Pages

Pages

Saturday, January 31, 2015

Mlinda wa Oljoro, Dihe Makonga aitamani Azam fc




Mlinda mlango wa Oljoro dihe makonga (Wa pili kushoto)  akiwa na kikosi chake hicho


Arusha

Mlinda mlango namba moja wa timu ya Maafande ya Jkt Oljoro yenye makazi yake jijini Arusha Dihe Hassani Makonga amujikuta akiitamani nafasi ya siku moja kuitumikia club ya Azam kama goli kipa wa timu hiyo.

Akizungumza na gazeti hili Makonga alisema kuwa pamoja na kuitumikia club ya Oljoro inayoshiriki ligi daraja la kwanza kundi B’ kwa sasa lakini matarajio yake makubwa ambayo amekuwa akiota kila kukicha ni siku moja kujikuta akitumia club ya Azam ambayo imekuwa ikiwajali sana wanamichezo wake pia kuwa na kituo kizuri cha soka.

“Mimi kwa sasa ndoto yangu kubwa ni siku moja kutumikia club ya Azam hivyo kwa sasa ninapambana kuhakikisha naipandisha oljoro kwa hali na mali ambapo nimekuwa nafanya  mazoezi yangu hata mda wa ziada kuhakikisha malengo yangu yanatimia ili kuwatendea haki, najua nitapata sifa ya kunisaidia kuitumikia club ya ndoto zangu” alisisitiza Makonga

“Unajua mimi tangu mdogo napenda mpira na namshukuru sana kocha wangu aliyenianzishia safari ya kutimiza ndoto zangu za kuwa mwanasoka wan chi hii kama mlinda mlango ambae ni Chalse Boniface Mkwasa kwa kunianzishia hili na mimi kuitendea haki leo na nitajivunia sana katika maisha yangu kuipandisha oljoro ambayo nikiwa ligi kuu itakuwa nafasi nzuri kwangu hivyo niwashauri na wachezaji wenzangu wanaoota siku moja kutumikia club kubwa wajitume sana waachane na starehe ili wafanikiwe”

Dihe makonga ambae ni mlinda mlango chipukizi, kwa mara ya kwanza anaitumikia club kubwa ya ligi daraja la kwanza lakini amekuwa na mafanikio makubwa sana katika timu hiyo hasa baada ya kuwa tegemezi na kufanikiwa kuwa kikosi cha kwanza huku akikubalika sana na wachezaji wanzake na mashabiki wa mkoa huu kummuamini hasa akiwa mlangoni katika michuano yoyote anaposimama langoni.

mwisho

Tukio lililobaki kichwani kwangu leo hadi kesho

Katika matukio niliyofuatilia na mwisho wa siku nikalia kama mtoto mdogo
 baada ya kushindwa kutetea haki ya muhusika,  baada ya kufa 
ni pamoja na hili, lililomhusisha mtoto wa kike
mwenye umri wa miaka mitano, amefariki duniani huko mkoani
Kilimanjaro, baada ya kubakwa na babake mzazi.
 
unajua ilikuwje?
 
  mtoto huyo alifanyiwa unyama na
babake aitwae Elisha Wazaeli, (38), huko Mang’ola, wilaya ya Karatu,
mkoani Arusha.
 
Kifo cha mtoto huyu ambacho kimewasikitisha watu wengi, kilitokea
Juni 4, mwaka 2014 katika hospitali ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi,
alikokuwa akipata matibabu.
 
mazingira ya tukio hadi kufikia kifo cha mtoto huyo, kwa taarifa za
 awali zilizotolewa kwa jeshi la
polisi zinaonyesha ya kuwa mtuhumiwa alisafiri na mtoto wake huyo hadi
Karatu  eneo alilomfanyia unyama huo.
 
“Alikaa na mtoto huyo huko Karatu kwa siku nne na baada ya kumfanyia
unyama huo, alirudi na mtoto huyo hadi Ngaramtoni, Arusha wanakoishi
lakini baba huyo alitofautiana na mama wa mtoto huyo kabla ya mama
huyo kumchukua mtoto na kwenda nae eneo la Kahe, Moshi, Vijijini, Mkoa
wa Kilimanjaro na wakati akisafiri na mwanae huyo
kwenda Mang’ola alimwacha mkewe Arusha Mjini.
 
baada ya kufika Kahe mtoto huyo alianza kuugua na
alipopelekwa katika hospitali ya TPC aligundulika anaumwa homa ya
matumbo na kupatiwa tiba na dawa lakini pamoja na tiba hiyo bado
alikuwa akisumbuliwa na maradhi.
 
