Pages

Pages

Sunday, December 29, 2013

MATUKIO YA KUSIKITISHA YALIYOFUNGA MWAKA 2013 MKOA WA ARUSHA.


Alama ya jiji la Arusha.


Tunapokaribia kufunga mwaka 2013 na kuupokea mwaka wa 2014, yapo matukio makubwa mawili ya kusikitisha yaliyotikisa mkoa huu wa Arusha ambao umepoteza maisha ya ndugu zetu na kujeruhi wengine huku baadhi yao wakipoteza viungo vyao vya mwili.
                                                           
kanisa la Mt. Joseph Mfanyakazi lililoko jijini Arusha


Tukio la kwanza ni mlipuko wa bomu lililotokea katika kanisa la katoliki la mtakatifu joseph mfanyakazi parokia ya olasiti tarehe 05/05/2013 na kusababisha vifo vya watu watatu(3) na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa.

Tukio hilo linalofananisha na vitendo vya kigaidi, lilitokea majira ya saa tano asubuhi, wakati balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu Francisco Padilla na Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Arusha, Josephat Lebulu walipokuwa wakiendesha ibada ya kuzindua Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Olasiti lililoko nje kidogo ya jiji la Arusha.
                                                   
kila mtu akitafuta pa kukimbilia kunusuru maisha yake baada ya kulipuliwa kwa bom hilo
bom lilivyoua na lilivyojeruhi.
                                   
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha


Katika taarifa za uchunguzi wa awali wa jeshi la polisi mkoani hapa, ulifanikiwa kuwakamata watuhumiwa tisa(9)  na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo la mlipuko wa bomu kanisani.

 Watuhumiwa hao ni victor Ambros Kalist, (20), dereva wa bodaboda na mkazi wa kwa Morombo; Yusuph Lomayani Josee (18) mwendesha bodaboda mkazi wa kwa Morombo na George Bathlomeo Silayo (23) mfanyabiashara na mkazi wa Olasiti.

Watuhumiwa wengine waliokamatwa ni raia watatu toka nchi za falme za kiaruabu (UAE) Abdul Aziz Mubrak (30) mfanyakazi wa mamlaka ya mapato katika falme za kiarabu, Fouad Saleem Ahmed Al Hareez Al Mahri (29) mfanyakazi wa kikosi cha zimamoto katika Falme za Kiarabu, Saeed Abdulla Saad (28) askali polisikitengo cha traffic katika falme za Kiarabu, pamoja na raia mmoja wa Saudi Arabia Al-Mahri Saeed Mohseens (29)

Raia hao wa kigeni walikamatwa pamoja na wenyeji wao wawili ambao ni raia wa tanzania wenye asili ya Yemen.  Majina ya watanzania hao ni Mohamed Suleiman Saad, (38) mkazi wa ilala jijini Dar es Salaam na Jasm Mubarak (29) mkaazi wa mtaa wa Bondeni jijini Arusha.
                                              
balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu Francisco Padilla kushoto na Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Arusha, Josephat Lebuluwalipotembelea majeruhi katika hospitali ya mkoa Arusha, mount meru kuwapa pole na kuwaombea
                                      
mh, Bilali nae alifiika Arusha na kutoa pole kwa majeruhi.


Hata hivyo mwisho wa siku Raia hao wa Saud Arabia waliachiwa huru kwa madai ya kutohusika ambapo alishikiliwa kijana Ambros (20) dereva wa bodaboda na mkazi wa kwa Mrombo jijini hapa ambapo alifikishwa mahakamani na hadi leo kesi yake inaendelea.

Kinachosikitisha zaidi ni baadhi ya majeruhi ambao bado hawajapona lakni hakuna wa kuwahudumia kama mwanzo serikali ilivyoahidi kuwahudumia matokeo yake matembezi ya viongozi wengi waliofika Arusha kuwapa pole na kuwaahidi kuwahudumia imekuwa kama nguvu ya soda huku baadhi wakijipatia maarufu wa bure kwa kuahidi bila kutekeleza,    JAMANI MUOGOPENI MUNGU.
                                                  
mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha mjini Lema wakiingia kwenye mkutano.


Tukio la pili lililoinua hisia za wakazi wa jiji hili la Arusha ni mlipuko mwingine wa bomu la kutupa kwa mkono kwenye  Mkutano wa Chadema wa kumaliza kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani mjini Arusha,

Aidha mkutano huo ulivunjika baada ya bomu kulipuka na kuua watu wanne na wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa. Bomu hilo lililipuka  dakika chache kabla ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe kumaliza kuhutubia mkutano huo uliofanyika katika Viwanja vya Soweto mjini Arusha na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi wa mkoa huu.

bomu hilo lililopuka karibu na jukwaa walilokuwa wamekaa viongozi wa Chadema, wakati Mbowe na Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema wakiwa katika hatua za kumaliza kuhutubia.
                                   
bom lilipoangukia watu wawili walifariki papo hapo akiwemo kiongozi wa chama hicho kata.
    


Taarifa zilidai kuwa kuna mtu aliyeonekana akirusha kitu kinachodaiwa ni bomu hilo kwenye eneo la jukwaa karibu na gari la matangazo la chama hicho, lakini alipokuwa akifuatiliwa, polisi nao walikuwa wameanza kudhibiti watu kwa kulipua mabomu ya machozi na kupiga risasi za moto hali iliyozidisha taharuki.

Baada ya tukio hilo watu waliokuwa katika mkutano huo walitawanyika wakikimbia kuokoa maisha yao huku wakimwacha Mbowe na Lema na viongozi wengine wakiwa bado wako jukwaani pamoja na waliopoteza maisha na kujeruhiwa vibaya.


Hata hivyo kufuatia mlipuko huo, uchaguzi huo mdogo wa udiwani ulihairishwa kwa muda na baadae kufanyika wiki moja kabla huku CHADEMA ikibahatika kunyakua kata hizo zote ambazo ni Kimandolu, Themi, Elerai na Kaloleni.

Katika tuki hili pamoja na viongozi mbalimbali kuahidi wakiwemo wa dola kuwa watafanya uchunguzi wa kina kuwabaini waliohusika na tukio hilo lakini hadi leo hii hakuna uhakika wa nani anatuhumiwa kuhusika na tukio hilo zaidi ya fununu za awali kuwa bomu hilo lilirushwa na kuratibiwa na viongozi wa chama hicho wenyewe, INAWEZEKANAJE...... SIJUI!!!!!!!!!!!!
WALIOJERUHIWA
                                             
watoto nao waliumia sana
BERTHA BLOG inaiombea mkoa wetu wa Arusha mema kwa mwaka huu tunaoupokea kesho wa mwaka mwaka 2014 kusiwepo na matukio haya tena ya maafa.

No comments:

Post a Comment