Pages

Pages

Sunday, December 29, 2013

MATUKIO YA KUSIKITISHA YALIYOFUNGA MWAKA 2013 MKOA WA ARUSHA.


Alama ya jiji la Arusha.


Tunapokaribia kufunga mwaka 2013 na kuupokea mwaka wa 2014, yapo matukio makubwa mawili ya kusikitisha yaliyotikisa mkoa huu wa Arusha ambao umepoteza maisha ya ndugu zetu na kujeruhi wengine huku baadhi yao wakipoteza viungo vyao vya mwili.
                                                           
kanisa la Mt. Joseph Mfanyakazi lililoko jijini Arusha


Tukio la kwanza ni mlipuko wa bomu lililotokea katika kanisa la katoliki la mtakatifu joseph mfanyakazi parokia ya olasiti tarehe 05/05/2013 na kusababisha vifo vya watu watatu(3) na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa.

Tukio hilo linalofananisha na vitendo vya kigaidi, lilitokea majira ya saa tano asubuhi, wakati balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu Francisco Padilla na Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Arusha, Josephat Lebulu walipokuwa wakiendesha ibada ya kuzindua Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Olasiti lililoko nje kidogo ya jiji la Arusha.
                                                   
kila mtu akitafuta pa kukimbilia kunusuru maisha yake baada ya kulipuliwa kwa bom hilo
bom lilivyoua na lilivyojeruhi.
                                   
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha


Katika taarifa za uchunguzi wa awali wa jeshi la polisi mkoani hapa, ulifanikiwa kuwakamata watuhumiwa tisa(9)  na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo la mlipuko wa bomu kanisani.

 Watuhumiwa hao ni victor Ambros Kalist, (20), dereva wa bodaboda na mkazi wa kwa Morombo; Yusuph Lomayani Josee (18) mwendesha bodaboda mkazi wa kwa Morombo na George Bathlomeo Silayo (23) mfanyabiashara na mkazi wa Olasiti.

Watuhumiwa wengine waliokamatwa ni raia watatu toka nchi za falme za kiaruabu (UAE) Abdul Aziz Mubrak (30) mfanyakazi wa mamlaka ya mapato katika falme za kiarabu, Fouad Saleem Ahmed Al Hareez Al Mahri (29) mfanyakazi wa kikosi cha zimamoto katika Falme za Kiarabu, Saeed Abdulla Saad (28) askali polisikitengo cha traffic katika falme za Kiarabu, pamoja na raia mmoja wa Saudi Arabia Al-Mahri Saeed Mohseens (29)

Raia hao wa kigeni walikamatwa pamoja na wenyeji wao wawili ambao ni raia wa tanzania wenye asili ya Yemen.  Majina ya watanzania hao ni Mohamed Suleiman Saad, (38) mkazi wa ilala jijini Dar es Salaam na Jasm Mubarak (29) mkaazi wa mtaa wa Bondeni jijini Arusha.
                                              
balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu Francisco Padilla kushoto na Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Arusha, Josephat Lebuluwalipotembelea majeruhi katika hospitali ya mkoa Arusha, mount meru kuwapa pole na kuwaombea
                                      
mh, Bilali nae alifiika Arusha na kutoa pole kwa majeruhi.


Hata hivyo mwisho wa siku Raia hao wa Saud Arabia waliachiwa huru kwa madai ya kutohusika ambapo alishikiliwa kijana Ambros (20) dereva wa bodaboda na mkazi wa kwa Mrombo jijini hapa ambapo alifikishwa mahakamani na hadi leo kesi yake inaendelea.

Kinachosikitisha zaidi ni baadhi ya majeruhi ambao bado hawajapona lakni hakuna wa kuwahudumia kama mwanzo serikali ilivyoahidi kuwahudumia matokeo yake matembezi ya viongozi wengi waliofika Arusha kuwapa pole na kuwaahidi kuwahudumia imekuwa kama nguvu ya soda huku baadhi wakijipatia maarufu wa bure kwa kuahidi bila kutekeleza,    JAMANI MUOGOPENI MUNGU.
                                                  
mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha mjini Lema wakiingia kwenye mkutano.


Tukio la pili lililoinua hisia za wakazi wa jiji hili la Arusha ni mlipuko mwingine wa bomu la kutupa kwa mkono kwenye  Mkutano wa Chadema wa kumaliza kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani mjini Arusha,

Aidha mkutano huo ulivunjika baada ya bomu kulipuka na kuua watu wanne na wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa. Bomu hilo lililipuka  dakika chache kabla ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe kumaliza kuhutubia mkutano huo uliofanyika katika Viwanja vya Soweto mjini Arusha na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi wa mkoa huu.

bomu hilo lililopuka karibu na jukwaa walilokuwa wamekaa viongozi wa Chadema, wakati Mbowe na Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema wakiwa katika hatua za kumaliza kuhutubia.
                                   
bom lilipoangukia watu wawili walifariki papo hapo akiwemo kiongozi wa chama hicho kata.
    