Mama yake alipomchunguza zaidi aliambiwa na mtoto huyo ya kuwa
anaumwa na sehemu zake za siri na alipomhoji zaidi ndipo alipomwambia
ya kuwa babake alimuingilia kimwili wakiwa Karatu,ambapo  mamake
alimchunguza sehemu zake za siri na kukuta ameharibika vibaya  huku
akitoa harufu mbaya
 
mama huyo alitoa taarifa kwa jeshi la polisi ambapo maofisa wa
jeshi hilo walimchukua mtoto huyo na kumpeleka hospitali ya Mawenzi
kwa uchunguzi zaidi na matibabu hadi alipofariki dunia juzi.
 
Ukweli ni kwamba mtoto Yule alipopelekwa polisi  Juni 4
alikuwa ameharibika vibaya sehemu zake za siri,kwani alikuwa akitoa
harufu ya kuoza,na baada ya kufika, alipelekwa hospitali ya
Mawenzi kwa ajili ya matibabu ambapo alilazwa,lakini alifariki dunia
ilipofika saa Moja usiku 
 
Hata hivyo baada ya mtuhumiwa kugundua swala hilo, limefika 
katika vyombo vya  sheria alikimbia.

wito wangu, wazazi jamani chonde chonde waleeni watoto wenu vema 
nikimaanisha muwe karibu nao hata lisaa kwa siku na kuzungumza nao
 kama kuna tatizo itakuwa rahisi kukuambia hasa hasa mama
pia wakagueni watoto wenu mara mara kwa mara sehem za siri
 msisubiri aoze kama huyu kwani angegundua mapema mwanae anaumwa 
angemuwaishia tiba na kifo hicho kisingemkuta malaika huyu

Mungu ailaze roho ya mwanamwali wake mahala pema peponi

Madiwani Moshi wam'maliza mkurugenzi wao


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
 Tuhuma za rushwa na uporaji wa mali za Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, zimesababisha vurugu zilizopelekea kikao cha Baraza la Madiwani kumkataa Mkurugenzi, Shaaban Ntarambe, huku likipitisha azimio la kumburuza mahakamani kwa ubadhirifu.
 
Meya wa Manispaa hiyo, Jaffary Michael, akizungumza mara baada ya kuvunjika kwa Kikao cha Bajeti ya Mapato na Matumizi ya Manispaa hiyo kwa mwaka 2015/2016, alisema madiwani hao wamepanga kumwandikia barua Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (pichani), wakimtaarifu kuhusu hatua watakazochukua dhidi ya Mkurugenzi huyo, ikiwamo kufungua mashtaka mahakamani.
 
“Tumetenga zaidi ya Sh. milioni 124 kwa ajili ya kufanya usajili wa viwanja vyetu, lakini fedha hiyo hiyo imeanza kutuletea balaa,
Madiwani wangu wamejiridhisha, nami ni shahidi,” alisema.
 
Alisema Mkurugenzi amehusika baada ya kuondoa kwa siri, zuio la Baraza kwa Msajili wa Hati na kutengeneza hati kwa ajili ya kuwapatia matajiri wachache waliojificha nyuma ya kikundi, kinachojiita Mawenzi Sports Club, akishirikiana na watendaji …viwanja vyote vya umma vilivyobaki havina hati haviko salama tena,” alisema Meya.
 
Kabla ya kuvunjika kwa kikao hicho, ambacho kilihudhuriwa pia na Katibu Tawala wa Wilaya ya Moshi (Das), Remida Ibrahim, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya; Diwani wa Kata ya Rau (Chadema), Peter Kimaro, baada ya sala alimshambulia Ntarambe, akidai amehusika katika uporaji wa uwanja wa Mawenzi wenye hati namba 10660 (056035/12).
 
Baada ya hoja hiyo, madiwani 24 kati ya 29 wanaounda Baraza hilo, walitoka nje wakitaka Mkurugenzi huyo awajibike kwa kujiuzulu wadhifa wake au aondoke Moshi kabla ya kumburuza mahakamani.
 
