Pages

Pages

Friday, November 28, 2014

mtoto anusurika kifo katika jaribio la kutaka kumwiba mtoto mwenzie........


Hatari! Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 8 (jina linahifadhiwa kimaadili), mkazi wa Kihonda mjini hapa anayesoma darasa la kwanza kwenye Shule ya Msingi Noto Sosario, anadaiwa kutumika kumwiba mtoto mwenzake kisha kukamatwa na kunusurika kuuawa na wananchi wenye hasira zaidi ya 300.
Mtoto mwenye umri wa miaka 8 anayedaiwa kutumika kumwiba mtoto mwenzake.
Tukio hilo la kushangaza lililonaswa na Ijumaa Wikienda lilijiri wiki iliyopita mishale ya saa 8:00 mchana maeneo ya Majengo Mapya, Kata ya Kihonda jirani na nyumbani kwa aliyekuwa staa wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, marehemu Alberth Keneth Mangweha ‘Ngwea’.
Raia wenye hasira kali wakimsubiri kwa hamu mtoto huyo nje ya nyumba aliyohifadhiwa.
Akizungumza na mwanahabari wetu, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Mama Seleman alisema: “Mtoto huyu alikamatwa kwa jirani yangu, Asha Tembo akidaiwa kutaka kuiba mtoto wa mama huyo kwa njia za kichawi hivyo mama huyo aliamua kupiga kelele na kumuitia mwizi.
Kamanda akimbana mtoto huyo kwa maswali.
“Mtoto alikuwa amevaa nguo nyeusi ndipo umati ukajitokeza na kuanza kumshambulia kwa maneno makali huku wengine wakimpiga vibaya na kutishia kumuua.
Makamanda wa Polisi wakimchukua mtoto huyo kwa usalama zaidi.
“Baada ya kuona watu wanazidi, nikaamua kumwokoa na kumficha ndani kwangu.
“Nikiwa ndani umati wa watu ulitishia kuchoma nyumba yangu lakini nilifunga milango kisha nikawaita polisi wakaja kumuokoa mtoto huyo.”
Mtoto huyo akichukuliwa kwenye 'Defender' kuelekea kituo cha Polisi.
Kwa upande wake, mtoto huyo alisema: “Bibi ndiye huwa ananituma. Kwa sasa niko kwenye ulimwengu wa giza na mateso makubwa. Naye mama mzazi wa mtoto huyo, Maria Vicent alisema: “Mwanangu nilimzaa akiwa salama lakini tangu atoke Moshi (Kilimanjaro) kwa bibi yake amekuwa wa ajabu hivyo nimepanga kumpeleka kwenye maombi.”

chnazo : global pubisher.

Saratani ya Tezi dume

Watu wengi wamekuwa na shauku ya kutaka kujua ugonjwa wa saratani ya tezi dume, huku wakidhani ni mpya. Lakini ukweli ni kuwa umekuwapo miaka mingi na wengi wameugua.
Takwimu zinaonyesha wanaume wengi huugua ugonjwa huu unaoongezeka kwa kasi ya hali ya juu.
Kulingana na utafiti uliofanywa na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORIC), kutoka mwaka 2006, zinaonyesha kuwa kila mwaka kumekuwa na ongezeko la kesi mpya ya wagonjwa saratani ya tezi dume.
Novemba ya kila mwaka, jumuiya za kimataifa huadhimisha tukio ambalo hujulikana kama Movemba.
Maadhimisho hayo huhusisha kukuza kwa masharubu, kukusanya fedha na kuleta mwamko na ufahamu wa masuala ya afya kwa wanaume kama vile saratani ya tezi dume.
Jina hilo la Movemba ni mchanganyiko wa neno ‘Masharubu na Novemba’.
Maadhimisho hayo ya mwezi mzima yanalenga kuongeza ufahamu na mwamko kwa kupima ili kugundua mapema.
Mwaka jana peke yake zaidi ya Dola za Marekani 120 milioni zilikusanywa.
Hadi sasa, Movemba imekusanya zaidi ya Dola 550 milioni kupitia wanachama wake milioni nne katika nchi 21 duniani kote.
Waziri mstaafu wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa alinukuliwa akisema asilimia 10 ya wagonjwa wanaosumbuliwa na aina mbalimbali za saratani wamejitokeza hospitalini kwa uchunguzi na matibabu.
Anasema asilimia 90 iliyobaki hawajafanya jitihada zozote kuhudhuria uchunguzi na matibabu.
Akizungumzia juu ya uchunguzi wa hali ya tezi dume nchini, Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Hospitali ya Apollo yenye makao makuu India, Dk Prathap Reddy anasema kuwa ugonjwa huo unaathiri watu wengi na kusababisha vifo vingi nchini kwa sababu ya ukosefu wa ufahamu wa kina juu ya ugonjwa huo.

Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kaskazini

Wanaharakati kutoka shirika la Kwieco la mkoani Kilimanjaro wakiwa katika maandalizi ya maadhimisho ya siku 16 za kupingaukatili wa kijinsia.
Maandamano ya kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yakipita katika mitaa mbalimbali ya mji wa Moshi.
Mkurugenzui wa shirika la KWIECO ,Elizabeth Minde (mwenye miwani myeusi) akiwa katika maandamano hayo.
Brass Band ya Chuo cha Polisi ikiongoza maandamano ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa kanda ya kaskazini yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.
Maandamano yakiingia katika viwanja vya manyema ambako maandamano hayo yalikomea na kufuatia na burudani mbalimbali sanjari na hotuba toka kwa mgeni rasmi.
Afisa habari wa shirika la KWIECO ,Veronica Ollomi akitoa maelezo juu ya utendaji kazi wa shirika kwa mgeni rasmi Mtumwa Mwako alipotembelea bana la shirika hilo .
Afisa habari wa KWIECO ,Veronica Ollomi akitoa zawadi kwa mgeni rasmi Mtumwa Mwako.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili,mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Mtumwa Mwako akipitia hotuba yake ,shoto kwake ni mwenyekiti wa kamati ya maadhimisho ya siku hiyo ,
Mkuu wa dawati la jinsia mkoa wa Kilimanjaro ,Mrakibu wa jeshi la Polisi ,Grace Lyimo pia alikuwa miongoni mwa washiriki wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ,Elizabeth Mushi akisoma risala mbele ya mgeni rasmi katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya manyema mjini Moshi.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa kanda ya kaskazini ,Dk Mtumwa Mwako akitoa hotuba yake katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Manyema.
Mratibu wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili kanda ya kaskazini ,Hilary Tesha (katikatika)akijadiliana jambo na baadhi ya washiriki katika maadhimisho hayo katika viwanja vya Manyema mjini Moshi.
Wanaharakati kutoka mashirika mbalimbali yanayopambana na vitendo vya unyanyasaji pamoja na ukatili wa kijinsia katika mikoa ya Kilimanjaro ,Arusha na Manyara wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi(hayupo pichan                                                                                                                                                                                                     chanzo libeneke la kaskaizni  

Spika wa bunge la EALA asimamishwa siku 11

http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2014/08/215.jpg
Dk Margaret Zziwa.


Dar es Salaam.
 Bunge la Afrika Mashariki limemsimamisha kwa siku 21 Spika wake, Dk Margaret Zziwa huku likifufua hoja ya kumwondoa kiongozi huyo madarakani ambayo iliwekwa kando Aprili 1, mwaka huu.


Kadhalika, Bunge hilo liliafiki hoja iliyotolewa na mbunge kutoka Tanzania, Abdullah Mwinyi ya kumzuia Dk Zziwa kujihusisha na shughuli zozote za nafasi ya Spika mpaka hapo uchunguzi dhidi ya tuhuma dhidi yake utakapokuwa umekamilika na kuwasilishwa bungeni.