Taarifa zilidai kuwa kuna mtu aliyeonekana akirusha kitu kinachodaiwa ni bomu hilo kwenye eneo la jukwaa karibu na gari la matangazo la chama hicho, lakini alipokuwa akifuatiliwa, polisi nao walikuwa wameanza kudhibiti watu kwa kulipua mabomu ya machozi na kupiga risasi za moto hali iliyozidisha taharuki.

Baada ya tukio hilo watu waliokuwa katika mkutano huo walitawanyika wakikimbia kuokoa maisha yao huku wakimwacha Mbowe na Lema na viongozi wengine wakiwa bado wako jukwaani pamoja na waliopoteza maisha na kujeruhiwa vibaya.


Hata hivyo kufuatia mlipuko huo, uchaguzi huo mdogo wa udiwani ulihairishwa kwa muda na baadae kufanyika wiki moja kabla huku CHADEMA ikibahatika kunyakua kata hizo zote ambazo ni Kimandolu, Themi, Elerai na Kaloleni.

Katika tuki hili pamoja na viongozi mbalimbali kuahidi wakiwemo wa dola kuwa watafanya uchunguzi wa kina kuwabaini waliohusika na tukio hilo lakini hadi leo hii hakuna uhakika wa nani anatuhumiwa kuhusika na tukio hilo zaidi ya fununu za awali kuwa bomu hilo lilirushwa na kuratibiwa na viongozi wa chama hicho wenyewe, INAWEZEKANAJE...... SIJUI!!!!!!!!!!!!
WALIOJERUHIWA
                                             
watoto nao waliumia sana
BERTHA BLOG inaiombea mkoa wetu wa Arusha mema kwa mwaka huu tunaoupokea kesho wa mwaka mwaka 2014 kusiwepo na matukio haya tena ya maafa.

MAWAZIRI WALIOENGULIWA WAMPA KIBARUA RAIS KIKWETE


Rais Kikwete anafanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri ikiwa imepita miezi 18 tangu alipowang’oa mawaziri wanane kutokana na tuhuma mbalimbali.   

DAR ES SALAAM. 
RAIS Jakaya Kikwete anatarajia kuipanga upya safu ya Baraza lake la Mawaziri wakati wowote, huku baadhi ya naibu mawaziri wakipewa nafasi kubwa ya kuteuliwa kuwa mawaziri kamili.


Hatua hiyo inatokana  na uamuzi wake wa  kutengua uteuzi wa mawaziri wanne alioufanya siku tisa zilizopita, mawaziri hao walishutumiwa kushindwa kuwajibika  katika utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili.

Ripoti ya kamati ndogo ya  Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira iliyoundwa kuchunguza operesheni hiyo, ilieleza kuwa athari zilizotokana na operesheni hiyo zilisababishwa na wizara nne zilizokuwa zikiongozwa na mawaziri hao.

Waliong’olewa katika sakata hilo ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David.

Rais Kikwete anafanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri ikiwa imepita miezi 18 tangu alipowang’oa mawaziri wanane kutokana na tuhuma mbalimbali.

Historia inaonyesha kuwa Rais Kikwete amekuwa na utaratibu wa kuwapa uwaziri wabunge ambao amewateua, huku akiwapandisha naibu mawaziri kuwa mawaziri.

Kwa mujibu wa Ibara ya 66 (1) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kama ilivyofanyiwa marekebisho inampa mamlaka Rais kuwateua wabunge 10, mpaka sasa ameshawateua wanane na kubakiza nafasi mbili pekee.
Kati ya wabunge wanane walioteuliwa na Rais Kikwete, watano walipewa wizara za kuziongoza.

Wabunge hao na wizara zao kwenye mabano ni Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) na Profesa Makame Mbarawa (Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia).

Wengine ni Profesa Sospeter Muhongo (Nishati na Madini), na Saada Mkuya na Janet Mbene (wote ni Naibu Mawaziri wa Wizara ya Fedha).

Kutokana na utamaduni huo, Dk Asha-Rose Migiro anapewa nafasi kubwa ya kuingia kwenye baraza jipya la mawaziri, kwani naye hivi karibuni ameteuliwa kuwa mbunge.