Mgogoro huo ulilipuka zaidi baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji, Ardhi na Mazingira, Rey Mboya, kudai eneo hilo limeporwa kutokana na nguvu ya watendaji kuamua kutengeneza hati nyingine kinyemela.
 
Wakati vurugu hizo zikitokea, madiwani wanne wa CCM, Apaikunda Naburi (Mawenzi),  Priscus Tarimo (Kilimanjaro), Miriam Kaaya (Viti maalum) na Michael Mwita (Kaloleni), walijibizana kwa maneno makali na Meya kwa madai ameshindwa kutenda haki kwa kumruhusu Tarimo kuuliza swali kabla ya kuanza kwa kikao.
 
Mbunge wa Moshi Mjini (Chadema), Philemon Ndesamburo, alisema licha ya Halmashauri hiyo kuongozwa na Chadema, hawawezi kuungana na kukubali watendaji wachache na baadhi ya wanasiasa kuiba mali za umma.
 
Kwa mujibu wa kumbukumbu za Halmashauri hiyo, Mkurugenzi wa Mipango Miji na Ramani wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, mwaka 2001 aliidhinisha eneo hilo ni mali ya umma baada ya kupigwa kwa picha za anga kati ya mwaka 1998 na 1999

Friday, January 30, 2015

sababu 10 zinazosababisha wanawake kuzeeka bila kuolewa

 

 

 

Pamoja na kuwa kuna wanawake husita kuolewa, lakini jambo hili si kubwa sana kwa wanawake kama ilivyo kwa wanaume.

 Kwa kiasi kikubwa katika suala la kutaka kuingia ndani ya ndoa, wanawake ni wengi ambao hutaka kufunga ndoa kuliko ilivyo kwa wanaume. Hilo tunaliona wazi tokana na shamra shamra awazo nazo mwanamke wakati wa maandalizi ya shughuli za Ndoa na Harusi. 


Hata hivyo, kwa wale wanawake wachache ambao husuasua kuolewa hizi ni baadhi ya sababu zinazopelekea kusuasua huko. (Izingatiwe hii ni kwa wanawake ambao hawajawahi kuolewa kabisa)

 

1.Vigezo vilivyopitiliza viwango (hasa kwa muonekano)


Wanawake wengi hasa wa umri mdogo (lakini unatosha kuolewa) hutumia muda mwingi katika kuchagua aina ya mwanaume ambaye angependa awe mume wake.Wanawake hawa hujiamini zaidi na kusimamia sifa zile ambazo huamini ni muhimu mwanaume wa kumuoa awe nazo.  


Vigezo hivyo huwa hata kwa misingi ya muonekano wa mwanaume huyo – kuna wale ambao hutaka mwanaume huyo wa kumuoa awe na sifa kama vile, mrefu, aliyejazia kifua, mtanashati, sauti nzuri n.k. 


Inaweza kuwa kama mzaha na ikaonekana ni kipengele kidogo sana lakini bado kuna wale ambao anaweza kuwa tayari kuolewa ila hataki sababu tu huyo mwanaume hafananii vile ambavyo yeye anataka mumewe awe.

 

2.Kutaka mwanaume tajiri

 

Kuna wanawake ambao tayari wameshajiwekea akilini kuwa hatakubali kuolewa na mwanaume yeyote yule ambaye hana pesa nyingi.


 Yupo tayari kuolewa ila si kwa mwanaume mwenye uwezo wa kawaida – hata ikitokea mwanaume ana uwezo kidogo wa kuweza kujitosheleza, yeye bado huona huyo mwanaume hamfai hadi pale tu atakapo pata yule ambaye anahisi ataishi maisha ya kifahari.


 Hivyo hukazana kusubiri na kujitahidi kuwinda aina ya mwanaume ambaye atakuwa na uwezo mkubwa, bila kujalisha kama huyo mwanaume kampita sana umri.



 

3.Kutompata Mwanaume Ampendae

 

Hili ni kama tu vile ilivyo kwa wanaume ambao huamini ndoa haiwezekani na haifai bali tu hadi pale umpatapo yule ambaye unampenda na unaamini anakupenda pia.  


