Pages
(Move to ...)
Home
Habari za Kitaifa
Mapenzi
Urembo
Michezo
▼
Pages
(Move to ...)
Home
Habari za Kitaifa
Urembo
Mapenzi
Michezo
▼
Monday, February 9, 2015
KESI YA RAIA WA INDIA WALIOPATA PASSPORT KWA UDANGANYIFU YARINDIMA ARUSHA
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Hakimu Mkazi wa Mahakama kuu ya Arusha ,Gantu Mwankuga ameahirisha kesi ya Raia wenye asili ya India wanaodaiwa kujipatia passport kwa kutumia vyeti vya kuzaliwa ile hali si raia wa Tanzania .
Watuhumiwa hao waligunduliwa Novemba mwaka jana na Ofisi ya Uhamiaji Arusha na kufikiwa mahakamani kujibu tuhuma hizo kwa mara ya kwanza Januari 20 mwaka huu.
Gantu amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Ghansyam Vakaria (53),Kaushik Ghansian (32),Nautam Ghansian ambaye ana uraia wa Uingereza.
Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani leo mbele ya hakimu kesi yao imetajwa kwa mara ya pili kesi hiyo itatajwa tena Februari 17 mwaka huu.
Kwa upande wake Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Arusha Ndelema Mwakipesile amesema kuwa Watuhumiwa hao waliishi nchini tangu mwaka 1986 wakiwa na kibali maalumu cha kuishi baada ya kibali kuisha walihitaji kuongeza muda na kujikuta wakitumia njia ya udanganyifu kujipatia passport kinyume na sheria.
“Watu hawa walimtumia ndugu mmoja anayefahamika kwa jina la Karia ambaye kwa sasa ni marehemu aliyefanyia mpango wa kupata vitambulisho vya kuzaliwa vya nchini walivyo vitumia kuombea passport na kupewa baadae walichunguzwa na kubainika si raia wa Tanzania ,suala hili lipo mahakamani litatolewa hukumu” Alisema Ndelema
Mkuu huyo amewaasa Watanzania kuwa makini na kutowatumia mawakala wa mitaani kupata huduma za uhamiaji badala yake wafike moja kwa moja kwenye ofisi zao kwani hawana mawakala.
Kesi hiyo raia hao inatarajiwa kutajwa tena Februari 17 mwakahuu,kesi hiyo yenye namba 16 /2015 huku watuhumiwa wakikana mashtaka na kudaiwao ni raia wa Tanzania,kitendawili ambacho kitateguliwa na mahakama.
chanzo prince media
No comments:
Post a Comment
‹
›
Home
View web version
No comments:
Post a Comment