Na Bertha Ismail - Arusha
Mkuu wa
wilaya ya Arumeru, Nyirembe Munassa Sabi amewataka wachezaji wa hapa mkoani
Arusha kucheza soka kwa upeo wa kulipwa zaidi kuliko kuchukulia kama mazoezi au
kujifurahisha ili kupata nafasi ya kuchezea timu kubwa za kimataifa na kupatia
fedha kupitia michezo.
Mkuu huyo
aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wachezaji wa timu nane zilizoshiriki
mashindano ya ndondo yaliyojulikana kama “vipaji cup” vilivyofanyika katika
uwanja wa Ilboru vilivyoko wilayani Arumeru Mkoani Arusha ambapo small galilaya
fc ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa kombe hilo.
“Wachezaji
wengi wa Tanzania pamoja na kucheza mpira na wengine kutumikia vipaji vyao vya
soka lakini hawana upeo wa kuona kama mpira ni ajira bali wengi wao wanacheza
kupata umaarufu hali ambayo haiwasaidii bali chezeni kwa kuwa na upeo wa
kucheza soka la kulipwa kwani hapo ndipo utaweza kuweka nguvu zako kubwa
kucheza vema na hatimaye kuwa kama ajira yako na kuitangaza nchi kimataifa”
“Tunajua
hali ya nchi yetu na viongozi wenu wa soka bado hawajaweka mikakati mizuri Ya
kuhakikisha wachezaji wa nchi hii wanafaidika na michezo ndio maana mnakata tamaa
lakini kwa wenzetu wa nchi za nje mtu anaechezea hata ligi daraja la tatu
analipwa na wanafanya usajili wa vipaji bora lakini hapa kwetu mchezaji
anaetambulika ni hadi ligi kuu na kuika huko si leo mtakuwa mmesota sana, hivyo
ninyi jitahidini kucheza kwa upeo wa kimataifa mtapata nafasi ya kucheza katika
nchi hizo mlipwe vema” alisema mkuu huyo
Alisema kuwa
wachezaji wa ligi za ngazi za chini hawalipwi hapa nchini kutokana na viongozi
wa soka kutokuwa na upeo wa kuzitautia ligi hizi ufadhili wa kuzidhamini hali
ambayo ukata huo huwafikia hadi wachezaji na kucheza soka lisilo na viwango
kutokana na wengi wao kuwaza majukumu yao na umasikini hali ambayo wengi huamua
kuacha kucheza soka kukabiliana na hali ya maisha na vipaji vyao kupotea.
Mashindano
hayo ya vipaji cup yaliyoandaliwa na mwalim Joseph Zephania Laizer
yalishirikisha timu nane za wilayani humo ikiwemo small galilaya, Red star,
enterspot fc, moivo, red star, nature united,
kiurei, minara mitatu, na Ilboru ambapo mshindi wa kwanza small galilaya
alitwaa kombe la fedha taslim shilingi laki moja, mshindi wa pili ikichukuliwa
na red star na kufanikiwa kuzawadiwa fedha taslim 50,000 na mshindi wa tatu enterspot
na kupatiwa 30,000.
Mwisho…..
No comments:
Post a Comment