Wengi katika kundi hili huamini kuwa mafanikio ya ndoa kigezo kikubwa ni kupendana tu na mengine hufuata kwenye sababu ya upendo. Kunawanawake vigezo vya mwanamme awe vipi havina umuhimu kabisa katika kutaka kuamua kuolewa.


 Yeye kikubwa anataka ampate mume ambaye atampenda kwa dhati na huku akiwa na matumaini kuwa huyo mume atampenda na yeye pia kwa dhati.  Huyu mwanamke anaamini msingi bora wa ndoa ni mapenzi ya dhati kati ya yeye na mmewe basi! Hana haraka hadi pale atakapompata mwanaume akampenda ndipo atakapokuwa tayari kuolewa.  

 

4.Kuchagua mno Wanaume wa Kumuoa (SO SELECTIVE)

 

Kuna wale wachache ambao akili hubadilika kama kinyonga; wasioridhika wala kujitambua ni nini wanataka ama mwanaume wa aina ipi wanataka. 


Akija wa mwenye uwezo atasema nataka wa kuchuma nae, akija asiye na uwezo atatoa sababu tu hata kama kumlaumu kuwa inaonyesha hajitumi kutafuta maendeleo. 


Akija wa kabila hii, atasema hapana hao wana tabia hii mimi siitaki! Yaani kwa ufupi ni mtu asiyeisha kutoa kasoro za wale ambao wanajitokeza kutaka kumuoa.


 Hatimaye inaweza tokea muda wa kuolewa ukapita na akaishia kupunguza uchunguzaji lakini ikiwa hata wanaume wa umri wa kufaa kumuoa kutokuwepo tena katika soko.

 

5.Kujiona ni mzuri sana

 

Kuna wanawake ambao ni kweli Mwenyezi Mungu kawajaalia uzuri hasa (uzuri wa muonekano), anakuwa ni mzuri kiasi kwamba wake kwa waume wote wanamkubali kwa uzuri huo na hata wote kumtamani.


 Hata hivyo hapo hapo kuna wale ambao huwa ni wazuri kawaida – ila kwa mtazamowake hujiona ni mzuri mno hakuna mfano kama yeye; kitendo ambacho kwa wachache kwenye kundi hili hufanya kujiona yeye ni yeye na kuwa kwa yeyote kuwa na yeye huyo mtu anatakiwa atambue kuwa ana bahati sana. 


Kitendo hiki hukuza nyodo za hali ya juu ya mwanamke mwenye mtazamo huu, kiasi kwamba wanapojitokeza wanaume kutaka kuoa – anaweza onyesha tabia kama maringo, dharau na kiburi.

 

6.Kujiona ana Umri mdogo

 

Binti yeyote wa miaka 18 na kuendelea anaruhusiwa kuolewa endapo tu karidhia kuolewa.


 Wanawake wametofautiana mipangilio yao ya kimaisha, kuna wale akiwa katika umri wa kuolewa hutamani sana kuolewa na kuna wale ambao hupenda kuolewa wakiwa wakubwa zaidi.


 Katika kundi hili umri kuwa mdogo hutegemeana, kuna mwingine anakuwa na umri wa miaka 25 na bado akajiona mdogo na hali kuna mwingine anakuwa na miaka 20 na akajiona ni mkubwa na anafaa kuolewa. 


Hii pia ni kwa wanawake wale ambao huwa na malengo ya kutotaka kuharakisha katika ndoa.


 Anapokuwa na umri ambao anaweza kuolewa lakini yeye hayupo tayari kwa muda huo, huwa ni kikwazo kwake kuingia katika ndoa.

 

7.Maradhi hasa UKIMWI

 

Hili kama lilivyo kwa wanaume -  Pamoja na kuhamasishwa kwingi na wataalamu wa maradhi ya HIV/AIDS kuwa mtu hata ukiwa umeathirika unaweza kuwa na mahusiano na hata kuoa na kuwa na watoto; bado haisaidii sana kwa vijana wanaojitambua kuwa ni waathirika wakiwa bado ni wadogo, hawajaoa/olewa ama kuwahi kuwa na mtoto. 


 Wengi sana hukata tamaa na huona ni kheri kubaki walivyo kuliko kuingia katika ndoa, hasa tokana na imani kuwa wanawake wakizaa wakati ni waathirika; afya hudhoofika zaidi.

