Arusha
Chama
cha Taekwondo mkoa wa Arusha imeamua kuingia katika shule za sekondari
kusaka vipaji vipya vya mchezo huo lengo ikiwa ni kuongeza nguvu na kasi
ya mchezo huo mkoani hapa ikiwa na maandalizi ya mapema ya timu bora
itakayowakilisha nchi kwenye mashindano ya Olimpic hapo baadae.
Akizungumza
na gazeti hili kocha wa timu ya Taekwondo Arusha Richard Kitolo alisema
kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya kuona mchezo huo unadumaa mkoani
hapa kutokana na kukosekana kwa vipaji vipya vya vijana wenye vipaji na
mchezo huo.
“Tumeamu
kuingia mashuleni kutafuta vipaji vipya vya mchezo wa Taekwondo ikiwa
ni kama maandalizi ya kushinda mashindano ya olilpiki hapo baadae hivyo
kutokana na kukosekana kwa vipaji vipya tumeingia mashuleni na tumeanza
na shule ya sekondari Braeburn na edmundi rise”
Kocha
huyo ambae ni mmiliki wa Club ya Triple A’ taekwondo alisema kuwa
wamekuwa na uhaba mkubwa wa wachezaji wa mchezo huo hasa mkoani Arusha
hivyo wameamua kutafuta wenyewe katika shule za sekondari kote mkoani
hapa wakisaidiana na walimu mbalimbali lengo ikiwa ni kufanya makali ya
mchezo huo kutisha kimatifa hapo baadea
‘Unajua
kwa sasa wanafunzi wa shule za sekondari ndio wenye uwezo mkubwa wa
kuonyesha uwezo wa vipaji vyao hivyo tumeamua kujikita huko na tunaomba
walimu waturuhusu kuwafundisha wanafunzi wao mchezo huo kwani mbali na
mazoezi ya kujilinda lakini pia inawafanya wawe na akili kutokana na
mazoezi pia tunawafundisha nidhamu”
Alitumia
fursa hiyo kuwaomba wazazi wa wananfunzi hao kuwaruhusu kutoa mazoezi
hayo mda wa jioni kwa watoto wao kwani mbali na kuwa na uwezo wa
kujilinda lakini pia itawasaidia watoto wao kupata ajira hapo baadae
endapo watafanya vizuri
mwishooooo
No comments:
Post a Comment