Pages

Pages

Sunday, March 31, 2013

Ni simanzi, taharuki zatawala D’Salaam



Rais Jakaya Kikwete akifuatilia zoezi la uokoaji kwenye jengo la ghorofa 16 lililoanguka katika Mtaa wa Indira Gandhi jana. Kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova na Mkurugenzi wa Kitengo cha Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Meja Jenerali, Sylvester Rioba.


Zoezi la kutafuta miili iliyokwama katika vifusi inaendelea, zaidi ya maiti 22 zapatikana.
Dar es Salaam. Idadi ya watu waliokufa kutokana na kufukiwa na kifusi cha jengo la ghorofa 16 lililoporomoka juzi asubuhi jijini Dar es Salaam, imefikia 22.
Habari zilizopatikana kutoka eneo la uokoaji na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova zinaeleza kuwa miili iliyopatikana imepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Jengo hilo lililokuwa likijengwa mkabala na Msikiti wa Shia Ithnasheri ulioko Barabara ya Indira Gandhi na Kampuni ya Lucky Construction Limited liliporomoka saa 2.30 asubuhi wakati mafundi na vibarua wakiendelea na ujenzi huku chini watoto wakicheza mpira na mama lishe wakiendelea na biashara zao kama kawaida.
Rais Kikwete
Rais Jakaya Kikwete ambaye jana pia alifika katika eneo la tukio, kama ilivyokuwa juzi, alipata taarifa fupi ya maendeleo ya uokoaji kutoka kwa Mkuu wa Mkoa, Said Meck Sadik na Kamanda Kova.

Baada ya kupewa taarifa hiyo, Rais Kikwete alimwagiza Kamanda Kova kuhakikisha wahusika wanakamatwa akiwamo Mkadiriaji Majengo (Quantity surveyor), mchora ramani za majengo (Architecturer), Mhandisi Mshauri (Consultant) na Mhandisi wa Jiji la Dar es Salaam. Juzi baada ya kutembelea eneo la tukio, Rais Kikwete aliagiza wahusika wote wa ujenzi huo wachukuliwe hatua kali.
Habari zilizopatikana jana zilidai kuwa Diwani wa Kata ya Goba, Wilaya Kinondoni, Ibrahim Kisoka ambaye ndiye mmiliki wa kampuni ya ujenzi, na Mhandisi Mshauri kwa pamoja wamejisalimisha Kituo Kikuu cha Polisi na hadi saa 8:00 jana mchana walikuwa wakihojiwa.
Awali Kamanda Kova aliwaambia waandishi wa habari kuwa amemtaka mmiliki wa Kampuni ya Lucky Construction Limited ambaye ni Diwani wa Kata ya Goba, Kisoka na wahusika wengine kujisamilisha kituo cha polisi, kabla hawajaamua kutumia nguvu kumtafuta.
Pinda atembelea eneo la tukio
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alifika eneo hilo saa 3:41 asubuhi, kujionea hali ilivyo, lakini hakutoa tamko lolote. “Sina la kusema,” alisema Waziri Mkuu alipoulizwa na waandishi wa habari kutoa kauli ya serikali kuhusiana na tukio hilo.

Hata hivyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi aliyefuatana na Pinda, alisikika akimwagiza Kamanda Kova kuhakikisha mchora ramani wa jengo hilo naye anatiwa nguvuni kwa kuwa jengo hilo lilikuwa la ghorofa 10, lakini likajengwa hadi 16. Mtu mwingine ambaye anatafutwa na jeshi la polisi kukamatwa ni Mhandisi Mshauri.
Lukuvi alimwagiza Kova kuwa watu waliokuwa karibu na jengo jingine la ghorofa 15 lililojengwa na mkandarasi huyo, kuhama mara moja na ubomoaji ufanyike bila kuleta madhara.
Mwenyekiti wa CUF
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba alitumia fursa hiyo kuitaka Serikali kuwabana makandarasi wasio na sifa kwani wanahatarisha maisha ya watu.
“Huu ni uzembe, wahandisi wa jiji walikuwa wapi? Wasimamizi na washauri walikuwa wapi hadi jengo linafikia ghorofa 16?” Alihoji Profesa Lipumba.

Profesa Lipumba aliitaka Bodi ya Makandarasi (CRB) kufuta leseni ya kampuni hiyo, kwani imeonyesha kuwa haiwezi kusimamia ujenzi na hivyo kusababisha vifo.
chanzo:mwananchi

