Hatari! Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 8 (jina linahifadhiwa kimaadili), mkazi wa Kihonda mjini hapa anayesoma darasa la kwanza kwenye Shule ya Msingi Noto Sosario, anadaiwa kutumika kumwiba mtoto mwenzake kisha kukamatwa na kunusurika kuuawa na wananchi wenye hasira zaidi ya 300.
Tukio hilo la kushangaza lililonaswa na
Ijumaa Wikienda lilijiri wiki iliyopita mishale ya saa 8:00 mchana
maeneo ya Majengo Mapya, Kata ya Kihonda jirani na nyumbani kwa
aliyekuwa staa wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, marehemu Alberth Keneth
Mangweha ‘Ngwea’.
Akizungumza na mwanahabari wetu, mmoja wa
mashuhuda wa tukio hilo, Mama Seleman alisema: “Mtoto huyu alikamatwa
kwa jirani yangu, Asha Tembo akidaiwa kutaka kuiba mtoto wa mama huyo
kwa njia za kichawi hivyo mama huyo aliamua kupiga kelele na kumuitia
mwizi.
“Mtoto alikuwa amevaa nguo nyeusi ndipo umati ukajitokeza na kuanza
kumshambulia kwa maneno makali huku wengine wakimpiga vibaya na kutishia
kumuua.
“Baada ya kuona watu wanazidi, nikaamua kumwokoa na kumficha ndani kwangu.
“Nikiwa ndani umati wa watu ulitishia kuchoma nyumba yangu lakini nilifunga milango kisha nikawaita polisi wakaja kumuokoa mtoto huyo.”
Kwa upande wake, mtoto huyo alisema: “Bibi ndiye huwa ananituma. Kwa
sasa niko kwenye ulimwengu wa giza na mateso makubwa. Naye mama mzazi wa
mtoto huyo, Maria Vicent alisema: “Mwanangu nilimzaa akiwa salama
lakini tangu atoke Moshi (Kilimanjaro) kwa bibi yake amekuwa wa ajabu
hivyo nimepanga kumpeleka kwenye maombi.”“Nikiwa ndani umati wa watu ulitishia kuchoma nyumba yangu lakini nilifunga milango kisha nikawaita polisi wakaja kumuokoa mtoto huyo.”
chnazo : global pubisher.
No comments:
Post a Comment