Wananchi wakiwa katika eneo la
uchimbaji mora kata ya Moshono jijini Arusha wakiangalia zoezi la
uokoaji ukiwa unaendela mara baada ya watu 17 kupoteza maisha baada ya
kufukiwa na kifusi hicho leo
Wanajeshi wakiwa wamebeba mwili wa marehemu juu ya machela mara baada ya kuutoa katika kifusi hicho mapema leo
Mbunge Lema akiwasili katika eneo hilo
Watu 13 wamefariki
dunia baadaya ya kuangukiwa na kifusi cha Moram katika eneo la Moshono
jijini Arusha huku wengine 4 wahofiwa kupoteza maisha baada ya
kufukiwa na kifusi hicho
Tukio hilo la
kusikitisha lilitokea leo jiji hapa majira ya saa 5:30 asubuhi baadaya
ya mvua kubwa kunyesha katika machimbo hayo ambayo inasemekana ndo
chanzo cha tukio hilo
Hata hivyo vikosi
mbalimbali vya uokoaji vilifika katika eneo hilo pamoja na viongozi
mbalimbali waliwasili katika eneo hilo tayari kushuhudia hali halisi
pamoja na kushiriki zoezi la uokoaji
Jamiiblog ilishuhudia
kila baada ya dakika 5 maiti ilikuwa ikitolewa ndani ya kifusi hicho
kilichokuwa kimewafunika wachimbaji hao
Pia majeruhi wawili
walikimbizwa katika hospitali ya Mkoa Mt. meru pamoja na miili ya
marehemu kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo
Mkuu wa Mkoa huu
Magessa Mulongo alisema kuwa tukio hilo ni la kusikitisha na hivyo
kuagiza machimbo yote ya mchanga kufungwa hadi hapo serikali itakapotoa
amri ya kuendelea na shughuli za uchimbaji
Mbunge wa jimbo la
Arusha mjini Godbless Lema pamoja na Mbunge wa Arumeru Mashariki
walifika katika eneo hilo kusaidia shughuli za uokoaji
Meya wa jiji hili
Gaudence Lyimo alisema tukio kama hilo lilitokea mwaka 1997 ambapo watu
7 walipoteza maisha hivyo uongozi wa jiji uliwaagiza wachimbaji kutumia
katapila badala ya mikono
Hata hivyo wananchi
waliishutumu vikali serikali kwa kushindwa kuboresha miundo mbinu ya
eneo hilo kwa kuwa tukio kama hilo si mara ya kwanza kutokea hivyo
walidai kuwa ni uzembe wa hali ya juu
Zoezi la utambuzi wa miili unatarajiwa kufanyika kesho katika hospitali ya Mt.meru
bertha blog inawapa pole na kuwatia moyo ndungu jamaa na marafiki waliopoteza ndugu zao katika tukio hilo
chanzo: jamii blog
No comments:
Post a Comment