na Bertha Ismail - Arusha
Bingwa wa
kimataifa wa mbio za baiskeli mtanzania Richard Laizer ameng,ara katika mbio za
taifa na kuibuka mshindi wa kwanza baada ya kuwazidi washindani wenzake zaidi ya 70 kutoka
mikoa sita ya Tanzania bara.
Laizer kutoka
Arusha aliyerejea hivi karibuni kutoka Afrika ya kusini alitumia muda wa saa
3:27:01 kunyonga baiskeli yake umbali wa kilomita 133 na kujishindia kitita cha
shilingi laki nne, akifuatiwa na anaeshikilia ubingwa wa taifa Hamis Hussein
aliyemaliza wa pili kwa kutumia saa 3:28:30 na kujishindia shilingi laki mbili
huku mpanda baiskeli kutoka mwanza Sunga Duba alikiibuka wa tatu kwa kutumia
saa 3:28:40 kumaliza mbio na kujishindia laki moja na nusu taslim.
Mashindano
hayo
yaliyoandaliwa na club ya Arusha cycling kwa lengo kujifua kwa ajili ya
mashindano mbalimbali ya kimataifa yalishirikisha washindani wa
kitaifa na kimataifa ambapo vijana ( 20- 45) walichuana kumaliza mapema kilometa
133 huku
wanawake na vijana wadogo (under 20) wakichuana kwa kilometa 80 pamoja na wazee (45-..)ambao wengi wao walitoka mataifa ya ulaya
, Amerika na Australia.
Kwa upande
wa wanawake mpanda baiskeli mkongwe Sophia Hussein aliibuka mshindi wa kwanza kwa
kutumia saa 3:10:05 na kufuatiwa na
mpinzani wake Sofia Adson aliyetumia saa 3:22:11 huku mpanda baiskeli chipukizi
Jamila Jumanne akimaliza wa tatu kwa kutumia saa 3:55:14 wote wakiwakilisha
mkoa wa Arusha.
Wageni toka
nje ya nchi walitamba katika mbio za wazee baada ya Steven Charmly toka
Australia kushika nafasi ya kwanza na kufuatiwa na Thaday Peterson toka Amerika
aliyekuwa pili na wa tatu akiwa ni Hendry Banderland kutoka Uholanzi.
Kadhalika
kwa upande wa vijana wadogo, Kijana chipukizi Kelvin Didas (14) aling’ara katika
mbio hizo na kuwakilisha vema baada ya kuwatoka wenzake umbali mrefu na
kufuatiwa na David Philemon huku nafasi ya tatu akiibuka Mussa Husein wote
kutoka mkoani Arusha.
Akizungumza
na waandishi wa habari baada yam bio hizo, katibu msaidizi wa Arusha Cyclin
Club, Thaday Peterson alisema kuwa mbali na kuvutiwa na mabadiliko makubwa ya msichana
Sophia Hussein aliyeshika namba moja kutokana na kumshirikisha mashindano ya
kimaifa Afrika Kusini msimu uliopita lakini zaidi amevutiwa na vijana wadogo.
“Kiukweli
Sophia baada ya kushiriki mashindano ya Afrika kusini ameonyesha mabadiliko
makubwa, lakini ukiachana na hayo uwezo walionao hawa vijana wadogo pia ni
mkubwa sana hali inayovutia kuwekeza zaidi kwao hasa katika kuwashirikisha
katika mashindano ya kimaifa na hii imetufanya sisi tuwe na kiu ya kuwatafuta
vijana wadogo zaidi kwa wanaume na wanawake ili kutusaidia kufanya vema zaidi”
Mwisho…………………………..
No comments:
Post a Comment