Uamuzi wa Bunge hilo ulifikiwa juzi mchana, ikiwa ni hitimisho la mkutano wa saa nne ambao ulimchagua mbunge kutoka Uganda, Chris Opoka-Okumu kusimamia mchakato wa kumwondoa Dk Zziwa madarakani kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa Eala.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgMcREAJO2eHsa90YMaEJ5X2MWlCh2Hrt0LdmpFwZNjvTApab4mYYdp36L8509fI3L4eLIxR7LRPl-D7_IhoHvQ2Cf0mwKkOr5RiraLp1i_mSYXTuGE2EvrCID7fvK9kcZY4hMilT9cbKkL/s640/shy-rose.jpg 
Shy-Rose Banji.
Taarifa ya kusimamishwa kwa Zziwa imewekwa katika tovuti ya Eala ikionyesha chini ya uongozi wa Okumu, Kamati ya Sheria, Kanuni na Haki ya Eala imepewa siku 21 kuchunguza tuhuma zinazomkabili ili kubaini iwapo alikiuka sheria na kanuni za uendeshaji wa Bunge kiasi cha kusababisha taasisi hiyo kushindwa kutekeleza wajibu wake.


Msemaji wa Eala, Bobi Odiko aliliambia gazeti hili jana kuwa kusimamishwa kwa Spika Zziwa kunamaanisha kwamba Bunge hilo halitaweza kukutana tena kwa siku chache zilizobaki hadi pale kamati itakapokuwa imemaliza kazi yake.


“Siwezi kusema kwamba lini Bunge litakutana na kukutana kwake kutategemea mambo mengi ikizingatiwa kwamba Spika amesimamishwa, kwa hiyo tusubiri siku hizo 21 zipite ili kamati ikamilishe kazi yake,” alisema Odiko.


Habari zaidi kutoka Nairobi ambako Bunge hilo linaendelea na vikao vyake zinasema uamuzi wa kumweka kando kisha kuanza kumchunguza Dk Zziwa uliibuliwa Jumanne jioni muda mfupi baada ya spika huyo kuamua kuahirisha kikao baada ya kutoa uamuzi ambao haukukubaliwa na wabunge karibu wote waliokuwamo ukumbini. Uamuzi huo ni wa kutangaza kufuta mchakato wa kumwajibisha Mbunge wa Tanzania, Shy-Rose Bhanji uliofikiwa katika kikao kilichomalizika mjini Kigali, Rwanda.


mwishoni mwa Oktoba, 2014 kwa maelezo kwamba uwasilishaji wa hoja husika na mchakato wa majadiliano haukuzingatia kanuni.


Badala yake, Zziwa alisema taarifa rasmi za mjadala huo zitakuwa moja ya nyaraka za siri za EALA hatua iliyopingwa na wabunge wengi.


Shy-Rose anatuhumiwa kufanya vurugu na vitendo vingine vya ukiukwaji wa maadili wakati wa ziara ya viongozi waandamizi wa EALA katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Ulaya (EU), Brussels, Ubelgiji.


Wakati wa kikao cha Kigali, ilitolewa hoja ya kumvua ukamishna wa Bunge hilo lakini uamuzi haukufanyika baada ya kukosekana kwa akidi ya wabunge kutoka Tanzania.


Kwa mujibu wa kanuni za EALA, hoja hiyo ilipaswa kuwa ya kwanza katika kikao cha sasa na ilipaswa kuendelezwa katika hatua ya wabunge kupiga kura, suala ambalo halikufanyika kutokana na uamuzi wa Dk Zziwa kutangaza kufuta mchakato wa hoja hiyo.


Baada ya Bunge kuahirishwa Jumanne jioni, wabunge karibu wote walikutana juzi asubuhi na kuandika waraka kwa Katibu wa EALA ambao ulisainiwa na wabunge 33 kati ya 44 wa kuchaguliwa, wakimtaka afike katika ukumbi ili waweze kufanya uamuzi wa kumchunguza spika.


Katibu wa EALA, alifika ukumbini hapo juzi saa 6.30 mchana, hatua iliyowezesha kufanyika kwa mchakato wa kumchagua, Okumu kisha kutolewa kwa hoja ya kufufua mchakato wa kumchunguza kisha kumwondoa madarakani Dk Zziwa.


Naye Mwanasheria wa EALA alisema asingeweza kutoa mwongozo kwa wakati huo mpaka akasome kwanza hansard, hivyo walikubaliana kukutana juzi asubuhi ambapo alitoa mwongozo uliowawezesha wabunge kusaini waraka wa kumwita Katibu wa EALA. Uamuzi huo ulifanywa mbele ya mawaziri wa nchi zote, isipokuwa Rwanda ambayo haikuwa na mwakilishi.


MWANANCHI