Wabunge ambao wameteuliwa na Rais lakini hakuwapa uwaziri mpaka sasa ni Zakia Meghji, James Mbatia na Dk Asha-Rose Migiro.
                                                                                               MWANANCHI

MGOGORO WA ARDHI KUHAMIA KITETO,...WAKULIMA WAVAMIWA NA KUCHINJWA KAMA MNYAMA




WILAYA ya Kiteto imeingia kwenye orodha ya maeneo yanayotisha kwa mauaji ya kinyama baada ya wakulima kuuawa mara kwa mara na wafugaji kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kugombea ardhi.

Miongoni mwa waliouawa kinyama Dec 20 kwa kuchinjwa shingo yake ni Juma Mlagwa (49) wa Kitongoji cha Kalikala Kata ya Njoro (Kiteto) ambaye alivamiwa nyumbani kwake usiku na kundi la vijana wa kifugaji masai (makorianga)

Imeelezwa kuwa wakati anavamiwa zilisikika Risasi zikipigwa juu Kitongojini hapo na baada ya watu kuendelea kujificha ndani vijana hao walianza kunyinyizia nyumba zao mafuta aina ya petrol kisha kuwasha moto

Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Ally Mussa Mwenyekiti wa Kitongoji hicho alisema siku hiyo haitasahaulika mashani mwake kwa yaliyotokea kutokana na vitendo hivyo akisema ilikuwa mara ya kwanza kuona mtu anachinjwa hadharani.

“Nilichomewa Pikipiki zangu mbili pamoja na vitu mbalimbali vya ndani zikiwemo nguo vyakula, lakini nilichonusuri ni roho yangu ambayo hadi leo nasema najivunia uhai nilio nao”alisema Mwenyekiti huyo

Alisema chanzo cha mauaji hayo ni jamii ya kifugaji wamasai kuingiza mifugo yao kwenye shamba la mmoja wa wakulima Kitongojini hapo na baada ya kukatazwa walimpiga kisha nae kupigwa ndipo wakakusanyana kupanga uvamizi huo.

Hata hivyo baada ya kufikishwa taarifa kwa viongozi wa Serikali walidaiwa kulifika Kitongojini lakini walikataa kwenda kuongea nao km chache kwa madai kuwa ni uongo kwamba hakuna watu waliokusanyana

Akielezea hayo Mwenyekiti huyo alisema tatizo ni uongozi dhaifu kuanzia ngazi ya Kitongoji hadi Wilaya ambapo alidai kuwa ukabila umeshamiri kwa viongozi kujiona kuwa wanahaki ya kutfanya utetezi katika upande mmoja

Kwa upande wake Lairumbe Mollel Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya akizungumzia sakata hilo alimzodoa mwenyekiti huyo wa Kitongonji kuwa ni muongo kwani baada ya wao kufika kabla ya tukio alikataa kuwataja wahusika

Hata hivyo kauli hiyo ilionekana kutokuwa na mashiko baada ya mwenyekiti huyo wa Kitongoji kuonyesha udhaifu wa viongozi hao akisema baada tu ya kufika hawakuweza hata kukubali kupelekwa walikoweka kambi vijana hao wa kimasai

“Baada ya kufika walitaka nisema majina ya walioleta fujo na nilipowataka twende eneo la tukio wakakata nakuona kuwa hawakuwa na njia njema kisha wakarejea Kiteto ambapo usiku vijana hao wakatekeleza azima yao ya kuchinja mtu mmoja na kumpiga mwingine risasi kisha kuwajeruhi watu saba”alisema Mwenyekiti huyo wa kitongoji

Waliofariki katika uvamizi huo ni pamoja na Juma Malagwa (49) ambaye alichinjwa shingo, Yohana Ivo (33) ambaye alipigwa sehemu mbalimbali za mwili na kusababisha kifo pamoja na watu wengine saba kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto kwa kujeruhiwa kwa fimbo na mapanga

Waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto ni Hoti Daniel (38) Emanuel matias (21) Juma Bahati (13) Mwajuma Hamisi (20) Habiba Ally (16) Mwajuma Martin pamoja na Musa Juma (16) aliyepelekwa Dodoma kwaajili ya matibabu

Hata hivyo mkuu huyo wa Mkoa wa Manyara Elaston Mbwillo akiwa katika kitongoji hicho aliwapa siku 30 viongozi wa Wilaya ya Kiteto kuweka utaratibu wa kuwatambua wananchi hao ili kuondoa tofauti zao waweze kufanya kazi bila bughdha

“Ninyi wananchi mwende kujisajili Kijijijini ili Serikali iwatambue kwani maisha bora kwa wananchi yatapatikana kwa kufahamika mlipo ili mpatiwe huduma za jamiiambazo kwa sasa hamna hata moja”alisema Mbwillo,

Chanzo, jumamtanda blog

Saturday, December 28, 2013

HATIMAYE KANISA KATOLIKI PAROKIA YA MTAKATIFU JOSEPH MFANYAKAZI LILILOKO OLASITI JIJINI ARUSHA LIMEZINDULIWA LEO RASMI.