 

8.Kutaka maisha ya Tamthilia (Ndoa za kuishi kwa furaha milele)

 

Kutokana na kukua kwa idadi ya tamthilia nyingi ambazo huonyesha maisha ya kimagharibi zaidi; kumekuwa na dhana kwa baadhi ya wanawake kutaka hayo maisha ya tamthilia yawe na kwao pia.


Hilo linafanya vigezo ambavyo mwanamke huyo anatumia kuchagua ama kukubali mwanaume kumuoa kutotimiza yale ambayo yeye binafsi anatarajia.  


Wengi hushindwa kutambua kuwa hakuna maisha ya furaha milele, na hasa kuwa maisha ya maigizo yapaswa kuchanganya na zako kuweza kufanya maamuzi ya kipi kiigwe na kipi kiachwe kama kilivyo.

 

9.Kuona taasisi ya Ndoa kama Utumwa


Mtazamo huu kwa wanawake wenye msimamo huu, huchangiwa na baadhi kama haya:

 

Usomi: Aina ya usomi ambao hupelekea kwa baadhi kuwa na tafsiri tofauti juu ya ndoa, haki, majukumu na mengine mengi.

 

Kushuhudia ndoa mbovu: Hii inaweza kuwa ya wazazi/walezi wake wenyewe (pengine mama aliteswa sana), na hata ndugu wa karibu kama vile kushuhudia kila ndoa ya ndugu yake anayoijua mwanamke huishi kwa mateso, manyanyaso na maisha ya taabu na kuonewa.

 

- Kuwa na uwezo sana wa kujitosheleza ambao unaweza kumtimizia na kufanya lolote lile ambalo anataka katika maisha. Kwake kuwa na mwanaume kama mume kwake anaona kama ni utumwa.

 

10.Kutokuwa kabisa na mshipa wa hisia za kufanya mapenzi

 

Kuna wanawake wale wachache waliozaliwa hivyo. Hawana hisia yoyote ile ya kimwili ya kuweza kupata hisia za kuweza kujisikia ama kutamani kufanya mapenzi. 


Wengi wa aina hii ya wanawake huwa ni waoga sana wa kuwa karibu na mwanaume, na kwa wale ambao wamewahi hata jaribu baadhi huona kama kitendo cha ndoa ni kero, unyanyasaji na uchafu.  


 Hivyo wazo la kuwa akiolewa anatarajia kufanya kitendo cha ndoa mara kwa mara kinamvunja kabisa hamu ya kutaka kuolewa.


Mgombe mwenyekiti matatani baada ya kusaini posho 20,000 bila kibali

Aliyekuwa mgombea mwenyekiti kupitia chama cha mapinduzi mtaa wa lolovono amejikuta akiwekwa chini ya ulinzi mkali wa mgambo wa kata ya sokon one baada ya kusaini posho ya halmashauri ya jiji la Arusha shilingi 20,000 bila kibali.
 
Mgombea huyo aliyejulikana kwa jina la Sudy Salum Kienda alikamatwa kufuatia barua enye tamko la mkurugenzi wa jiji la Arusha kumtaka mtendaji wa kata ya sokon one Meery Laurence kumtia hatiani mgombea huyo baada ya kubainika kusaini posho ya shilingi 20,000 kama mwenyekiti wa mtaa huo hali isiyo halali.

Akizungumza na mtuhumiwa huyo, Merry alisema kuwa january saba mwaka huu washindi wa kiti cha wenyeviti waliitwa kwenye semina elekezi ya utendaji wa kazi ambapo baada ya semina hiyo mtuhumiwa (Sudy )alihudhuria mkutano huo kimakosa na kusaini posho isiyokuwa yake hivyo kuichafulia jina halmashauri ya jiji la Arusha.

Akiwa chini ya ulinzi alipotakiwa kujibu tuhuma hizo sudy alikiri kuchukua fedha hizo huku akijitetea kuwa hakujua kama ni kosa ambapo hata hivyo aliamua kuirejesha mikononi mwa mtendaji huyo.

“Mimi sikuwa na nia ya kuiba hii hela kama mnavyonituhumu bali mimi nilifika pale nikimuulizia mtu aliyeniita ndio nikaambiwa saini hapo uchukue hela na mimi nikachukua sikujua ni ya wenyeviti maana nisingechukua kuepuka kunidhalilisha kiasi hiki.

