Washambuliaji hao ambao hutumia pikipiki, katika
siku saba wamemuua mwanamke mmoja na kuwajeruhi wanne kwenye matukio
tofauti lakini bila kuiba chochote.
Mwanamke aliyeuawa ni Shamim Rashid, mkazi wa
Sakina baada ya kupigwa risasi alipokuwa akijiandaa kuingia nyumbani
kwake juzi , tukio ambalo limekuja takriban siku tatu tangu mwanamke
mwingine, Frola Porokwa kunusurika kifo.
Porokwa mke wa mkurugenzi wa Shirika la Pingos a
Forums, Edward Porokwa, alipigwa risasi akiwa jirani kuingia nyumbani
kwake kwake pia eneo la Sakina, iliyompata pembeni ya kifua na kutokea
mgongoni.
Katika matukio yote mawili, watuhumiwa hao hawakupora chochote huku wakitoweka na pikipiki zao aina ya boxer .
Wakizungumza na mwananchi Juzi katika msiba wa
Shamin, baadhi ya waombolezaji walitaka Jeshi la Polisi kuimarisha
uchunguzi juu ya matukio hayo.
“ Tunaimani na jeshi letu litawakamata wahusika,
lakini jambo hili linatutia hofu wanawake kuendesha magari
usiku,”alisema Khanifa Haji.
Kufuatia matukio hayo Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, limeanza msako mkali dhidi ya watuhumiwa hao.
Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas
alisema katika kukabiliana na uhalifu huo jeshi lake , Serikali kwa
kushirikiana na wadau wataweka Kamera maalumu zenye uwezo za kubaini
vitendo viovu kwenye sehemu mbalimbali ili iwe rahisi kuwakamata
wahusika.
“Msako mkali umeanza na tuna uhakika wa kuwakamata watuhumiwa hawa na wengine,”alisema.
Wakati huo huo, polisi imefanikiwa kumkamata Adam
Mussa Pakasi mkazi wa Siwandeti wilayani Arumeru akiwa na bunduki
iliyotengenezwa kienyeji inayotumia risasi za Shotgun,risasi 38 na ganda
moja la risasi iliyotumika pamoja na mafuta ya kusafishia bunduki.
Sabas alisema matukio ya uhalifu yanayohusiana na
kupotea kwa maisha ya watu ni miongoni mwa mambo nyeti yanayochunguzwa
kwa umakini na tahadhari.
No comments:
Post a Comment