Mafundi wakikamilisha hatua za mwisho jana.
Makaburi ya watu watatu waliouawa na mabomu May 5,mwaka huu.
Maandalizi ya vya mwilini.
Mafundi wakijenga eneo lilipotua Bomu kama kumbukumbu ya kudumu iliyopoteza maisha ya watu na kujeruhi.
Balozi wa Baba Mtakatifu nchini,Fransisco Padilla hatimaye leo amezindua Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Olasiti ambalo lilikua lizinduliwe May 5 mwaka huu lakini zoezi hilo lilisitishwa baada ya kutokea shambulio la bomu la kutupwa kwa mkono lililosababisha watu 3 kufariki dunia na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa.
Uzinduzi huo uliofana kwa shangwe na furaha baina ya waumini wa dhehebu hilo na wakazi wa Arusha kwa ujumla ulifanikiwa kuhudhuriwa na maaskofu kutoka sehem mbalimbali katika pembe za nchi ya Tanzania waliokuwa wakimpongeza balozi Fransisco kwa ujasiri wake wa kurudi kwa kazi hiyo.
   

GAZETI LA MTANZANIA KURUDI MTAANI KWA KWA YA AJABU KIHABARI...

Limerudi tena!!!!
Mwani Nyangassa na Esther Bhoke Wakiwa wamepozi katika picha, baada ya uchovu wa mizunguko yao, makamanda hao wako katika harakati ya kuliuza gazeti hilo ambalo limefunguliwa kutoka kifungoni.
Poz kwa Poz, Wafanyakazi wa New habari (2006) Ltd, "#TEAM Mauzo"wakiwa wamepozi katika picha ya pamoja baada ya kuzunguka jiji la Dar es salaam kufanyA mauzo ya copy ya gazeti la MTANZANIA.

Wednesday, December 25, 2013

ZITTO KABWE AWAUMBUA MBOWE NA SLAA MCHAMA KWEUPE UWANJANI KIGOMA

                                                             


MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, amejibu mashambulizi kwa viongozi wa Chadema, kutokana na kile alichosema wanazunguka na kusema maneno yasiyo ya ukweli. 



Akihutubia maelfu ya wananchi waliokusanyika katika Uwanja wa Mwanga Centre, Kigoma mjini, alisema alichukua kadi ya uanachama wa Chadema mwaka 1993 wakati huo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbrod Slaa akiwa bado yuko CCM. 



"Wakati hao wenye midomo mikubwa wanaoongea sasa, walipokuwa wamekumbatia watawala, nyinyi mlikuwa mnapigwa mabomu kutaka mageuzi, eti leo wao wapinzani zaidi kuliko sisi na ndiyo maana hatuwezi kuwaachia.



Hatuwezi kukubali, hatutoki, demokrasia ni mchakato na mwenzenu nimekuwa kwenye mchakato huu. Kadi yangu ya Chadema nimeichukulia kwenye uwanja huu, tarehe moja mwezi wa nne mwaka 1993, nikiwa na miaka 16, wakati nachukua kadi yangu, Katibu Mkuu wa chama changu alikuwa yuko CCM.
Akizungumza kile alichosema ni uongo unaosambazwa na viongozi wa juu wa chama hicho, Katibu Mkuu Dk Slaa na Mwenyekiti wake Mbowe waligawana maeneo Mbowe akaenda Kanda ya Ziwa na Dk Slaa Kanda ya Magharibi. 



Alisema kwenye mikutano hiyo, Mbowe anasema kuwa endapo mbunge huyo atarudi yeye Mbowe atajiuzulu, suala alilosema linaonyesha kuwa tayari ameshafukuzwa bila hata utetezi wake kusikilizwa. 




Alisema baada ya viongozi hao kuzungumza na kusema mambo hayo na yeye aliamua kurudi nyumbani Kigoma na baada ya kuona hilo Dk Slaa akahoji mbunge huyo anafanya vikao hivyo kama nani.



"Mimi nimekata rufaa, wajumbe wa baraza kuu wa Mtwara, Ruvuma wanaandika barua wanataka mkutano mkuu, Katibu Mkuu akiwa Igunga anasema hiyo ni haramu na hao wafuasi wa Zitto watafanya Zitto afukuzwe, si __wamwamesha nifukuza? takachokuja kunijadili, hivyo si wameshanifukuza ?