UCHAGUZI KENYA ULIKUWA HURU NA HAKI ,KENYETTA NI RAIS

Mahakimu wa mahakama kuu wakitangaza uwamuzi wao kuhusiana na kesi ya Odinga

Mahakama Kuu Kenya yasema Uhuru alichaguliwa kihalali

Uhuru Kenyatta alichaguliwa kihalali, mahakama yasema
Uhuru Kenyatta alichaguliwa kihalali, mahakama yasema
 ...........................................................................................................................................
Mahakama ya juu zaidi nchini Kenya, imeamua kuwa rais mteule Uhuru Kenyatta atasalia kuwa rais mpya wa Kenya baada ya kusema kuwa uchaguzi ulifanywa kwa njia huru na ya haki.
Uchaguzi wenyewe ulifanyika tarehe nne mwezi Machi, ambapo hesabu ya kura ilimpa ushindi Kenyatta kwa zaidi ya laki nane.
Rais wa mahakama hiyo jaji mkuu Willy Mutunga alisema kuwa mahakama imekubali kwa kauli moja kuwa uchaguzi ulifanywa kwa njia ya huru na wazi na kuwa Kenyatta na mgombea mwenza wake walichaguliwa kihalali.
Uamuzi huu una maana kuwa Uhuru Kenyatta ndiye ataapishwa kama rais mpya wa Kenya tarehe tisa mwezi ujao
Kesi hiyo iliwasilishwa katika mahakama ya juu zaidi na mpinzani mkuu wa Kenyatta, Raila Odinga baada ya uchaguzi uliofanyika mapema mwezi huu.
Matokeo rasmi yalionyesha kuwa Uhuru alishinda uchaguzi kwa kumpiku Raila kwa asilimia 50.07 huku Raila akipata asilimia 43.28. Matokeo haya yalizuia kufanyika kwa duuru ya pili ya uchaguzi kwa kura 8,100.
Bwana Odinga aliishutumu tume huru ya uchaguzi na mipaka kwa kuhujumu matokeo ya uchaguzi ili kumpa ushindi Uhuru Kenyatta.
Uchaguzi wa urais, wabunge na wajumbe wengine wa serikali, ulifanyika tarehe nne mwezi Machi, ukiwa wa kwanza tangu uchaguzi uliokumbwa na ghasia mwaka 2007 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya elfu moja.
Bwana Kenyatta na mgombea mwenza wake ,William Ruto,wanakabiliwa na kesi katika mahakama ya jinai kwa kuchochea ghasia za mwaka 2007. Hata hivyo wamekanusha vikali mashtaka.
Mahakama ya juu zaidi inaweza kuthibitisha ushindi wa Kenyatta au kuubatilisha uamuzi wa wakenya na hivyo kuitisha uchaguzi mpya.
Vyovyote matokeo yatakavyokuwa kuna wale watakaoghadhabika mno.
Rais anayeondoka mamlakani, Mwai Kibaki amewataka wakenya kuwa watulivu na kukubali uamuzi wa mahakama lakini wengi wanatagemea sana idara ya mahakama ambayo imekuwa na mageuzi makubwa na ambayo sasa watu watu imani nayo.
Mawakili wa Odinga wanasema kuwa kesi yao ilihusisha madai ya kuhujumu hesabu ya kura pamoja na matatizo ya usajili wa wapiga kura na vile vile matatizo ya mitambo ya usajili wa wapiga kura.
Mnamo Ijumaa mahakama ya juu zaidi ilidurusu matokeo ya kura katika vituo 22 vya kupigia kura. Na pande zote mbili zilisema matokeo yalithibitisha misimamo yao.
Kenyatta ameutaja uchaguzi huo kama ishara ya kukuwa kwa demokrasia Kenya na ulifanywa kwa njia ya amani.
Tume ya uchaguzi, pia imesisitiza kuwa uchaguzi ulikuwa huru licha ya hitilafu za kimitambo
Wachunguzi wa kimataifa nao walisema kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki na kuwa tume huru ya uchaguzi uliendesha uchaguzi huo kwa uwazi.

Friday, March 29, 2013

Hatma ya Urais wa Kenyatta leo




















Nairobi, Kenya
JOPO la Majaji sita nchini Kenya leo wanatarajia
kuweka historia mpya watakapokuwa wakiandaa uamuzi wa uhalali wa uchaguzi Mkuu uliofanyika Machi 4 mwaka huu.
Watu mbalimbali ndani nan je ya nchi hiyo watafuatilia kesi hiyo iliyofunguliwa na Mgombea wa Muungano wa CORD Raila Amolo Odinga ya kupinga matokeo ya Urais yaliyomuweka Uhuru Kenyatta madarakani.
Uamuzi wa Jopo la Majaji sita wa Mahakama ya Juu nchini humo ndiyo itakayo maliza ubishi kama Kenyatta ataendelea kubaki Ikulu ama atarudi kwenye Uchaguzi huo. 
Huu ni uchaguzi wa kwanza nchini Kenya kupingwa Mahakamani chini ya Katiba Mpya ya nchi hiyo.
Odinga alifungua kesi katika Mahakama hiyo baada ya kudai kwamba haridhiki na matokeo ya Urais kutokana na wizi wa kura uliofanywa na Mgombea wa Jubilee Uhuru Kenyatta.

AIBU KWA TAIFA!


KWELI ni aibu kwa taifa kama la Tanzania, lenye ulinzi uliotimia lakini ni ajabu sana kuwaona wanawake wanaoishi mjini kwa kutegemea biashara haramu ya kuuza miili ‘machangudoa’ wamefikia kuifanya jirani kabisa na makazi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mizengo Pinda. WANASWA NA MAPAPARAZI
Wiki iliyopita, mapaparazi wetu  waliwanasa machangudoa hao wakiwa wanazurura kwenye Barabara ya Kenyatta inayopita mbele ya makazi ya waziri mkuu takriban mita 80 kutoka barabarani kwa lengo la kujiuza.
Ili kulijua hilo kwa undani, mapaparazi wetu walijifanya wateja kabla ya kuwapiga picha ili kuweza kuzungumza nao mawili matatu kuhusu kuwepo eneo hilo lenye heshima zake.  
Mmoja wa ‘wauza sukari’ hao aliyejitambulisha kwa jina la Hawa, mkazi wa Kinondoni, alikiri yeye na wenzake kufanya biashara hiyo kwenye eneo hilo.
“Ni kweli mimi na wenzangu tunapiga kambi eneo hili, huwa ikifika usiku tunaanzia kule Coco halafu tunakuja hadi huku, lakini mbona maswali mengi, unataka tufanye biashara kama vipi sepa,” alisema changu huyo akianza kupandisha jazba.

WATEJA WAO WAKUBWA NI HAWA
Kikubwa walichokiongea machangu hao walisema barabara hiyo yote hupitwa na viongozi wakubwa na wafanyabishara ambao baadhi yao ni wateja wao wakubwa. Wakasema hawamwamini sana mteja anayekwenda na Bajaj au Bodaboda kwa vile wanasumbua kutafuta eneo la kufanyia ngono.
“Wateja wetu wengi ni wale tunaomalizana ndani ya gari, hawa wa Bajaj na Bodaboda wengi wanataka kwenye majani, ni rahisi kukamatwa na polisi wa doria,” alisema changudoa mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Suzy lakini hakuwa tayari kutaja yaliko makazi yake.

CHAKUJIULIZA SASA
Inakuwaje wauza miili hao watanue eneo ambalo kimazingira linapitiwa na viongozi mbalimbali wazito kama vile mabalozi wa nje waliopo Tanzania, mawaziri, akiwemo waziri mkuu mwenyewe ambaye ni jirani kabisa na makazi yake?

ASKARI WAPO WAPI?
Yapo madai kwamba, askari wanaovalia mavazi ya kiraia ambao wanapaswa kuhakikisha usalama wa eneo lote la Coco Beach wanakaushia matendo hayo kwa kile kinachodaiwa wanapozwa na kitu kidogo.
“Askari wapo, lakini sema baadhi yao wanatufahamu, kwa hiyo ikitokea na sisi mambo yetu yamekaa vizuri tunachekiana,” alisema Suzy.
chanzo: GLOBAL PUBLISHER

MUNGA AWATAKA WANASIASA KUACHA KUAMUA BILA KUSIKILIZA WATAALAM KUHUSU ELIMU

    Bw Joseph J. Mungai  akifafanua jambo  wakati  alipowasilisha  barua  yake  ya  wazi  kwa  tume  ya elimu ya kufeli kwa asilimia 60 kwa wanafunzi wa kidato cha nne  mwaka jana 
...............................................................................................
 