Akizungumzia hali hiyo, mwenyekiti halali wa mtaa huo wa lolovono, Priscus Kwai (CHADEMA) alisema kuwa si mara ya kwanza kwa mwenyekiti huyo wa CCM kutaka kiti hicho kwa nguvu kwani awali siku ya kuapishwa pia alijaribu kumrubuni mtendaji huyo ili kuapishwa kama mshindi wa kiti hicho ambapo mtendaji alikataa.

“Huyu jamaa ameshika nafasi ya tatu lakini amekuwa akitaka kiti hiki kwa nguvu ambapo mwanzo alisambaza mtaani nimemuuzia kura na amenipa nyumba na gari na akaja kwa mtendaji alfajiri siku ya kuapishwa na kusema yeye ndio mshindi lakini mtendaji aligundua hilo na kunisubiri hadi saa tatu mda wa kuapishwa nikafika na akaona aibu akaondoka” alisema Kwai

“Baada ya kushindwa kuapishwa siku hiyo akaanza kunitishia maisha kuwa nitaona kama nitafika mbali, ambapo siku ya semina iliyofanyika golden rose iliyoendeshwa na mkurugenzi alienda na kujitambulisha yeye kama mwenyekiti halali wa lolovono na kusaini hela ambayo baadae baada ya kufuatilia ilijulikana kuwa amechukua hela bila halali na ndio tukapigiwa sim tukaenda kumkamata”

Aidha katika uchaguzi wa wenyeviti uliofanyika hivi karibuni, mtaa wa lolovono nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Priscus Kwai (chadema) kwa kuwa na kura 802 na nafasi ya pili ikichukuliwa na Mosses Losingo (NCCR) kwa kura 333 huku nafasi ya tatu ikienda kwa Suddy Salum Kienda wa CCM

Ukweli Kuhusu Tevez Aliyekatwa Uume Wake Baada ya Kuwazulumu Madawa ya Kulevya Wenzake

HABARI ZA UHAKIKA JUU YA SAKATA LA JUMAANNE TEVEZ. Nikweli kwamba huyu bwana yuko South Africa Pretoria. Bwana Tevez alodhaminiwa mzigo na vijana wenzake huko Bondeni kwamba akauze kisha alete Mpunga. Mdhamini alikuwa ni Kijana wa Kibongo anayeonekana pichani anayeitwa Jeff Katili mtoto wa Ilala ambaye maskani yake ni South. TEVEZ baada ya kuchukua mzigo uliokuwa na thamani ya takriban milioni mia moja na hamsini (150,000,000/=) aliingia mitini hakurudi tena. Kilichotokea Jeff baada ya kubanwa na wana akawaambia kuwa tulieni nitamleta tu.

 Basi Jeff akamrubuni Tevez kuwa njoo Kuna kazi.. Tevez akaingia mzima mzima akaenda hadi Pretoria wiki iliyopita na kufikia kwa Jeff Katili na kupata mapokezi mazuri kama kawaida. Baada ya kufika walitoka kwenda matembezi KWAZULU NATAL... wakiwa huko walifikia kwa washkaji zao wa kibongo lakini kwenye nyumba ambayo ilikuwa kama holi haina chochote ndani. Chini lilitandikwa karatasi la nailoni ili kuepusha damu isitapakae. Alibanwa juu ya mzigo na mtesaji mkubwa alikuwa Jeff Katili mwenyewe ambaye ni mdhamini. Tevez hajang'olewa jicho bali alipigwa Ngumi hadi jicho likaenda ndani... NGUMI YA MTOTO WA KIUME.

Ameteswa sana na amekatwakatwa na viwembe mwili mzima. Zakari yake haijakatwa kama picha zilivyoonyesha bali imekatwa na viwembe. Taarifa zilitumwa kwa kaka yake na akina Jeff na kuwataka watume pesa la sivyo wanamuua. familia kupitia kaka yake imeshatuma pesa nusu na sas anatibiwa hukohuko South na atarejea punde. Uzushi kuwa amekufa hauna ukweli na hizi ni habari kamili kutoka kwa watu wa karibu na familia hiyo.

