wa zaidi ya
futi 12 zilidumu kwa takriban nusu saa, huku mashuuda wakisema kuwa joka huyo alizidi kuwa mkubwa kila alipopigwa au kukatwa.
Taarifa za
ndani zinadai kuwa mmiliki wa chatu huyo alipopigiwa na mlizi wa nyumba
hiyo juu ya tukio hilo alitoa kauli ya kutokuuwawa kwa chatu wake huku
akidai kuwa huyo ni mama yake mzazi na kutoa onyo kuwa akikuta kauwawa
atampiga mtu risasi
“Huyo chatu hawawausu naomba mumuache msimuuwe kama kuna mtu mama yake amemleta basi amuuwe
chanzo; jamii blog
No comments:
Post a Comment