ALIYEKUWA waziri  wa  elimu na mbunge mstaafu  wa  jimbo la Mufindi Kaskazin Joseph Mungai  awaonya  wanasiasa  kuacha  kuamua bila  kuzingatia ipasavyo utafiti na ushauri wa kitaaluma kuhusu Elimu ya Taifa letu.

Mungai aliyasema hayo leo  wakati akiwasilisha barua  yake ya wazi  kwa tume ya elimu  ya kufeli kwa asilimia 60 mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012 iliyoundwa na  waziri mkuu Mizengo Pinda .

Alisema  kuwa ili  kukuza  kiwango cha elimu nchini ni  vema  wanasiasa  wakaachana kabisa na utaratibu  wa  kuingilia na kutoa ushauri wao katika elimu bila kuwasikiliza wataalam kwani  kwa kufanya  hivyo kunachangia  elimu  kuyumba .

“Ninawapongeza kwa kuteuliwa na ahsante kutupa fursa wadau wa elimu kuwaletea maoni na  au/ushauri”

“Mimi ni mdau wa elimu, niliyewahi kuwa Mwenyekiti mwanzilishi wa Mufindi Education Trust (MET) iliyoanzisha katika wilaya ya Mufindi        na kuziendesha  kwa mika      zaidi    ya 10 Sekondari  9 za: (1) JJ Mungai (2) Sadani ( 3) Itengule  ( 4) Igowole ( 5) Itandula ( 6) Mgololo ( 7 ) Kibengu ( 8) Mdabulo na ( 9) Nyololo; ambazo sasa ni za serikali. Aidha nimewahi kuwa waziri wa Elimu na Utamaduni  mwaka 2000 hadi 2005”

Alisema  kuwa  Kufeli mwaka 2012 kidato cha Nne (KIV) kwa asilimia 60 halikuwa tukio lililoibuka ghafla bali waliofeli ( Division 0) mtihani huo waliongezeka kutoka mwaka 2007:9.7% ; 2008:16.3%; 2009:27.5%; 2010:49.6%; 2011:46.4% na sasa 2012:60%

Mungai  alisema  kuwa Kabla ya hapo waliofeli kidato cha Nne (KIV) WALIPUNGUA kutoak mawka 1998:24:3%:; 1999:20.0% 2000:21.6% 2001:22.6%, 2002:12.7%; 2003:12.2%, 2004:8.7%, 2005:10.7%, 2006:10.9%, na 2007:9.7% wastani wa kufeli 2004 hadi 2007 ni 10%.

Tazama hotuba ya bajeti ya Waziri wa Elimu na Utamaduni ya mwaka 2005/2006 kielelezo Na. 75.4 ukurasa wa 100; na BEST ( Basic Statics in Education, National Data) ya miaka  husika.

Wakati Kati ya 2004 na 2007 waliofeli kidato cha Nne  walikuwa wastani wa 10% ambayo   inavumilika. Kwa nini kati ya 2007 na 2008 kulikuwa na mruko kutoka 9.7% hadi 16.3%? Huo ukawa ndio mwanzo wa kuonge zeka  kila    mwaka    hadi kufikia 60%       ya mwaka huu!!!!! Wizara ya Elimu na OWM-TAMISEMI baada   ya  matokeo mabaya ya mwaka 2010 walifanya  “utafiti kudadisi sababu   za ufaulu huo mbaya” na taarifa yake ipo kwenye maktaba a Wizara” na iliandaliwa kauli ya waziri isomwe Bungeni”, lakini  hadi leo haikusomwa.   Ukweli ulifichwa; na mficha ugonjwa kifo kitamuumbua. Nukuu zangu kutoka Taarifa moja     isiyo   ya siri ya ndani    ya wizara ya Elimu.
 
“Kwa maoni yangu maboresho ya Elimu ya Serikali ya Awamu ya Tatu ambayo  yanaweza kusomwa katika maandiko   mawili    ya Wizara   ya Elimu     yaitwayo: (a) Nyaraka za Elimu 1999 hadi 2005, na ( b) Sheria ndogo za Elimu au kanuni za Elimu zilizotungwa kuyapa maboresho   hayo uzito w akisheria yamepelekwa NYARAKA ZA KALE (ACHIVES) kabla  ya wakati wake….Maboresho yamewekwa kando moja     baada ya jingine  au  hayakusimamiwa ipasavyo na Elimu yetu imerudi  ilivyokuwa kabla  ya mwaka 2000”
 
Kuhusu  ushauri  wake kwa elimu ya Tanzania  alisema  kuwa  Elimu ni nyenzo muhimu   sana kuliko zote katika kuboresha nguvu kazi ya Taifa na kuchochea  maendeleo  ya nchi ameamua kutonyamaza na kuwa muwazi kabisa, ingawaje mimi ni mwanasiasa  niliyestaafu. Kwa hiyo NASHAURI mambo yafuatayo:
 
Kwanza  kuwe na utaratibu  sahihi wa kupanda madarasa kwa ufaulu ( achievement based progression)  uliowekwa na waraka wa Elimu Na. 1& 2 wa 2002 urejeshwe na uimarishwe   bila  kuchelewa kuasnzia Darasa la kwanza,  la pili na la Tatu ambayo      Mwalimu Mkuu siku zote anayo madaraka    ya kukalilisha, kama mwanafunzi   hajazijua “K” 3: kusoma, kuandika na kuhesabu.
 
Alisema Mungia  kuwa jambo la  pili  ni tume ya Mhe. Waziri Mkuu ifanye kwanza REJEA ya maandiko ya Wizara ya Elimu  niliyoyataja akatika 4(a) na (b) hapo  juu yaliyomo maboresho ya         elimu ya 2002-2005 yaliyofanikisha kufaulu vizuri  katika   Elimu ya Msingi na Sekondari miaka       ya 2004-2007; badala ya kutumia muda mwingi na fedha nyingi kugundua upya gurudumu.
 