Mwalimu atuhumiwa kubaka mwanafunzi wake

kamanda Koka Moita


Moshi.
 Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mwalimu mmoja wa shule ya sekondari kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa kidato cha tatu na kumuumiza sehemu za siri.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Koka Moita alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 11:45 katika chumba cha maabara shuleni hapo.
Kamanda Moita alisema mwalimu huyo alimwita mwanafunzi huyo katika chumba hicho na kuanza kumtomasa mwilini na baadaye alimvua nguo kwa nguvu, kisha kumuingilia.
Alisema kutokana na maumivu aliyoyapata alipelekwa Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi kwa matibabu. Kamanda Moita alisema mtuhumiwa baada ya kutenda kosa hilo alikamatwa.
Katika tukio jingine; Faustine Macha (45) ameuawa kwa kupigwa na rungu kichwani na kuvunjwa miguu kisha kutupwa shambani.
Kamanda Moita alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 12:00 jioni katika Kijiji cha Kinango wilayani Moshi Vijijini. Alisema marehemu alipigwa na watu wawili baada kulewa na kuanza kutukanana.
Kamanda Moita alisema watuhumiwa hao wanashikiliwa kwa tuhuma za mauaji. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Kilema.

chanzo: mwananchi

WATANZANIA 10 KUWAKILISHA MASHINDANO YA BAISKELI AFRIKA KUSINI

na Bertha Ismail  - Arusha
Chama cha mchezo wa baiskeli Taifa (CHABATA) kinatarajia kupeleka wachezaji 10 nchini Afrika kusini kuwakilisha nchi kwenye mashindano ya kusaka bingwa wa bara la Afrika yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi February tisa hadi 14 mwaka huu huku wakikabiliwa na changamoto lukuki.
Akizungumza na gazeti hili mwenyekiti wa Chama cha mchezo huo nchini Godfrey Jax Mhagama amesema kuwa mashindano hayo yanayoshirikisha nchi zaidi ya 30 za bara la Afrika yanafanyika kila mwaka ambapo kwa Tanzania wachezaji hawa watakuwa wanaifanya nchi kuwa mara ya tano kushiriki.
Mhagama alisema kuwa wachezaji hao wanatarajia kuondoka nchini February sita mwaka huu kulingana na upatikanaji wa fedha wa dola 12,000 (milioni 20) ambapo amesema kuwa kwa sasa chama hicho kina nusu ya fedha hizo.
“Kwa mwaka huu tunatarajia kupeleka wachezaji 10 miongni mwao wasichana wakiwa ni wawili na wanaume nane, lakini hilo litafanikiwa endapo wadhamini watajitokeza kutusaidia kupunguza gharama kwani hadi sasa tuna dola 6000 na bajeti yetu kwa hao watu 10 ni dola 12,000 hivyo kama tukikosa itabidi tuangalie namna ya kupunguza idadi” alisema mhagama.
“Kwa sasa nitumie fursa hii ya chombo chenu kinachosomwa na watu wengi nchini kuliko vyombo vyovyote kuwaomba wadau wajitokeze kusaidia timu hii ikafanye vema huko Afrika kusini kwani endapo tukifanikiwa kupeleka wachezaji wengi zaidi ndio tutakuwa katika nafasi nzuri ya kushinda lakini watu wachache huwa rahisi kuachwa”
Miongoni mwa wachezaji hao wane wanaotoka mkoani Arusha akiwemo msichana mmoja imebainika kuwa bado hawajaingia kambini hadi leo ambapo kila mmoja anafanya mazoezi mkoani kwake huku vifaa vyao ikiwemo baiskeli kutokuwa na uimara wa mashindano.
Akijibu swala hilo Mhagama alisema kuwa ni kweli hadi leo wachezaji hawajaingia kambini kufanya mazoezi kutokana na kutokuwa na fedha za kugharamia mahitaji yao hali iliyosababishwa na ukosefu wa ufadhili kwa kupatiwa ahadi na makampuni mbalimbali zisizotekelezeka.
“Ni kweli kama ulivyowaona hawajaingia kambini kutokana na kukosa fedha za kugharamia kambi, huku wadau wakituahidi tu bila kutekeleza lakini naomba niwahakikishie wadau kuwa hilo pamoja na kuwa kama sehem ya madhara kwetu lakini wasiwe na wasiwasi kwani tutajitahidi kuwa katika nafasi nzuri”
mwisho..................