KAKA AMCHINJA MDOGO WAKE KISA BABA KUMUANDIKISHA MALI MDOGO WAO


Mtoto Kalebu Simwelu(6) enzi za uhai wake, mtoto huyu alichinjwa na kaka yake kwa madai kuwa baba yake alimrithisha mali zote.
Mwili wa marehemu Kalebu ukiingizwa katika makazi yake ya milele katika makaburi ya Nakonde nchini Zambia.
Katekista wa Kanisa katoliki la Tunduma Daud Lwila akiendesha
Ibada ya mazishi katika makaburi ya Nakonde nchini Zambia
Umati wa waombolezaji waliohudhuria maziko ya mtoto Kalebu aliyeuawa kwa kuchinjwa na kaka yake aliyedai kuwa baba yao amemrithisha mali zote.
Ndugu na jamaa wakiendelea na mazishi katika makaburi ya Nakonde nchini Zambia ambako mtoto Kalebu alizikwa.
KATIKA hali isiyo ya kawaida mmoja wa watoto wa Diwani wa Kata ya Nkangamo Weston Simwelu(55) ambaye watoto wake waliuawa kwa kuchinjwa na kunyongwa,Enock Simwelu(23) amekiri kufanya mauaji hayo kwa madai kuwa yametokana na baba yao kumrithisha mali zote marehemu mdogo wao.
Mauaji hayo yalitokea Disemba 19 eneo la TAZARA katika mji mdogo wa Tunduma ambapo wauaji walivamia nyumbani kwa Diwani huyo na kufanya mauaji ambapo walimchinja kwa kisu mtoto Kalebu Simwelu(6) na mfanyakazi wa ndani Sista Nyirenge(17) na miili yao kuficha sebuleni nyuma ya kochi.
Imeelezwa kuwa Enock pamoja na nduguye wa mama mmoja Gabriel walishirikiana kwa pamoja kufanya mauaji hayo kwa madai ya baba yao kufanya upendeleo kwa  mdogo wao Kalebu(6) ambaye ni mtoto wa mke mdogo wa baba yao.
‘’Chanzo cha mauaji hayo kimebainika, mtoto wa mke mkubwa wa Diwani, Enock amekiri kuhusika na mauaji hayo ameshirikiana na nduguye Gabriel Simwelu, madai yao, baba yao amemwandikisha mali zote marehemu Kalebu, mtoto wa mke mdogo wa Diwani,’’amesema Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Barakael Masaki katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi kwa Vyombo vya habari iliyotolewa na Kamanda Masaki ni kwamba mmoja wa watuhumiwa walioshikiliwa kwa ajili ya mahojiano ambaye ni kaka wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Enock Simwelu(23) amedai kukiri kufanya mauaji hayo akishirikiana na mdogo wake aliyemtambulisha kwa jina la Gabriel Simwelu(19).
Kulingana na taarifa hiyo ni kwamba mtuhumiwa huyo alidai kuwa yeye amehusika moja kwa moja na mauaji hayo kutokana na tatizo la baba yake kuandikisha mali zote kwa mdogo wao ambaye ni mtoto wa mke mdogo Kalebu Simwelu.
Kamanda Masaki alisema kuwa mauaji hayo pia yalifanywa kwa kushirikiana na jirani na rafiki yao aliyefahamika kwa jina la Patrick Msigwa(18) mkazi wa eneo la Majengo katika mji mdogo wa Tunduma.
Mara baada ya kutokea kwa mauaji hayo Jeshi la Polisi liliwanasa watu watano wakiwemo watoto wa mke mkubwa wa Diwani Simwelu ambapo kulingana na madai ya awali ni kwamba chanzo kilitokana na mgogoro wa kifamilia.
Wakati tukio hilo la mauaji linatokea Baba wa marehemu Simwelu alikuwa shambani katika kijiji cha Kipaka ilhali mama mzazi wa mtoto Tumaini Yohana(29) alikuwa kazini katika Ofisi ya Halmashauri ya mji wa Tunduma.
Aidha mazishi ya mtoto Kalebu yalifanyika Disemba 21 kwenye makaburi ya Nakonde katika mji mdogo uliopo nchini Zambia na kuhudhuria na umati wa wakazi wa mpakani mwa Tanzania na Zambia ambapo mwili wa mfanyakazi wa ndani Sista Nyirenge yalifanyika katika kijiji cha Isansa wilayani Mbozi.
 
PICHA KWA HISANI YA SHOMI MTAKI-TUNDUMA

Sunday, December 22, 2013