Wakati jambo la tatu alisema ni Taasisi  ya Elimu   Tanzania ( Tanzania  Institute of   Education –TIE) iagizwe na iachiwe  kutekeleza wajibu  wake wa kisheria chini ya Sheria ya Elimu ya 1995 wa kuandaa na kuboresha mitala.
Pia wanasiasa tuache kuamua bila  kuzingatia ipasavyo utafiti na ushauri wa kitaaluma kuhusu Elimu ya Taifa letu.
 
“Kutokana  na uamuzi mbaya na kuchelewa kuchukua  hatua ya marekebisho kila inapobidi; Elimu yetu imerudi ilikokuwa  kabla ya mwaka 2000. Rika zima la kielimu limepotea!!!sasa tunavuna kilichopandwa vibaya. Kwa hiyo TUJISAHIHISHE kwa kuacha kuingilia na kuamua bila kuzingatia  utafiti na ushauri fwa kitaaluma ili tusije kuumbuliwa tena na matokeo mabaya kama    hayo ya kidato cha Nne   ya mwaka 2012. Aidha inafaa matokeo ya mitihani    yawe yanatangazwa kwa uwazi hata kama ni mabaya kwa sababu, narudia “ anayeficha maradhi       kifo kitamuumbua”

MAJERUHI WA GHOROFA DAR WAFIKIA 19 WANNE WAPOTEZA MAISHA

    Hiki ndicho kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15.
    Winchi likiokoa mabaki ya moja ya gari lililoangukiwa na kifusi.
VIDEO IKIONYESHA JINSI JENGO LILIVYOANGUKA JIJINI DAR LEO.
   Rais Jakaya Kikwete (katikati) akiangalia hali ya uokoaji inavyoendelea.
    Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, akitoa maelekezo ya jinsi ya kuondoa kifusi eneo la tukio.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki (katikati) akifuatilia shughuli ya uokoaji.
    Watu mbalimbali wakiondoa kifusi.
   Askari aliyejuu ya farasi akihakikisha usalama eneo hilo.
   Baadhi ya watu wakilisukuma gari ambalo pia lilikuwa kwenye ajali hiyo.
  Mama Salma Kikwete (kulia) na Rais Kikwete wakiangalia kifusi.
   Kijana aliyenusurika katika ajali hiyo akinywa kahawa.
LEO majira ya saa mbili na nusu asubuhi Watanzania wameingia kwenye vilio baada ya jengo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es Salaam, kuanguka na kuwafunika watu waliokuwa eneo hilo na kusababisha wengine kupoteza maisha. Mpaka sasa haijajulikana idadi kamili ya watu waliokuwemo ndani yake,.

  Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea, huku nondo nyembamba zikionekana na kuacha maswali miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo.
  Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea.
 Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea.

Taarifa  zilizotufikia mchana  huu zinadai  kuwa  idadi ya majeruhi  wa ghorofa  lililoporomoka  jijini Dar es Salaam imefikia  18  wakati  watu  wanne  wanadaiwa  kupoteza maisha na jitihada za uokoaji  bado  zinaendelea .

