Halmashauri
ya wilaya ya Ngorongoro imetupia lawama Chama cha soka mkoa wa Arusha
(ARFA) kukataa kuruhusu wilaya hiyo kushiriki kwenye mashindano ya ligi
kwa madai ya kutokutambua uongozi wa soka.
Akizungumza
na gazeti hili Afisa utamaduni na michezo wa wilaya hiyo Bakari Gaima
alisema kuwa wamekuwa na kiu kubwa ya kushiriki ligi za taifa ili
kuonyesha uwezo wao katika kusakata soka lakini wamekuwa wakinyimwa haki
hiyo na uongozi wa chama cha soka mkoa.
“Jamani
ninyi mlioko karibu na mjini tusaidieni huku sisi tunanyimwa haki zetu
za kucheza mpira na kila tukitaka tushiriki ligi kwa kuandaa timu bingwa
wa wilaya yetu anakataliwa kwa madai kuwa sisi hatuna hatuna chama sasa
tunachoshindwa kuelewa ni chama kipi hicho wakati tuna uongozi??”
“Mwanzo
Katibu wa soka mkoa alisema kuwa wilaya yetu hatuwezi kushiriki ligi
kwa sababu hatuna uongozi hivyo tukaamua kufanya uchaguzi wa kuwachagua
viongozi wetu wa soka na tukafanya ligi ya wilaya lakini tulipopeleka
jina mwaka jana tukaambiwa uongozi wetu ni batili kwa kuwa
hatujazingatia kanuni za katiba mpya zilizotolewa na TFF”
“Hata
hivyo tukaamua kutaka ujua kanuni mpya za TFF tukaambiwa kuwa katibu
huyo atakuja kutuletea katiba hiyo na kuisoma tuielewe na kuzindua chama
cha soka ambayo hiyo itakuwa tiketi ya sisi Ngorongoro kushiriki ligi
lakini unaambiwa hadi leo hakuna kilichofanyika hadi leo na bado
tunaambiwa hatuna sifa”
“Mwaka
jana kabla ya ligi ya mkoa kuanza tulikwenda hadi mjini ambayo ni zaidi
ya kilimeta 430 kufuata hiyo katiba mpya maana tunaona tunacheleweshwa
kushiriki ligi lengo ni tufuate taratibu hizo tufanye uchaguzi na bingwa
wetu wa wilaya akachuane mkoani lakini cha kushangaza chama cha soka
mkoa ulitunyima katiba hiyo kwa madai watakuja wenyewe hadi leo
hatujawaona, jamani mbona mnatutenga?? Alilalama Afisa michezo Gaima.
Alisema
kuwa mabingwa hao wa wilaya ilishindikana kushiriki ligi hiyo hadi leo
wanasubiri huku ligi ya mkoa imefikia hatua ya sita bora huku wakilalama
kuwa wamekuwa wakitengwa tangu kuanzishwa kwa wilaya hiyo kwani hata
mashindano ya copacocacola walitakiwa kuandaa timu lakini wakashindwa
kupewa taarifa ni lini kuleta timu hiyo kucheza hadi mda ukapita.
Kwa
upande wake katibu wa soka mkoa wa Arusha Adam Brown alikanusha
kuwatenga kisoka wilaya hiyo huku akisema kuwa mfuko wa mkoa kwa sasa
hauna fedha hivyo wanasubiri hadi ipatikane wapate kwenda kuzindua chama
hicho na kuwasomea katiba mpya ya Shirikisho la soka.
“Unajua
wilaya ile iko mbali ndio maana unashindwa kwenda bila kuwa na pesa
hivyo tunajipanga kama hela ikipatikana tutakwenda na sio kweli kwamba
tunawatenga ila tumewaambia hawawezi kushiriki ligi bila kuwa na chama
kinachotambulika na TFF na kama wakikamilisha hilo Afisa michezo
ataitisha kamati na kufanya uchaguzi” alisema Brown.
No comments:
Post a Comment