kamanda Koka Moita |
Moshi.
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mwalimu mmoja wa shule ya sekondari kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa kidato cha tatu na kumuumiza sehemu za siri.
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mwalimu mmoja wa shule ya sekondari kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa kidato cha tatu na kumuumiza sehemu za siri.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Koka Moita
alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 11:45 katika chumba cha
maabara shuleni hapo.
Kamanda Moita alisema mwalimu huyo alimwita
mwanafunzi huyo katika chumba hicho na kuanza kumtomasa mwilini na
baadaye alimvua nguo kwa nguvu, kisha kumuingilia.
Alisema kutokana na maumivu aliyoyapata alipelekwa
Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi kwa matibabu. Kamanda Moita alisema
mtuhumiwa baada ya kutenda kosa hilo alikamatwa.
Katika tukio jingine; Faustine Macha (45) ameuawa kwa kupigwa na rungu kichwani na kuvunjwa miguu kisha kutupwa shambani.
Kamanda Moita alisema tukio hilo lilitokea juzi
saa 12:00 jioni katika Kijiji cha Kinango wilayani Moshi Vijijini.
Alisema marehemu alipigwa na watu wawili baada kulewa na kuanza
kutukanana.
Kamanda Moita alisema watuhumiwa hao wanashikiliwa kwa tuhuma za mauaji. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Kilema.
chanzo: mwananchi
No comments:
Post a Comment