SERIKALI YATANGAZA NAFASI 1,134

Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi nafasi hizo za kazi ambazo zinapatikana katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz ni kwa ajili ya Waajiri mbalimbali wa ofisi za umma.
Daudi alifafanua kuwa Waajiri hao ni pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Katibu Mkuu wizaraya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa, Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo Jinsia na Watoto, Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Ajira, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara. Katibu Mkuu Wizara ya Sayansi na Teknolojia, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Katibu Ofisi ya Rais Maadili.
Wengine ni Katibu Tawala wa Mkoa Kagera, Iringa, Ruvuma, Mbeya, Mwanza, Shinyanga, Manyara, Dar es Salaam, Morogoro, Geita, Pwani, Mara, Kilimanjaro, Lindi, Singida, Tabora, Tanga, Katavi na Arusha, Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Iringa, Songea, Shinyanga,
Morogoro, Singida, Kigoma/Ujiji na Temeke.
Nafasi nyingine ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Mufindi, Kyela, Rungwe, Mbeya, Chunya, Biharamulo, Bukoba, Muleba, Namtumbo, Songea, Morogoro, Makete, Mkuranga, Mbinga, Tunduru, Ukerewe, Sengerema, Ilemela, Busega, Maswa, Meatu, Shinyanga, Kishapu, Kilosa, Msalala, Rufiji, Rorya, Ruangwa, Lushoto, Mkinga, Mpanda, Monduli, Ngorongoro,Kigoma, Nachingwea, Rombo, Same, Singida, Urambo, Tabora, Babati, Mbulu, Simanjiro, Kiteto, Handeni, Pangani, Kibondo, Chamwino, Mtwara, Nanyumbu, Mpwapwa, Kongwa naTandahimba. Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe, Kibaha, Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na TEMESA.
Katibu huyo amesema kuwa nafasi hizo zilizotangazwa zimegawanyika katika kada zifuatazo; Mchambuzi Mifumo ya Kompyuta daraja la II – (Nafasi 10), Afisa Vipimo II – Nafasi 6, Mpima Ardhi daraja la II (Nafasi 26), Mhandisi daraja la II – Ufundi Umeme – Nafasi 9,  Afisa Mipango Miji daraja la II– Nafasi 13, Mhandisi daraja la II - Ujenzi (Nafasi 16), Mhandisi daraja la  II - Maji (Nafasi 13), Afisa Misitu daraja la II (Nafasi 7), Afisa wa Sheria daraja la II – nafasi 3, Mtakwimu Daraja la II – nafasi 8, Mthamini daraja la II – Nafasi 7,  Mkadiriaji Ujenzi daraja la II  – nafasi 4, Afisa Ufugaji Nyuki Daraja la II – nafasi 1, Mhandisi Daraja la II – Nishati (Nafasi 3), Msanifu Majengo Daraja la II– (nafasi 3) na Mjiolojia Daraja la II – Nafasi 7, Fundi Sanifu daraja la II (Ujenzi) -Nafasi
26, Mvuvi Msaidizi Daraja la II – nafasi 8 na Fundi Sanifu Msaidizi (Maji) -nafasi 19.
Nafasi nyingine zilitotangazwa na Serikali ni Nahodha Daraja la II – Nafasi 6, Fundi Sanifu daraja la II - Haidrolojia -Nafasi 6 ,Fundi Sanifu Daraja la II -Nafasi 6, Msaidizi Misitu Daraja la II – nafasi 7, Fundi Sanifu Daraja II – Ramani – Nafasi 6, Fundi Sanifu Daraja la II –Maendeleo ya Jamii– Nafasi 3, Dereva Mitambo Daraja la II– nafasi 1,  Mpiga chapa msaidizi- Nafasi 5, Operata wa kompyuta msaidizi - nafasi 3, Fundi Sanifu Daraja la II - Migodi – nafasi 9, Polisi Msaidizi– Nafasi 5, Mpokezi–Nafasi 1, Katibu Mahsusi daraja la III-nafasi 10, Mlinzi –Nafasi 100, Dereva Daraja la II – nafasi 178,   Msaidizi wa Ofisi– Nafasi 30, Afisa Kumbukumbu daraja la II– nafasi 1,  Mwenyekiti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya – nafasi 5, Afisa Mtendaji wa Kata Daraja la III– nafasi 10, Afisa Mtendaji wa Kijiji Daraja la II– nafasi 6.
Aidha, kada nyingine ni Afisa Mtendaji wa Kijiji daraja la III) – nafasi 232, Afisa Mtendaji Mtaa daraja la III– nafasi 3, Afisa Lishe daraja la II– nafasi 4, Fundi Sanifu Daraja la II - Ufundi na Umeme, Afisa Biashara msaidizi– Nafasi 1, Mchapa Hati daraja la II – Nafasi 1,  Mhandisi Daraja la II –Baharini-(nafasi 1), Dereva Mitambo Daraja la II – (nafasi 1), Dereva wa Vivuko daraja la II – Nafasi 3, Mkufunzi Mwandamizi Daraja II - Nafasi 1, Mkufunzi Daraja ii - Nafasi 2, Fundi Sanifu Msaidizi (bomba)–nafasi 3, Fundi Sanifu Msaidizi (Umeme) –Nafasi 4, Mkufunzi Daraja II– nafasi 3, Mkufunzi daraja la II -Jiolojia – nafasi 1, Mkufunzi Msaidizi– Jiolojia – nafasi 1, Fundi Sanifu daraja II -Ubunifu Mipango Miji – nafasi 1, Fundi Sanifu daraja II- Urasimu Ramani – Nafasi 5, Fundi Sanifu daraja II- Uchapaji Ramani –Nafasi 4, Fundi Sanifu Daraja la II -Maabara– nafasi 13, Fundi Sanifu Msaidizi (Ujenzi– nafasi 1), Fundi Sanifu daraja la II -Nafasi 4, Wakufunzi wasaidizi – nafasi 54 na Mhasibu Mkuu daraja II.
Katibu alifafanua kuwa nafasi 949 zilizoko katika tangazo la Kiswahili ni kwa ajili ya Waajiri walioainishwa hapo juu na kwa Tangazo la nafasi wazi 185 zilizoko katika tangazo la lugha ya Kiingereza ni kwa ajili ya Taasisi na Wakala mbalimbali za Serikali.
Daudi amesema mwisho wa kupokea barua za maombi ya kazi ni tarehe 9 Aprili, 2013.
Aidha, amewataka waombaji wote wa fursa za ajira kufungua matangazo yote mawili ya kazi na kuzingatia masharti ya Matangazo yote kama yalivyo katika lugha ya Kiingereza na Kiswahili kabla ya kutuma maombi yao.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Ofisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.  27 Machi, 2013
Kwa maelezo zaidi; wasiliana na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
kwa Barua pepe; gcu@ajira.go.tz  au Simu; 255-687624975

RAIS JAKAYA KIKWETE, MAKAMU WAKE DKT. BILAL, WAZIRI MKUU, MIZENGO PINDA WASHIRIKI KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA MBUNGE WA CUF DAR LEO


Rais Jakaya Kikwete, akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani CUF, Salim Hemed Khamis, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa baada ya kuuguaa ghafla wakati akiwa katika Kikao cha Kamati ya Bunge cha Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam juzi. Marehemu mefariki kwa ugonjwa wa shinikizo la damu.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri Mstaafu, Edward Lowasa, na viongozi wengine wakishiriki shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia CUF, aliyefariki jana mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zimefanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Machi 29, 2013. 
Katibu wa Bunge la Jamhuri, John Joel, akisalimiana na Samuel Sitta, katika Ukumbi wa Karimjee wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia CUF, aliyefariki jana mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zimefanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Machi 29, 2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya ndugu wa marehemu wakati viongozi wakiondoka kwenye ukumbi wa Karimjee baada ya kushiriki katika shughuli za kuaga mwili wa marehemu, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba, Salim Hemed Khamis (CUF), aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Adam Malima, wakizungumza nje ya ukumbi wa Karimjee, baada ya kushiriki shughuli ya kuaga mwili wa marehemu,Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia Chama cha CUF, aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Waombolezaji wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu,Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia Chama cha CUF, aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakiingiza kwenye gari tayari kuelekea uwanja wa ndege kwa safari ya kuelekea Pemba kwa maziko, yatakayofanyika leo. Picha na OMR.

WAANDISHI WAANDIKE MAKALA ZAIDI KULIKO HABARI ZA MATUKIO


Waandishi wa habari wametakiwa kujikita zaidi kwenye habari za kiuchunguzi na utafiti (makala) kuliko habari za matukio pekee hali itakayowasaidia kupata mafanikio makubwa kwenye fani na katika maisha yao sanjari na kujenga heshima katika jamii.

Rai hiyo imetolewa na mkurugenzi wa Jambo Arusha Publisher ambae pia ni mmiliki wa gazeti la Kutoka Arusha Anjelo Mwoleka alipokuwa Akihutubia kwenye mahafali ya chuo cha Uandishi wa habari na utangazaji Arusha (AJTC) yalifanyika hivi karibuni kwa Mrombo iliyoko wilaya ya Arusha mkoani hapa.

