na Bertha Ismail - Arusha
Wanariadha
Fabian Nelson na Catherine Lange wamefanikiwa kujiweka katika nafasi nzuri ya
kuwa miongoni wa wanariadha watakaotumika kuunda timu ya Taifa itakayowakilisha
nchi katika mashindano ya Dunia hapo mwezi march mwaka huu Beijin nchini China.
Wanariadha
hao wameonyesha uwezo wao wa kukata upepo mkoani Arusha kwenye mashindano ya
wazi ya wanariadha kutoka mikoa ya Kanda ya kaskazini lengo ikiwa ni kujipima
uwezo wa kushiriki mashindano ya Kitaifa yanayotarajiwa kufanyika mkoani Arusha
February 21 mwaka huu.
Fabian
Nelson akiwa miongoni mwa wanaume 19 walioshiriki mbio za kilomita 12 alishika
nafasi ya kwanza kwa kumaliza kwa kutumia dakika 34:54:31 akifuatiwa kwa karibu
na Gabriel Gerald kwa kutumia dakika 35:23:77 huku Uwezo Lukinga akiwa nafasi
ya tatu kwa kutumia dakika 35:39:36.
Wasichana
nane walikimbia umbali wa kilomita nane ambapo Catherine Lange alikaa mbelena kuwa namba moja kwa kutumia
mda wa dakika 27:27:05, akifuatiwa kwa karibu na Magdalena Crispine aliyetumia
dakika 27:39:17 na namba tatu akiwa ni Anjelina Tsere aliyetumia dakika
28:43:96 kumaliza mbio zake.
Katika mbio
hizo wako wanaume 20 pia walioshiriki mbio za kilomita nane ambapo mshindi wa
kwanza alikuwa Josephat Joshua kwa kutumia dakika 23:44:84 akifuatiwa na
Tumaini Habiye aliyetumia dakika 24:31:53 na namba tatu alikwenda kwa Yohana
Elisante kwa kutumia dakika 24:36:58.
Mashindano
hayo ya wazi pia yalishirikisha wanafunzi waliokimbia umbali wa kilomita sita
na Amina Mohamed aliwaacha wenzake na kuwa namba moja kwa kutumia dakika
23:12:93 akifuatiwa na Neema Kisuda kwa kutumia dakika 24:12:33 huku namba tatu
ikichukuliwa na Yasmini Yusuph kwa kutumia dakika 27:59:33.
Akizungumzia
mashindano hayo katibu wa chama cha riadha mkoa wa Arusha Alfredo Shahanga
alisema kuwa lengo la mashindano hayo ya kanda ni kuangalia uwezo wa wanariadha
hao na kuweza kuwapa nafasi ya kuunda timu itakayowakilisha mikoa hii kwenye
mashindano ya kitaifa kama mwanzo wa safari ya kuelekea mashindano ya Dunia.
“Tumefanya
haya mashindano kuangalia uwezo wa wanariadha wetu na tuchague watakaoweza
kuunda timu ya mkoa ili watuwakilishe kwenye mashindano ya riadha ya kitaifa
yanayoratibiwa na kamati ya riadha Taifa ambayo yamepangwa kufanyika February 21
hapa hapa Arusha”
“Mashindano
hayo ya kitaifa yatachagua timu nzuri ya riadha Taifa itakayokuwa inajifua
tayari kwenda kuwakilisha nchi kwenye mashindano ya dunia march 23 huko Beijin
Nchini China, baada ya kufanyiwa mchujo wa kuridhisha lengo ikiwa mwaka huu
tupate ushindi siyo kusindikiza kila mwaka” alisema Shahanga.
Mwisho,………..
|
No comments:
Post a Comment