Mwoleka ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo alisema kuwa Waandishi wengi wa sasa wanashindwa kuendelea kifani na kimaisha na wengine hata kudharaulika na jamii kwa kupenda kuandika habari za matukio hasa za kipolisi au za mikutano hali ambayo inashusha hadhi ya taaluma ya Uandishi wa habari hivyo kila mwandishi apende zaidi kuandika habari za kiutafiti,

“Waandishi wengi utakuta kazi yao kubwa ni kuandika tu habari za matukio na mikutani kuwa kamanda wa mahala Fulani amesema wa mkoa huu amesema……..na sasa imefikia hadi sasa wanaandaliwa taarifa (press) kwa kujulikana kuwa hawapendi kujishughulisha, hivyo niwaombe tu kuwa hali isiendekezwe kama kweli wewe ni mtu unayependa kuendelea kifani na maisha kwa ujumla badala yake andaeni vipindi vya redio na televisheni au kuandika makala kwenye magazeti kwani itakusaidia kujua mambo mengi na kukupa heshima kama mwandishi mzuri” alisema Mwoleka.

Mbali na hilo pia amewataka waaandishi wasiwe na ukomo wa elimu bali wawe na hamu ya kujiendeleza zaidi ikiwemo masoma ya kujikita katika habari za aina moja, pia wawe waadilifu kimaadili na mavazi ili kuweza kurahisisha kupata habari kwenye vyanzo vya habari au wadau sanjari na kutokutegemea kuajiriwa zaidi kuliko kujiajiri,

“Niwaombe tu leo mnapomaliza elimu yenu mkiingia kazini mkawe waadilifu kwa kuvaa mavazi ya heshima pia mnapoenda kwa wadau msiwe wa kwanza wa kuwatishia wadau kuwapa pesa ili msiwaandike vibaya kwani huo ni wizi kama wizi mwingine hali itayopelekea kupigwa, kutekwa au hata kuteswa kwa tabia zisizo za kimaadili” aliongeza Mwoleka.

Mwoleka pia aliwataka wahitimu hao kufuata vigezo tisa za mwandishi bora kuwa ni pamoja na kuzingatia matumizi mazuri ya lugha, kuwa na uhakika wa habari wanazoziandika, kuwa vyanzo vingi vya habari pia kufanya utafiti wa kutosha juu ya habari watazozinadika, kuzingatia usahihi wa habari, pia kuwa makini katika matumizi ya takwim sanjari na uwiano wa habari wanazoziandika.

Awali katika risala iliyosomwa na wanafunzi hao walisema kuwa katika chuo hicho wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo jengo maktaba, vifaa vya kusoma kwa vitendo kama kamera za picha za kawaida, video na mike za kutosha.

akimkaribisha mgeni rasmi mkurugenzi wa chuo hicho cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha( AJTC) Joseph Mayagila alisema wanafunzi wanaohitimu kwa siku hiyo ni wanafunzi 52 kwa ngazi tofauti ikiwemo ngazi ya cheti na stashahada ya uandishi wa habari na utangazaji.

Thursday, March 28, 2013

AOWA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI KWA NG"OMBE 45

Sehemu ya ng"ombe wanaopelekwa kwa ajili ya mahali

Zahanati ya kijiji cha Malangali ambayo mwanafunzi huyo alikuwa akipima na sasa ameamua kuikwepa zahanati hiyo kukwepa mkono wa sheria

**  Kufuatia sakata hilo Diwani viti maalumu atishiwa kuuwawa

** Polisi waingilia kati sakata hilo                                                    


Mkazi wa Kijiji cha Mpona Kata ya Totowe Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya anatuhumiwa kumwachisha masomo mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Totowe    kwa kumuoa  kisha kumpa ujauzito.
  
Mwananchi huyo aliyefahamika kwa jina la Ndugu  Shigala Mwachanya anatuhumiwa kutenda kosa hilo kwa kumpa ujauzito mwanafunzi aliyejulikana kwa jina la Ngolo Jiguma(19) ambaye amesitisha masomo yake kutokana na ujauzito alionayo ambapo wazazi walipatana kulipana Ng’ombe 45 kama fidia ambapo tayari Ng’ombe 20 wameshatolewa.
  
Aidha kutokana na Mwanafunzi huyo kutambua kuwa  Wazazi wake wametenda kosa ameamriwa kuto hudhulia kliniki katika kituo cha afya cha Malangali na badala yake amekuwa akienda katika Zahanati ya Totowe ili kukwepa kukutwa na vyombo vya sheria.
Uongozi wa  Kijiji hicho umeanza kulifuatilia sakata hilo baada ya kupata taarifa kutoka kwa Mkuu wa Shule aliyokuwa akisomaMwanafunzi huyo Frank Mwakisyala ambapo juhudi hizo zinaonekana kugonga ukuta kutokana na kutishiwa kuawa na mtuhumiwa.
  
 Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho  Ndugu Yaledi Mwanguku amesema kuwa   suala hilo lipo juu ya uwezo wake hivyo alilazimika kulipeleka suala hilo kwenye uongozi wa kata kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
  
Diwani wa Viti Maalumu kata hiyo Christina Kibwana ambaye alionekana kulipokea suala hilo na kuanza kulifuatilia pia alidai kuwa alipokea ujumbe mfupi wa maandishi ukimtaka ahame kijijini hapo lasivyo aache kulifuatilia sakata hilo na asipoacha angeuawa.
  
Diwani huyo amesema ujumbe huo wenye maneno ya kutishia yalikutwa kwenye barua nje kidogo nje ya nyumba yake ambapo aliongeza kuwa baada ya kuona hali hiyo aliamua kutoa taarifa katika kituo  kidogo cha Polisi cha Galula Wilayani Chunya.
Diwani huyo ameendelea kulalamika kuwa baada ya kutoa taarifa katika kituo hicho hakuna dalili wala hatua zozote zilizochukuliwa ambapo alisema kuna dalili za Rushwa ambayo inasemekana kuwa Polisi walipewa Rushwa ya Shilingi Milioni Moja na Nusu(1500,000/=).
  
Amesema kutokana na kutoonekana kwa hatua zozote aliamua kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Chunya ambapo walimkamata mtuhumiwa huyo kisha kufunguliwa kesi katika Mahakama ya Wilaya ya Chunya.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Totowe kupitia Chama cha Mapinduzi, Godian Wangala  amethibitisha kutokea kwa matukio yote hayo na kuongeza kuwa amesikitishwa na kitendo cha Mwananchi huyo pamoja na wazazi kwa kumwachisha masomo na kumsababishia Mwanafunzi kumnyima haki ya kupata elimu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani  amekiri kupokea taarifa hizo na kuahidi kulifanyia kazi kwa ukaribu zaidi na kuhakikisha wahusika watachukuliwa hatua zinazostahili.

MTUHUMIWA WA MAUWAJI YA MWANAHABARI DAUDI MWANGOSI KUFIKISHWA MAHAKAMANI LEO


Huyu  ndie mtuhumiwa wa mauawaji ya Mwangosi (kulia)
 
MTUHUMIWA  wa kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa chanel ten mkoani
Iringa, marehemu Daud Mwangosi ambae  upelelezi  wake bado  kukamilika anatarajiwa kufikishwa mahakamani  leo machi 28  kwa mara nyingine .
 
Kesi  hiyo  yenye mvuto mkubwa kwa  wakazi wa mkoa  wa Iringa na watanzania pamoja na dunia kwa ujumla imekuwa ikiendelea kutajwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa  wa Iringa na hadi sasa ni zaidi ya mara 10 mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani kwa staili mbali mbali .


Katika  kesi hiyo ambayo mtuhumiwa  wake ni  askari  wa  kikosi  cha kutuliza ghasia mkoa  wa Iringa
(FFU) Pasificus Cleophace Simon (23) mwenye namba G 2573 mbali ya  wananchi  wengi  kuwa na mvuto na kasi hiyo ila kwa upande wa jeshi la polisi mkoa  wa Iringa bado  askari wamekuwa  wakimficha mtuhumiwa  huyo ili asipigwe  picha na  wanahabari .

Monday, March 25, 2013

UGONJWA WA MAHINDI KUTOKA KENYA WAWAATHIRI WANANCHI KATA YA KIKWE MERU

Na Queen Lema, MERU

ZAIDI ya Hekari 300 kutoka katika kata ya Kikwe Wilayani Meru mkoania
Arusha zimeharibiwa vibaya na ugonjwa mahindi kutoka Nchini Kenya hali
ambayo itafanya wakulima washindwe kupata mahindi wakati wa mavuno

Akiongea na “Majira”mapema jana diwani wa kata hiyo bw Emanuel Silayo
alisema kuwa hali hiyo ya ugonjwa ambayo imekumba kata hiyo ya Kikwe
inaashiria njaa kubwa sana kwa kuwa mazao ya mahindi shambani hakuna
huku wakulima wakiwa wameshapanda

Silayo alisema kuwa Miezi michache iliyopita wakulima waliweza kupanda
mazao ya nafaka hasa mahindi lakini baada ya mahindi kuchomoza
yalianza kushambuliwa na ugonjwa hadi kufa

Alisema kuwa pamoja na kuwa mahindi hayo yamekufa wakati wakulimna
wengi wamepanda kwa ajili ya mategemeo ya chakula katika eneo hilo la
Kikwe lakini mahindi machache sana yameweza kusalia hali ambayo bado
ni kiashirio kikubwa sana cha Njaa

“tunaomba msaada kwa sasa jamani kwa kuwa mahindi ambayo tumeyalima
yameliwa yote na wadudu  na inavyosemekana ugonjwa huu wa mahindi
umetokea Nchini Kenya sasa kama hatutaweza kusaidiwa tena kwa haraka
ni wazi kuwa tutakufa kwa njaa ilihali Serikali ina uwezo mkubwa sana
wa kuokoa hili janga”alisema

Katika hatua nyingine alisema kuwa mbali na eneo hilo la Kikwe kuweza
kukabiliwa na changamoto hiyo ya ugonjwa wa mahindi lakini kwa sasa
ugonjwa huo tayari umeshaweza kuambukiza hata maeneo ya jirani na kata
hiyo.

Alifafanua kuwa kama tahadhari haitaweza kuchukuliwa kwa haraka sana
basi huenda wakati wa mavuno ndani ya mwaka huu kusiwe na mavuno
kabisa hivyo baa la njaa kuweza kutawala katika Wilaya hiyo ya Meru.

Akiongelea Ugonjwa huo wa mahindi kutoka nchini Kenya Afisa Kilimo
Wilaya ya Meru,Grace Solomoni alisema kuwa ugonjwa huo ni hatari sana
kwa kuwa unashambulia zao la mahindi hadi kufa lakini bado mkulima
anaweza kupata angalau kiasi kidogo

Grace alisema kuwa kwa mujibu wa taararibui za kilimo mara baada ya
shamba kuathiriwa na ugonjwa huo shamba linapswa kupumzishwa kwa
kipindi cha miaka mitatu ili vijidudu vife lakini kama wakulima
wataendelea kulima basi watasababisha  vijidudu hivyo kuzaliana kwa
wingi sana

“ni kweli huu ugonjwa wa mahindi umeingia katika kata hiyo  pamoja na
eneo la Nkoandrua lakini wakulima wanapswa kufuata taratibu za kilimo
bora kwa kuhakikisha kuwa wanawatumia zaidi wataalamu ili kuendelea
kuyafanya mashamba yao kuwa na ubora tena wa hali ya juu lakini kama
watajiongoza wao wenyewe wataweza kusabisha hata rutuba kuondoka
kabisa”aliongeza Grace

CHADEMA ARUSHA WAMVAA OCD BAADA YA OCD KUTOA LUGHA ZA MATISHO KWA VIJANA WA ARUSHA MJINI

Na Mwandishi wetu,Arusha


Chama cha Demokrasia na Maendelo,mkoa wa Arusha(CHADEMA) kupitia Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Goodbless Lema amemtaka Kamanda wa polisi Wilaya ya Arusha Mjini ,Bw Gilles Muroto kuomba radhi wananchi hususani Vijana ndani ya siku tatu mara baada ya Kamanda huyo kusema na kudai kuwa vijana wa Arusha Mjini ni wavuta bangi

Akiongea na vyombo vya habari mapema leo Mbunge Lema alisema kuwa kauli ziliztolewa na Kamanda huyo siku ya jana wakati akizuia maaandamano ya leo ambayo yalikuwa yamepengwa kufanywa na chama hicho

Aidha Lema alisema kuwa wakati kamanda huyo anapita huku akiwa na gari la Polisi lenye namba za usajili T 1848 aliwatangazia vijana kuwa wao ni wavuta bangi, na wanywa viroba na mtu yoyote atakayejitokeza kwenye maandamano basi atavunjwa mguu

Lema aliendelea kudai kuwa kwa kamanda kama yeye hapaswi kutoa kauli hizo ambazo zinalenga kuchochea uchochezi na ubaguzi ndani ya Mji wa Arusha badala yake alipaswa kutumia zaidi busara ambayo ingewafanya vijana hata kama kuna maandamano wasiweze kuandamana

Alifafanua kuwa kwa kuwa ametoa lugha za uchochezi dhidi ya Vijana ambao wapo ndani ya jimbo lake basi anatakiwa kutumia hilohilo gari la polisi kuomba radhi wananchi wa jimbo lake ndani ya siku tatu lakini kama hataweza kufanya hivyo basi wao kama chama wataweza kuchukua hatua kali zaidi

“jana majira ya mchana katika eneo la Mbauda hadi kwa Muorombo Kamanda huyo alitoa lugha hizo za Uchochezi dhidi ya Vijana na kudai kuwa kama Vijana watajitikeza katika maandamano atawavunja miguu sasa huu ni uonevu tena wa hali ya juu sana hivyo tumeazimia kwa kauli moja kuwa anapaswa kuomba radhi kwa kauli ambazo amezitoa kama hatafanya hivyo tutaenda mbele zaidi kwa kumchukulia hatua ili iwe fundisho kwa viongozi wengine”aliongeza Lema.

Mbali na hayo Lema alidai kuwa suala hilo la kuwatolea Vijana wa Arusha Mjini maneno kama hayo  ni suala la kukandamiza chama hicho lakini pia katika Kumbukumbu zao zinaonesha kuwa alishwai kukataa baadhi ya barua ambazo ziliplekwa na Chadema hali ambayo inaonesha wazi kuwa huo ni ukandamizaji tena wa hali ya juu sana.

“Unapokuwa kiongozi kama OCD unatakiwa kutenda haki kwa vyama vyote hata kama hukipendi lakini ndio ilishatokea lakini kama unabagua hadharani hadharani na kutumia kofia yako basi utakuwa ni miongoni mwa watu wenye dhambi nyingi sana hivyo basi ni vema kila kiongozi akatenda haki”aliongeza Lema

Hataivyo akiongea kwa njia ya Simu na gazeti hili ili kujibu shutuma zinazomkabili OCD huyo alidai kuwa yeye sio msemaji wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha lakini msemaji ni Kamanda wa Polisi mkoa,wakati naye Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Arusha,Liberatus Sabas  alidai kuwa mpaka sasa bado hajapokea malalamiko hayo,hivyo atayafanyia kazi

Saturday, March 23, 2013

HUU ni ukatili kwa 100%


Marehemu Martha Charles (22) baada ya kuchinjwa shingoni na mume wake, Isack Nzwalile. (29).
HUU ni ukatili kwa 100%! Martha Charles (22), mkazi wa Nyahanga wilayani hapa ambaye ni mtumishi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama ameuawa kinyama kwa kuchinjwa shingoni na mume wake, Amani lina habari ya kusikitisha.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Afande Onesmo Lyanga alisema tukio hilo lilitokea katikati ya wiki iliyopita ambapo pia alimtaja mume anayedaiwa kutekeleza unyama huo kuwa ni Isack Nzwalile (29), mfanyabiashara wa bucha la nyama ya ng’ombe.
 
Isack Nzwalile aliyemchinja mkewe, Martha Charles.
Afande Lyanga alisema mtuhumiwa alimchinja  mkewe wakiwa wamelala chumbani kwenye nyumba ya wazazi wa mwanaume huyo na baada ya kufanya ukatili huo alikimbia.
Jessica Elialinga (19) baada ya kuchinjwa na mpenzi wake, Musa Petro (27).
Habari za uhakika zilizopatikana kutoka katika familia ya marehemu zilisema chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi wa kifamilia ambapo mtuhumiwa alianza kwa kumlaumu mama yake mzazi kwa kitendo cha kumtafutia kazi mkewe katika Halmashauri ya Mji wa Kahama wakati yeye alikuwa hataki mkewe afanye kazi.
Musa Petro aliyemchinja mpenzi wake Jessica Elialinga.
Habari zilizopatikana eneo la tukio kutoka kwa mmoja wa ndugu anayeishi na familia hiyo, Paul Edward alisema mbali na kuchinjwa shingoni pia marehemu alikatwakatwa sehemu mbalimbali za mwili wake.
Marehemu Martha Charles (kulia) enzi za uhai wake akiwa na rafiki yake.
Edward alisema usiku wa tukio akiwa amelala katika moja ya chumba ndani ya nyumba hiyo, alisikia kelele za ugomvi kutoka kwenye chumba cha wanandoa hao hali iliyomfanya apige kelele zilizowafikia majirani ambao walifika kutoa msaada.
Akasema majirani hao sanjari na yeye walimkuta mtuhumiwa ameshamchinja mkewe kwa kisu na kutoweka kusikojulikana.
Marehemu Martha Charles akiwa na mumewe, Isack Nzwalile wakifurahia maisha enzi za uhai wake.
Nao majirani waliokwenda kutoa msaada ambao hawakupenda majina yao yatajwe gazetini, walisema walikuta mwili wa Martha ukiwa kitandani huku amekatwa na kitu chenye ncha kali katika eneo lote la shingo, ndipo walipomchukua na kumkimbiza hospitali lakini tayari alikuwa ameshakata roho.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, Noel Mkisi alisema baada ya muuaji huyo kutoroka usiku huohuo jitihada za kumsaka zilianza.
Tukio la kuchinjwa kinyama kwa mwanamke huyo limetokea siku chache baada ya hivi karibuni, mchuna ng’ombe Musa Petro (27) naye kumuua kwa kumchinja kwa kisu mpenzi wake, Jessica Elialinga (19).
 
Jessica Elialinga enzi za uhai wake.
Naye Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Maduka ya Nyama Kahama, Faraji Mohamed akiongea na gazeti hili alisema Petro ni mfanyakazi wa Nzwalile katika duka lake la nyama (bucha) ambapo alishangaa kusikia Nzwalile amemchinja mke wake kama alivyofanya mfanyakazi wake, Petro.
Wakati tunakwenda mitamboni habari zilizopatikana kutoka Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kahama na kudhibitishwa na OCD George Simba zilisema mtuhumiwa huyo amekamatwa.
Chanzo; Globa publisher